Sasa, tuyajadili maneno hayo:
Sheikh Muhammad kwanini hakutoa taarifa ya Mut'a ya ki Istilahi? Kwa faida ya wasomaji wetu, hapa tutatoa taarifa ya Mut'a:-Mut'a ni: "Kukuoza mwanamke nafsi yake kwa kutaja mahari, na kwa muda maalumu".
Sheikh baada ya kutoa taarifa yake akasema:-Sallaaaala! Si upuuzi huo, yaani Ndoa ya Mut'a ni upuuzi! TUNAULIZA:- Ikiwa anakubali ilikuwako kwa Mtume S.A.W. hiyo ni upunzi? Mtume S.A.W. anafanya upuuzi? Au wakati huo ilikuwa na Shahidi? au Waili? au mirathi? au chakula?
Pengine Sheikh anaona ajabu vipi mke wa Mut'a atakuwa Zawj hali ndoa yake haina: Shahidi, Walii, Chakula, mirathi. Hilo lisimshtue! Hata kwa ndoa ya daima huwezekana hilo.