rudi maktaba > Fiqh > Yaliyomo >

UTANGULIZI

Kwa mara ya kwanza baada ya maombi mengi kutufikia, tumefanikiwa kuyakusanya yaliyokuwa sahali kwetu juu ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kijitabu hiki kilicho mbele yako, ewe msomaji mtukufu, ni sehemu isiyo tofauti na mafunzo ya Islamu juu ya haki ya Mwislamu kwa nduguye Mwislamu.

Hapo awali, tuliyakusanya baadhi ya makala na kuyaweka katika kijigazeti tulichokiita 'HIDAYA YA RAMDHANI' lakini baada ya kukabiliwa na maombi mengi kutoka kote katika Jamhuri na kwingineko tumeamua kugeuza tirazi kwa kutengeneza kijitabu hiki ambacho ni rahisi kwa kila mmoja wetu kukihifadhi kwa matumizi ya kila mwaka.

Tunataraji Waislamu wote watanufaika kwa yaliomo, Inshaalah.

Ductoor A. Kadir Sudi
20th June, 1981 A.D.
17th Shaban, 1401 A.H.