rudi maktaba >Fiqh >Yaliyomo >

KUTOA A U KUOMBA SADAKA

Kimeandikwa na : SHEIKH HURRI ‘AAMILI

Kimekusanywa na kutarjumiwa na : AMIRALY M. H. DATOO

MANENO MAWILI

Bismillahir Rahmanir Rahiim

Natanguliza kumshukuru Allah swt pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na Ma-Imamu a.s. walionijaalia Tawfiqi ya kuweza kuwaleteeni mbele yeni kitabu hiki.

Mimi nimekitarujumu kitabu Dhambi Kuu la kutokulipa Zaka, Khums na Sadaka katika Kiswahili na wakati nikiwa nikiifanya kazi hiyo, niliona itakuwa afadhali iwapo Sadaka pia nitakitayarishia kitabu chake. Na hivyo ndicho hiki kipo mikononi mwenu.

Kwa hakika sisi tunakuwa daima tukitoa sadaka lakini hatujui habari zaidi kuhusu Sadaka na hivyo nimevutiwa na kazi aliyokuwa ameifanya Marehemu Mullah Asghar M.M.Ja’afer, aliyekuwa Mwenyekiti wa World Federation of Khoja Shi’a Ithna-Ashery Muslim Communities, na hivyo nimekitarjumu katika Kiswahili.

Kitabu hiki cha Sadaka ni sehemu ya Kitabu kiitwacho Wasa’il as-Shi’a mlango wa Kitabuz - Zakaat cha Sheikh Hurri ‘Aamili.

Vile vile kumeongezewa habari za Elimul Hadith na Majma’ul Hadith kutokea juhudi zilizofanywa na Maulama wa Kishi’a.

Ni matumaini yangu kuwa kitabu hiki kitatufaidisha sote na tutakuwa na moyo zaidi wa kutoa Sadaka.

TUJIELIMISHE KUHUSU ILIMU NA MENGINEYO …