TABIA ZAKE NJEMA

Imamu Ali An-Naqi [a] alikuwa na tabia njema kama zile za kila mmoja, wa watu wa ukoo wa Mtukufu Mtume [s]. Akiwa nje au ndani ya jela, tabia ya maisha ya Imamu Ali Naqi [a] iliyojulikana sana ilikuwa ni sala, ibada na huruma kwa viumbe vya Mungu.

Popote pale alipoishi alipokuwa jela alitayarisha kaburi na mahaIi alipokuwa akisalia. Alipoulizwa maana yake, alijibu kuwa alitaka kila mara kuliweka wazo la kifo mbele akilini mwake. Hakika hilo liIikuwa jibu la kufaa kwa matakwa ya watawala dhaIimu kwa lmamu [a] kuwa aache kuitangazia Imani ya kweli na kuitii serikali ya kiupotovu isiyokuwa na msimamo. Alikuwa akisema kuwa mtu aliye tayari kufa wakati wowote hawezi kutishwa mpaka akatishika.

Ingawa milki ya ukoo wa Bani Abbas ilikuwa imezorota sana, lmamu [a] hakufikiria kuiangusha na serikali haikuweza kupata kisingizio cha kuyahalalishia mateso waliyompa.

Chuki aliyoionyesha Muntasir na mtumwa wake wa Kirumi aitwaye Baghir aliyempenda kwa baba yake Mutawakkil, kugawanyika kwa utawala na maangamizi ya watu wenye vyeo vya juu serikalini na mwishowe uamuzi wa wanawe Mutawakkil wa kumwondoIea baba yao kiti cha enzi, na wakati wa utawala wa Musta'in kuondoka kwa Yahya bin Ami Alawi, kuanzishwa serikali ya kujitegemea huko Tabaristan na Hasan bin Zaid, maasi ya watumwa wa Kituruki katika mji mkuu wa nchi, kukimbia kwa Musta'in kutoka katika mji huo mkuu na kwenda Baghdad, na mwishowe kulazimishwa kujiuzulu na baadaye kuuwawa na Mu'ttaza; na vitendo vya uchochezi vya watumwa wa Kirumi katika zama za Mu'ttazz, Mu'ttazz kutokuwaamini ndugu zake na mwisho wa maisha ya Bani Mu'awiyyah na kufungwa kwa Muwaffaq huko mjini Basrah, matukio yote haya yalimtoa Imamu [a] katika hali ya kudhaniwa kuwa anahusika na kitendo chochote cha kisiasa. Je, hii haionyeshi uwezo wa hali ya juu na usio na kifani wa Imamu [a] katika kujali zaidi ujumbe wake licha ya majaribu hayo yote ambayo kwa kweli yangeweza kabisa kumwambukiza mtu wa kawaida?

Ustahimilifu uIioonyeshwa na Imamu kwa serikali ambayo alijua kuwa ni ya kidhalimu na haribifu kwa sheria ya Islamu na kwamba imemuwekea taabu nyingi mno, inaonyesha kuwa ni tabia bora mno ya kiakili (inayotokana na Mwenyezi Mungu) ambayo ingeweza kuufanya Mwenge wa Mwanga Mtukufu kuendelea kuwaka.