KUFARIKI KWAKE

Imamu [a] aIifariki dunia mnamo tarehe 3 ya mwezi wa Rajab, mwaka 254 Hijiriya. Wakati wa kufariki kwake mwanawe Imamu Hasan Askari [a] tu ndiye aliyekuwepo na kutayarisha maziko yake na sala, na wakamzika ndani ya nyumba yake aIimokuwa akiishi. Hapo ndipo kaburi lake lisimamapo kuyabariki macho ya mahujaji waendoa kulizuru.