rudi maktaba >Fiqh >Yaliyomo >

 

UWIANO WA NDOA YA MUT'A NA YA DAIMA

  • Ndoa ya Mut'a na ya daima, hazithibiti ila kwa kufungamana na matamko mawili: IJABUN na QABUL (Nimekuoza, Nimekubali).
  • Kufungamana kwa ndoa mbili hizi hakupatikani ila kwa moja kati ya matamko matatu haya: ZAWWAJ'TUKA, ANKAH'TU KA, MATTA'ATUKA.
  • Ndoa mbili hizi hupatisha haramu kwa: Nasabu, Ukwe, Kunyonya.
  • Mtoto wa Mut'a ni kama mtoto wa ndoa ya daima, anazo haki zote.
  • Mke atakaa eda baada ya kumalizika muda wake katika ndoa ya Mut'a, (atakaa eda hedhi mbili, ikiwa mwanamke hapati hedhi basi atakaa siku arobaini na tano) kama ambavyo atakaa eda baada ya kuachika mke wa ndoa ya daima. Itakapokuwa wawili hawa walikwisha ingiliwa.
  • Hakuna eda kwa mwanamke ambae hakuingiliwa, iwe ni ndoa ya daima au ndoa ya Mut'a.
  • Haijuzu kumuoa Shangazi ya mke wa Mut'a (binti ya kaka yake, au binti ya dada yake) ila kwa idhini ya mkeo.
  • Haifai kabisa kumwingilia mke wa Mut'a akiwa katika hali ya siku zake za hedhi au nifasi. Kama ambavyo inakatazwa kwa mke wa daima.
  • Kile kitendo cha kumwingilia mke wa Mut'a kinatoa haki kwa mtoto kuwa ni wa mume huyu, hata kama maji yake (manii) alimwagia nje. Ndivyo ilivyo pia katika ndoa ya daima.
  • Mahari katika ndoa ya Mut'a ni kama katika ndoa ya daima, hakuna kiwango maalum, iwe kidogo sana au nyingi sana. Soma Quran 4:20.
  • Haifai kwa mwanamke wa Kiislamu kuolewa Mut'a na kafiri, kama ambavyo mwanamume haifai kumuoa mwanamke kafiri isipokuwa Ahlulkitabi.
  • Ikigundulika aibu yoyote inayotengua ndoa, basi palepale ndoa huvunjika. Ikiwa alikuwa hajamwingilia basi hana mahari, na kama alikwisha kumwingilia, na mwanamke hakujua kutoka mwanzo aibu hiyo, basi atapewa mahari yote waliyokubaliana. Ikiwa wakati wakifunga ndoa mwanamke alijua hili la kuvunja ndoa akalificha, basi huyo ni malaya hana mahari.
  • Mke wa ndoa ya daima na wa ndoa ya Mut'a, wanapaswa kukaa eda mara mume wao anapokufa, kwa muda wa miezi minne na siku kumi.
  • Eda ya mwenye mimba ni kuzaa mimba yake, iwe ni mke wa daima au wa mut'a.
  • Mume wa ndoa ya Mut'a ana haki ya kumwachia muda wote waliokubaliana kuowana, na kuanzia hapo atakuwa si mkewe tena. Kama ambavyo, mume wa ndoa ya daima anayo haki ya kumpa talaka mkewe.
  • Mume wa ndoa ya Mut'a akimwachia mkewe muda wote waliokubaliana kuowana kabla ya kumwingilia, itapasa ampe nusu ya mahari. Ikiwa walikaa na mke huyo muda wote uliotajwa katika ndoa yao, ukamalizika bila va kumwingilia, itapasa ampe mahari yote.
  • Mume na mke waliowana kwa Mut'a wana haki ya kuongeza muda zaidi kabla ya kumalizika wa kwanza.
  • Sasa tumwangalie Sheikh Muhammad Sharif Famau, yeye anasema: Kuna kauli mbili kuhusu Mut'a:-

    1. Jamhurus sahaba wanaharamisha. Hii ni kauli ya Ali bin Abi Talib, Umar bunul Khattab, Ibnu Masuud, Ibnu Umar, Ibnuz Zubeir, Maimamu wanne, na mattabii wengi.
    2. Kisha akasema:- Kwa Sayyidna Ali peke yake kuharamisha Mut'a kumepokewa Hadithi thamanta a'shara (kumi na nane).

    3. Kuwa Mut'a inafaa, Hii ni kauli ya Ibnu Abbas, Ubayya bin Kaab, A'taa, Jabir bin Abdiliah, Abu Said Alkhudury.