rudi maktaba >Fiqh >Yaliyomo >

 

MAJIBU YETU

  • Ni wazi hili ni jambo Mukhtalafun fihi kwa hiyo halina Ijamaus Sahaba, basi, huweza kuliharamisha.
  • Kwa nini hakuzitaja hizo riwaya kumi na nane za Imam Ali ili tuzijibu?!
  • Sisi tunasema:- Siyo kweli kuhusu Imam Ali, kama tutakavyoonyesha katika kitabu hiki, na hapo atakapozitaja riwaya nyingine.
  • Sasa, tutazichambua hoja zake, moja moja, nazo ni hizi:-

    1. Imepokewa kwa Ibnu Shihab, kutoka kwa Abdullahi na Alhasan, watoto wa Muhammad bin Ali, kutoka kwa baba yao, kutoka kwa Ali bin Abi Talib A.S. kwamba: Mtume S.A.W. amekataza ndoa ya Mut'a siku ya Khaybara na amekataza kula nyama ya punda wa mjini."
    2. Imepokewa na Umar bin Alharith na Allaith bin Saad, kwamba Rabi'i bin Sabura Al'jahniy amewasimulia kutoka kwa baba yao, kwamba: Mtume S.A.W. amekataza ndoa ya Mut'a mwaka wa Fat'hu."
    3. Imepokewa kwa Abdul Azizi bin Umar bin Abdul Azizi kutoka kwa mtu mmoja wa Sabrini (Rabi'i bin Sabura) kutoka kwa baba yake kuwa yeye amesema. Nimemsikia Mtume S.A.W. anasema katika Hija ya mwisho: Hakika Mwenyeezi Mngu ameharamisha ndoa ya Mut'a, basi msiikaribie na yeyote aliye naye (mke wa Mut'a) na amwache."
    4. Amesema Ismail kutoka kwa Az'Zuhry. Tulikuwa kwa Umar bin Abdul'Azizi tukajikumbusha Mut'a, mtu mmoja aitwaye Ar'Rabii bin Sabura akasema:- Nashuhudia kuwa baba yangu amesema kwamba: Mtume S.A.W. amekataza ndoa hiyo katika Hija ya mwisho.
    5. Imepokewa kwa Sufyani bin Uyayna kutoka kwa Az'Zuhry' kutoka kwa Ar'Rabii bin Sabura kutoka kwa baba yake kwamba: Mtume S.A.W. amekataza ndoa ya Mut'a mwaka wa Fat'hu Makka.

    Hizo ndizo hadithi alizotutajia Sheikh Muhammad Sharif Famau, kisha akasema: "Hizi ni hadithi ambazo zaonyesha kuwa ndoa ya Mut'a ni haramu."

    MAJIBU YETU

    Tunasema:- Kama hizo ndizo hadithi alizozitegemea Sheikh basi ametegemea kamba mbovu. Kama tutakavyoona hivi sasa inshaallah.

    1. Hadithi ya Imam Ali A.S. siku ya Khaybara, haikubaliani na tukio la tarikh siku hiyo, kama walivyosema wazi haya wanazuom wengi wa kisunni.
    2. Amesema Ibnu Qayyim AI'jawaziyya:- Kisa cha Khaybara, hakuna sahaba aliyeowa Mut'a mwanamke wa kiyahudi mahala hapo. Wala Mtume S.A.W. hakutoa ruhusa ya jambo hilo, wala hakuna yeyote aliyepokea (habari hizi kwa usahihi) katika vita vya Khaybara na wala hapakuwa pakitajwa Mut'a mahala hapo, si kwa kufanya Mut'a wala kuharamisha Mut'a."

      TAZ: Zadul Maad J. 2 uk. 143.

      Anaendelea kutusimulia lbnu Qayyim:- "Kwa hakika Khaybara hapakuwako wanawake wa kiislamu, bali walikuwako tu wanawake wa kiyahudi. Na ruhusa ya kuowa Ahlul kitabi ilikuwa haijatolewa bado, kwa sababu ruhusa hiyo imekuja bada ya tukio ya Khaybara.

      TAZ: Fat'hul Bari J. 7 uk.483

      Fat'hul Bari J. 9 uk. 168

    3. Ikiwa ni hivyo, Imam Ali A.S. hawezi kuwa mjinga hivyo wa kutojua aliyoyajua Ibnu Qayyim na Ibnu Hajar.
    4. lililothibiti kwa Imam Ali A.S. katika vitabu vyetu vya kishia nikwamba:- "Alikuwa akihalalisha". Na katika vitabu vya kisunni nikwamba: "Alikuwa akilaumu Umar bunul Khattab kuiharamisha".

    TAZ: Tafsirul Tabari J. 5 uk. 9

    Kwa hiyo, hadithi hiyo imeanguka!! Katika hadithi tano ailizotuletea zimebaki hadithi nne.

    Alipotoa hadithi hizo alijuwa zina Idhtirab, mara:

    Siku ya Khaybara, mara hija ya mwisho, mara Fat'hu Makka.

    Sheikh Muhammad Sharif Famau alijitetea kwa mfano wa mtu anaemdai shilingi elfu moja, kuna mashahidi watatu:-

    Shahidi wa kwanza anasema:- "Aliona nikimkopesha shilingi elfu moja mwaka 1981.

    Shahidi wa pili anasema:- "Aliona nikimkopesha shilingi elfu moja mwaka 1982.

    Shahidi wa tatu anasema:- "Aliona nikimkopesha shilingi elfu moja mwaka 1983.

    Sheikh Muhammad akauliza:- Muhimu n, HAL THABATAT TAHRIM AM LAM YATH'BUT? Maana yake Je! Umethibiti uharamu au haukuthibiti?