SALA NA NAMNA YA KUSALI

Sala ni moja kati ya nguzo ambazo uislam umejengewa juu yake,ikikubaliwa matendo mengine nayo hukubaliwa,na ikikataliwa matendo mengine nayo hukataliwa.

Na sala ni za aina mbili

Sala za faradhi.(wajibu)

2. Sala za sunna

1.SALA ZA FARADHI ZA KILA SIKU NI TANO :

A. Swalatus -subhi : sala ya asubuhi au ya al-fajri nayo ina rakaa mbili

B. Swalatudh

C. -dhuhri (sala ya adhuhuri) ina rakaa nne

D. Swalatul- asri (sala ya alasiri) nayo ina rakaa nne.

E. Swalatul -maghribi (sala ya magharibi) ina rakaa tatu.

F. Swalatul- isha (sala ya isha ) ina rakaa nne

2. SALA ZA SUNNA

Ama sala za sunna ni nyingi sana na muhimu zaidi ni sunna ziswaliwazo kila siku kabla ya sala au baada ya sala,nazo nikama zifuatazo:

1.Rakaa nane kabla ya sala ya adhuhuri ni kwa ajili ya adhuhur.

2.Rakaa nane baada ya adhuhuri na kabla ya sala ya alasiri kwa ajili ya sala ya alasiri.

3.Rakaa nne baada ya sala ya magharibi kwa ajili ya magharibi.

4.Rakaa mbili : huswaliwa kwa kukaa na huzingatiwa kuwa ni rakaa moja kwa kusimama, nazo husaliwa baada ya sala ya isha kwa ajili ya isha.

5.Rakaa nane za sala ya usiku (Swalatul laili)

6.Rakaa mbili baada ya swalatullaili (Ashafii)

7.Rakaa moja ya witri baada ya shafii .

8.Rakaa mbili za alfajiri kabla ya sala ya alfajiri.

YAZINGATIWAYO KATIKA SALA YA FARADHI:

Ili sala iwe sahihi ni lazima kuyazingatia mambo yafuatayo :

1.WAKATI: haifai kusali sala yoyote kabla ya wakati wake.

2. QIBLA: niwajibu kuelekea qibla katika sala zote na katika sehemu za sala zilizo

sahaulika pamajo na kuwepo uwezekano wa kufanya hivyo.

3.KUJISITIRI :

Niwajibu kwa hiyari kusitiri sehemu za siri. Katika sala na katika sehemu ziambatanazo na sala.Kama sehemu iliyo sahaulika au sijda ya sahau.Hata kama hakuna mtu awezae kumuangalia.au katika giza.

Na uchi wa mwanamume katika sala ni sehemu ya siri ya mbele na nyuma, na mwanamke ni mwili wake wote hata kichwa na nywele.isipo kuwa uso. Na vitanga vya mikono, na nyayo.

NGUO YA KUSALIA :

Huzingatiwa katika nguo ya kusalia mambo yafuatayo :

1. Iwe twahara.

2. Iwe ni nguo ya halali-( isiwwe ni ya kunyang`anya.).

3. Isitokane na sehemu za mzoga zenye uhai .

4. Isitokanena wa nyama ambao si halali kuliwa.

5. Isiwe nguo ya dhahabu –kwa wanaume – hata kama ni pambo. Kama pete, ama wanawake inajuzu kwao hata kama ni nguo ya dhahabu.

6. Isiwe ni nguo ya hariri halisi – kwa wanaume –na haifai kwa wanaume kuivaa hata nje ya sala kama dhahabu.

3.SEHEMU YA KUSALIA:

Haifai kusalia sahemu iliyo nyang'anywa, au kuporwa, au kusalia sehemu bila ridhaa ya mmiliki wake, sawa iwe sala ya faradhi au sunna, hata kama rakaa na sijda utazitekeleza kwa kuashiria.

MAMBO YA WAJIBU KATIKA SALA:

Mambo ya wajibu na yaundayo sala ni kumi na moja:

1.Nia.

2.Takbiratul-Ihraam.

3.Al-kiam (kusimama).

4.Kusoma.(al'hamdu na sura ).

5.Kusoma dhikri.

6.Rukuu (kurukuu)

7.Sujuud (kusujudu).

8.Tashahud (kusoma shahada).

9.Kutoa salam .

10.Mpangilio.

11.Kufuatanisha.

Kati ya vitendo hivyo kuna ambavyo arkaan (nguzo katika sala),navyo ni vitendo ambavyo vikipungua au kuzidi kwa maksudi au kwa kusahau sala hubatilika, navyo ni vitano.

1.Nia.

2.Takbiratul-Ihraam

3.Kusimama.

4.Rukuu.

5.Sujuud (sijda). Na vilivyo bakia sio ruknu(nguzo),sala haibatiliki kwa kupungua au kwa kusahau.

UFAFANUZI

1.NIA :

Tumekwisha elezea katika udhu kuhusu nia ya kuwa ni kukusudia kufanya kitendo au kusali kwa ajili ya kuwa karibu na Mwenyezi Mungu na kujikurubisha kwake,na inatosha kukusudia kwa ujumla bila kuanisha kuwa ni faradhi au sunna adaa au kadhaa na haizingatiwi kuwa ni lazima utamke nia hiyo bali inatosha kukusudia kimoyo.Na huzingatiwa Ikhlas katika nia .ikiwa nia hiyo itachanganyika na riyaa(kutaka kujionyesha au kuonekana)sala inabatilika iwe ya faradhi au sunna.

2. TAKBIRATUL-IHRAM(takbira ya ufunguzi) :

Na huitwa kwa jina lingine takbira ya ufunguzi nayo ni kama ifuatayo:(Allahu akbar) na haifai kutumia neno lingine mfano wa hilo katika lugha ya kiarabu wala kutumia tafsiri yake,na ikikamilika mambo ambayo hubatilisha sala huwa ni haramu kuyafanya.Nayo ni ruknu .Sala itabatilika kwa kukosekana kwake kwa makusudi au kwa kusahau.

3.AL-QIAM(kusimama):

Kusimama ni ruknu wakati wa kusoma Takbiratul-Ihraam,vile vile wakati wa kwenda katika rukuu,nacho ni kisimamu kilicho ungana na rukuu ,kwa mfano mwenye kutoa Takbiratul-Iharam hali ya kuwa amekaa sala yake inabatilika,au akirukuu hali ya kuwa amekaa kwa kusahau.

4.AL-QIRAA-A(kisomo):

Ni wajibu katika sala ya faradhi au sunna katika rakaa mbili za mwanzo kusoma suratul-Fatiha(al-hamdu),na nilazima hasa katika sala ya faradhi kusoma sura kamili baada ya Al-hamdu.

Na ni lazima usomaji uwe ni sahihi kama kanuni za tajwid zinavyo tutaka kusoma.

5.RUKUU:

Rukuu ni wajibu mara moja katika kila rakaa,sawa iwe sala ya wajibu au sunna,kama ambavyo ni ruknu hubatilika sala kwa kukosekana rukuu kwa makusudi au kwa kusahau,pia sala hubatilika kwa kuzidi rukuu kwa makusudi au kwa kusahau.Na niwajibu katika rukuu mambo yafuatayo:

1.Kuinama kwa unyenyekevu hadi ncha za vidole kufikia kwenye magoti.

2.Kusoma dhikri kama ifuatavyo:((subhana rabiyal-adhimi wabihamdihi))au waweza kusoma:((subhanallah))mara tatu.Na sharti kuisoma kwa lugha ya kiarabu,na kufuatanisha na herufi kuzisoma vizuri,na kutobadilisha haraka zake.

3.Kubakia kwa muda na kutulia kwa ajili ya kusoma dhikri.

4.Kuinuka na kusimama kwa muda akiwa ametulia.

5.Na anapo simama atasema:((samiallahu liman hamidahu)).

6.SUJUUD(sijda):

Ni wajibu sijda mbili katika kila rakaa moja,na sijda zote mbili kwa pamoja ni ruknu(nguzo) katika sala ikiwa zitakosekana kwa pamoja sawaa kwa makusudi ao kwa kusahau au zikizidi sala itabatilika,na haitabatilika ikiwa itapungua moja wapo au kuzidi moja wapo.

Na sijda inathibiti kwa kuweka paji la uso au sehemu yoyote ya uso inayo weza

kusimama na kuchukua nafasi yake,kwa makusudio ya kunyenyekea katika hali maalum.Na sijda ina timia kwa viungo vifuatavyo:

KWANZA:

1. Vatanga viwili vya mikono.

2. Magoti mawili.

3. Vidole gumba vya miguu.

4. Paji la uso kwa kiasi kinacho tosheleza.

Nilazima paji la uso liwe juu ya kitu kinacho faa kusujudu juu yake kama ardhi na vinavyo mea huu ya ardhi kwa sharti visiwe ni vyenye kuliwa au kuvaliwa.

PILI :

Kusoma dhikri kama alivyo tangulia kwenye rakaa isipo kuwa kwenye sijda utasoma dhikri ifuatayo : ((SUBHANA RABIYAL-AALAA WABIHAMDIHI)) mara tatu.

TATU :

Kubakia na kutulia kwa ajili ya kusoma dhikri ya wajibu,kama ilivyo tangulia kwenye rukuu.

NNE :

Wakati wa kusoma dhikri sehemu au viungo vya sijda viwe vime thibiti mahali pake.

TANO :

Kuinuka kutoka kwenye sijda ya kwanza na kukaa kwa utulivu.

SITA :

Kulingana sehemu ya paji la uso na sehemu ya magoti na vidole gumba vya miguu,na sehemu hiyo ikitofautiana iwe ni kwa kiasi cha upana wa vidole vinne vilivyo unganishwa.

7. TASHAHUD :(kushudia)

Tashahud ni wajibu mara mbili katika sala yenye rakaa nne au tatu ya kwanza baada ya kumaliza rakaa mbili za mwanzo na baada ya kumaliza na kuinua kichwa kutoka kwenye sijda ya mwisho ya rakaa ya pili na tashahudi ya pili husomwa baada ya kuinua kichwa kutoka kwenye sijda ya mwisho katika rakaa ya mwisho ya kila sala,nayo ni wajibu na si ruknu,akiacha mtu kwa makusudi sala inabatilika,na akiiacha kwa kusahau itambidi kuitekeleza.

Na katika tashahud husemwa maneno yafuatayo :

( (Al hamdu lillah : ((Bismillahi wabillahi wal-hamdulillahi,wa khairul-asmaai lillahi,au wakhairul-asmail-husna kallaha lillah,Ash-hadu anlaa ilaha illa llah wahdahu la sharika lahu,wa-ash-hadu anna mohamma`dan abdahu warasuluhu allahumma swali ala muhammadin wa-alii mohammad)).

Na wakati wa tashahud nilazima iwe juu ya mapaja,na baada ya kusmaliaaaa mtume utasema ((Watakabbal-shafaa-atahu war-faa daraja tahu)) hii ni katika tashahud ya kwanza,na wakati anapo simama atasema ((Bihauli llahi waquwaatihi aqumu wa ak'udu))na wakati wa kusimama inambidi mwanamke kuya ambatanisha mapaja yake kwa ajili ya kusimama.

8.SALAM :

Ni wajibu kutoa salam katika kila sala na ndio tendo la mwisho katika sala na baada ya salam tayari mtu anakuwa ametoka kwenye sala na anaweza kufanya chochote alicho katazwa akiwa kwenye sala.

Na salam ina mifano miwili :

Mfumo wa kwanza : ((Assalaam alayna wa ala abadi llahi swalihina))

Mfumo wa ya pili : ((Assalaam alay kum))na uta ongeza ((warahma tullahi wabara katuhu))ama kauli isemayo ((Assalaam alayka ayyuhannabiyu warahmatullahi wabarakatuhu))si katika mfumo wa salam ya wajibu bali ni sunna.

Na nilazima kuisoma salam kwa kiarabu kama ambavyo ni wajibu kusomwa kwa kukaa na kwa utulivu.

9.MPANGILIO :

Ni wajibu kupangilia kati ya vitendo vya sala kama tulivyo elezea,ikiwa mtu atabadilisha utaratibu kwa kutanguliza na kuchelewesha akifanya hivyo kwa makusudi sala inabatilika.

10.KUFUATANISHA :

Ni wajibu kufuatanisha kati ya vitendo vya sala,kwa maana ya kuto tenganisha na kuweka mwanya kati ya vitendo hivyo kiasi kwamba itapelekea kufutika sura ya sala kulingana na wanasheria wa fiqhi,kwa maana hii sala itabatilika kwa kuwepo mwanya iwe kwa makusudi au kwa kusahau.

QUNUT

Qunut ni wajibu katika sala zote,sawa ziwe za faradhi au sunna,na imetiliwa mkazo na kusisitizwa sana kwenye sala za jahri,(sala zisomwazo kwa kupaza sauti)hasa sala ya asubuhi, sala ya ijumaa,na sala ya maghrib.Na qunut husomwa baada ya kusoma Al-hamdu na sura katika rakaa ya pili na kabla ya rukuu,isipokuwa katika sala ya ijumaa, kwani sala ya ijumaa inakunuti mbili ya kwanza kabla ya rukuu katika rakaa ya kwanza ,na ya pili baada ya rukuu katika rakaa ya pili.

Na ni sunna kwenye kunuti kusoma dua ifuatayo : ((Laailaha illa llahul-halimul-karim,Laailaha illa llahul-aliyul-adhim,subhanallahi rabbis-samawatissab-I,warabbul-ardwina ssabb-I,wamafihinna wama bayna hunna,warabbul-arshil-adhwiim,wal-hamdu Lillahi rabbil-aalamiin)).

TAAKIIBAT

Taakiibati ni kujishughulisha na kusoma dua na nyuradi baada ya

kumaliza sala,na nyuradi ni kama zifuatazo kusema ((Allahu akbar))mara tatu baada ya kutoa salam,ukiwa ameinua mikono,pia kusoma tasbihatu zahra kama ifuatavyo :

Kusoma takbira mara thalathini na nne (34) kisha utasema (Al-hamdu lillah)) mara thala thini na tatu (33),kisha atasoma tasbihi au atamsabbihi mwenyezi mungu mara thalathini na tatu (33) pia atasoma suratul-fatiha,na ayatul-kursiy,na aya shahida llahu,pia ayatul-mulki na zingine nyingi.

MAMBO YABATILISHAYO SALA

Mambo yafuatayo ikiwa yatatokea wakati wa sala, sala itabatilika.

Nayo ni kama yafuatayo :

1.Hadathi,sawa iwe hadathi ndogo au kubwa

2-kugeuka na kutoka kwenye qibla bila ya udhuru kiasi kwamba kutaondoa hali kuelekea qibla kuzingatiwako kwenye sala. 3 -Kufanya matendo ya futayo sura ya sala,kama kuruka ruka,na kuchupa,na kujishughulisha na mabo mengine.

4-Kuzungumza kwa makusudi,na kuzungumza kuna thibitika hata kama ni kutamka herufi moja yenye kueleweka

5-Kucheka kwa kutoa sauti hata kama si kwa hiyari hapana shaka kwa kutaba samu.

6-Kulia kwa makusudi na kulia huko kukiwa ni kwa sababu ya mambo ya kidunia,au kumkumbuka maiti,ama ikiwa ni kwa ajili ya kumuogopa mwenyezi mungu,au ni kwa sababu ya shauku ya maridhio yake au kwa ajili ya unyenyekevu hakuna tatizo.

7-Kula na kunywa,hata kama ni kigodo,ikiwa ulaji na unywaji huo ni wenye kuondoa sura ya sala.

8-kufunga mikono,nayo ni kuweka mkono mmoja juu ya mwingine kwa unyenyekevu na kuonyesha adabu kama ilivyo zoeleka kwa wasio kuwa mashia,hakika ufungaji huo wa mikono ni wenye kubatilisha sala,sawa amefanya hivyo kwa kukusudia kuwa ni sehemu ya sala au hapana.

9-Kukusudia kusema neno ((Aamin)) baada ya kusoma suratul-fatiha,hakika neno hilo hubatilisha sala ikiwa maamum atalisema kwa makusudi tofauti na hali ya takia

ama akisahau hakuna tatizo.

NAMNA YA KUSALI

Baada ya kutawadha na kuyatekeleza au kuyazingatia yote yazingatiwayo kwenye sala kama nguo za kusalia,sehemu ya kusalia,utaanza sala yako kama ifuatavyo :

Utanza kwa Nia,na katika Nia ndio utaainisha aina ya sala na utasema ((Uswalli Swalatu,subhi,au dhuhri,au alasri,na zinginezo, na Nia ita ambatana na takbiratul-ihram.Kwa mfano utasema :Nia :((uswali swalatu subhi qurbatan ila llah)) ((Allahu akbar)).Baada ya takbir utasoma suratulfatiha (al-hamdu na sura kamili).Baada ya sura utakwenda rukuu :na utasema :

((subhana rabiyal-adhwimi wabihamdihi, mara tatu Allahumma swali ala muhammadin wa ali muhammad)).Utainuka na kusimama kidogo na utasema :((samia llahu liman hamidah)) ((Allahu akbar))-utakwenda sajda na utasema (( subhana rabiyal-aala wabihamdih)) mara tatu,baada ya sijda ya kwanza utainuka na kusema Allahu akbar,kisha utakaa na kupumzika kidogo na utasema (astaghafirullaha rabbi wa atubu ilayhi))kisha utasema Allahu akbar na kwenda kwenye sijda ya pili na atarudia maneno yale yale uliyo yatumia kwenye sijda ya kwanza.Baada ya sijda ya pili utainua kichwa na kusema Allahu akbar-na hapo rakaa moja itakuwa ime malizika na uta simama kwa ajili ya rakaa ya pili.

Na katika rakaa ya pili utasoma kama ulivyo soma katika rakaa ya mwanzo.Na baada ya kusoma al-hamdu na sura na kabla ya rukuu utasoma kunuti,baada ya kunuti utakwenda rukuu,baada ya rukuu utafanya sijda mbili na baada ya hapo utakaa chini na kusoma tashahudi kwa kusema :

((Bismillahi wa billahi wakhairul asmaul-husna kuluha li llahi.Ash-hadu anla ilaha illa llahu wahdahu la sharika lahu wa asha-hadu anna muhammadan abduhu warasuluhu allahumma swali ala muhammadin wa ali muhammad))na utatoa salam kwa kusema :

((Assalamu alayka ayyuha nnabiyu warahmatullahi wabarakatuhu,Assalam alayna wa ala ibadi llahi swalihina,Assalam alaykum warahmatullahi wabara kaatuh))Na hapo sala ya subhi itakuwa imemalizika na baada ya salam utasema :((Allahu akbar))mara tatu huku ukiinua mikono.

Ama katika sala ya adhuhuri,alasiri au magharibi na isha,baada ya tashahudi ya mwanzo hutatoa salam bali utasimama kwa ajili ya rakaa ya tatu na utasema :((Bihauli llahi waquwwatihi akuumu wa akuudu)).Na katika rakaa ya tatu utasoma tasbihi mara tatu nayo ni kama ifuatavyo :

((subhana llah wal-hamdu lillahi wa lailaha illa llahu allahu akbar))mara tatu kisha utarukuu na kusema maneno yale yale kama ilivyo tangulia.

Baada ya rukuu utasujudu sijda mbili na baada ya kumaliza utasimama tena kwa ajili ya rakaa ya nne na utafanya vile vile kama ulivyo fanya kwenye rakaa ya tatu.

Baada ya kumaliza sijda mbili za mwisho katika rakaa ya nne,utasoma tashahud na kutoa salam,na sala itakuwa imemalizika .Na ni sunna kutao takbir mara tatu kwa kusema :((Allahu akbar))

Baada ya kumaliza sala utasoma tasbihatu azzahra kisha dua na sala itakuwa imemalizika.