rudi maktaba >Fiqh >Yaliyomo >

12. UBORA WA MWANAMME.

Kama tulivyoona mapema wazazi ni mabwana wa watoto.Hadi hapo vijana wanaume wanapohusika sheria hii inaendelea.Ama wasichana,baada ya kuolewa ubwana wa wazazi wao unakwisha na wao wanaingia chini ya hukumu za mabwana wao.

Mwanamke mmoja alimwuliza Mtume s.a.w.w.:"Ewe Mtume wa Allah swt, je ni nani anayo haki zaidi juu ya mwanamme?"Mtume s.a.w.w.alimjibu: "Wazazi wake."Baadaye alimuuliza:"Je nani mwenye haki zaidi juu ya mwanamke?" Mtume s.a.w.w. alimjibu: "Bwana wake."

Wakati mmoja walimwuliza Mtume s.a.w.w.:"Sisi tunawaona baadhi ya watu wakiwasujudia baadhi ya watu wao." Mtume s.a.w.w.aliwajibu:"Iwapo mimi ningekuwa na uwezo wa kumruhusu mtu yeyote kumsujudia mtu mwingine basi ningemwamurisha mwanamke amsujudie bwana wake."

Imam Jaafer Sadique a.s. amesema: "Allah swt alimtumia ujumbe Mtume s.a.w.w., mwambie Fatima a.s. daima amtii Ali a.s. kwa sababu iwapo Ali a.s. hataridhishwa, basi mimi sitaridhishwa."

Na kwa sababu hii ndiyo maana Mtume s.a.w.w.alimwambia Fatima a.s. :-

"Ewe Fatima, iwapo mwanamke atafanya ibada ya Allah swt kwa miaka sabini lakini atakufa katika hali ya kutomtii bwana wake (na bwana wake atakuwa hakufurahishwa naye ), basi mwanamke huyo atakuwa miongoni mwa wakazi wa Jahannam."