rudi maktaba >Fiqh >Yaliyomo >

11. NAFASI YA MWANAMKE NI NYUMBANI

Vyovyote vile,mwanamme amefanywa kuwa mlinzi wa mwanamke, kwa sababu ya mwili wake wenye nguvu na akili na busara yake na kwa sababu amewajibishwa kumstiri na kumshughulikia mke wake. Hivyo kwa sababu hizi na zinginezo mwanamke amelazimishwa kumtii bwana wake.

Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema:"Wanawake waliotukuzwa kuliko wote mbele ya Allah swt ni wale ambao ni watiifu kwa mabwana zao na ambao wanabakia katika mipaka ya nyumba zao."

Iwapo wanawake watabakia katika mipaka yao kimaumbile na kwa kuwatii mabwana zao na kutimiza wajibu waliowekewa na Allah swt, watatimiza wajibu wao na kwa hakika ndio wale wanaostahili kuitwa wanawake wanaotukuzwa kuliko wengine.

Tunaelewa kuwa leo taasisi yoyote au kikundi chochote kiwe cha siasa au hata michezo inahitaji kiongozi. Hivyo ni jambo la kustaajabisha mno kuona kwa wale wanaotetea usawa wa jinsia (yaani usawa wa mwanamke na mwanamme) wanapokanusha kuwa mwanamme si kiongozi katika unyumba.Je nyumba inakwenda kiholela au kuna mipango inayopangwa na kutekelezwa kwa ushirikiano wa wawili hivyo kuwapo kwa kiongozi mwenye maamuzi ya mwisho ni muhimu sana hata kama itakuwa ni maswala ya nyumbani.

Wataalamu wa mambo ya kale wanasema:"Katika zama za kale mwanamke alikuwa huru alikwenda alikotaka, alifanya kile alichokitaka yaani kwa kifupi alikuwa ni bwana mwenyewe. Lakini katika zama hizo za kale alikuwa hana heshima yoyote wala utukuzo wowote, kwa sababu kulikuwa hakuna familia kila mmoja alikuwa akiishi peke yake.

Lakini familia zilipoanza kutokezea,hali ilianza kubadilika kutokezea mizunguko ya familia, mwanamke alipoteza uhuru wake na ilimbidi akubali kanuni na vishindikizo vingine vya kifamilia, lakini papo hapo alijipatia heshima na utukuzo wa hali ya juu mambo ambayo alikuwa hakuyafikiria hapo kabla.

Katika nchi za Magharibi ushirikishwaji wa mwanamke umewafanya wanawake wengi sana kuacha kuolewa, kwa kifupi mwanamke mfanyakazi wa nchi za Magharibi amepoteza ile hali na matamanio ambayo mwanamke kimaumbile wa umri wao anatakiwa awe nayo. Kwa sasa wao si wanaume wala wanawake kwani wao ni kikundi cha katikati baina ya mwanamme (yaani si mwanamume wala si mwanamke ). Wao si wanaume kwa sababu wanatofautina kimaumbile na wala wao sio wanawake kwa sababu hisia zao, mawazo yao na shughuli zao zinatofautiana na zile za mwanamke.

Mtu hawezi kupanda jahazi mbili kwa wakati mmoja hivyo lau yeye atajiingiza katika mambo ya kuchuma mapesa basi watoto wake watanyimwa haki yao ya mapenzi ya utunzwaji wa mama.