KUZALIWA NA KULELEWA KWAKE

Imamu Ali Naqi [a] alizaliwa mnamo tarehe 5 Rajab, mwaka wa 214 Hijiriya mjini Madina. Aliishi na baba yake kwa muda wa miaka sita tu na kisha ilimbidi Imamu Muhammad Taqi [a] kusafiri kwenda Iraq na alifariki huko mnamo tarehe 29 Dhul Qada mwaka 220 Hijiriya. Na kisha Imamu Ali Naqi [a] ilimbidi achukue madaraka wa Uimamu. Katika tukio la namna hiyo ni wapi basi ambako tunaweza kupata chanzo cha upeo wa kisomo chake na Uchamungu wake kama si Neema ya Mwenyezi Mungu tu?