rudi maktaba >Fiqh >Yaliyomo >

9. MIPAKA YA KIISLAMU.

Hadi sasa hivi sisi tumekuwa tukiangalia mipaka ya kikudura ya wajibu wa mwanamme na mwanamke (Yaani wajibu wa bibi na bwana).Sasa hebu tuangalie vile Uislamu unavyoweza kutuongoza katika mipaka ya Din.

Kama iliyoelezwa hapo mwanzoni kuwa Uislamu unataka kumwelimisha kijana wa kiumme ili anapokuwa awe mtu wa matendo: na kuwaelimisha wasichana ili wanapokuwa wawe malkia wa nyumba.

Hadithi hii ifuatayo itawapa mfano wa kanuni za Kiislamu. Imam Muhammad Baqir a.s. amesema:

"Kwa hakika Fatima a.s. alichukua jukumu la wajibu wa kazi zote za nyumbani kama kusaga unga, kupika mikate, na usafi wa nyumba kwa ujumla; na Ali a.s. alichukua wajibu wa kazi zote za nje ya nyumba, kama kuleta kuni za kupikia na kuleta vitu vya kupika, n.k. "

(Biharul Anwaar, Jalada 10).

Kwa mujibu wa Hadithi hii tuliyoisoma tunaona mipaka baina ya wajibu wa bwana na bibi ni ukuta wa nyumba. Mwanamke ni mkuu katika chochote kile kilichopo katika kuta nne za nyumba na mwanamme ni mkuu katika mambo yote yaliyo nje ya kuta hizo.

Uislamu umemkomboa mwanamke dhidi ya matatizo na michafuko yote ya dunia;ili kwamba aweze kuzingatia na kutimiza wajibu wake vyema katika mambo ya unyumba.