rudi maktaba >Fiqh >Yaliyomo >

13. UTIIFU KWA MISINGI YA MAPENZI.

Itatubidi lazima tukumbuke sheria iliyo ya uchokozi na udhalimu, kamwe hawezi kuwa sahihi. Hivyo misingi ya mamlaka ya bwana yamewekwa kwa mapenzi na wala sio vitisho na uonevu. Allah swt anatuambia katika Qurani Tukufu sura Ar-Rum 30:21

"..... naye Amejaalia mapenzi na huruma baina yenu..."

Katika Aya hii tunaona maneno mawili mapenzi na huruma,yametumika katika mapenzi ya unyumba.Kwa kawaida mwanamke tukiongelea ukweli anampenda bwana wake zaidi mno. Yeye yuko tayari, kujitolea nafsi ,mwili wake kwa ajili ya mume wake. Hivyo mapenzi ndivyo yanavyotelezea hali hiyo.

Kwa upande mwingine mapenzi ya mwanamme kwa mke wake yana sura tofauti kimaumbile - hapo hakuna swala la kujitolea. Na hivyo ndivyo huruma inavyotumika.

Vyovyote vile mapenzi, utiifu na huruma ndio mambo ya kutimiza katika maisha ya mwanadamu: Kudhatiti mambo ya nyumbani na uzazi.