rudi maktaba >Fiqh >Yaliyomo >

24. TALAKA.

Kuna baadhi ya mizozo na sura katika maisha ya ndoa ambazo zinashindikana kutatuliwa katika misingi mbalimbali, na hali ya maisha ya kifamilia inakuwa haivumiliki. Katika hali kama hizo, kunakuwa na njia mbili tu za kufanya ambazo zinakuwa zimebakia:

1
.Kumwachia bibi na bwana katika hali hiyo hiyo walivyo, ambavyo kwa mujibu wa aya ya Qurani tukufu ni adhabu ya motoni

2
.Kuwaachanisha na kuwatenganisha na mfungamano wa ndoa (talaqa), ili kwamba kila mmoja wao atafute mwenzake atakayeweza kupatana naye ili maisha yao yawe mema na mazuri.

Akili zetu zinakubaliana na utaratibu wa na. 2 na ndivyo vivyo hivyo Uislamu pia unaunga mkono.

Ukristo unapendelea hali ya kwanza yaani kuwalazimisha bibi na bwana waishi pamoja hata kama watachukiana kiasi gani,na hoja hii inatokana na maneno ya Yesu:-

Biblia inatuambia katika Mathayo, 5 : 31 - 32.

"...Kila mtu amwachaye mkewe,isipokuwa kwa habari ya uasherati,amfanya kuwa mzinzi; ...

Tujiulize sisi kama binadamu iwapo zinaa peke yake ndiyo inayoharibu maisha ya ndoa? Je hasira kali au kutafuna haki ya mwenzako au ndizo pia zinazoleta mfarakano katika maisha ya ndoa, Je kudharau kumjali mke kwa kumpa haki zake, uaminifu, kumgeuka mke au kutojali havitoshelezi kufanya nyumba yako ikawa Jahannam?

Ni lazima hapa sisi tujaribu kujua busara ya talaqa ilivyo katika maswala mengi yaliy onyeti, kama ilivyoruhusiwa katika Islam. Leo hata wale watu ambao hawakubaliani na talaqa wanaiambia Serikali katika bunge ipitishe Sharia na muswada kuhusu talaqa, katika Sharia za nchi, mambo ambayo mara nyingi yanapingwa na Kanisa na dini nyinginezo kwa sababu dini hizo hazina mwanya zaidi katika maswala haya.

Dini ya Hindu haitambui talaqa; nao pia katika nchi ya India wametengeneza Sharia na muswada katika Sharia zao za nchi.

Waangilikana nao pia wanapinga talaqa; nao kwa kupitia Sharia ya bunge (ambamo Askofu ndio mhusika mkuu -member) Wamekubali kutenganishwa na mahakama yaani talaqa. jambo la kuvutia hapa ni kwamba mkuu wa nchi, mtawala ni mkuu wa Kanisa la Kiangilikana; ambaye anapinga talaqa na papo hapo akiwa katika wadhifa wake wa mkuu wa nchi, anaidhinisha Sharia ya bunge ikiruhusu talaqa.

Je kwa nini Mfalme Edward VIII alimuoa mwanamke aliyepewa talaqa, na papo hapo maelfu kwa maelfu ya raia wake walikuwa wakipewa talaqa chini ya mamlaka yake? Je inamaanisha kuwa dini ya Kikristo inasheria mbili ? Sharia zake; moja kwa ajili ya watu wakubwa na Sharia nyingine kwa ajili ya watu wa kawaida?

Kanisa la Roman Katholiki linapinga kabisa talaqa. Lakini wamelazimishwa kwa ukweli sugu wa maisha kiasi kwamba wametafuta njia ya kuvunja ndoa bila ya kuita talaqa. Iwapo mtu anasubira ya Job (Ayub) na fedha na mapesa ya Qarun anaweza kupata baada ya kuomba amri kutoka Vatikan, kuwa ndoa yake ilikuwa imekwisha na batil kuanzia mwanzoni.

Mastaajabisho au siyo? Jambo lililogumu hapa ni kwamba atakayepata ni yule tu ambaye yuko katika tabaka la matajiri."Katika miaka ya karibuni, Papa Paulo wa VI ameonyesha utaratibu .....kuwa inaweza kutatua hata ya kesi ya miaka 20. Pamoja na Vatikani za kuweka malipo, gharama za Rot zimebakia juu sana, mara nyingine katika maelfu ya dola na ikiwafanyia wale wenye utajiri."

Iwapo ndoa hiyo itasemwa kuwa hiyo ndoa tokea mwanzoni ilikuwa ni batil sasa watoto waliozaliwa katika kipindi hicho watakuwa na nafasi gani katika Sharia zao? Je tutasema watoto hao ni wana haramu?

Italia chini ya shinikizo la Vatikan imejaribu kuzuia Sharia ya uhalalishaji wa talaqa. Lakini kule Italia pia Sharia imeshapitishwa yaani muswada umepitishwa na imeshakuwa Sharia. Mara pale Sharia ilipopitishwa ya talaqa maelfu ya watu waliomba wapatiwe talaqa, wengi ambao walikuwa wameachana na wake zao miaka 20 au 30 iliyopita.

Ndio tunaona binadamu anavyoweza kuteseka kwa kanuni na Sharia kama hizo.Sio kutaabika na kuteseka tu kunakotokea bali kunawashawishi na kuwasukuma watu kujiingiza katika madhambi (zinaa).Je inawezekana bibi na bwana walioachana kienyeji miaka 20 au 30 iliyopita wakabaki bado wako safi? Bila shaka kila mmoja wao yaani bibi na bwana watakuwa wametaka kutimiza haja zao za kijinsia pamoja na watu wa nje ambao hawakuolewa nao na wengineo humo watakuwa wamewazaa watoto wengi na bila shaka katika kipindi cha miaka 20 - 30 wengine wamekuwa mababu wa wajukuu na watoto wanaharamu ambao amezaa mtoto na mjukuu nje ya ndoa.

Kwa hiyo tukiangalia maswala kama hayo tunaona kweli kuwa Uislamu umetoa mwongozo ulio sahihi na mambo ambayo yanakubalika na akili yetu ili kufanya maisha yetu yakawa mazuri na fanaka.

Kwa kuwa kitabu hiki kinazungumzia mambo ya ndoa hivyo maudhui ya talaqa sitayazungumzia zaidi lakini nimeonelea nigusie kidogo ili tupate kidogo fununu juu ya desturi na Sharia za Kiislamu ni kwa ajili yetu na ubora wetu na kwa ajili ya mustakbali, hivyo msomaji iwapo atapenda kufanya utafiti juu ya swala la talaqa anaweza kujiendeleza au Insha Allah nikifanikiwa nitajaribu kutayarisha kitabu juu ya talaqa na mirathi.

T A M A T I .