rudi maktaba > Fiqh > Yaliyomo >

KUMSALIA MAITI

Sala Ya Mait: Lazima iwe baada ya kuvishwa sanda na kutia HUNUUT (KUPAKA KAFURI kwenye VIUNGO VYA KUSUJUDIA). Kuanzia maiti mwenye umri wa miaka sita (6) huwa faradhi kusaliwa sala ya maiti.

Sala ya maiti haina Adhana wala Kukimu na pia hakuna rukuu wala sijda, lakini inakusimama tu, na ina Takbira tano tu (badala ya sala tano za faradhi za kila siku). Hakuna shuruti ya kuwa na wudhuu lakini ni sunna kuwa nao. Ni sunna pia wakati wakutoa kila Takbira, anyanyuwe mikono hadi masikioni mwake yule mwenye kuswali.

Namna Ya Kumsalia Maiti:

Mwenye kumsalia lazima asimame nyuma ya jeneza (jeneza liwe mbele yake) asiwe mbali nae, aelekee Qibla, kichwa cha maiti kiwe upande wa kulia wa mwenye kumsalia, na miguu upande wa kushotona awe amesimama. Akiwa maiti mwanamume basi ni sunna kusimama kati-kati na akiwa maiti mwanamke, asimame sawa na kifua cha maiti. Huwezi kumsalia maiti asiyekuwa mbele yako ijapokuwa akiwa mjini humo.