Mambo yamuwajibishayo mtu kuoga ni sita:
1-Janaba.
2- Hedhi.
3- Nifasi.
4- Istihadha.
5- Kumgusa maiti.
6- Kifo.
Ina thibitika janaba kwa mambo mawili: 1- kutokwa na manii katika sehemu za siri kama ilivyo zoweleka, na sehemu nyingine yoyote ikiwa utokaji huo ni wa kawaida, ama ikiwa si utokaji wa kawaida kutakuwa na ish’kaali, na umaji maji utokao katika sehemu hizo baada ya manii na kabla ya kufanya istibraa ya mkojo hukumu yake ni sawa na janaba.
2- kukutana kijinsia kati ya mwanamke na mwanaume, hata kama hawakutoa manii, na maingiliano hayo yawe ni sehemu ya mbele au ya nyuma, na kufanya hivyo kunamfanya mtu awe na janaba awe mwanamke au mwanamume, na ihtiyaati inasema kuwa yeyote atakae ingiliwa hata kama si mwanamke itakuwa ni juu ya wote wawili muingiliaji na muingiliwaji kuoga janaba.
Mas’ala: Inawajibika kuoga janaba kwa ajili ya mambo manne: 1- Wakati wa sala ya wajibu isipokuwa sala ya maiti ( kumsallia maiti). 2- Sehemu za sala zilizo sahaulika, vile vile sala ya ihtiyaat, na katika sijda ya sahau, si lazima kuwa na twahara japokuwa ni ahwat kuwa na twahara. 3- Twawafu ya wajibu hata kama itakuwa ni sehemu ya hajji ya wajibu au umra ya sunna. 4- funga, na ufafanuzi wake utafatia.
Mas’ala: Ni haramu kwa mwenye janaba mambo yafuatayo: 1- Kugusa jina tukufu la Mwenyezi Mungu na majina yake mengine matukufu, pia sifa zake maalum kwa kauli iliyo ahwat, na kauli ya ahwat ni kuwa majina ya maasumiin pia. 2- Kugusa maandishi ya Qur’ani. 3- kuingia msikitini hata kama ni kwa kuchukua kitu msikitini, ndio, si haramu kuvuka msikitini kwa kuingilia mlango mmoja na kutokea mlango mwingine na kadhalika.
4- kukaa msikitini. 5- kuweka kitu msikitini hata kama ni katika hali ya kukatiza msikitini au kukiweka kwa kutokea nje. 6- kuingia katika msikiti mtukufu wa makka na msikiti wa mtume (s.a.w) hata kama ni katika hali ya kukatiza. 7- Kusoma sura moja wapo kati ya sura nne za azaaim, nazo ni aya ambazo pindi zisomwapo huwajibika kusujudu sijda ya wajibu, na kauli ya ahwatul awlaa ni kuwa haipaswi kusoma aya yoyote katika sura za azaaim ambazo kuna aya ya sajda ya wajibu nazo ni (alifu laam tanziil, Haamim sajda, Suratun najm, na suratul alaq)
Mas’ala: Sehemu za makaburi ya maasumiin huambatanishwa na hukumu za misikiti kwa kauli ya ahwat na haiunganishwi na hukumu hiyo arwaqatiha…….- ikiwa haija thibiti ya kuwa ni msikiti kama ilivyo thibiti kwa baadhi- kama ambavyo
haviunganishwina hukumu hii viwanja vya sehemu hizo tukufu japo kuwa kauli iliyo ahwat inasema ni vema kuziunganisha sehemu hizo na hukumu hizo.
Mas’ala: kuna aina mbili za uogaji: 1- Uogaji wa kupiga mbizi. 2- Uopgaji wa utaratibu.
!- Uogaji wa kupiga mbizi nao una aina mbili: !- Kupiga mbiozi kwa mara moja na kupiga mbizi kwa taratibu.
Na aina ya kwanza ni kuuzamisha mwili wote kwenye maji na kufunikwa sehemu zote, na kitendo hicho hufanyika kwa mara moja na huzingatiwa kuwa kuzama ndani ya maji taratibu ni utangulizi wa ghusli hiyo.
Na aina ya pili ni kuuzamisha mwili katika maji kidogo kidogo pamoja na kuhakikisha kuwa mwili wote unazama kama kawaida, kwa hivyo basi kuzamisha kiungo kimoja kimoja inakuwa ni sehemu ya ghusli na sio utangulizi wake kama ilivyo katika aina ya kwanza na kauli ya adh’har ni kuwa aina ya pili ni sahihi kama ilivyo kuwa ya kwanza.
Na katika sehemu ya pili huzingatiwa kuwa kila kiungo cha mwili kiwe nje ya maji kabla ya kukizamisha kwenye maji kwa makusudio ya kuoga, na katika sehemu ya kwanza inatosha tu mwili wote au baadhi kuwa nje ya maji kisha ukavizamisha ndani ya maji kwa makusudio ya kuviosha.
2- Uogaji wa utaratibu: na kauli ya ahwat ya wajibu kuhusiana na namna yake ni kuwa, kwanza ataosha kichwa chote na shingo, kisha sehemu ya mwili iliyo bakia, kama ambavyo ni ahwat kuosha nusu ya upande wa kulia kwanza, kisha nusu ya upande wa kushoto, japo kuwa kauli iliyo adh;har ni kuwa hakuna utaratibu katika kuosha pande hizi mbili kwani inajuzu kuziosha kwa pamoja au kwa aina yoyote ilie nyingineyo.
Ni wajibu katika kuosha kila upande au kiungo kuchukua sehemu kidogo ya upande au kiungo kingine, sehemu ambayo inaungana nayo, ikiwa hutafahamu mpaka wa sehemu ya wajibu isipo kuwa kwa kufanya hivyo.
Mas’ala: Kauli ya ahwat ya wajibu ni kuwa ghusli ya taratibu haithibiti kwa kukitingisha kichwa au shingo kisha pande mbili kwa lengo la kufanya ghusli- ikiwa kiwili wili chote kimo ndani ya maji- vile vile kuvitikisa baadhi ya viungo vikiwa ndani ya maji kwa lengo la kufanya ghusli, na pia wamesema kuwa ghusli ya kupiga mbizi itathibiti mara moja kwa kukitikisa kiwili wili kikiwa ndani ya maji kwa lengo la kufanya ghusli.
Lakini hukumu hii ina ish’kaali na kauli ya ahwat ni kuwa haita tosheleza kufanya hivyo , ndio ikiwa ata piga mbizi na maji yakawa haya kuenea sehemu zote za kiwili wili chake na akanuwia ghusli ya kupiga mbizi kwa sehemu iliyo bakia ambapo nia hiyo ikawa sambamba na kufika maji kwenye sehemu hizo au ikiwa aliweka nia na kukusudia kufanya ghusli mwanzoni mwa kupiga mbizi hadi wakati wa kuenea maji sehemu yote ya mwili wake, katika kusihi kwake kuna kauli.
Huzingatiwa katika ghusli masharti yote yazingatiwayo katika udhu, isipo kuwa ni kwamba ghusli inatofautiana na udhu katika sehemu mbili: 1-katika ghusli haizingatiwi kuwa kiwili wili kioshwe kutokea juu kwenda chini na limeelezwa hilo katika udhu kwa upana. 2- Kufuatanisha hakuzingatiwi katika ghusli bali huzingatiwa katika udhu.
Mas’ala: Ghusli ya janaba hutosheleza katika udhu, na kauli iliyo wazi ni kuwa hukumu hiyo huzihusu hata ghusli zinginezo za wajibu au zele zilizo thibiti kuwa ni sunna pia, isipo kuwa ghusli ya istihadha mutawassit (ya kati) kwani ni lazima kutawadha baada ya kuoga- kama tutakavyo eleza hapo baadae- na kauli ya ahwat na iliyo awlaa ni kuwa ni bora kutawadha katika ghusli zingine pia- tofauti na ghusli ya janaba- kwa kutawadha kabla yake.
Mas’ala: Ikiwa mukallaf (anae takiwa kutekeleza hukumu za sheri) anazo ghusli za aina tofauti kama ghusli ya janaba, ghusli ya siku ya ijumaa, ghusli ya Hedhi, na mengineyo itajuzu kwake kufanya ghusli moja kwa lengo la ghusli zote na hiyo inatosheleza katika ghusli zilizo bakia, kama ambavyo ina juzu kunuwia ghusli ya janaba tu, na ghusli ya janaba inatosheleza katika ghusli zilizo bakia, ama ikiwa atanuwia ghusli nyingine tofauti na ghusli ya janaba hakuna shaka kuwa ghusli hiyo itatosheleza tu kwa ghusli aliyo inuwia, ama ghusli hiyo kutosheleza katika ghusli zingine kuna ishkaali na kauli iliyo adh’har ni kuwa itatosheleza, ndio katika kutosheleza ghusli yoyote kwa ghusli ya siku ya ijuma kuna ishkaali, ikiwa hakukusudia ghusli hiyo lau kwa sura ya ujumla,.
kisha yaliyo tajwa ya kuwa inatosheleza ghusli moja katika ghusli kadhaa hukumu hiyo itatumika katika ghusli zote za wajibu na sunna- ghusli za sehemu fulani au wakati fulani au kwa ajili ya lengo lingine- lakini kutumika hukumu hiyo katika ghusli zingine zilizo amrishwa kwa sababu ya kufanya vitendo kadhaa- kama kumgusa maiti baada ya kumuosha – pamoja na sababu nyingi hapo kutakuwa na ish’kali.
Mas’ala: Ikiwa mtu atatokwa na hadathi ndogo wakati akioga au katikati ya ghusli ya janaba itambidi kuikamilisha ghusli hiyo, na kauli ya ahwati ni kuwa itambidi wakati huo kutawadha baada ya ghusli, na hapo anayo hiari ya kubadilisha kwa kutumia ghusli ya kupiga mbizi badala ya ghusli ya utaratibu au kinyume chake na wakati huo hakuna haja ya kutawadha bila ya ishkali yoyote.
Mas’ala: Ikiwa atatia shaka ya kuwa ameoga ghusli ya janaba au hapana, atajengea ya kuwa hakuoga, na ikiwa atatia shaka ya kuwa ameoga au hapana baada ya kumaliza kusali haitamlazimu kuirudia sala hiyo-isipokuwa sala hiyo ikiwa ni ya wakati maalum na shaka hiyo ikatokea katika wakati wa sala hiyo na kisha akatokwa na hadathi ndogo baada ya sala, kauli ya ahwat inasema ni vema kuirudia wakati huo- na ni wajibu juu yake kuoga kwa kila kitendo ambacho kukitenda kwake ni sharti kuwa na twahara katika kuswihi kwake, au kujuzu kwake ni lazima uwe na twahara ya hadathi kubwa, bila kutofautisha kati ya sala au laa hata kama ni kugusa maandishi ya Qur’an, na ghusli hili lina weza kufanyika kwa aina mbili:
Kwanza awe na yakini ya kuwa ameamrishwakufanya ghusli hiyo na amri hiyo ima ni ya wajibu au sunna- kama vile akikusudia kuoga ghusli ya ijumaa ua ghusli ya janaba kwa mara nyingine baada ya sala na wakati huo ni juu yake kutosheka na ghusli hiyo katika kufanya kila kitendo kinacho hitaji twahara katika kutekelezwa kwake sawa awe ametokwa na hadathi ndogo au laa.
Pili: Iwe kinyume na hivyo kwa mfano kufanya ghusli hiyo kutokane na ihtimali au kuwe na ihtimali ya kuwa huenda janaba ilibakia, janaba ambayo ameitiliashaka ya kuwa ameoga janaba hiyo kabla ya sala au laa, na wakati huo atatosheka na ghusli hiyo katika kutekeleza kitendo ambacho kutekelezwa kwake ni sharti kuwa na twahara kutokana na hadathi kubwa tu, kama kujuzu kukaaa msikitini, ama matendo ambayo ni sharti kuwa na twahara katika kuyatekeleza kwake hata kama ni kutokana na hadathi ndogo haitatosha katika kitendo hicho kuoga tu bali itawajibika kutawadha pia ikiwa ghusli hiyo itatanguliwa na kutoka kwa hadathi kinyume na ikiwa haikutoka kabla.