rudi maktaba > Fiqh > Yaliyomo >

JARIY-DATAIN

Ni sunna iliohimizwa sana kwa SHIA WA AHLUL-BAIT (A. S.) kuwekewa maiti vijiti viwili vibichi vya mti wa mtende, kiasi cha urefu wa kila kijiti kiwe mkono mmoja, ambao huitwa "JARIY-DATAIN". Huandikwa juu ya maiti hayo jina lake na Ia baba yake maiti na Shahadatain, na majina ya Maimamu kumi na wawili (a.s.). Maiti huwa haadhibiwi vijiti vinapokuwa vibichi mpaka kukauka.

Sunna hii ya kuwekewa vijiti viwili vya mtende imeanzia zama za Mtume ADAM (A.S.) alipofanya wasia na ikaendelea zama za Mitume wote na ikawachwa zama za JAHILIA na Mtume wetu (s.a.w.) akaanzisha upya, na inafaida sana kwa maiti. Siku moja Mtukufu Mtume (s.a.w.) alipita kwenye kaburi la maiti ambaye alikuwa ana aadhibiwa akaamrisha yaletwe vijiti vya mtende na papo hapo akakata vipande viwili, kimoja akakifukia kwenye kichwa na cha pili kwenye miguu, na akasema, "Sasa atapunguziwa adhabu".

Moja katika vijiti hivyo kiwekwe mkononi ya kulia karibu na shingo la maiti kwa kugusanana maiti na cha pili upande wa kushoto juu ya kanzu chini ya shuka. Vijiti hivi viwe vya mtende au mkomamanga hata ya mnazi yanafaa, na ikiwa yote hayo hayapatikani basi, vijiti vya aina yoyote vinafaa na bora vile vinavyochelewa kukauka.