rudi maktaba >Fiqh >Yaliyomo >

SEHEMU YA PILI

25. MUTA' : NDOA YA KUKATIZA AU MKATABA.

Kuhusiana na somo hili la muta', nimejaribu kugawa hili somo katika sehemu tatu ambazo zote ziko zinashikamana kwani kila sehemu inaelezea jambo moja kwa kinaganaga.

Sehemu ya kwanza inahusiana sana na namna hii ya ndoa katika Islam ilivyokuwa na ambavyo ipo bado na masharti yake na kanuni zake na namna inavyobidi kutekelezwa kwa mujibu wa madhehebu haya. Shia Ithna Asheria na ambavyo inavyohukumiwa na 'Ulamaa wa Madhehebu haya. Sehemu ya pili pia inajishughulisha sana na kueleza ubora na umuhimu wa ndoa kama hii katika jamii ya Islam kwani inasaidia kukomesha uovu na uharibifu uliozagaa katika jamii ya Kiislamu na suluhisho lake, hatimaye sehemu ya tatu inaelezea uovu mwingine ambao umeikumba jamii ya Kiislamu ambavyo mwanamke anatoka nyumbani mwake na kwenda kufanya kazi nje kwa ajili ya mambo yasiyo na misingi na hatimaye nyumba inapoteza ule ubora na hadhi yake ya kifamilia, n.k.

Sehemu ya kwanza:

Sharia takatifu kuhusu hii ndoa.

Katika kusoma mapokeo na maandishi ya maarifa ya Sharia kuhusu ndoa hii ya kipindi kifupi, kuna mambo fulani fulani ambayo yanabidi kwanza yafikiriwe na yamefafanuliwa vyema kwa mujibu wa Fatawa za ulamaa wa Madhehebu ya Shia Ithna Asheria.

Katika mpokeo huo,kuhusu somo hili,neno muta' ndilo litumikalo sana. Inawezekana kusemwa kwa sababu ya habari zielezwamo katika Qurani kuhusu hii ndoa ya kukatiza. Katika aya hiyo, neno Istimuta limetumika na ambavyo neno Muta' limetokana nalo. Kutokana na mapokeo ya Ma-Imam a.s. au kwa kutokana na mapokeo ya Khalifa Omar, unalipata neno hilo la muta' kwa mfano Khalifa Omar amesema,"wake wawili wa vipindi vifupi wanaruhusiwa." Au Jabir ambaye asema,"sisi tulinufaika sana na ndoa ya muda mfupi wakati wa Mtukufu Mtume s.a.w.w."Vile vile katika mapokezi mengine yaliyo pokelewa na Shu'ba bin Muslim ambaye anasema,

"Mimi nilimwendea Asma binti Abu Bakr. Nilimuulizia kuhusu hii ndoa ya kukatiza nae”.

Kwa ujumla neno muta' linatumika zaidi sana hata kuliko wakati wa Mtume s.a.w.w. au nyakati za wafuasi wake na pia hata wakati wa Imam. Hata wale wanaoipinga hii ndoa pia wanalitumia sana hili neno.Maneno mengineyo yalinganayo na hayo pia hutumika kama vile tamatu' na istimuta'.Hilli analitumia neno hili katika maandishi yake yote na vile vile Shahrihni, lakini kila pale panapohusiana na ndoa ya kukatiza neno tamatu' na Istimuta' pia yanatumiwa.

Wale wanaolitumia neno muta'' wanadhania kuwa aina hii ya ndoa ni kwa ajili ya kusuhubiana. Watu wale watumiao ndoa ya kukatiza wanakuwa na mawazo mawili ya kuoa na kwa muda wa ndoa lazima ieleweke vyema.

Katika vitabu vya elimu ya Sharia za Sunni, kuna ubishano kuhusu hili jambo la ndoa ya kukatiza, iwapo aina hii ya ndoa ni ya muda uliodhaniwa wa kipindi kifupi. Bila shaka wote wanakubaliana kuwa ni aina moja na sawa kabisa, kwani isipokuwa Wahanafii, ambao wanasema kuwa iwapo neno tamatu' linatumika wakati wa kusoma ndoa basi hapo ndipo patakuwa sawa na aina hii ya ndoa ya kukatiza. Hata hivyo, somo hilo sio la muhimu kwao Sunni kwani ndoa iliyo haramu kwao ni ile iliyokatazwa na ambayo ni hii ya kukatiza.

Ilikuwa na picha iliyo wazi mbele yetu kuhusu neno hili la muta' (enye faida), basi inatubidi sisi hapa chini tuzungumzie maelezo kutoka kwa Madhehebu ya Shia na Sunni.

Sheikh Tusi katika kitabu chake Majma' ul Bayan, ambayo ni maelezo juu ya Qurani, anasema yafuatayo juu ya aya hii ya Qurani."Na wale wanaofaidika nao.." (4 :24) kwamba kufaidika na 'inamaanisha kuwaridhisha na matamanio na furaha ya mtu.Maana hii pia inaelezwa na Hassan Mujahid Ibn Zaid na Sa'di.Kwa hiyo maana ya aya hiyo ni kwamba kwa kuwa unafaidika kutoka kwao basi "uwape mahari yao kama mlivyopatana."

Imam Fakhru Razi katika maelezo yake juu ya aya hii anasema: "Kustareheka (Istimuta') maana yake ni kufaidika kutoka kwao. Kwa mathalani, inasemekana fulani bin fulani amefaidika kutokana na jitihada za mwanamke au fulani bin fulani amefariki akiwa yu bado kijana na hakuufaidia ujana wake. Allah, aliye mkuu wa kila kitu asema, "kwa hiyo wewe umestareheka (umefaidika) hisa yako," yaani wewe umefaidika bahati yako na utajiri katika dunia hii. Wewe umenufaika na wenzako wa dunia."

Ndoa isiyo ya kudumu inayo masharti manne ambayo kwa kutimzwa kwake ndiko kunako halalishwa:-sigha yake ambayo ni lazima isomwe; masharti yatimizwe kwa lazima na pande zote mbili zinazohusika; muda wa kudumu hii ndoa iidhinishwe na kuthibitishwa; na mahari yakubaliwe, lazima iwe kwanza.

Kanuni zake :

Ndoa ya muta' inategemea mkataba, kwa hiyo makubaliano na uhakikisho ndivyo vitu vinavyohitajiwa sana.Uhakikisho hapa, kama ilivyo katika ndoa ya kudumu ni lazima itolewe na mwanamke. Mtunzi wa al-Mitajir anadai kuwa wote wawili:mwanamke na mwanamme ni lazima waukubali huo mkataba kwa hiari yao. Katika hali hii,mkataba wa ndoa ya aina hii basi itakamilika kati ya kanuni hizi:"Mimi naolewa na wewe;" Mimi ni mke wako wa muda......;" mimi nadaiwa na wewe (mimi ni wako nilivyo)."

Sayyid Murtaza anasema kuwa mkataba wa ndoa ya kukatiza inawezekana kukubalika baada ya kutamka neno ambalo linaweza ndoa hii kuwa ya kihalali, lakini hii haithibitishwi! Mtungaji wa as-Mis'alik anasema: "Mimi napendelea kuwa kanuni au matamshi yote matatu yasomwe." Kwa hivyo inaonekana kuwa hao watu wanakubaliana kwamba ndoa ya kukatiza haiwezi kukubalika iwapo mtu yeyote atatumia maneno ya kuwa nayo, kodisha, azima au mchango."

Kwa kukubali kwa mwanamme ni lazima atamke hayo maneno yanawezekana, "Mimi nakubali ndoa na faida zake. "Na iwapo mwanamme atasema,"Mimi nakubali na nimeridhika;" au maneno yale yaelezayo hayo, basi mkataba utakuwa sahihi.

Siyo lazima kuwa uhakikisho utangulie makubaliano kwani mkataba unahusiana na makubaliano kwanza ndipo kuhakikisha kinafuata.Lakini itakuwa ni sawa iwapo itatokea hivyo wote wanakubaliana nayo.Asema, "Iwapo mwanamme atasema,"Mimi nakuoa wewe na mwanamke akasema: "Mimi naolewa na wewe" basi ndoa hii itakuwa ni sahihi.

Kuhusiana na ndoa hii ya kukatiza na usomaji wake, Allamah Hilli, anasema kuwa ni lazima isomwe katika nyakati zilizopita lakini 'Ulamaa wengineo wanasema kuwa jambo la muhimu kwamba nia lazima iwe wazi inayoweza kueleweka kwa kweli, kuna maandishi mengi sana yanayoelezea aina hii ya ndoa na ambavyo inatubidi tuyajue hayo.

Kama vile inavyonakiliwa kutoka Imam Ja'afer - us- Sadiq a.s., ambapo Abu ibn Taghlub alipomwuliza Imam kuwa anapaswa amwambie nini mwanamke yule ambaye atakuwa naye katika faragha kwa muda mfupi,Imam alijibu: "Sema mimi nakupa wewe kwa muda (kadha wa kadha )kwa mujibu wa kitabu cha Mungu na mila na utamaduni wa Mtukufu Mtume s.a.w.w. bila ya urithi au kurithiwa kwa ajili ya siku kadha wa kadha na dirham kadha wa kadha."

Katika kunakiliwa kutoka ibn Yahya kwa kupitia kwa Hisham ibn Salim, ilisemwa "Mimi niliuliza kuwa: "Je ndoa ya kukatiza ni nini?" Je huo mkataba utatimizwa vipi?"Yeye alijibu:"Mimi nakuoa kwa muda wa siku fulani kwa kiasi cha Dirham kadha wa kadha. Katika kuongezea zaidi katika mapokeo ya maandishi na maelezo ya hapo awali, kuna mapokeo mengine manne kuhusu ndoa ya kukatiza, kama ilivyoelezwa katika kitabu cha al - Wasa'il.

Katika mkataba huu, ni lazima makubaliano na kuhakishiwa yafaywe kati ya mtu mwenye kuoa na mwenye kuolewa au kwa wakili wao au baba yao Kwa hiyo inawezekana kwa baba mzazi kusema, "Mimi namwoza binti (kwa fulani bin fulani ) kwa maamuzi na maelewano kwa mujibu wa amri yake mwenyewe." Iwapo mtu atajifanyia mambo tofauti na hayo kinyume na Sharia, basi mkataba huo utakuwa sio kamili, batil.

Kwa sababu ya ndoa tu ndivyo mwanamke anakuwa halali kwa mwanamme. Na hivyo hii imegawanyika katika sehemu mbili:"Yeye kudumu na ile ya muda au kipindi kifupi."Ndoa ya kudumu ni ile ambamo muda kati ya mke na mume haujulikani.Mke anayechukuliwa katika ndoa ya namna hii anaitwa 'wa kudumu' mkataba wa kipindi kifupi ni ile ambamo muda wa mke na mume unajulikana. Tuseme mwanamke anaolewa kwa muda wa saa moja au siku moja au mwezi mmoja au mwaka mmoja au ziada ya hapo. Masomo ya ndoa kama hii ya muda wa kukatiza inaitwa sigha na yenyewe inaitwa muta'

Sharia za kutimiza ndoa ya muta'

(Nambari zilizoandikwa katika vifungu ni nambari za Fatawa zilizotolewa na Ulamaa wa Madhehebu ya Shia Ithna Asheria na ambazo zimetolewa na Mujtahid Sayyid Ali Husseini Sistani, Najaf-i-Ashraf, Iraq.

(2430) Kufanya muta' (ndoa ya muda mfupi) pamoja na mwanamke ama kwa ajili ya kutaka raha ya kusuhubiana, au kwa sababu nyingine yoyote ile, basi ni sahihi.

(2431) Ni tahadhari ya faradhi kuwa mwanamme asikose kusuhubiana naye mwanamke aliyefanya naye muta' kwa kipindi cha miezi minne yaani inambidi isipite kipindi hicho bila kusuhubiana na mwanamke aliyefanya naye muta'.

(2432)Iwapo mwanamme aliyefanya muta' na mwanamke, ataweka shuruti kuwa mume wake huyo hatasuhubiana naye basi ndoa hiyo itakuwa ni sahihi na vile vile shuruti lake hilo pia linakubalika, kwa hivyo mume atafaidika kwa starehe zinginezo tu bila ya kusuhubiana naye. Hata hivyo iwapo atakubali kusuhubiana naye hapo baadaye,mwanamke anaweza kusuhubiana na bwana wake huyo, na sharti hili linatumika katika ndoa ya kudumu.

(2433)Mwanamke aliyeolewa kwa muta'hawi mustahiki wa kupewa gharama zake hata kama atashika mimba.

(2434))Mwanamke aliyeolewa kwa muta' hastahiki kulala na bwana wake, na wala hana urithi bwana wake na wala bwana wake pia hamrithi mke wake aliyeolewa kwa muta'. Hata hivyo iwapo mmoja wao anaweka sharti na kurithiana basi swala hilo ni ishkal, lakini hata hivyo lazima ichukuliwe tahadhari katika kuweka maanani na utekelezaji wake.

(2435) Iwapo mwanamke ambaye ameolewa kwa muta' alikuwa hajui kuwa yeye si mustahiki wa gharama wala kulala na bwana wake lakini ndoa yake itakuwa sahihi bado, na kutokujua huko yaani kubakia katika hali ya ujahili vile vile atakuwa na haki ya kudai chochote kwa bwana wake.

(2436)Iwapo mwanamke aliyeolewa kwa muta' atatoka nje ya nyumba bila ya ruhusa bwana wake na kwa vyovyote vile haki ya bwana wake itakuwa imevunjwa basi kutoka kwake nje ni haramu. Na iwapo haki ya bwana wake itakuwa imesalimika ichukuliwe tahadhari iliyosisitizwa kuwa mwanamke huyo asitoke nje ya nyumba bila ya ruhusa ya bwana wake.

(2437)Iwapo mwanamke atampa ruhusa mwanamme ya kuwa wakili wake katika kusoma nikah ya muta' pamoja na mwanamke huyo kwa kipindi fulani na kwa kiasi fulani cha mahari, na badala yake huyo mwanamme yaani wakili akasoma nikah ya kudumu pamoja na mwanamke huyo au anasoma nikah ya muta' pamoja na mwanamke huyo bila ya kubainisha wazi wazi kipindi cha muda au kiasi cha mahari, basi ndoa hiyo itakuwa batil.Lakini iwapo mwanamke ataridhia na kutoa ruhusa kwa mapatano hapo mbeleni basi ndoa hiyo itakuwa sahihi.

(2438)Ili kutaka kuwa mahram (yaani ambaye huwezi kumuoa na anakuwa ni jamaa wako wa karibu ), baba au babu mzaa baba wanaweza kumuingiza mtoto wao asiyebaleghe au msichana wao asiyebaleghe katika ndoa pamoja na mtu mwingine kwa kipindi kifupi, ili mradi haitatokezea ufisadi.Hata hivyo,iwapo wao watamuoza mvulana mdogo au msichana mdogo ambaye kwa vyovyote vile hawezi kupata starehe ya kusuhubiana katika kipindi hicho, basi katika sura hii usahihi wa ndoa kama hiyo ni ishkal.

(2439)Iwapo baba au babu mzaa baba wa mtoto asiyekuwapo, wakamuoza kwa mtu ili kutaka kuwa mahram, bila kujua iwapo mtoto yuko hai au amekufa, basi kusudi litapatikana iwapo katika kipindi katika ndoa, mtoto atakuwa na uwezo wa kusuhubiana.Iwapo hapo baadaye itakuja kujulikana kuwa mtoto huyo hakuwa hai wakati wa kusomwa ndoa hiyo basi itachukuliwa kuwa ni batil.Na wale wote ambao walikuwa ni mahram sasa watakuwa na-mahram.

(2440)Iwapo bwana atakuwa amempatia zawadi bibi wake aliyemuoa kwa muta' katika kipindi hicho, na atakapokuwa amemuachia na kama alikuwa amesuhubiana naye basi itabidi ampatie vitu vyote vile alivyokuwa ameahidi kumpa. Na lau kama alikuwa hajasuhubiana naye basi itambidi ampe nusu ya mahari yake, ingawaje achukue tahadhari iliyosisitizwa mno kuwa itambidi ampe mahari kamili.

(2441)Iwapo mwanamme ataingia katika muta' pamoja na mwanamke na mwanamke atakapokuwa katika kipindi cha Iddah kabla ya kuisha basi inaruhusiwa mwanamme kumuoa mwanamke huyo kwa ndoa ya kudumu au ndoa ya muta'.

Msomaji anashauriwa kusoma habari zaidi juu ya masharti hayo katika sura izungumziayo hukumu za ndoa.

Sehemu ya pili .

Leo wale wenye kuwa na mafikara ya Magharibi, baada ya uchunguzi na upekuzi wa historia na kwa kujionea maovu yaliyozagaa katika jamii za siku hizi, wamegundua na kuafikiana kuwa yale mafunzo ambayo wa-Mashariki wanayashikilia (eti maendeleo ya kuleta jamii nyuma ) na ambao wamezubaa, ndizo za kufuata na ambazo ndizo funguo za kukomesha maovu katika jamii za siku hizi na katika siku zijazo.

Jambo ambalo ni la maana la kulizungumzia hapa ni kuhusu hii ndoa ya muda -muta' ambayo itasaidia sana kuepusha balaa ya ndoa-na -talaqa za kila siku katika jamii zetu.Hali ya maisha inaonyesha na kutuambia kuwa binadamu anatenda mambo haraka vile wakati umwelekezavyo. Wanamafikara wa Magharibi na wana-Sharia wa Magharibi leo hii wanasema kuwa talaqa ni jambo ambalo lishughulikiwe haraka iwezekanavyo.Wao wanadhani kuwa talaqa haraka inatokana na ndoa iliyofungwa kwa urahisi na hivyo mtu anao uhuru wa kujiamulia vile aonavyo bora kwake bila ya kuzingatia ubora na heshima ya jamii, kwani kuoa na kuachana ni vitu viwili vilivyo pamoja. Na hivyo ikiwa harusi itakuwa na ugumu ndani yake basi hata talaqa pia itakuwa ni vigumu kutolewa. Lakini hata hivyo wao imewabidi kuamua na kuafikiana kuwa ndoa lazima iwe ni sawa na mkataba kama vile mikataba mingine yote. Na hivyo umuhimu kidogo pungufu upewe ule upande wa muda mrefu wa hisa ya mwanadamu.

Mtazamo huo unashabihiana sana na ule mkataba: Ndoa ya kukatiza ya muda uliokubaliwa kwani katika aina hii ya ndoa, siku zinakubaliwa na kiasi cha mahari kinaafikiwa na makubaliano pia yanaafikiwa.Katika utaratibu huu, mwanamme anayo haki ya kujichagulia mwanamke amfaaye na vivyo hivyo mwanamke anao uhuru na kwa hiari yake mwenyewe ya kumchagua bwana amtakaye mwenyewe kwa muda ule atako yeye/wao.Iwapo bwana na bibi wakipendana zaidi basi wanaweza kuurefusha muda wa mkataba wao.Iwapo patatokea matatizo, basi bwana anaweza kumrudishia siku zake mwanamke. Au iwapo mwanamke anaweza kumrudishia kiasi cha mahari ya siku zilizobakia na hapo akaachana nae. Vile vile katika ndoa ya kukatiza iwapo mtoto atazaliwa basi ni wa baba kama vile ilivyo katika ndoa ya muda mrefu. Lakini kama vile inavyopingana na ile ndoa ya muda mrefu (katika ndoa ya muda mrefu kuzaa mtoto ndiyo jambo la kwanza kutamaniwa na wazazi), ambavyo katika ndoa ya kukatiza haimaanishi kuzaa watoto bali kitu cha muhimu ni maana katika ndoa ya kukatiza ni kuepusha na kutokomesha umalaya katika jamii. Kwa hivyo, wale wasio na nia ya kuiendeleza hii ndoa au wale wasio na hakika nayo, basi ni lazima wafanye nia kutoka mwanzoni kuwa wao hawana lengo la kuzalisha watoto katika kipindi cha ndoa hii.

Kwa desturi, katika kila maendeleo na maumbile ya kila jamii,ndoa ni jambo la muhimu kabisa kwa sababu binadamu anajielekeza yeye mwenyewe kwa jambo la kuoa. Hii ni imani ya kila mtu na hata maumbile yake yanonyesha, kwani hata Mwenyezi Mungu (swt)alipoanza kuumba, alimuumba Adam na baadaye alimuumba Hawa kama mshiriki wake wa maisha. Anasema katika Qurani Tukufu:-

'Enyi watu mcheni Mola wenu ambaye amekuumbeni katika nafsi (asli) moja. Na akamuumba mkewe katika nafsi ile ile. Na akaeneza wanaume wengi na wanawake kutoka katika wawili hao......'(4:1)

Kwa kawaida mtu anapooa, yeye anakuwa na mabadiliko ya kiroho, kwani anatakasika, na kuanza maisha mapya. Kwa hiyo bwana na bibi wanaitwa pea au jozi. Kwa sababu binadamu wameumbwa kwa jozi, kwani kama kila jozi bila ya kuwa na nyenzie huwa haikukamilika. Ndivyo vivyo hivyo, Adam bila ya Hawa alikuwa hajakamilika na vile vile Hawa bila Adam alikuwa naye hajakamilika. Kwa hiyo mojawapo ya malengo ya ndoa ni kutafuta umbo kamili la binadamu kwa mtazamo wa kiroho kitakatifu.Anaelezea Allah swt katika Qurani:

'Na katika Ishara zake (za kuonyesha ihsani zake juu yenu) ni kuwa amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu ili mupate utulivu kwao, naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Bila shaka katika haya zimo Ishara kwa watu wanaofikiri.' (30:21 )

Hata Mtume Mtukufu s.a.w.w. amehimiza sana kuhusu ndoa hadi hapo aliposema wazi kuwa ndoa ni nusu ya dini. (Wasa'il vol 14 uk 5 seh:1 ). Imenakiliwa kuwa Mtume s.a.w.w. amesema:

"Mwenyezi Mungu aliye mkuu, amesema 'popote pale nitakapo kuongezea mambo mema ya duni hii na bora wa Waislamu, mimi nitawapa moyo wa kunyenyekea, ulimi utakaokuwa ukimkumbuka Allah swt, mwili imani ambao utakaokuwa unastahimili shida na taabu na yule mwenzie ambayo anayo imani ambayo alikuwa akiiomba kwa machozi ya masikitiko, amfanye mtu kuwa furaha na starehe .............."

(Wasa'il :vol. 14; 23; seh. :9).

Kwa mtizamo wa nidhamu, ndoa inaweza kutumika kama kampeni mojawapo ya kufuta umalaya na ile nidhamu isiyokubaliwa na jamii ambayo binadamu anapotaka kumaliza hamu yake ya uume au ya kike au nyege, basi inambidi kusuhubiana na mwenzake.Kwa kawaida tabia ya mwanadamu ya kujituliza nyege za kusuhubiana zinaweza kutulizwa tu kwa njia ya ndoa. Wakati ambapo wanyama wanakuwa na nyege za kusuhubiana kwa kufuatana na msimu tu na ndivyo kusema kuwa wanyama huwa hawana ile hamu ya kusuhubiana kila wakati watamanipo kusuhubiana, ila ni binadamu tu ambaye yuko tayari kabisa daima wakati wowote ule na mahali popote pale. Ile hamu ya kusuhubiana na msisimko huwa uko katika kila msimu na kila mahari.Basi iwapo hapatakuwapo na mwongozo au Sharia za Allah swt kati ya uhusiano wa mwanamme na ule wa mwanamke basi mwanadamu atakuwa ni mwovu zaidi hata kuliko wanyama kwa kufuatana na misisimko ya kutaka kusuhubiana na mwenzake.

Wakati uliopita, kila yule mwenye uwezo, alijenga kama ngome kwa ajili yake na humo aliweka wake wengi. Yeyote yule aliyekuwa hajiwezi kwa hamu ya kusuhubiana, basi alikwenda huo na kufanya umalaya. Katika nyakati za jahiliyyan katika Arabia na wakati wa ufalme wa Shah wa Iran, majumba kama hayo yalikuwa yamezagaa kila mahala. Siku hizi vyote vimeangamizwa huko Iran na Arabia.Ubaya na adhabu ya kutenda umalaya umerudiwa kila mara katika Qurani Tukufu adhabu kali imetolewa kwa kutenda uovu huo. Watu walianza kupinga na wale wenye imani hawakurudia kutenda hayo maovu tena. Mubadi katika maelezo yake ananakili mapokeo ya Hadith.Yeye anasema, "Abu Hureirah alisema kuwa Mtume s.a.w.w. amesema 'kwa watu wa aina tatu ambao Mungu atawasaidia......(miongoni mwao ni yule )mtu ambaye anaomba maghfirah kwa Mungu huku akitaka kuoa." Yeye pia amesema, "Popote pale nyie mumwonapo mtu mwenye tabia nzuri na ni mwenye imani, mwozeni mtoto wenu wa kike. Kwani, kwa kutofanya hivyo basi ufisadi utakuingilia."Mu'badi anasema,"Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema hayo na Shaf'i anathibitisha hayo, 'mtu ambaye anao uwezo wa kuoa na anataka kuoa na ni afadhali kuwa huyo mtu atafute mwanamke wa kumwoa na kwa kufanya hivyo ni afadhali kuwa huyo mtu atafute mwanamke wa kumwoa na kwa kufanya hivyo ni bora zaidi hata ya sala za usiku - nawafil. Hata hivyo hilo wimbi la tamaa na msisimko yanapotaka kumghalibu mtu basi yeye anaweza kutuliza kwa kufunga saumu. Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema, "vijana! Yeyote yule ambaye anaweza kujitunza mwenyewe, basi waoe kwani ndoa ni kinga ya macho yenu.Ndoa inamwepusha binadamu kwa kutenda matendo maovu, lakini iwapo mtu hana uwezo, basi afunge saumu, kwani saumu kwa mtu kama huyu haina madhara yoyote kwake. Lakini kwa mtu yule ambaye hana misisimko na tamaa za kila mara za kutenda maovu haya na hana mpango wa kuoa wakati huo, basi sala za usiku (nawafil) ni bora zaidi kwake yeye.Tabarasi katika maelezo yake ameleta zaidi ya Hadith ikiwemo ile iliyonakiliwa na Abu Hureirah kutoka kwa Mtume Mtukufu s.a.w.w.,"Iwapo mtu ana mtoto wa kiume basi ni lazima amtafutie mke na asipofanya hivyo na ambapo huyo mwana akatenda dhambi, basi wote wawili ni dhamana wa adhabu ya madhambi hayo."

Dunia ya siku hizi, kwa tahzibu na imani imezidi kurudia ile hali ya miaka ya ujinga. Kwa haraka sana inarudia hali ya kusonga nyuma, na hii sababu yake ni kuwa binadamu amefuata mkumbo unaopita bila hata ya kufikiria na wala kutojali hali bora ya maisha wa ustaarabu wao.Ile Ne'ema ya Mwenyezi Mungu ya kumpa binadamu fursa ya kutambua kipi ni kibaya na kipi ni kizuri imeshakwisha potea kabisa, kwani siku hizi mwanadamu hayuko tayari hata kuufuata utamaduni wao wala hathaminiki kuufuata tena. Mkumbo wa maisha haukuathiri maji na ardhi tu bali yamemfanya hata mwanadamu asiwe na akili za kufikiria, na kila hisa iongezekavyo ndivyo jamii pia huendelea kurudi nyuma vile vile na hata kupotoka.Katika nchi zile ambazo bado wanazingatia utamaduni na ustaarabu wao wa kale, hali hii ya upotofu ni mdogo kuliko ile ya nchi za mfumo wa Magharibi ambao hawana bahati ya kuyazingatia hayo. Kwani leo wao wanayoyazingatia ni ustaarabu wao wenyewe.Lakini sikitiko kubwa ni kwa wale vijana wenye akili timamu na fahamu timamu wanaoendelea na kuiga vioja viovu vya Magharibi.Wao wanachukulia ule uhusiano wa kiume na kike bila ya vizingiti ati ndiyo alama kubwa kabisa ya maendeleo ya jamii lakini hawatambui kuwa kufanya hivyo wao wanajidhihirisha wazi wazi uovu na ustaarabu wa jamii yao.

Katika nchi za Magharibi, maana halisi ya ndoa imetimuliwa mbali kutoka mizizi yake. Sharia ya kawaida imeiwakilisha ndoa na hii ni kwa sababu wa mkumbo wa maisha unaowafanya wapotezwe na zile kanuni zao za dini na mila hadi mtu kufikia hatua ya kutoamini kuwa kuna Mungu, au kuna siku ya Qiyama tu' Mapenzi ndiyo malipo yake kwani wao wanavutiwa na tamaa zao tu. Enzi za zamani pia watu walikuwa wakifanya aina hii ya mapenzi lakini malipo yao yalikuwa ni mapenzi ya Mungu kwani mapenzi ya mtu na Mungu ni thabiti wakati mapenzi kati ya mwanamme na mwanamke ni ya kulaghai tu. Iwapo tunawaona waumini wakituambia kuwa dunia hii siyo ya kudumu bali ni uwanja wa majaribio kwa hivyo wao wanajaribu kujijenga na kujitayarisha kuishi katika dunia itakayo dumu milele kwa kujiepusha na kila matakwa (yasiyo bora ) ya mioyo yao na kufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu swt, kama alivyosema Allah swt katika Qurani Tukufu.

"......Ambao uwapatapo msiba husema: "Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake yeye tutarejea (atatupa jazaa yake)." (2:156)

Katika kila desturi na utamaduni na ustaarabu, uhusiano kati ya mwanamke na mwanamme hasa ni kwa kupitia ndoa tu ambayo inatimizwa kwa Sharia na kanuni za kidini au njia ile iliyo halali. Katika utamaduni zinginezo,sababu kuu ya kuoa ni kustawisha familia. Kama ilivyo (familia ) nyumba ni kiini cha shughuli na mafunzo yote ya jamii ambapo mafunzo wayapatayo memba wa familia na watoto ili siku zijazo warithi wazazi wao na kudumisha jina lao na sifa zao na za jamii nzima kwa ujumla - na hii ndiyo kiini cha ndoa. Kila mtu anataka abakie na ukumbusho wake baada ya kifo chake. Iwapo kila mtu na familia wakitambua wajibu wao na shughuli atakazo kuzifanyia familia yake kwa upendo na kwa kushirikiana vyema na wenzake, basi kutakuwa na usalama na amani na bongo tulivu miongoni mwao.

Ikiwa itatokea utaratibu na mazingara kama haya, basi wanawake wanafunza mafunzo bora kabisa watoto wao na pia wanatunza nyumba zao vyema na wanaume wao wanashughulikia mambo mengineyo ya jamii hii, pia ni lengo mojawapo la ndoa kwani jamii au familia inaumbika kwa mambo haya ya usalama na uwema wa jamii unatokana na upole na usalama wa akili, ya kila familia, na hapo ndipo nchi imara inajengeka kutokana na jamii bora kama hizi. kwa hiyo kutuliza akili na usalama wa mwili wa jamii ni usalama na ubora wa familia. Papo hapo ndipo panapotokea mategemeo ya maendeleo ya nchi na hii ndiyo sababu kuu kati ya chi na jamii ambayo yanatokana na mambo hayo hayo niliyoyalezea hapo awali.

Sehemu ya tatu.

Bila shaka tumesoma sehemu ya kwanza na ile ya pili katika mfululizo wa aina hii ya ndoa ya kukatiza au muta', kwa hivyo hadi hapa tumeona na kushuhudia namna vile wana wa Magharibi walivyopoteza ile imani ya ndoa kihalali na vivyo ndivyo walivyokosa ile imani na ubora wa familia. Kwa hakika hali hii ni mbaya na hatari kabisa. Katika hali hii pia kuna matumizi mabaya ya maisha ya mwanadamu kuhusu uhuru wa mwanamke kuwa sawa na mwanamme. Wote wanawake na wanaume wanasema ni lazima wanawake wawe sawa katika jamii. Kwa hakika hakuna tofauti yoyote kati yao kwani wote ni sawa kuanzia pale walipozaliwa, lakini wao hawakuelewa maana halisi ya usawa huu. Wao wanadhani kuwa mwanamke pia awe na kazi katika jamii kama vile alivyo mwanamme.Hiki ndicho chanzo cha kumfanya mwanamke kutoa mguu wake nyumbani na kwenda kufanya kazi pamoja na wanaume katika maofisi na wala sio nyumbani tena na ambavyo hawataki tena kubakia nyumbani kufanya kazi za nyumbani za kulea na kuwaelimisha watoto wao kwani ikiwa mwanamke atabakia nyumbani akitunza nyumba yake na akabakia kuwa mke mtiifu na mpole, basi heshima yake itakuwa ni dumi ya ile ya mwanamme ambavyo nikinyume cha Udemokrasia. Mawazo haya ni yale kutoka kwa miaka ya viwanda ambapo wanahitaji nguvu za wanawake (kuvutia ) kusukuma biashara yao mbele ya makampuni au viwanda. Upande mwingine wao wanasema kuwa mwanamke anayo haki sawa na ya mwanamme na pengine husema kuwa wanawake wako huru kwa hivyo mwanamke lazima aache nyumba yake na atoke nje kwenda kufanya kazi pamoja na wanaume kwani mambo haya mawili ni lazima katika haki ya upande wao.Kwa hivyo kila usikiapo 'Usawa na uhuru wa wanawake' basi uelewe kuwa wanaviwanda wanawatumikisha wanawake katika kazi zao za viwandani na sababu nyingine ni kwamba eti familia yao haijitoshelezi kimaslahi na hivyo ndivyo wanawake hawana budi kwenda kufanya kazi nje ya nyumba zao.

Hoja yangu kubwa ni kwamba wanawake wa dunia hii wasijaribu kuwaiga wale wanawake wa Magharibi kwa sababu nchi zao ni za viwanda na ili kuwa sawa wote inawabidi wanawake pia wajilazimishe kufanya kazi katika sekta hii ya uchumi na hivyo ndivyo adhaniavyo mwanamke wa Magharibi. Hapo ndipo migongano ya kila aina ya kupangiwa kazi huwa zinatokea. Huu ni ukweli kuwa hali hii ya namba hii ipo bado ingali ikiendelea katika nchi za Ukomunisti mwanamke kwanza kabisa inambidi achukue koleo nzito na aanze kutengeneza na kujenga barabara kwa mtazamo wa uchumi na wa viwanda, na hapo ndipo ajionapo yu sawa na wanaume.Upande mwingine,iwapo mwanamke inambidi kwenda kufanya kazi nje ya nyumba yake, basi ni lazima awaache watoto wake chini ya walezi wengine au chini ya ulezi wa serikali. Hapa utaratibu na shughuli za nyumbani zinagawanyika kati ya mwanamke na mwanamme na hapa ndiyo maana halisi ya nyumba inapofifia. Nyongeza ya hapo, wakati mwanamme na mwanamke wanapokuwa sawa katika kila sehemu, basi ule ubora na udhaifu wa mwanamme unaanza kuujongelea ule wa mwanamke na mwanamke mienendo yake inazidi kukaribia ile ya kiume. Hapo ndipo tutasema kuwa mwanamme si mwanamme halisi tena na mwanamke pia si mwanamke halisi tena. Itakuwa ni bora iwapo nitawadokezea ile Hadith ya Mtume Mtukufu s.a.w.w.:

"Mwenyezi Mungu atalaani kabila nne za watu na Malaika wataitikia 'aamin.' Moja ni yule mtu mwanamme ambaye anajigeuza au kujilinganisha au anafanya au kujilinganisha na ile mienendo ya mwanamke wakati ambapo Mungu amemuumba yu mwanamme na vile vile yule mwanamke ambaye anamuigiza mwanamme wakati ambapo yeye ameumbwa na Mungu kuwa mwanamke."

Mwenyezi Mungu alimuumba Adam kwanza na baadaye Hawa. Wanasema kuwa kabla ya kuumbwa Hawa, Adam alikuwa hajakamilika kama mwanamme na hapo baada ya kuumbwa kwa Hawa basi Adam alikamilika kuwa mwanamme kwa kuota ndevu.Kwa hiyo maana halisi ya maneno hayo ni kwamba mwanamme bila ya mwanamke hawezi kukamilika na vile vile mwanamke bila ya mwanamme pia hajakamilika na hivyo ndivyo tuseme kuwa mwanamme ni mwanamme tu na mwanamke ni mwanamke tu.Iwapo mmoja wapo atakosa basi hakutakuwapo na ukamili wowote kati yao kimaumbile. Jambo kuu la kuzingatia na kulitazama ni la uchi-uume na ukike.Na hapa ndipo Mungu anapomkumbusha mwanadamu kuwa, aheshimu maumbile yake kama ni mwanamme basi abakie kuwa ni mwanamme na kama ni mwanamke abakie kuwa ni mwanamke. Lakini wao wamejidanganya na kujigeuza kwao kwa vile walivyoumbwa.

Kwa hivyo huu usawa sio ule wana wa Magharibi wachukuliavyo bali ni vile kama desturi, mila na utamaduni za dunia zielezavyo. Hapa inamaanisha kuwa pale popote palipo, mwanamme anazo shughuli zake za kuzifanya na vile vile mwanamke pia anazo shughuli zake,hivyo kwa vyovyote vile shughuli zitakapoongezeka ndivyo mwanamme ataendelea kukomaza ile hadhi yake ya kiume na ambazo ni kwamba mwanamke ataendelea kuwalea na kuwafunza watoto wake kila jema, kwani kwa kadri ya uwezo wake na kutunza familia yake vyema kwani hapo ndipo kutampa moyo mumewe kufanya kazi zaidi kwa nidhamu katika jamii.

Je kuna heshima gani kati ya mwanamke na mwanamme iwapo wote watakuwa 'sawa?'Mtu mashuhuri wa India anasema kuwa:"Ile heshima ya mwanamke kuwa sawa na mwanamme ni sawa na kusema kuwa Muasia kujigeuza kizungu."(yaani Muasia anajisahau na kujigeuza kuwa yuko anaishi kizungu ambavyo yeye siyo Mzungu bali ni Muasia kwa asili yake).

Katika Sharia za kiungwana za Japan, shughuli za mwanamke nyumbani ni sawa na kazi za mwanamme katika jamii na nusu ya mapato yote ya mwanamme ni haki ya mwanamke.Kwa hivyo, wakati wa kuachana, nusu ya mali yote ile aliyoichuma mwanamme baada ya ndoa na imekusanywa nyumbani, basi hiyo sehemu nusu ni ya mwanamke. Wao wanasema kuwa ule ushindi uliopatikana katika vita vya pili vya dunia, vilitokana na utunzi na malezi na mafunzo mema kabisa yaliyokuwa yakitolewa na mama zao na ambavyo kusema kuwa wafunzi bora wa watu ni mama.

Katika kila familia inayofuata mila na utamaduni, wazazi wana nguvu na sauti juu ya watoto wao.Nao watoto pia wanazo heshima, mapendo na uhusiano bora kabisa na wazazi wao. Hapa itabidi kusema kuwa yule mtu ambaye hataweza kuelewa huruma na mapenzi ya wazazi, basi hata baraka za Mwenyezi Mungu atazikosa. Inasemekana kuwa, "kwa mujibu wa Sharia za Manu, Mwalimu ni bora kuliko watu kumi wenye heshima.Baba mzazi ni sawa na walimu kumi kama hao lakini mama mzazi ni sawa na baba elfu moja kwa heshima na kama mwalimu."

Annealed kusema "Hata siku hizi, mama wa Ki-Hindu wana unyenyekevu na uwezo mkubwa wa kusema bado kuliko mama wazazi wengineo hata kama wakiwafananisha kiasi gani.Mama huwa anawahukumu wote hata kama wamekuwa wakubwa wala sio watoto tu kwani wanao uwezo zaidi wa kuhukumu nyumbani.Kwa maoni yangu mimi, wale watoto waliokulia katika desturi za Kizungu tu ndio wasio na adabu na heshima kwa wazazi kwa wazazi wao."

Ni heri iwapo tuanze kumalizia maneno yetu kwa kusema kuwa iwapo wanasheria katika nchi zisizo za Kiislamu wakijaribu kuingiza aina hii ya ndoa katika (ndoa ya kukatiza) Sharia zao, basi lazima uovu uliozagaa katika jamii zetu zitafutwa kwani hadi sasa wao wanazo zile Sharia zihusuzo ile ndoa ya muda mrefu (permanent marriage). Hii haimaanishi kuwa ndoa ya kukatiza iwakilishe ndoa ya kudumu, na popote pale mtu atakapo mpa mwenzake talaqa basi bila shaka Sharia wanazo tayari zilizotungwa na ambavyo ni imani kubwa. Lakini hili jambo la kuliingiza la ndoa ya kukatiza ni gumu sana kwani iwapo itakubaliwa basi lazima pia itolewe utaratibu halali wa kulitimiza.Kwa wakati huu, mimi sidhani iwapo aina hii ya ndoa ya kukatiza itawezekana au la.Hata hivyo mambo yafuatayo yanaweza kutupatia mwongozo wa kuyafafanua vyema.

Je nini maana halisi ya 'ndoa?' Je nini ukweli wa ndoa? Je ni nini maadhimio au mategemeo yake? Baada ya kuyajibu kwa ufasaha tu ndipo mtu anaweza kuelezea vyema ndoa ya kukatiza na nini mategemeo ya ndoa ya kukatiza na kuna tofauti zipi kati ya ndoa ya kukatizwa na ile ya muda mrefu.Kwa ufupi, kuandika haya kwa mifululizo sio kuthibitisha au kukanusha imani ilivyoeleweka kutoka kwa wanavyuoni na mtu asitende kinyume na maelezo yao. Kwani inavyojieleza wazi wazi msimamo wake wa ndoa hii ya kukatiza. Kwa mujibu wa wafuasi wa Madhehebu ya Shia Ithna-Asheria, ndoa ya kukatiza inaruhusiwa (halali) na ambavyo kwa mujibu wa Madhehebu ya Sunni, hii ndoa imeharamishwa. Mimi nimejaribu kuelezea vyote. Mimi azma yangu ilikuwa ni kuelezea wazi wazi ile ndoa ya kukatiza na msomaji atakuwa ameona kuwa hii ndoa inayo misingi mingi bora, sababu ya imani ambazo madhehebu yote mawili yanavyoelezea wazi wazi.

MWISHO WA MUTA'