MADHAMBI YAMFANYAYO MTU KUINGIA JAHANNAM

Makala haya yamekusanywa na kutarjumiwa na:
Amiraly M.H. Datoo

Hadithi hii ilisomwa na: Sheikh Akmal Hussein Taheri - Bukoba.

Mwanadamu yupo daima anatenda madhambi kutokana na nafsi yake mwenyewe. Malaika walipomwabia Allah swt kuwa mjumbe wake huyu atakuwa mtenda madhambi. Naye Allah swt akawaabia kuwa yeye ayajua zaidi kuliko wao.

Mtu kuchuma mali na kurundika

Mtu yule ambaye atakusanya fedha na kuziweka mahala pamoja bila ya kufaidika yeye wala kuwasaidia wengineo ambapo wapo ndugu zake Waislamu wenye shida ambapo maisha yao yamewawia magumu. Mtume s.a.w.w. amesema kuwa "ufukara ni mbaya zaidi ya ukafiri". Vile vile Imam Ali a.s. amesema Daima muchunge kuwa mwenye "shida masikini asikuijie bali ni wajibu wako wewe uwafikie."

Wakati mwingine mwanadamu hufikia wakati wa kukufuru ama kwa kukusudia au bila kukusudia. Siku moja mtu mmoja alikuwa akisafiri kwenda mji mwingine kwa ndege. Ndugu yake ambaye alikuwa akimsindikiza uwanjani hapo alimwuliza "Ewe ndugu yangu ! Je hautakuwa na shida ya fedha wakati ukiwa safarini ?" Ndugu yake ambaye alikuwa akisafiri alimjibu "Naam Ndugu yangu ! Mimi sitakuwa muhtaji wa Allah swt kwa muda wa juma moja hivi." Ndege iliruka na katika muda wa nusu saa hivi kulipatikana habari kuwa ndege hiyo imeanguka na wasafiri wote wameuawa.

Hapa siwezi kusema kuwa watu wote hao wamekufa kwa sababu ya kuadhibiwa mtu mmoja aliyetoa maneno ya kashfa dhidi ya Allah swt. Na kwa maani hii ndipo tunapoambiwa kuwa sisi tusijihusishe na mahala ambapo panapotendeka maasi na madhambi kwa sababu inawezekana adhabu za Allah swt zikateremshwa hapo na wewe ukakumbwa pamoja humo.

Kisa cha kijana mwenye madhambi

Ma'adh anasema: "Siku moja nilikuwa nkijiandaa kwenda kwa Mtume s.a.w.w. , na mara nikamwona kijana mmoja akilia mno, basi hapo nilimwuliza sababu ya kilio chake hicho. Huyo kijana alinibu kuwa yeye ni mwenye dhambi kubwa mno. Basi hapo nilimwambia aje pamoja nami kwa Mtume s.a.w.w. ili amwombee msamaha kwa Allah swt. Hapo huyo kijana alisema kuwa alikuwa akiona aibu kuja mbele ya Mtume s.a.w.w. kwa sababu ya dhambi zake." Hapo Ma'adh aliendelea na safari yake hadi kwa Mtume s.a.w.w. na kumwelezea yale yaliyotokea. Basi Mtume s.a.w.w.alimwambia akamlete yule kijana. Alipofikambele ya Mtume s.a.w.w. aliulizwa, 'Je umekuwaje, walia kwa nini? Hapo huyo kijana akasema, "Ewe Mtume wa Allah swt! Dhambi langu ni kubwa mno!" Hapo Mtume s.a.w.w.aliendelea kumwuliza, "Je kosa lako kubwa au mbingu? " Akajibu, 'Kosa langu!' 'Je kubwa au dunia nzima? Akajibu, kosa langu! Je kosa lako kubwa au msamaha wake Allah swt? Hapo huyo kijana akasita na hatimaye kukubali kuwa 'Msamaha wa Allah swt ni mkubwa! Bassi hapo Mtume s.a.w.w. alimwuliza, sasa niambie kosa lako. Huyo kijana akaanza kusema: "Ewe Mtume wa Allah swt! Palitokea kufariki kwa binti mmoja mzuri mno wa kabila la ansaar, na mimi nilikwenda usiku ule kulifukua kaburi ili kutaka kuiba sanda aliyokuwa amevishwa huyo maiti, shetani alinighalibu na kunifanya nikatenda tendo la kinyama kwa maiti huyo, binti aliyekuwa uchi mbele yangu. Hapo ndipo maiti hiyo ilipota sauti ya masikitiko na kunilaani kwa kuniambia kuwa Allah sw ataniingiza motoni na kuniunguza humo kuteketea. Ewe mtume wa allah swt kwahakika, baada ya matamshi hayo ya maiti huyo, mimi nimekosa furaha ya kila aina na nimeingiwa na woga na nadhani nitaweza kuangamia katika hali kama hii iwapo itaendelea kunisumbua. Hapo mtume s.a.w.w. alimwambia huyo kijana: "Ondoka haraka mbele yangu kwani inawezekana moto wa Jahannam ukanikumba nami pia." Je kwa nini Mtume s.a.w.w. alisema hivyo? kwa sababu dhambi lilikuwa kubwa mno!

Kwa mujibu wa riwaya, kijana huyo baada ya kuambiwa hivyo, aliondika akiwa amesikitika mno na kuelekea katika milima ya mji wa madina, huko alikaa kwa muda wa siku arobaini akiwa akilia na kuomba Toba kwa Allah swt. Baada ya siku arobaini kupita, alisema: "Ewe Allah swt! Iwapo umeshakwisha kuikubalia Toba yangu, basi naomba unijulishe kwa kumpitia Mtume wako. Na iwapo bado haujaikubali Toba yangu, basi naomba uniteremshie miale ya moto kutoka mbinguni ili inichome na kuniunguza ili niteketee kabisa!"

Basi hapo iliteremka Aya ya 134 - 135 ya sura Ali Imraan (3):

"Na wale ambao, wanapofanya tendo la kuaibisha au kudhulumu nafsi zao, wakamkumbuka Mwenyezi Mungu na kuomba msamaha wa madhambi yao, na ni nani awasamehee madhambi isipokuwa Mwenyezi Mungu? Na ambao hawabakii (kwa kukusudia) katika yale waliyoyafanya maovu hali walikuwa wakiyajua hayo."