JINSI  YA KUTAYAMMAM

  

 Picha no (1)  Hatua ya kwanza uta andaa mchanga wa kufanyia tayammam kama inavyo onekana katika picha namba moja.

   Picha no (2)  Kisha utaweka mikono juu ya mchanga au utapiga juu yake kama inavyo onekana katika picha namba mbili.

 

 Picha no (3)  Kisha utapaka paji la uso kwa kuanzia kwenye maoteo ya nywele kama inavyo onekana katika picha namba tatu, na uhakikishe umepaka paji lote la uso   kwa  upande wa kulia na kushoto.

 

Picha no (4)  katika kupaka utateremsha mikono hadi kwenye ncha ya pua  na utamalizia kwa kutumia ncha za vidole vidogo vya mwisho vya mikono.

 

Picha no (5)  Kisha utapaka mkono  wa kulia kwa kuanzia kwenye  zand  (maungio ya kitanga cha mkono) kama inavyo onekana  katika picha  namba tano na utapaka kwa kutumia mkono wa kushoto. 

  

 Picha no (6)  utapaka mkono   kwa kuanzia kwenye zand kama tulivyo eleza hapo juu na utamalizia kwenye ncha za vidole kama inavyo onekana katika picha namba sita.

 

  Picha no (7)  Baada ya kupaka mkono wa kulia utapaka mkono wa kushoto, na utafanya kama ulivyo fanya  kwenye   mkono wa kulia kwa kuanzia kwenye zand  kama inavyo onekana katika picha namba saba na utatumia mkono wa kulia.

 

 Picha no (8)  Utapaka mkono wa kushoto kwa  kuanzia kwenye zand  kama inavyo onekana katika picha namba saba na utamalizia kwenye ncha za vidole kama ionekanavyo hapo juu.  Na hapa tayammam itakuwa imemalizika.

Kama tulivyo elezea hapo kabla ya kuwa ni sunna  kupigapigo la pili kwa ajili ya kupaka mikono.