rudi maktaba > Fiqh > Yaliyomo >

MKE KUKAA EDA YA KUFIWA NA MUMEWE

Mwanamke mwenye kufiwa na mume kama hana mimba eda yake ni miezi minne (4) na siku kumi (10), na kama mwenye mimba eda yake mpaka azae, lakini iki wa amezaa kabla ya kupita miezi minne na siku kumi lazima akae eda hadi zipite, siku hizo.

Mwanamke mwenye eda ya kufiwa na mumewe, ni haramu kuvaa nguo za rangi; kujipamba kwa namna yo yote kwa mwili au kwa nguo kama kujitia manukato, kutia wanja machoni, mapodari, hina na kila jambo la kujipamba ni haramu kwake hata nguo nyeusi ikiwa ina nakshi au mkato wa kujipamba.

Eda huanzia siku ya kufa kwa mume ikiwa yupo hapo, na kama hayupo huanzia siku atakapopata habari hata kama kumepita muda mrefu sana. Katika muda huo wa eda hawezi kuposwa au kuolewa.

Uislamu unaamrisha unadhifu, basi wanaruhusiwa wanawake wenye eda kuoga kujisafisha na kuweka mwili safi, kukata kucha.

Anaruhusiwa kutoka nje kama ipo haja kama kununua mahitaji yake au kumwangalia jamaa au mgonjwa na kadhalika, asitoke nje paisipo na haja.

Tunaomba kwa Mola wetu atupe sote Twafiki ya kufuata maamrisho ya dini na kuepukana na yaliyoharamishwa au kufuata mambo ya Bida'a uzushi, usiona msingi.