hukumu za udhu

Udhu huwajibika kwa kutokwa na haja ndogo,au haja kubwa,au kutokwa na upepo katika sehemu ya kawaida,na huwajibika kutokana na usingizi au kulala,na mfano wa hayo, kama kuwa na wazimu, kuzimia,na kwa Istihadha ndogo.Na udhu hauwi wajibu tofauti na mambo haya tuliyo yataja, na huwa ni wajibu kutawadha pale ambapo mtu amekusudia kufanya matendo ambayo kufanywa kwake ni sharti mtu awe na twahara kama kusali,na ni moja wapo kati ya vitangulizi vya sala, kwa maana ya kuwa haisihi sala bila ya kuwa na udhu.Na udhu umegawanyika katika matendo ya aina mbili:

1-Matendo ya wajibu.

2-Matendo ya sunna.

SEHEMU ZA WAJIBU KATIKA UDHU

Sehemu za wajibu katika udhu ni nne:

1-Kuosha uso.

2-Kuosha mikono miwili.

3-Kupaka kichwa

4-Kupaka miguu miwili.

Ufafanuzi :

1) KUOSHA USO:

Niwajibu kuosha uso kwa kuanzia kwenye maoteo ya nywele hadi chini ya kidevum na huu ni urefu, na upana ni kati ya kidole gumba na kidole cha kati huu ndio upana wa uso,na sehemu iliyo njeya hapo kisheria haihesabiwi kuwa ni katika uso.Japo kuwa si vibaya kuzidisha sehemu iliyo tajwa.Na niwajibu kwa ihtiyatti

Katika kuosha kuanzia juu ya uso hadi chini.

2) KUOSHA MIKONO MIWILI:

Ni wajibu kuosha mikono miwili kwa kuanzia kwenye viwiko hadi kwenye ncha za vidole,na ni wajibu katika uoshaji kuanzia kwenye viwiko na kuelekea chini hadi kwenye ncha za vidole.

3) KUPAKA KICHWA:

Ni wajibu kupaka(mas,hi), sehemu ya mbele ya kichwa ,(utosini)nayo ni sehemu ya mwanzo ya kichwa iliyo karibu na paji la uso,na utapaka kichwa kwa unyevu nyevu ulio bakia kwenye mikono baada ya kuosha mikono,na nisunna kupaka kutumia vidole vitatu vilivyo unganishwa, na huo ni upana wa kichwa,na urefu ni kiasi cha urefu wa vidole vya mikono. Kama ambavyo ni sunna katika upakaji kuanzia juu hadi chini na hupaka kwa kutumia kiganja chia mkono wa kulia .

4) KUPAKA MIGUU MIWILI:

Ni wajibu kupaka miguu miwili kwa kuanzia kwenye ncha za vidole hadi kwenye sehemu ya juu ya maungio ya miguu(kaabaini)na (kaab)ni maungio kati ya unyayo na muundi wa mguu kwa kauli iliyo dhahiri.Na ni bora zaidi kutanguliza mguu wa kulia kabla ya mguu wa kushoto,na hupakwa mguu wa kulia kwa mkono wa kulia na mguu wa kushoto kwa mkono wa kushoto, japo kuwa inajuzu kutofautisha.

MASHARTI YA KUSIHI KWA UDHU

Ili udhu uwe sahihi ni lazima yazingatiwe masharti ya fuatayo:

1) KUANZA :

Utwaharaji wa maji: yaani ni sharti maji ya kutawadhia yawe twahara.

2) YAWE MUTLAQ:

Yasiwe yamechanganywa na chochote yaani yawe maji halisi.

3) UTWAHARA WA VIUNGU VYA UDHU :

Nisharti katika kutawadha viungo vya udhu visiwe najisi.

4) UHALALI WA MAJI:

Nisharti maji ya kutawadhia yawe halali ya siwe ni ya kuiba au kunyanganya(maghsub).

5) KUSIWE NA KIZUIZI KATIKA UTUMIAJI WA MAJI:

Nisharti kusiwe na kizuwizi cha kuzuwiya kutumia maji kama ugonjwa usababishao madhara ikiwa mtu atatumia maji.

6) NIA (kunuwia):

Nayo ni kukusudia kufanya tendo la udhu kwa lengo la kufanya ibada na kwa kujikaribisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.Na ni lazima kuendelea nia hiyo na kufanya matendo yote ya udhu kwa msingi wa nia hiyo.

7) KUTO SAIDIWA KATIKA UDHU :

Ni lazima kila mtu kuyatekeleza matendo ya udhu yeye mwenyewe kama kuosha na kupaka,lau kama mtu mwingine atamtawadhisha au kushirikiana nae udhu utabatilika,Ama ikiwa hakuweza kutawadha yeye mwenyewe isipokuwa kwa kupata usaidizi itajuzu kufanya hivyo na itakuwa ni juu yake kutia nia.

8) KUFUATANISHA:

Ni kufuatanisha katika uoshaji na upakaji ,kwa maana ya kuosha au kupaka kiungo kifuatacho kabla ya kilicho tangulia kukauka. Na ikiwa atachelewesha hadi viungo vyote kukauka udhu una batilika.

9) MPANGILIO KATI YA VIUNGO:

Ni lazima kupangilia katika viungo vya udhu,kwa kutanguliza uso kisha mkono wa kulia kisha mkono wa kushoto,kisha kupaka kichwa na kumalizia kwa kupaka miguu. Na nivizuri zaidi kuanza kwa kupaka mguu wa kulia kisha mguu wa kushoto.

MAMBO YA SUNNA KATIKA UDHU

Ni sunna katika udhu kuosha vitanga viwili kabla ya kuvingiza kwenye chombo cha maji mara tatu,na chombo cha kutawadhia kiwe upande wa kulia, na kuchota maji kwa kutumia chombo hicho,na kusema bismillahi,na kusukutua kinyani,na kuweka maji puani, na utafanya hivyo mara tatu.Na ni sunna kuosha mara mbili mbili kwenye sehemu za wajibu,na kusoma dua maalum katika kila tendo.

NAMNA YA KUTAWADHA

Baada ya kukamilika masharti ya udhu kama tulivyo eleza utaanza udhu kama ifuatavyo:

KWANZA:utaosha vitanga vya mikono mara tatu,na ni sunna kusema Bismillahi-rahamani rahim,kisha utasukutua mara tatu na kupandisha maji puani mara tatu .matendo hayo ni sunaa.

PILI: utatia nia ya udhu,na NIA ni lazima iambatane na uoshaji wa uso,au wakati wa kuosha vitanga vya mikono,na ni lazima nia hiyo iendele hadi mwisho wa udhu,na katika NIA utasema kama ifuatavyo: (nina tawaza kwa ajili ya kudiweka karibu na Mwenyezi Mungu ) kisha utaosha uso kwa kuanza kwenye maoteo ya nywele hadi chini ya kidevu,(huo ni urefu)na upana ni kati ya kidole gumba na kidole cha kati .Na ni sunna kusema ((Allahumma bayyidh wajhi yawma tas`waddul-wujuuh wala tusawwid wajhi yawma tabyadhul wujuuh)).

TATU: utaosha mkono wa kulia kwa kuanzia kwenye kiwiko hadi ncha za vidole.Pia utaosha mkono wa kushoto kama ulivyofanya kwa mkono wa kulia.Na ni sunna kusema :((Allahumma aatwiniy kitabiiy biya minniy,walkhulda fil-jinani biya sariy,wa haasibni hisaban yasiraa)) ,na ukiosha mkono wa kushoto utasema:((Allahumma lau tuutwiniy kitabiy bishimaliy wala min waraa-adhahriy wala taj-alha magh-luulatan ila unukiy,wa audhubika min mukatwa'ati niiraan.))

NNE: Kisha utapaka mbele ya kichwa (utosini)kwa unyevu nyevu wa mkono wako wa kulia,na ni sunna kusema ((Allahuma ghashiniy rahmataka wabarakatika))

TANO: Kisha utapaka juu ya miguu miwili (juu ya ungayo)na ni sunna kusema ((Allahumma thabbitiniy ala swiratika yawma tazaillu fihil-akdaam,waj'al saayiy fiyma yurdhwika anniy yadhal-jala`ali wal-ikraam)).

Na ukimaliza utasema :((Allahumma inniy as-aluka tamamal-wudhuu,wa tamama swalaa,wa tamama ridhiwaanika wal-janna)).