UDHU NA NAMNA YAKE

KWANZA:utaosha vitanga vya mikono mara tatu,na ni sunna kusema Bismillahi-rahamani rahim,kisha utasukutua mara tatu na kupandisha maji puani mara tatu .matendo hayo ni sunaa.

PILI: utatia nia ya udhu,na NIA ni lazima iambatane na uoshaji wa uso,au wakati wa kuosha vitanga vya mikono,na ni lazima nia hiyo iendele hadi mwisho wa udhu,na katika NIA utasema kama ifuatavyo: (nina tawaza kwa ajili ya kudiweka karibu na Mwenyezi Mungu ) kisha utaosha uso kwa kuanza kwenye maoteo ya nywele hadi chini ya kidevu,(huo ni urefu)na upana ni kati ya kidole gumba na kidole cha kati .Na ni sunna kusema ((Allahumma bayyidh wajhi yawma tas`waddul-wujuuh wala tusawwid wajhi yawma tabyadhul wujuuh)).

TATU: utaosha mkono wa kulia kwa kuanzia kwenye kiwiko hadi ncha za vidole.Na ni sunna kusema:((Allahumma aatwiniy kitabiiy biya minniy,walkhulda fil-jinani biya sariy,wa haasibni hisaban yasiraa))

NNe Utaosha mkono wa kushoto kama ulivyofanya kwa mkono wa kulia.na ukiosha mkono wa kushoto utasema:((Allahumma laa tuutwiniy kitabiy bishimaliy wala min waraa-adhahriy wala taj-alha magh-luulatan ila unukiy,wa audhubika min mukatwa'ati niiraan.))

TANO: Kisha utapaka mbele ya kichwa (utosini)kwa unyevu nyevu wa mkono wako wa kulia,na ni sunna kusema ((Allahuma ghashiniy rahmataka wabarakatika))

SITA: Utapaka juu ya mguu wa kulia (juu ya unyayo)na ni sunna kusema ((Allahumma thabbitiniy ala swiratika yawma tazaillu fihil-akdaam,waj'al saayiy fiyma yurdhwika anniy yadhal-jala`ali wal-ikraam)).

SABA: kisha utapaka juu ya mguu wa kushoto (juu ya unyayo)na ni sunna kusema ((Allahumma thabbitiniy ala swiratika yawma tazaillu fihil-akdaam,waj'al saayiy fiyma yurdhwika anniy yadhal-jala`ali wal-ikraam)).

Na ukimaliza utasema :((Allahumma inniy as-aluka tamamal-wudhuu,wa tamama swalaa,wa tamama ridhiwaanika wal-janna)).