SALA NA NAMNA YA KUSALI

1.NIA :

Tumekwisha elezea katika udhu kuhusu nia ya kuwa ni kukusudia kufanya kitendo au kusali kwa ajili ya kuwa karibu na Mwenyezi Mungu na kujikurubisha kwake,na inatosha kukusudia kwa ujumla bila kuanisha kuwa ni faradhi au sunna adaa au kadhaa na haizingatiwi kuwa ni lazima utamke nia hiyo bali inatosha kukusudia kimoyo.Na huzingatiwa Ikhlas katika nia .ikiwa nia hiyo itachanganyika na riyaa(kutaka kujionyesha au kuonekana)sala inabatilika iwe ya faradhi au sunna.

2. TAKBIRATUL-IHRAM(takbira ya ufunguzi) :

Na huitwa kwa jina lingine takbira ya ufunguzi nayo ni kama ifuatayo:(Allahu akbar) na haifai kutumia neno lingine mfano wa hilo katika lugha ya kiarabu wala kutumia tafsiri yake,na ikikamilika mambo ambayo hubatilisha sala huwa ni haramu kuyafanya.Nayo ni ruknu .Sala itabatilika kwa kukosekana kwake kwa makusudi au kwa kusahau.

3.AL-QIAM(kusimama):

Kusimama ni ruknu wakati wa kusoma Takbiratul-Ihraam,vile vile wakati wa kwenda katika rukuu,nacho ni kisimamu kilicho ungana na rukuu ,kwa mfano mwenye kutoa Takbiratul-Iharam hali ya kuwa amekaa sala yake inabatilika,au akirukuu hali ya kuwa amekaa kwa kusahau.

4.AL-QIRAA-A(kisomo):

Ni wajibu katika sala ya faradhi au sunna katika rakaa mbili za mwanzo kusoma suratul-Fatiha(al-hamdu),na nilazima hasa katika sala ya faradhi kusoma sura kamili baada ya Al-hamdu.

Na ni lazima usomaji uwe ni sahihi kama kanuni za tajwid zinavyo tutaka kusoma.

Bismil-lahir-rahmanir-rahim.
alhamdu lillahi rabbil-a'lamin.
ar-rahmanir-rahim.
maliki yawmid-din.
iyyaka na'budu wa iyyaka nasta'in
ihdinas-Siratal-mustaqim.
Siratal-ladhina an 'amta alayhim
gayril-magdubi alayhim walad-dalin.

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.

بسم الله الرحمن الرحيم

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote;

الحَمْدُ لله ربّ ِ العَالمَيْن

Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu;

الرَّحمن الرَّحيم

Mwenye Kumiliki Siku ya Malipo

مالِكِ يَوْمِ الدّين

Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada.

إيّاك نَعْبُدُ وإيّاك نَسْتَعين

Tuongoe njia iliyo nyooka,

إهْدِنا الصّراطَ المُسْتَقِيم

Njia ya ulio waneemesha, siyo ya walio kasirikiwa, wala walio potea.

صِراطَ الذَّينَ أنْعَمْتَ عَلَيْهِم غَيرِ المغْضُوب عَلَيهم ولا الضّاليْن

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.

بسم الله الرحمن الرحيم

Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee

 

قُلْ هُوَ الله أحَدٌ

Mwenyezi Mungu Mkusudiwa.

اللهُ الصَّمَد

Hakuzaa wala hakuzaliwa.

لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ

Wala hana anaye fanana naye hata mmoja.

وَلَمْ يَكُنْ لَّهُ كُفُواً أحَدْ

5.RUKUU:

Rukuu ni wajibu mara moja katika kila rakaa,sawa iwe sala ya wajibu au sunna,kama ambavyo ni ruknu hubatilika sala kwa kukosekana rukuu kwa makusudi au kwa kusahau,pia sala hubatilika kwa kuzidi rukuu kwa makusudi au kwa kusahau.Na niwajibu katika rukuu mambo yafuatayo:

1.Kuinama kwa unyenyekevu hadi ncha za vidole kufikia kwenye magoti.

2.Kusoma dhikri kama ifuatavyo:((subhana rabiyal-adhimi wabihamdihi))au waweza kusoma:((subhanallah))mara tatu.Na sharti kuisoma kwa lugha ya kiarabu,na kufuatanisha na herufi kuzisoma vizuri,na kutobadilisha haraka zake.

سُبْحَانَ رَبّيَ العَظِيم وَبِحَمْدِه

3.Kubakia kwa muda na kutulia kwa ajili ya kusoma dhikri.

4.Kuinuka na kusimama kwa muda akiwa ametulia.

5.Na anapo simama atasema:((samiallahu liman hamidahu)).

6.SUJUUD(sijda):

Ni wajibu sijda mbili katika kila rakaa moja,na sijda zote mbili kwa pamoja ni ruknu(nguzo) katika sala ikiwa zitakosekana kwa pamoja sawaa kwa makusudi ao kwa kusahau au zikizidi sala itabatilika,na haitabatilika ikiwa itapungua moja wapo au kuzidi moja wapo.

Kusoma dhikri kama alivyo tangulia kwenye rakaa isipo kuwa kwenye sijda utasoma dhikri ifuatayo: ((SUBHANA RABIYAL-AALAA WABIHAMDIHI)) mara tatu.  

سُبْحَانَ رَبّيَ الأعْلى وَبِحَمْدِه

Kubakia na kutulia kwa ajili ya kusoma dhikri ya wajibu,kama ilivyo tangulia kwenye rukuu.

QUNUT

Qunut ni wajibu katika sala zote,sawa ziwe za faradhi au sunna,na imetiliwa mkazo na kusisitizwa sana kwenye sala za jahri,(sala zisomwazo kwa kupaza sauti)hasa sala ya asubuhi, sala ya ijumaa,na sala ya maghrib.Na qunut husomwa baada ya kusoma Al-hamdu na sura katika rakaa ya pili na kabla ya rukuu,isipokuwa katika sala ya ijumaa, kwani sala ya ijumaa inakunuti mbili ya kwanza kabla ya rukuu katika rakaa ya kwanza ,na ya pili baada ya rukuu katika rakaa ya pili.

Na ni sunna kwenye kunuti kusoma dua ifuatayo: ((Laailaha illa llahul-halimul-karim,Laailaha illa llahul-aliyul-adhim,subhanallahi rabbis-samawatissab-I,warabbul-ardwina ssabb-I,wamafihinna wama bayna hunna,warabbul-arshil-adhwiim,wal-hamdu Lillahi rabbil-aalamiin)).

Rabbana atin-a fiddunya hasanah
wa fil akherati hassanah.
Wa qina adhab an nar.

رَبّنا آتِنا في الدُّنيا حَسنَةً وفي الآخِرَةِ حَسنَةٍ وقِنا عَذابَ النّار

7. TASHAHUD:(kushudia)

Tashahud ni wajibu mara mbili katika sala yenye rakaa nne au tatu ya kwanza baada ya kumaliza rakaa mbili za mwanzo na baada ya kumaliza na kuinua kichwa kutoka kwenye sijda ya mwisho ya rakaa ya pili na tashahudi ya pili husomwa baada ya kuinua kichwa kutoka kwenye sijda ya mwisho katika rakaa ya mwisho ya kila sala,nayo ni wajibu na si ruknu,akiacha mtu kwa makusudi sala inabatilika,na akiiacha kwa kusahau itambidi kuitekeleza.

Na katika tashahud husemwa maneno yafuatayo:

( (Al hamdu lillah: ((Bismillahi wabillahi wal-hamdulillahi,wa khairul-asmaai lillahi,au wakhairul-asmail-husna kallaha lillah,Ash-hadu anlaa ilaha illa llah wahdahu la sharika lahu,wa-ash-hadu anna mohamma`dan abdahu warasuluhu allahumma swali ala muhammadin wa-alii mohammad)).

أشهدُ أن لا إله إلاّ اللهُ وحدَهُ لا شريكَ لَهُ

وأشهَدُ أنَّ محمّداً عبدُهُ ورسولُه، اللهم صلّي على محمد وآل محمد

Na wakati wa tashahud nilazima iwe juu ya mapaja,na baada ya kusmaliaaaa mtume utasema ((Watakabbal-shafaa-atahu war-faa daraja tahu)) hii ni katika tashahud ya kwanza,na wakati anapo simama atasema ((Bihauli llahi waquwaatihi aqumu wa ak'udu))na wakati wa kusimama inambidi mwanamke kuya ambatanisha mapaja yake kwa ajili ya kusimama.

Ama katika sala ya adhuhuri,alasiri au magharibi na isha,baada ya tashahudi ya mwanzo hutatoa salam bali utasimama kwa ajili ya rakaa ya tatu na utasema:((Bihauli llahi waquwwatihi akuumu wa akuudu)).Na katika rakaa ya tatu utasoma tasbihi mara tatu nayo ni kama ifuatavyo:

((subhana llah wal-hamdu lillahi wa lailaha illa llahu allahu akbar))mara tatu kisha utarukuu na kusema maneno yale yale kama ilivyo tangulia.

سُبحانَ الله والحَمدُ لله ولا إلهَ إلاّ الله واللهُ أكْبر

Baada ya rukuu utasujudu sijda mbili na baada ya kumaliza utasimama tena kwa ajili ya rakaa ya nne na utafanya vile vile kama ulivyo fanya kwenye rakaa ya tatu.

Baada ya kumaliza sijda mbili za mwisho katika rakaa ya nne,utasoma tashahud na kutoa salam,na sala itakuwa imemalizika .Na ni sunna kutao takbir mara tatu kwa kusema:((Allahu akbar))

8.SALAM:

Ni wajibu kutoa salam katika kila sala na ndio tendo la mwisho katika sala na baada ya salam tayari mtu anakuwa ametoka kwenye sala na anaweza kufanya chochote alicho katazwa akiwa kwenye sala.

Na salam ina mifano miwili:

Mfumo wa kwanza: ((Assalaam alayna wa ala abadi llahi swalihina))

Mfumo wa ya pili: ((Assalaam alay kum))na uta ongeza ((warahma tullahi wabara katuhu))ama kauli isemayo ((Assalaam alayka ayyuhannabiyu warahmatullahi wabarakatuhu))si katika mfumo wa salam ya wajibu bali ni sunna.

Na nilazima kuisoma salam kwa kiarabu kama ambavyo ni wajibu kusomwa kwa kukaa na kwa utulivu.

السّلامُ عليكَ أيُّها النّبي ورحمةُ اللهِ وبركاته

السّلامُ عَلينا وعلى عِباد الله الصّالحِين

السّلامُ عليكُم ورحمةُ اللهِ وبركاتُه