SALA YA IJUMAA NA NAMNA YAKE.

Sala ya ijumaa ina rakaa mbili kama sala ya asubuhi, Ndio, inatofautiana  na sala ya asubuhi kwa kuwa sala ya ijumaa hutanguliwa na  khutuba mbili kabla ya yake, katika  khutuba ya kwanza khatibu husimama na kumsifu mwenyezi mungu  na kumhimidi na kuwausia watu kumcha mwenyezi mungu  na husoma sura fupi  katika  kitabu cha Allah kisha hukaa kidogo, na katika khutuba ya pili husimama na kumhimidi mwenyezi mungu na kumsifia na kumsalia mtume mohammad na kuwasalia maimamu wa waisilaam, na kauli ya ahwati inasema huongeza  kuwaombea msamaha waumini wa kike na kiume.

Mas’ala: Kauli ya ahwat  nikuwa  kumhimidi mwewnyezi mungu na kumsalia mtume katika khutba hutasoma kwa lugha ya  kiarabu, ama  sehemu iliyo bakia kama kumsifia Allah na kuusia kumcha mungu inajuzu kutumia lugha yoyote ilejapo kuwa inajuzu kuisoma kwa kiarabu pia, ama kauli ya ahwati ni kuwa ikiwa  wasio fahamu lugha ya kiarabu  kati ya watu walio hudhuria ni wengi zaidi basi itatumika lughu wanayo ifahamu.

Mas’ala:  Sala ya ijumaa ni wajibu takhyiir  (wajibu wa khiari) kwa kauli ya adh’har, yaani mtu  (mukallaf) siku ya ijumaa anayo hiyari ima kusali sala ya ijumaa kama  ikitimiza masharti  yafuatayo, na kati ya kusali sala ya adhuhuri lakini kusali sala ya ijumaa ni bora zaidi, na ikiwa ataisali sala ya ijumaa kwa masharti  yake haitakuwa na haja ya kusali sala ya Adhuhuri.

Mas’ala: Huzingatiwa katika sala ya ijumaa ya kuwa iswaliwe kwa jamaa, kwa hivyo haita swihi kuisali furada  (bila jamaa)

Mas’ala: Ni shartui katika  jamaaya sala ya ijumaa  kutimia idadi maalum nayo ni watu watano mmoja wao akiwa imam,  kwa hivyo basi haita kuwa wajibu sala ya ijumaa ikiwa haikutimia watu watano (waisilaaam) mmoja wao akiwa imam.

Mas’ala:  Pia ni sharti kuwa kweke wajibu kuwepo imama alie kusanya masharti ya kuwa imama au ya uimam kama uadilifu na mengineyo kati ya masharti yazingatiwayo kwa imam wa jamaa, kwa ivyo basi haita wajibika  sala ya ijumaa ikiwa hapakuwa na imam alie timiza masharti ya uimam.

Mas’ala: Huzingatiwa katika kusihi kwa sala ya ijumaa katika mji fulani au nchi fulani kusiwe na umbali kati ya ijumaa na ijumaa nyingine chini ya  farsakh (kilo meta) moja,  lau kama itasaliwa sala nyingine ya ijumaa  katika sehemu ambayo umbali wake ni chini ya farsakh (kilo meta) moja  sala zote mbili zita batilika ikiwa zitasaliwa kwa wakati mmoja bila kupishana, ama ikiwa moja wapo imeitangulia  nyingine hata kama ni kwa takbira ya ufunguzi, itaswihi ile iliyo tangulia na iliyo fuatia itabatilika.

Mas’ala: Kusaliwa sala ya ijumaa sehemu fulani inazuwia kusaliwa sala nyingine katika masafa kama hayo (umbali huo)  ikiwa ni sahihi na imekusanya masharti, ama ikiwa haiku tyimiza  masharti  kauli ya karibu ni kuwa haita zuwia.

Mas’ala:  Kuisali sala ya ijumaa katika mji ikiwa imetimiza  masharti na  ikawa alie isalisha ni imamul hujja (a.s) au anae muwakilisha,  wakati huo itakuwa ni wajibu  kwa kila mtu kuhudhuri na sio khiari tena, na ikiwa  alie isalisha sio imam, wakati huo haita kuwa wajibu kuhudhuria  kwa kauli iliyo adh’har bali inajuzu kusali sala ya adhuhuri.

Mas’ala: Si wajibu  kwa mwanamke wala mtumwa  wala msafiri  kuhudhuria katika sala ya ijumaa- hata kama ni wajibu kwake kukamilisha sala- na wala si wajibu kwa mgonjwa, kipofu,  mtu mzima, (mzee au kikongwe) wala kwa mtu ambae nyumba yake na sehemu inapo saliwa sala ya ijumaa kuna umbali wa zaidi ya  farsakh mbili, wala kwa yule ambae kuhudhuria kwake  kuna matatizo kama kukiwa na mvua au baridi na mfano wa hayo, kwa hivyo wote hawa si wajibu kwao kuhudhuria sala ya ijumaa hata  kama tukijaalia  kuwa ni wajibu au lazima kuhudhuria kama tulivyo fafanua hapo kabla katika mas’ala yaliyo tangulia.

SALA ZA SUNNA ZA KILA SIKU.

     Mas’ala:    Ni sunna kila siku kusali sala za sunna  usiku na mchana na idadi yake ni rakaa thalathini na nne:

1- Rakaa nane kabla ya sala ya adhuhuri kwa ajii ya adhuhuri. 2- Na rakaa nane kabla ya sala ya alasiri kwa ajili ya alasiri. 3- Rakaa nne baada ya sala ya magharibi kwa ajili ya magharibi. 4-  Rakaa mbili baada ya sala ya ishaa na husaliwa kwa kukaa na huhesabiwa kuwa ni  rakaa moja. 5-  Rakaa nane za sala ya usiku, na wakati wake ni kuanzia katikati ya usiku  kwa kauli iliyo mashuhuri na wakati wake huendelea hadi inapo chomoza alfajiri ya kweli, na bora zaidi ni kuisali mwishoni  mwa usiku. 6- Baada ya sala ya usiku husaliwa  rakaa mbili za shaf’i  na baada ya shaf’i husaliwa rakaa moja ya witri,  na rakaa mbili kabla ya sala ya alfajri,  na  inasemekana kuwa wakati wa kuanza kwake ni sawa na wakati wa sala ya usiku- baada ya kupita muda umtoshao mtu kuitekeleza- na huendelea  hadi linapo karibia kuchomoza jua.

Mas’ala:  Sala zote za sunna husaliwa rakaa mbili mbili – isipo kuwa sala ya witri, kwani sala hiyo ina rakaa moja- na nisunna kusoma kunuut katika sala hiyo, na ina faa kusoma al hamdu tu bila kusoma sura nyingineyo kama ambavyo inajuzu kusali baadhi tu ya sala hizo, bali inafaa katika sala ya usiku kusali sala ya shaf’i  pekee na witri au witri pekee,  na katika sunna ya alasiri waweza kutosheka kwa kusali rakaa nne tu, na ikiwa mtu atataka kutenganisha katika sehemu tofauti na hizi tulizo zitaja kauli ya ahwat ni kuwa utazisali kwa malengo ya kujikurubisha kwa mola tu hata kama  ni suna za magharibi ikiwa atataka kuzisali rakaa mbili.

Na kauli ya ahwat ni kuwa katika sala ya witri katika kunuut utasoma dua ifuatayo:  

((لا اله الا اللّه الحليم الكريم لا اله الا اللّه العلى العظيم سبحان اللّه رب الـسموات السبع و رب الارضين السبع و ما فيهن و ما بينهن و رب العرش العظيم و الحمد للّه رب الـعـالمين و صلى اللّه على محمد و آله الطاهرين ))

((Laa ilaha illa llaahul haliimul kariim, laa ilaha illa llahul aliyyul adhiim, subhana llahi rabbis samaawatis sab’i wa rabbil aradhwiinas sab’i wa maa fiihinna wama baina hunna warabbil arshil adhiim, wal hamdu lillahi rabbil aalamiin waswalla llahu alaa Muhammadin wa aalihi twahiriin)) 

Na inabidi kuwaombea waumini arobaini, na atasema: Astaghfiru llah rabbiy wa atubu ilayhi mara mia moja, na atasema pia: Hadhaa maqamul aaidhi bika minan   nnaar mara saba, kisha atasema: al af’wu  mara mia tatu.

Mas’ala: Katika safari sala za sunna za adhuhuri na alasiri huporomoka, na zilizo bakia hubakia  yaanihaziporomoki, na kauli iliyo awlaa ni kuwa atasali sunna ya baada ya isha kwa kutaraji kupata thawabu.

Mas’ala: Sala ya ghafira  ina rakaa mbili  na sala hii husaliwa kati ya sala ya magharibi na isha, katika rakaa ya kwanza  baada ya al hamdu husomwa  aya ifuatayo:                                                                                                                                    

((و ذا الـنـون اذ ذهب مغاضبا فظن ان لن نقدر عليه فنادى فى الظلمات ان لا اله الا انت سبحانك انى كنت من الـظـالـمـيـن فاستجبنا له و نجيناه من الغم و كذلك ننجى المومنين))

Na katika rakaaya pili baada ya al hamdu aya ifuatayo:

وعنده مفاتيح الغيب لا يعلمها الا هو و يعلم ما فى البر و البحر و ما تسقط من ورقه الا يعلمها و لا حـبه فى ظلمات الارض و لا رطب و لا يابس الا فى كتاب مبين))

 Kisha atasoma kunuut na atasema:

اللهم انى اسالك بمفاتح الـغـيـب الـتـى لا يـعلمها الا انت ان تصلى على محمد و آل محمد

      Kisha ataomba haja zake na kusema:

اللهم انت ولى نـعمتى و القادر على طلبتى تعلم حاجتى فاسالك بحق محمد و آله عليه و عليهم السلام لما قضيتهالي))

 Na inajuzu  huzihesabu rakaa mbili hizi kuwa ni katika sunna za magharibi.