rudi maktaba > Fiqh > Yaliyomo >

RUHUSA YA KULIA UFIWAPO

Ni sunna ya Mtukufu Mtume (s.a.w.) kumlilia maiti wako.

Mtukufu Mtume (s.a.w,) alimlilia Bwana ZAIDI (R.A.) na Bwana JA'AFAR (R.A.) na pia alimlilia Ami yake Sayidna HAMZA (a.s.) na mwanawe Sayidna lbrahimu (a.s.) Mtume (s.a.w.) alipomwona ami yake Hamza (a.s.) ameuwawa akalia, na alipoona namna Ilivyotendewa kinyama maiti tukufu ya Hamza (a.s.) akalia sana kwa kwikwi.

Kwa hivyo haikatazwi kulia bali inakatazwa kusema maneno yasiomridhisha Mwenyezi Mungu kama kusema "Umenionea umenichukulia mpenzi wangu" n.k. Kulia hakuna muda madhali roho inauma, inahuzuni unaruhusiwa kulia n kulia ni dawa.

AL-LAAHUM-MA TAQAB-BAL MIN-NAA
TAM-MAT BIL KHAYR.