rudi maktaba > Fiqh > Yaliyomo >

Jichagulie Mwenyewe

Sote tukiwa Waislamu haliisi na walio na gheri juu ya dini yetu tunapaswa kujihifadhi na kuutambua umuhimu wa uwajibu wetu. Katika Saumu hii ambayo huendelea nayo kila mwaka, tunapaswa kutambua kwamba wafungao wako makundi tofauti kadha wa kadha.

  1. Wako watu ambao wao ni vijana wa Kiislamu, lakini kwa bahati mbaya wao hawajali na wala hawafungi kamwe wakidai eti kufunga kulianzishwa na Masheikh waliokuwa hawana chakula, na kwamba mtu aliye na chakula kufunga ni kama upumbavu.
  1. Wapo watu wafungao lakini wao hufungana kujizuia chakula tu na kutotangamana na wake michana ya Ramadhani, ama katika mambo mengine wao huwa hawajali; kama kusengenya, kusema uongo, na kadhalika, huku wakiwa wamejisahaulisha kuwa hayo ni miongoni mwa yafuturishayo.
  2. Kundi jengine hufunga na kufanya baadhi ya yatakikanayo, lakini huwa wao ni wenye kukereka na Saumu, na huwa wao ni wenye kuomba na kutaka Saumu imalizike haraka.
  3. Hufunga tena kwa unyenyekevu na hushinda misikitini, lakini ufikapo usiku ama Ramadhani imalizikapo, huanza vioja na kuanza upya kuyarejelea yaliyokuwa marufuku nyakati za Ramadhani, basi watu wa namna hii, ni sawa na mtu aliyeweka akiba ya Sh. 50/- asubuhi, ili zimfae baadaye atakapopatwa na dhiki ya ghafla, na ufikapo usiku huzitumia zote katika starehe zisizo za lazima na kutobakisha kitu.
  4. Wa mwisho, ni wale wafungao kwa Imani kamili na baada ya Ramadhani kumalizika wanaendelea na majonzi ya kusikitika kwani hawajui kama watajaaliwa tena kuifikia Ramadhani nyengine. Kundi hili ndilo la wafungao kikweli wajulikanao kama "MOOMINOON" Yaani waumini halisi.

Ndugu mpendw, unatakiwa kujikagua ili ujuwe kundi ulimo hivi sasa, la sivyo, kiri kutojitambua wewe mwenyewe.

Tunawatakieni nyinyi na sisi mwisho mwema ili tufungapo tuimalize Saumu kwa baraka na amani ili iishapo tuwe kuendelea na utu wetu.