MABADILIKO YA KISIASA

Uimamu wa Imamu Ali Naqi [a] ulianza katika zama za utawala wa mfalme wa ukoo wa Bani Abbas aitwaye Mu'tasim ambaye alifariki mnamo mwaka 228 Hijiriya na alirithiwa na mfalme Waathiq Billah. Waathiq alifariki mnamo mwaka 236 Hijiriya na alirithiwa na mfalme mshari na mkatili zaidi wa ukoo wa Bani Abbas aitwaye Al-Muttawakil ambaye alifariki mnamo mwaka wa 250 Hijiriya. Baada ya hapo ulifuatia utawala mfupi wa Muntasir Billah ambaye naye alifariki baada ya miezi sita na akarithiwa na Musta'in Billah, lakini mnamo mwaka wa 253 hijirya alipoteza maisha yake pamoja na kiti chake cha enzi na alirithiwa na Mu'tazz Billah ambaye alikuwa mfalme wa mwisho wa zama za Imamu Ali Naqi [a].