rudi maktaba >Fiqh >Yaliyomo >

4.MAMBO YANAYOWABIDI BIBI NA BWANA WAYAJUE.

1. Wazoeane na kuambiana ukweli.

Mtu anapoposa ni kipindi kimoja ambacho kila upande unafanya njia ya kuvutia mwenzake. Siku hizi tunazuzuliwa kwa kuiga mambo ya sinema kiasi kwamba wengine wanajifanya ni waigizaji wa sinema ili mradi wawavutie wenzao.

Baada ya ndoa bibi na bwana wanakwenda kutembea safari ambapo ni bibi na bwana tu na hakika hilo ni jaribio mojawapo zuri na muhimu. Mara nyingi utaona bibi na bwana wanaona aibu na wanakuwa hawana uzoefu wa kuishi maisha kama hayo ni mambo ya kuvutia pia. Wakati mmoja, wakati bibi na bwana wako katika matembezi haya baada ya harusi mwanamke alipojaribu kupiga pasi nguo zake aliziunguza kwa sababu wengine mambo haya wanakuwa hawayafanyi na katika hali hiyo alishtuka sana kiasi kwamba alitaka kumficha bwana wake asipate kujua lakini kadiri muda unavyoendelea kupita watazoeana na hali kama hiyo itakwenda inapungua.Hata hivyo baadhi ya nyakati nyingine mambo kama haya yanaendelea na kwa hakika hizo ndizo sura za matatizo.

2. Uwe mwangalifu na usichukue mambo kwa pupa.

Iwapo kutokuelewana kwa kiasi kidogo kidogo kutakuwa kukiendelea na kuongezeka basi yanakwenda yanazaana. Milima inatengenezwa kwa punje ndogo ndogo,na ukianza kuzikusanya utashtukia unapata mlima.Hivyo mashitaka na tuhuma dhidi ya mwenzako yatajenga nyumba katika mioyo ya bibi au bwana. Watu kama hawa ukiwashindilia kabisa na kuwauliza yaliyotokea wiki iliyopita yaani juma lililopita utawasikia wakianza kutupiana lawama ambazo zimewaka moto kweli kweli.Kwa kutokuelewana, kwa kutotosheka katika hali kama hiyo hata ukifanya ishara yoyote basi mwenzako atakwambia wewe umenisengenya hivi ilhali wewe mwenyewe huna maana hiyo unayoambiwa na hivyo utaongeza moto huo wa kutokuelewana katika mioyo yenu. Hatua za pupa ziepukwe mtu yeyote anayempiga mwenzake ni mwehu, katili ni mnyama na mtu asiye na maendeleo kwa sababu amekiuka misingi ya kuheshimu na kumhifadhi mke wake.

3. Kutokuelewana kudhibitiwe na kuelezwa.

Kutokuelewana kati ya bibi na bwana ni vitu vya kawaida katika ndoa ambapo shaka haijatokezea.Katika hali hiyo inatakiwa maswala kama haya yachukuliwe kwa busara na kuelezwa kwa kiakili sio kwa mtu mwenyewe bali kwa mwenzake pia.Mara nyingine hatua hii haiwezekani hivyo kuna wazee wanaoweza kusaidia katika maswala ya ndoa. Hivyo ndiyo maana Islam imetoa amri kuwa kabla ya kutoa talaqa ushauri wa watu wenye hekima katika mambo ya ndoa waingilie kati na kujaribu kusuluhisha tofauti baina ya bibi na bwana. Kwa ushauri bora kusiwe na upande wa mwanamke au upande wa mwanamme bali wawe ni watu wa nje ya watu hawa wawili kwa sababu mtu asiweze kuvutia upande wa jamaa zake.

4. Mawasiliano na uaminifu.

Ninapenda kuwasisitizia kuwa mawasiliano ni muhimu kabisa katika ndoa yenye furaha na starehe. Bila ya mawasiliano baina ya bibi na bwana hofu inaendelea, mashaka inaongezeka na hali ya kutokuelewana itatokezea. Hivyo kuelewana lazima kuwepo na njia za kuwasiliana kuanzia wanapooana mwanzoni ili kwamba hata bibi na bwana wakiwa ni watu mashuhuri sana lakini waweze kuzungumza na kuelewana. Njia hii inawezekana isiwe rahisi lakini kama bibi na bwana wanajuana basi kuna mahali popote wanaweza kukutana katika maisha yao na kuzungumza. Daima uwepo na inakubidi uwe ukijaribu kuyaangalia matatizo yako,na muwe mkiheshimu uaminifu miongoni mwenu ujue namna ya kushukuru kitu chochote kidogo kile na uache kutoa shutuma za aina zozote kwa hivyo mawasiliano yatakuwepo.Itakubidi uanzishe mazungumzo yatakayomfurahisha mwenzako ili umvutie ashiriki katika mawasiliano yenu na wala usianze na mazungumzo na mashitaka na magumu ya maisha yako magumu ya kila siku kwa sababu utamfanya yeye achukizwe na mazungumzo yako asizungumze na wewe.Baadhi ya wanawake wanashitaki kuwa waume zao hawawashirikishi katika kazi zao au katika maisha yao ya kiofisi au kibiashara. Na hali hii ni kwa sababu wanatambua kuwa nyumba ni Jannat ambapo mwanamke yupo na hivyo anapotoka kwenye shughuli zake anakuja nyumbani apumzike na afarijiwe na mke wake mara nyingi, utaona wanaumme baada ya kuja nyumbani wanawaambia mambo mengine ya kazi zao ya ofisini au ya kibiashara hii haimaanishi kwamba anahitaji ushauri kutoka kwa mke wake bali anajaribu kupunguza uzito katika akili yake na kichwa chake na kwa sababu anakuwa na imani ya uaminifu na amana hiyo anayoiwekesha kwa mke wake anajua hatafanya khiana wala kumgeuka.

Katika maisha ya ndoa sio lazima kuwa ni maongozi tu yanayotakiwa kila siku kwa wakati mwingine hata kumgusa kidogo mwenzako au hata kuminya mkono kidogo yana mawasiliano ya aina yake na yana athari zaidi kuliko ya maneno.Hivyo mnapokutana baada ya bwana kushughulika ofisini na bibi kushughulika nyumbani mnapoonana mnazungumza nakidogo kujichangamsha, jambo ambalo litaweka njia ya mawasiliano kuwa bora na mazuri;na jambo lingine ambalo ni zuri kabisa katika mawasiliano ni hizi silabi tatu:"mimi ninakupenda sana." Na lau utaongezea maneno mengine mawili ya asante sana hapo litakuwa jambo zuri sana.

5.Kula chakula na maongezi.

Shughuli za kuridhisha za chakula na maongezi yanaunganisha familia pamoja.Baba anaweza kuwafurahisha kwa kuhadithia ujana wake, akiongelea mambo mengi yenye faida kama kuendesha baiskeli,kuroa samaki na kupanda farasi siku za Jumapili, vile vile mama pia anaweza kuanzisha mazungumzo juu ya utoto wake na ujana wake.Katika majumba mengine muda unakwenda mwingi wakati wanapokuwa mezani wanakula kwasababu familia wanapokuwa wanakula pamoja wanazungumzia mambo ya siku yaliyotokea mwingine anaongelea aliyoyasikia au kuyaona na mambo mengineyo hata wengine huzungumzia matukio mengine na kuzungumzia matukio ya Qurani,Hadithi n.k.

Hivyo inabidi wakati wa kukaa kula mazungumzo yatakayotokea yawe yenye kufurahisha na kupendeza na ichukuliwe tahadhari kuwa mtu yeyote asianzishe mazungumzo yale ambayo yanaweza kusababisha kutokea ugomvi au kutokuelewana wakati wa chakula.

6. Kuwa pamoja na familia.

Wazazi wawaulize watoto wao walichofanya shuleni na wamefanya na akina nani, na walichojifunza nacho. Na hali hii itakuwa ni ya kufurahisha mno kwa mzazi na watoto kwa sababu watajikuta wazazi katika mazungumzo na watoto wao.

Kuwachukua familia katika matembezi inawabidi wazazi watumie muda mwingi pamoja na familia yao na kuwachukua familia yao kimatembezi. Kuwafanya wao wakiwa ni moja ya shughuli zao. Kwa kuchukua nje ni njia moja nzuri kabisa kwa sababu inafungamanisha familia kwa pamoja na kufanya maisha ya ndoa yakawa ya raha na mustarehe.

Inawabidi wazazi waangalie kwa makini mavazi ya watoto na usafi wao na yote hayo uyafanye kwa sauti ya kuvutia na kupendeza, uwafundishe wao namna ya kufanya vyema zaidi kwa kuvutia.

Kufikiria shughuli za siku nzima, usikalie kusoma magazeti tu au kuangalia matatizo yako inakubidi pia ufikirie kuhusu familia yako vile utakavyoweza kuiendeleza na kutatua matatizo na kuleta ushirikiano na uelewano mwema miongoni mwa familia nzima.