rudi maktaba > Fiqh > Yaliyomo >

HUKUMU BAADA YA KUFA

Baada ya kufa ni sunna, (1) Kufumbwa macho yakiwa wazi (2) Kuzibwa kinywa kwa utepe utakaopitishwa chini ya taya na kufungwa tanzi juu ya kichwa, (3) Kunyooshwa mikono, miguu na mapaja yake, (4) Kufunikwa shuka na kama amekufa usiku, mahala hapo pawashwe taa wasimwache maiti kizani, (5) wapashwe wenye imani (Waislamu) majira za mazishi ili waweze kuhudhuria mazishi yake, na wafanye haraka upesi kuzikwa. Lakini kama hawana yakini kwa kufa kwake, basi wasubiri hata wayakinishe, na kama maiti mwenye mimba, na mtoto yu hai basi asizikwe mpaka apasuliwe upande wa kushoto na kutolewa mtoto na baadaye ashonwe.

Mtu akishakufa na kupoa mwili wake mtu yoyote atakayemgusa yule maiti kabla hajawoshwa ghusli tatu kwa viungo au mwili wake,, kwa sehemu yoyote ya mwili wake itamlazimu aoge GHUSLU MASSI Al- MAYYIT, yule mwenye kumgusa.