rudi maktaba >Fiqh >Yaliyomo >

 

NDOA YA MUT'A KATIKA QURAN

Muenyeezi Mngu amesaema: "Mnaostarehe nao katika wao, (Wanawake) basi wapeni mahari yao yaliolazimishwa" 4:24. Aya hii imeshuka katika ndoa ya Mut'a kama ilivyo atika Tafsiri zifuatazo:-

  1. Tafsirut Tabari J. 2 uk. 9
  2. Addurrul Manthur J. 2 uk. 140
  3. Tafsir Ibnu Kathir J. 1 uk. 486
  4. Mukhtasar Tafsir Ibnu Kathir J. 1 uk. 375
  5. Tafsirul Qurtubi J. 5 uk. 130
  6. Tafsirui Khazin J. 1 uk. 506
  7. Tafsirul Kash'shaf J. 1 uk. 519
  8. Tafsirul Kabir J. 3 uk. 200
  9. Tafsirul Maraghi J. 5 uk. 8
  10. Tafsirul Alus J. 5 uk. 5
  11. Tafsir Abi Hayyan J. 3 uk. 218
  12. Tafsir Mujahid uk. 152
  13. Ahkamul Quran, Alqadh Abubakar 1/162
  14. Ahkamul Quran, AIjassas J. 2 uk. 147

Hata Sheikh Muhammad Sharif naye anakubali, yeye anasema:-

"Kwa ufupi, nikaha ya Mut'a Aya iambiwayo kwamba ndiyo dalili ya nikaha ya Mut'a, japo wanazuoni wengi wa Ahlus Sunna wanasema:- "Famastamta'atum bihi minhunna faatuuhunna ujuura hunna" kwamba hii Aya ilikuja katika nikaha ya Mut'a, Aya hii haihusiani na nikaha ya Mut'a aslani". Mwisho wa kunukuu.

Kwa mujibu wa kauli yake Sheikh, wanazuoni wengi wa Ahlus Sunna wanasema Aya ilikuja katika ndoa ya Mut'a. Lakini yeye hakubaIi!! Amuweni nyinyi wasomaji wetu.

Mpenzi msomaji, tafadliali sikiliza kaseti zangu nilizozunguinza juu ya Mut'a tarehe 17-8-1988, kisha usikilize kaseti alizonijibu Sheikh Muhammad Sharif Famau tarehe 1-9-1989. Baada ya hapo jibu letu hili ulisome kwa makini na mazingatio yenye ikhlas ya kutafuta haki. Nataraji jibu la mushkeli huu utalipata inshaalla.