rudi maktaba > Fiqh > Yaliyomo >

MASWALA TOFAUTI

Ingawa kula kunabatilisha Saumu lakini kunasamehewa kwa mtu yeyote aliyekula kwa kusahau, vile vile kunywa. Ama kuyameza mate yaliyojaa kinywani, hakuna makosa. Kuyameza mabaki yali yaliyosalia menoni wakati wa kula ama kunywa, kunabatilisha.

Kukiangalia chakula kwa hali ya kukitamani na hali umefunga hakubatilishi Saumu. Lakini ni vizuri zaidi kutokiangalia ukiwa wakitamani.

Kudungwa sindano si makosa kwa mtu aliyefunga. Naam, ni vizuri kutumia Ihtiyat (yaani kujitoa mashakani) kwa kutodungwa sindano iliyo na chakula.

Kumbuka kwamba nia ni muhimu sana na Saumu haisihi pasina kutia nia. Kunuia huku ni kusema moyoni. "Nia yangu ni kufunga kesho kwa ajili Mwenyezi Mungu". Kadhalika amali zote za ibada hazisihi pasina nia maalum kama alivyosema Mtume (s.a.w): "Matendo yote hufanywa kwa nia". Na hivyo basi nia ni muhimu sana.

Mwenye Saumu akiazimia usiku kwamba mimi kesho sito funga basi Saumu ya siku hiyo haitasihi hata kama atabadili dhamira na kufunga tena hivyo basi atalazimika kuilipa siku hiyo. Na tukumbuke tena kwamba, mtu yeyote aliyeitengua Saumu haimfalii kula au kuendelea na vitendo vilivyokatazwa, bali analazimika kujizuia.

Kusukutua wakati wa kutawadha hakukatazwi lakini ni bora kukuepuka maana huenda maji yakakutangulia pasina kutegemea. Ama kule kupiga mswaki nako ni hivyo hivyo. Mtume (s.a.w.) alisema "Harufu ya mdomoni wa mwenye kufunga ni bora na yenye manukato zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko marashi yoyote yale".

Ukimlazimisha mkeo kumwingilia na hali yeye mwenyewe ha radhi utalazimika kulipa na kutoa kafara, na pia kuaziriwa kwa kupigwa viboko 50. Na lau nyote mtaridhiana mtalazimika kulipa, kutoa kafara na kuaziriwa kwa kupigwa viboko 25 kila mmoja.

Ingawa tulieleza kwamba kutoka manii kwa kujimai (kuingiliana mke na mume) kunabatilisha Saumu na wanaohusika na kitendo hivyo huwa na janaba, hukumu hii haimhusu aliyetoka manii mchana wa Ramadhani kwa kuota usingizini, bali ataoga tu na Saumu yake haina dosari.

Udhuru wa kutokwa damu ya hedhi ukitokea japo bado kidogo tu magharibi kuingia Saumu yako itakuwa batili, na hivyo basi utalazimika kuirudia.

Kuteta katika mchana wa Saumu na hatimaye kupigana ni jambo baya sana na hasa kwa kuwa mwezi huu ni wa kusameheana, kuhurumiana n.k. Pindi ufungapo unapomuona mtu yeyote akikuka bili na upuzi wowote ule, sema: "INNII SAAIM", yaani: HAKIKA YANGU MIMI NIMEFUNGA na ukifanya hivyo utakuwa umeukimbia uovu wote ambao huletwa ns shetani.

Kutengua Saumu kwa jambo lolote la haramu kama kuzini, kulewa, na kadhalika, adhabu yake ni:

  1. Kulipa siku 60 kwa siku mmoja iliyotenguliwa;
  2. Kuwalisha maskini 60;

(c) Kumwacha huru mtumwa;