rudi maktaba > Fiqh > Yaliyomo >

ADABU NA SUNNA ZA KWENDA NA JENEZA:

Thawabu ya kufuata Jeneza: Imepokewa hadithi kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.) kwamba amesema: "Habari njema na (bishara) nzuri ya kwanza atakayopewa yule maiti 'MUMIN' ataambiwa, 'Karibu' kwa hakika Mwenyezi Mungu Amemghufuria kila mwenye kufuata Jeneza lako, na Dua zote za wale waliokuombea ughufuriwe Ameyakubali. Imam JAFFER AS- SADIQ (A.S.) Amesema, "Kila mwenye kufuatana na Jeneza la mumin (mwenye imani) kwa kila hatua moja aaendayo mpaka arudipo mazishini ataandikwa thawabu elfu mia, na kufutwa madhambi elfu mia na kuongezwa daraja peponi elfu mia kwa kila hatua. Mtukufu Mtume (s.a.w.) Amesema:

Ni sunna kila mwenye kuona jeneza alikabili na kulipokea na kusema maneno haya:

Basi mwenye kusoma hayo, Malaika wote wa mbinguni watalia kwa kumhurumia msoma dua hiyo.

Wanatakiwa watu waende na maiti kwa heshima na adabu wasiongee na kuzungumza hasa mambo ya kidunia au habari ya yule maiti, bali waende na huku wanasoma dhikri kama "BIS-MIL-LAA-HI WA BIL-LAA-HI WASAL-AL-LAAHU ALAA MUHAM-MADIN WA AA-LI MUHAM-MAD AL-LAA-HUM-MAGH-FIR LIL MU'U-MINIY-NA WAL-MU'U-MINA-AT." Au dhikri yoyote ya Mwenyezi Mungu. Haifai kucheka wala kuamkiana (kutoa salamu) na kwenda mbele ya jeneza, wala kuendesha jeneza mbio mbio, isipokuwa kama inaogopewa maiti hiyo kuharibika au inanuka. lnafaa kuwa nyuma ya jeneza au pande mbili ya jeneza.

Ni sunna kubeba jeneza kwa mpango ufuatao:

  1. Kwanza beba upande wa kulia wa mbele wa maiti kwa bega lako la kulia (kushoto ya jeneza).
  2. Njoo kwenye mguu wa kulia wa maiti kwa bega lako Ia kulia (kushoto ya jeneza).
  3. Njoo kwenye mguu kushoto wa maiti kwa bega lako la kushoto (kulia ya jeneza).
  4. Nenda kwenye mkono wa kushoto wa maiti kwa bega lako la kushoto. Baadaye utarejea kama awali (Ia kulia mara moja tu ukishafuata sunna hiyo) unaweza kukamata mahali popote pa jeneza au fuata mpango ule ule wa awali.