rudi maktaba >Fiqh >Yaliyomo >

2.UTANGULIZI

Zipo riwaya nyingi mno ambazo zimenakiliwa kutoka Mtume s.a.w.w. na Maimamu a.s. ambazo zinasema kuwa mwenye kuoaanakuwa amejidhibiti vyema katika Islam na nusu ya sehemu ya imani inambidi afanye jitihada ili aweze kuiimarisha.Mwenye kuoa rakaa mbili za mwenye kuoa ni afadhali kuliko rakaa' sabini za mtu asiyeoa. Aliyeoa ni mpenzi wa Allah s.w.t.

Mtume s.a.w.w. amesema kuwa mtu asifanye uchelewesho katika kuoa kwani watoto watakaozaliwa watakuwa wakimtii na kumtukuza Allah s.w.t. ambapo ujira wake utakuwa ukipatiwa wazazi wao na mema yao pia yatakuwa yakilipwa wao.Vile vile amesema kuwa tuuendeleze Ummah wake ili aweze kuwa na fakhari Siku ya Qiyama.

Iwapo mwanamke mimba yake itaanguka basi Siku ya Qiyama mtoto wake huyo atakataa kuingia Jannat (Peponi) hadi hapo wazazi wake waingizwe nae pamoja.Limetolewa onyo kuwa "kufa bila ya kuoa ni vibaya mno."

Imam Jaafer as-Sadiq a.s. amenakiliwa akisema kuwa "Iwapo nitakuwa na dunia pamoja na vitu vyake vyote vikawa vyangu bila ya kupitisha usiku mmoja bila mwanamke,basi mimi siridhii hayo yote.Ni afadhali kukosa vyote hivyo kuliko kukosa mwanamke. Vile vile sala ya aliyeoa ni afadhali kuliko sala za kila siku pamoja na saumu za asiyeoa."

Vile vile kuna riwaya isemayo kuwa mtu atakapo kujitakasa mbele ya Allah swt,basi inambidi afanye harusi na kuoa katika hali ya umasikini na ufukara ni kuthibitisha imani na uaminifu juu ya Allah s.w.t. kwani Allah s.w.t. amesema "Oeni hata katika hali ya umasikini na ufukara kwani nitawaghaniisha."

Ipo katika riwaya kuwa muoe wake wazuri na mtu atakayeoa mwanamke kwa sababu ya tamaa ya mali au uzuri,basi atakosa vyote.Na atakayeoa kwa kuangalia dini na imani ya mwanamke,basi atapata mali na uzuri vyote.

Katika kumsifu mwanamke,ni bora kuliko dhahabu na fedha na mwanamke mwovu ni mbaya sana kwani hata mchanga ni afadhali kuliko yeye. Mwanamke mwenye gharama ndogo na vilevile anazaa watoto kwa urahisi na mwanamke mwenye mahari ndogo basi ni mwema na mwanamke mwenye gharama kubwa na mwenye kuzaa watoto kwa mushkeli na mwenye mahari kubwa,basi mwanamke kama huyo si mwema.

Ni Sunnah kusoma nikah wakati wa usiku,kwani Allah s.w.t. ameufanya usiku kuwa mapumziko na starehe na inapoangukia Qamar dar Aqrab (nyota iwapo katika Nge) basi msifanya nikah na kunapokuwa joto kali,iwapo kutakuwapo na ndoa,basi kunauwezekano wa kuachana.Vile vile kusifanywe ndoa siku ya jumatatu kwani siku hiyo ni mbaya mno na iwapo itakuwa ni siku ya kuzaliwa kwa Ma'sum a.s. au Idd basi hakuna shida yoyote.Haifai kuoa katika tarehe 26,28 na 30 za kila mwezi.

Kuoa si faradhi lakini iwapo kuna hatari ya kutumbukia katika maasi,basi itakuwa ni faradhi kuoa,na kwa mjane kolewa si vibaya,kwani kubakia pekee mara nyingi inakuwa mushkeli kimaisha na hivyo haitakiwi kujitumbukiza katika magumu ya maisha ambapo tunaweza kujiepusha.Kwa hakika ni jambo la kusikitisha kuona katika jamii yetu wajane wakitupwa bila kujali na kudharauliwa kama ni wenye nuksi ambapo inatubidi sisi kuwajali na kuwatunza na kuwaoza inapowezekana ili wao nao waweze kuishi maisha kama wengineo wote.

Ipo Hadith inayosisitiza mno kabisa kumfanyia na kumgharamia mtu harusi na nikah kwani inayo thawabu adhimu.Kila neno litakalosemwa na kila tendo litakalotendwa na kila hatua itakayochukuliwa,Allah swt atampa thawabu za sala za usiku na saumu za mwaka mzima.Na huko Jannat atampatia Hur al-Ain elfu moja wakiwa na majumba yaliyorembeshwa kwa Yaquti na vito vya thamani.

Ipo riwaya inayosema kuwa atakayemwozesha mjane, basi Siku ya Qiyama atakuwa miongoni mwa wale

waliorehemiwa na Allah swt.

Atakaye suluhisha baina ya bibi na bwana,basi Allah swt atamjaalia thawabu za mashahidi elfu na hatua zozote zile atakazozichukua katika kufanyisha suluh na matamshi yote yatakayotoka atapatiwa thawabu za ibada za mwaka mzima.