SHIDA NA MATESO

Kwa ajili ya matatizo ya kiutawala yaliyokuwa yakisababishwa na vita na kuhamishiwa Baghdad mji mkuu na pia kwa kuwa umri wa Imamu ulikuwa mdogo, mfalme Mutassim hakumsumbua Imamu [a]. Baada ya Mutasim, Waathiq naye alimnyamazia Imamu [a]. Lakini mara tu Mutawakkil alipokalia kiti cha utawala ulianza wakati mgumu sana kwa Imamu [a]. Mutawakkil alikuwa nduguye Waathiq na ni mwanawe Mu'tasim naye alikuwa adui mkubwa wa Nyumba ya Mtukufu Mtume [s].

Katika muda wa miaka kumi na sita tangu Imam Ali Naqi [a] atwae Uimamu, sifa yake ilienea kote katika ulimwengu wa Kiislamu. Watu walikuwa wakimiminika toka pande zote kujifunza lolote lile waliloweza kutoka kwa wakili huyu wa Hekima ya Mwenyezi Mungu (Imamu [a]). Ilikuwa imepita miaka minne tu ya utawala wa Mutawakkil wakati gavana wake wa Madina alipoanza kumsumbua Imamu [a]. Alianza kwa kumpa usumbufu wa kila aina na halafu akaanza kumwandikia Mutawakkil akizua kila aina ya uongo juu ya Imamu [a] kama walivyofanya wafalme wengine waliomtangulia. Kwa mfano, alimwandikia barua Mutawakkil akisema kuwa Imamu [a] amekusanya watu wengi na angeweza kuuvamia utawala wake wakati wowote ule apendapo (Imamu [a]) kufanya hivyo.

Imamu [a] alijulishwa hila hiyo mapema. Hivyo mara moja alimwandikia Mutawakkil akiifichua hila hiyo. Mutawakkil alichukua hatua za kuisuluhishi wa kiserkali alimfukuza kazi gavana huyo wa Madina. Lakini alipeleka kikundi cha jeshi chini ya Uongozi wa Yahya bin Harsimmah kumwomba kirafiki Imamu [a] kuutembelea mji mkuu wa Sammarah kwa muda wa siku chache hivi. Imamu [a] alijua wazi maana ya ukaribisho huo lakini hakuweza kukataa kwani ukaribisho wenyewe ulionyesha kuwa ni wa kirafiki na vile vile Imamu [a] alijua kuwa angelilazimishwa kama akikataa. Hivyo aliondoka Madina (kwenda Sammarah) kwa kusitasita.

Barua ya Mutawakkil kwa Imamu [a] ilionyesha heshima yote astahiliyo na kikundi cha jeshi kilipelekwa chini ya kisindikizo cha hila. lakini mara tu Imamu [a] alipofika Sammarah, badala ya Mutawakkil kutoka yeye mwenyewe na kumkaribisha Imamu [a] au japo kumkaribisha kwenye ikulu yake tu, aliamrisha Imamu [a] apelekwe akakae kwenye "Khan-us-Sa'alik" (nyumba ya maskini) iliyokuweko nje ya mji. Ingawa watu wa ukoo wa Mtukufu Mtume [s] walikuwa kila mara tayari kuishi na maskini, madhumuni ya Mutawakkil ni kutaka kumfedhehesha Imamu [a]. Imamu [a] alikaa huko kwa muda wa siku tatu na baadae Mutawakkil alimfunga katika nyumba ya mtu moja aitwaye Zarraqi na aliamrisha watu wasiruhusiwe kuonana naye.

Kama vile Uchamungu wa Imamu Musa Kazim [a] ulivyoathiri walinzi wa jela alimofungiwa, Zarraqi nae pia katika muda mfupi sana alielewa kuwa mfungwa wake alikuwa mtu apasikaye kuheshimiwa badala ya kumfedhehesha na hivyo alibadilisha tabia yake kwa Imamu [a]. Lakini mara tu Mutawakkil alipojua habari hizo, aliuhamishia ulinzi wa Imamu [a] kwa mtu mwingine asiyekuwa na huruma naye na ambaye Imamu [a] aliishi chini ya ulinzi wake kwa muda wa miaka kumi na miwili. Alikuwa akipitisha siku na mausiku katika sala na ibada. Alifunga mchana na kuswali wakati wa usiku.

Mwili wake ulikuwa jela lakini sifa yake nzuri ilienea Iraq nzima. Kila nyumba ilikuwa ikizungumzia Uchamungu wa Imamu [a] na ukatili wa Mutawakkil jambo ambalo lilimfanya mdhalimu huyu achukiwe na raia wake.

Wakati ulifika ambapo Fath-i-Khaqan ambaye licha ya kuwa mfuasi mkuu wa ukoo wa Mtume [s] aliteuliwa kuwa waziri mkuu kwa sababu ya uwezo wake wa pekee. Kwa ombi Ia Ibn Khaqan, Mutawakkil alikipunguza kifungo cha jela kwa Imamu [a] na badala yake kikawa kizuizi cha kuwekewa mipaka na alimpa kiwanja cha kujenga nyumba yake mwenyewe chini ya kutotoka mjini Sammarah.

Kuridhika kibinafsi kwa Imamu [a] kwa wakati huo kulikuwa mfano wa pekee. Ingawaje alikuwa akiishi mjini, Imamu [a] hakuonyesha kutaka jambo loIote Ia raha wala hakumwomba Mutawwakil ampunguzie taabu alizomuwekea. Maisha ya kiibada na uchamungu aliyokuwa akiyaendesha katika jela yaIiendele. Hata hivyo hakuachwa aendelee na mambo yake kwa raha mustarehe: kila mara nyumba yake ilikuwa ikipekuliwa ili kutafuta silaha au barua ambazo zingeweza kuonyesha nia ya Imamu [a] kutaka kuipinga serikali. Juu ya hayo siku moja alialikwa kwenye baraza la mfalme ambao wafuasi wema wa mfalme walikuwa wakishughulika kunywa mvinyo na pombe. Mjinga mmoja aliyekosa adabu alithubutu hata kumpa lmamu [a] kikombe cha mvinyo. MIinzi wa uadilifu, Uchamungu na sheria (za Islamu) alichukizwa sana. Lakini kwa utulivu mkubwa alijibu, "Samahani, mwili wangu na damu yangu, na ile ya baba zangu havikuwahi kunajisiwa na kitu hiki." Kama pangelikuwepo bado wazo la adabu katika kichwa cha mdhalimu huyu alingeliacha kabisa kuendelea na utovu wake wa adabu kwa lmamu [a]. Lakini bila aibu alisema, "Haya basi kama huwezi kufanya hivi (yaani kunywa mvinyo), basi tuimbie wimbo wo wote ule." Imamu [a] alijibu, "Hata hivyo sijui". Halafu alishikilia kuwa Imamu [a] asome aya za Qur'ani Tukufu. Hapo Imamu [a] aliona kuwa sasa wakati umefika wa kuigeuzia meza usoni mwa mnafiki huyo. Kwa sauti ya kuchoma moyo alisoma aya chache za Qur'ani Tukufu zilizojaa mawazo mazuri ya uchamungu na udanganyifu wa raha za ulimwengu aliwakumbusha mwisho wa wale waliojitosa katikati ya raha hizo wakiwa wamemsahau kabisa Muumba wao. Mara moja mawazo haya safi yaliyotoka kinywani mwa Imamu [a] yaliyojaa Uchamungu yalitoa matokeo yake. Wote wale waliokuwa wakifurahi (tafsiri hiyo walianza kulia kwa uchungu na Mutawakkil mwenyewe alitokwa na machozi. Vikombe vya mvinyo viliwadondoka kutoka mikononi mwao na wote waljiona kana kwamba wamo kwenye ndoto. Mara tu waliporudi katika hali ya kawaida, Mutawakkil alimwambia Imamu [a] arudi nyumbani kwake. (Soma nyongeza ya Kwanza).

Mshituko mwingine ambao ilibidi Imamu auvumilie ni Mutawakkil kupiga marufuku kwa mtu yeyote kwenda kuhiji huko Najaf na Karbala na kutishia kuwa wale watakaovunja sheria hiyo watapata adhabu ya kifo. Hakuishia hapo. Aliamrisha kuvunja kwa makaburi ya Najaf na Karbala na kulimwa kwa ardhi yote izungukayo kaburi la Imamu Husain [a]. Haikuwezekana kwa wafanya ibada katika kaburi hilo la Imamu Husain [a] waonyeshe unyonge wowote ule wa kutokwenda kulizuru kaburi hilo. Matokeo yake ni kwamba damu ya watu wengine wengi wasiokuwa na hatia ilimwagika. Kwa kila mmoja wa Mashahidi hao, moyo wa Imamu [a] ulihisi kama vile mtu ahisivyo kwa mwili na damu yake.

lmamu [a] alikuwa akiishi katika hali ambayo haikumpa nafasi yoyote ya kuwapelekea maelekezo watu hawa... Mambo hayo yaliendelea mpaka alipokufa Mutawakkil.

Mfano mwingine wa kutokuwa na haya kwa Mutawakkil ni kwamba katika baraza lake yalifanywa maigizo ya kumdhihaki Hadhrat Ali bin Abi Talib [a] ambayo hata mtoto wa Mutawakkil alishindwa kuyanyamazia maigizo hayo na kuona yakiendelea.

AIimwambia baba yake, "Unaweza kusema lolote lile lakini unaposema kuwa Ali alikuwa wa ukoo wa kabila yako usiwaruhusu hawa wachekeshaji waovu kutumia lugha ya matusi kwake". Badala ya Mutawakkil kuwa mpole alimtukana mwanawe na akatunga mashairi yalivokuwa na maneno ya matusi mabaya kwa mwanawe huyo na mama yake na akawapa wachekeshaji wayaimbe ili kuwafurahisha wasikilizaji.

Msiba mwingine wa kuhuzunisha ni ile shahada ya Bwana Ibn-Us-Sakit Baghdadi aliyekuwa mtaalam wa sarufi na elimu ya lugha katika zama hizo. Mutawakkil alimteua Bwana huyu kuwa mwalimu wa watoto wake. Siku moja Mutawakkil alimwuliza "Unawapenda watoto wangu zaidi au Hasan na Husain", "Ibn-Us-Sakit alijibu, "Nampenda zaidi Qambar, mtumwa wa Ali kuliko watoto wako. Mutawwakil alitoa amri ung'olewe ulimi wake na hivyo ndivyo mfuasi huyu wa Imamu Ali [a] alivyowahi, kupata Shahada yake.

Misiba hii yote ya kuhuzunisha ilimshtua Imamu [a]. Zaidi ya hayo, matendo ya kishari ya Mutawakkil aliyowatendea watu yaliwafanya watu hao kuwa mabaya juu yake na wanawe mwenyewe waligeuka kuwa maadui wake wakuu. Na mwanawe aitwaye Muntasir alimwua Mutawakkil kwa kumtumia mtumwa wa Kirumi aitwae Baghir, na baada ya hapo watu walipata afueni kutokana na mateso yake. Muntasir aliondoa ile amri ya baba yake iliyozuia watu kwenda kuhiji Najaf na Karbala na akayatengeneza kidogo yale makaburi yaliyobomolewa. Hakuonyesha chuki maalum kwa Imamu [a]. Lakini Muntasir alifariki mara tu baada ya kutawala kwa muda wa miezi sita. Alirithiwa na Musta'in ambaye naye hakuonyesha chuki yoyote kwa Imamu [a].

Hivyo, tangu hapo Imamu [a] aliishi Sammarah; kwa sababu Imamu aIijega nyumba yake huko au kwa sababu watawala wenyewe walikuwa hawataki arudi Madina na katika muda huo hapakuwekwa kizuizi cho chote kilichowekwa na watawala, hivyo wapenda elimu walianza kumkusanyikia Imamu [a]. Hali hii ilisababisha wasiwasi kwa Mu'tazz ambaye alirithi kiti cha enzi kutoka kwa Musa'in na alimwua Imamu [a] kwa kumpa sumu.