rudi maktaba >Fiqh >Yaliyomo >

14. KUDHIBITI MAMBO YA NYUMBANI.

Kwanza kabisa ni muhimu kuwa mwanamke aweze kuweka maanani mapato ya bwana wake kuliko dunia nzima.

Ndipo hapo itambidi aweze kuweka malengo ya matumizi katika misingi hiyo. Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema: "Allah swt atamjalia nguo sabini elfu huko Jannah yule mke ambaye atakuwa ameridhika kwa kiasi cha mapato mume wake anachokipata kwa uwezo wake."

Kwa wale wanaokwenda kinyume na busara hii,Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema: -

"Hakuna mwanamke ambaye anamuomba mume wake zaidi ya uwezo wake, na asiyetosheka kwa kile anachopata cha kuishi - kiwe kidogo au zaidi - wala kutosheka na neema anayojaliwa na Allah swt, isipokuwa atakuwa ni miongoni mwa wale ambao matendo yao mema hayakubaliwi, na madhambi yao hayatasamehewa na Allah swt atakuwa daima akiwachukia hadi hapo hao wanawake watakapotubu."

Ni ukweli kwamba matatizo ya kinyumbani yanamchukiza mtu sana kiasi cha kwamba wakati fulani hata subira yake inashindikana, ni kwa sababu hii kuwa Mtume Mtukufu s.a.w.w.ameahidi baraka kwa watu wenye maswala kama hayo, amesema: -

Iwapo mwanamke atatokwa na machozi wakati wa kupika kwa sababu ya moshi, Allah swt atamwandikia thawabu za shahidi (waliouawa katika njia ya Allah swt) ambao macho yao yanatokwa na machozi kwa hofu ya Allah swt.

Na iwapo mwanamke huyo anaye msaidizi katika mambo ya nyumbani na hivyo anapata fursa kidogo basi asiupoteze huo wakati; badala yake, muda huo utumike katika shughuli zingine zenye manufaa katika mipaka yake ya nyumbani.Mtume Mtukufu s.a.w.w.amesema:"Kazi nzuri kabisa ya mwanamke ni ufumaji; kwa sababu kwa kila uzi mmoja anasamehewa dhambi moja na kupewa thawabu moja."

Mwanamke amevutiwa katika utunzaji wa nyumba bora katika maneno yafuatayo:-

"Mwanamke yeyote katika nyumba ya mme wake, anapohamisha kitu kutoka nafasi moja hadi nafasi ya pili kwa nia njema, Allah swt anamwangalia (kwa baraka), na yeyote yule anayetazamwa na Allah swt kwa rehema, basi kamwe haadhibiwi."

Kwa hivyo tunaona katika maswala ya nyumbani mwanamke inambidi aangalie mambo yote mazuri kwa nia njema ya kuendeleza nyumba ya bwana wake na anayekuwa na nia mbaya ya kusema anachukua vitu nje ya nyumba yake bila ya bwana wake kujua kwa nia mbaya basi huyo naye atapata adhabu za Allah swt.