ADHANA NA IQAMA

Mas’ala:  Ni sunna kutoa adhana na kukimu katika sala za faradhi za kila siku  sawa iwe ni adaa au kadhaa.

Na kushuhudia kwa kusema  ash’hadu anna aliyan waliyyu llah. Hiyo ni kukamilisha shahada ya mtume au ujumbe wa mtume,na kusema hivyo ni sunna hata kama si sehemu ya adhana au iqamah, na vile vile kumsalia mtume na ahli zake pindi litajwapo jina lake tukufu.

Mas’ala:  Sunna hii  ya kuadhini na kukimu husisitizwa sana   hasa katika sala ya magharibi na sala ya alfajiri kati ya faradhi za kila siku,  kama ambavyo imesisitizwa sana   kwa wanaume na hasa iqamah, bali kauli ya ahwat ya sunna kwa wanaume ni kuwa haipaswi kuiacha, na adhana na iqama  haikutiliwa mkazo  na kusisitizwa kwa wanawake.

Mas’ala: Sunna ya adhana na Iqama huporomoka  katika sehemu zifuatazo: 

1- pindi akiingia katika sala ya jamaa amboyo kabla yake ilitolewa adhana na kukimiwa sawa awe alieingia kwenye sala hiyo ni  imam au ma’amuum.

2- Pindi akiingia msikitini na safu za jamaa zikawa  hazikutengana  na kupatikana nafasi baada ya kumaliza sala, ikiwa atataka kusali peke yake wakati huo si lazima kwake kuadhini na kukimu- bali kauli ya ahwat ni kuwa  asitoe adhana isipokuwa kwa siri au pole pole- na ikiwa atataka kusali sala nyingine ya jamaa  hata anza kwa kuadhini na kukimu lakini kwa sharti kuwa sehemu iwe ni ile ile –yaani- isiwe sehemu nyingine tofauti na ilipo saliwa jamaa ya kwanza  na sehemu ambayo imesihi kusalia jamaa ya kwanza na iwe katika jamaa ya mwanzo wali adhini na kukimu.

3- Pindi  atakapo sikia  adhana na iqama mtu mwingine kwa ajili ya sala  adhana na iqama hiyo itatosheleza  na haitakuwa na haja ya kuadhini na kukimu,  lakini ikiwa hapakuwa na mwanya kati ya sala yake na kati ya adhana na iqama aliyo isikia,  na hakuna tofauti kati ya kuwa alie adhini na kukimu ni imam au maamum  au mtu mwingine mwenye kusali sala ya furada  (pekee)

Mas’ala:  Adhana huporomoka katika sala ya pili kati ya sala zenye kushirikiana  katika wakati, ikiwa atakusanya kati ya sala hizo pale ambapo atatekeleza sunna ya kukusanya- kama  ikiwa atakusanya kati ya sala ya adhuhuri na alasiri siku ya arafa katika wakati wa mwanzo na magharibi na isha usiku wa iddi katika sehemu ya muzdalifa katika sala ya pili- bali katika sehemu  zote ambazo ni sunna kukusanya kwa kauli iliyo adh’har, wakati wowote atakapo kusanya kati ya sala mbili za faradhi adaa’an  adhana ya pili huporomoka, vile vile ikiwa atakusanya kati ya sala mbili za kadhaa na kuzisali kwenye kikao kimoja wakati huo adhana ina anguka isipokuwa katika sala ya mwanzo,  na ihtiyat inasema yawezekana kuiacha adhana  katika sehemu zote  kwa kuwa si sheria bali haipaswi  kutoa adhana na iqama katika sehemu mbili za mwanzo moja kwa moja hata kama ni kwa kutaraji kuwa kufanya hivyo ni kujikaribisha kwa Allah.

Mas’ala:  Huzingatiwa nia katika adhana na iqama, pia utaratibu na kufuatanisha na iwe ni katika wakati wa sala, na huzingatiwa katika iqama mtu awe na twahara na atoe iqama  kwa kusimama, na ni makruhu kuzungumza baada ya kusema  qad qaamatis salaa isipokuwa litakalo husika na sala tu.

NAMNA YA KUADHINI:

الله اکبر
Allahu akbar X 4

اشهد ان لا اله الا الله
Ash-hadu an lla ilaaha illa llaah X 2

اشهد ان محمد رسول الله
Ash-hadu anna muhammada rrasuulullaah X 2

اشهد ان عليا ولی الله
Ash-hadu anna ALiyan waliyyu llaah X 2

حی علی الصلوة
Hayya-alaa salaah X 2

حی علی الفلاح
Hayya-alal falaah X 2

حی علی خير العمل
Hayya-alaa kheyril-amal X 2

الله اکبر
Allahu akbar X 2

لا اله الا الله 
Laa-ilaaha illa llaah X 2

NAMNA YA KUKIMU :

الله اکبر
Allahu akbar X 2

اشهد ان لا اله الا الله
Ash-hadu an lla ilaaha illa llaah X 2

اشهد ان محمد رسول الله
Ash-hadu anna muhammada rrasuulullaah X 2

اشهد ان عليا ولی الله
Ash-hadu anna ALiyan waliyyu llaah X 2

حی علی الصلوة
Hayya-alaa salaah X 2

حی علی الفلاح
Hayya-alal falaah X 2

حی علی خير العمل
Hayya-alaa kheyril-amal X 2

قد قامت الصلوة
Qad qaamatis salaa X 2

الله اکبر
allahu akbar X 2

لا اله الا الله

Laa ilaaha illa llaah X 1