Ukweli Katika Minyororo (Imamu Ali Naqi [a])

Kimeandikwa na : Maulana Sayyid Ali Naqi Saheb

Kimetafsiriwa na : Maalim Dhikiri Omari Kiondo

IMAMU KATIKA QUR'AN NA HADITHI

MWENYEZI MUNGU ANASEMA:

(Ewe mwanadamu! Ikumbuke) siku Tutakapowaita kila watu pamoja na Imamu wao; basi atakayepewa kitabu (chake cha Amali) kwa mkono wa kulia, hao watavisoma vitabu vyao (kwa furaha);

(Bani Israel, 17:71)

MTUKUFU MTUME [s] AMESEMA:

"Ye yote yule afaye pasi na kumjua Imamu wa zama zake, atakuwa kafa kifo cha ujinga."

MTUKUFU MTUME [s] AMESEMA:

"Hao (Ulul Amr watajwao mwenye Qur'ani 4:59) ni Makhalifa wangu na Maimamu wa Waislamu baada yangu. Wa kwanza ni Ali, kisha ni Hassan, kisha ni Husayn, kisha ni Ali bin Husayn, kisha ni Muhammad bin Ali, kisha ni Jaafar bin Muhammad, kisha ni Musa bin Jaafar, kisha ni Ali bin Musa, kisha ni Muhammad bin Ali, kisha ni Ali bin Muhammad, kisha ni Hassan bin Ali, kisha ni Muhammad bin Hassan (Mahdi)..."

("KifayatuI Athar" na "Rawdhatul Ahbab", vya Hafidh Jamaluddin Muhaddith).