rudi maktaba > Fiqh > Yaliyomo >

NAMNA YA KUFUKIA KABURI

(a) KiIa aliyoko hapo atabaruku naye kwa kusukuma mchanga kwenye kaburi kwa mgongo wa mkono wake wa kulia, na mwengine kwa majembe. Hala hala jamaa zake maiti wasitie mchanga, na makruhu na huleta ugumu wa moyo kama ilivyopokewa hadithi Tukufu ya Mtume (s.a.w).

(b) Likishajaa kaburi linyanyuliwe kidogo kiasi cha kipimo cha vidole vinne wazi na kutandazwa kufanya kama mraba.

(c) Liwekwe alama ya kujulisha kuwa kaburi hili ni la nani.

(d) Litiwe maji juu ya kaburi, mtiaji aelekee Qibla na aanzie kumwaga kutoka kichwani hadi miguuni, tena azunguke akirudia rudia hadi kichwani na maji ya faidi yamwagwe kati ya kaburi hilo. Ni sunna kutia maji vivyo hivyo, kila siku hadi siku arobaini au miezi arobaini.

(e) Baada ya kutia maji waliohudhuria watie vidole vyao kwa kuvizamisha kidogo ili ibakie alama za vidole katika kaburi upande wa juu na kusoma sura ya "IN-NAA AN-ZAL-NAAHU" mara saba, na kumwombea maiti kwa Mwenyezi Mungu amghufurie.

(f) Baada ya kuondoka watu kwenye kaburi ni sunna alakiniwe kwa mara nyingine, (mara hii kwa sauti kubwa) ukifanya hivyo yule maiti hataulizwa maswali (ni sunna walie jamaa karibu sana au mtu alioruhusiwa na huyo ndio asome Talikini mara hii).

(g) Hasa ni sunna mara tatu kulakiniwa (i) wakati wa kukata roho (ii) akishalazwa kaburini (iii) Na mwisho baada ya kuondoka watu kwenye kaburi.

(h) Baada ya hayo yote, ni sunna kuwapa mkono wa rambirambi wafiwa, hufuatia matanga uchache wake siku moja na isizidi siku tatu. Ni sunna kuusia mali (Fedha) kwa ajili ya kulisha katika matanga yake.

(i) Ni sunna majirani wawapelekee wafiwa chakula kwa muda wa siku tatu kwa kuwa wao wameshughulika na msiba huo, sio wafiwa wawapikie watu. Ni karaha sana kwenda kula chakula matangani, ipo hadithi kwamba kufanya hivyo (kwenda kula) ni vitendo vya watu wasiokuwa waislamu katika zama za Jaahiliya.