Tafsirul Qurtubi J.5 uk. 133
Al'Mughuniya Ibnu Quddama J. 7 uk. 571
"Amesema Ibnu Abdil Hakami, nimemsikia Shafii akisema:
Amesema: Hajjaji bin Artat, Hautimii muruwa wa mtu (heshima) mpaka awache sala ya jamaa nikamwambia, Mwenyeezi Mngu na auondoe murua huu." Amesema Al'Asmai:- Mtu wa kwanza kupokea rushwa Basra katika ukadhini Hajjaji bin Artat."
Sasa, tuache hadithi zilizothibiti, tushike ya mtu, Ambae anaona ni murua kuacha sala ya jamaa? Mtu ambae ndiye kadhi wa kwanza kula rushwa Basra? Hadithi hiyo haina mashiko tupa nje. La ajabu zaidi hapa ni kwamba, japo baadhi ya Masheikh wao wanaharamisha ndoa ya Mut'a, lakini wanaruhusu kujipuli!! Na baadhi ya masheikh wao wamejawizisha Hadaa, kumuowa mwanamke ukinuia utamwacha baada ya muda fulani kufika bila ya yeye kujua!! Fat'wa hii ni ya lbnu Taymiyya.
Fat'wa ya kujipuli, angalia vitabu:- Alhalalu Walharamu uk. 161
Sublus Sallami J. 3 uk. 974.
Na vingine vingi katika wanazuoni wa Kihanafi na Hanbali waweza kuyapata hayo ya kujawizisha Ponyeto (Kujipuli)