SAFARI KWENYE KITABU

AL IMAM MOHAMMAD BIN ALI AL BAQIR

Nilipokuwa nikizifunua kurasa za kitabu nilichokuwa nikikisoma, niliona ni kana kwamba nimeingia katika mji wa zamani. Mji wenyewe ulifanana na mji wa kiislamu. Na wengi wa watu walio kuwa wakipita mbele yangu walikuwa wamevalia aina ya mavazi ya kiislamu.

Lakini la kushangaza ni kwamba, baadhi ya mambo yaliyo dhihiri yalipingana na maadili ya kiislamu. Kwani baadhi ya watu waliokuwa wakipita mbele yangu, walikuwa wakicheka kwa sauti na kupepesuka kutokana na ulevi. Na pia walikuwa wakitokwa na maneno machafu yasiyofaa kuzungumzwa mbele za watu. Vile vile nilisikia sauti ya nyimbo na miziki zilizotokea sehemu mbali mbali.

Nilipokuwa nikiendelea na safari, nilikutana na mvulana aliekuwa ameralia aina ya mavazi ya kiislamu. Nilipoutazama uso wake, nilimuona anaelekea kuwa mwenye adabu na tabia nzuri.($7)

Aliponikaribia, nilimsalimia. Nae alisimama na huku anatabasamu, na akaitikia salamu yangu kwa namna ilio bora. Kisha alinambia, “Yaonekana umgeni katika mjo huu, kwani mavazi yako yaonyesha hivyo.”

“Naona, mimi nikama ulivyo sema. Lakini hayo sio muhimu ewe ndugu yangu”. Ninacho kuomba, ni unieleze kuhusu mji huu. Kwani kutokana na namna ya majengo na mavazi ya watu wake, yaonyeshavyo ni mji wa kiislamu. Lakini la kushangaza ni kwamba, nashuhudia baadhi ya mambo yaliyo kinyume na uislamu. je, sababu yake ni nini ?

Ghafla nilimuona kijana amebadilika na akapatwa na huzuni. Mara machozi yalianza kumdondoka na huku akisema, kizazi cha Umayya ndicho sababu ya haya yote. Kwani kilitumia utawala wao kwa kufanya wapendavyo”.

“kizazi cha umayya!! Kwani bado wako kwenye utawala ?!! » Niliuliza.

“je unakijua kizazi hiki?” kijana aliniuliza.

“Ndio najua mengi kukihusu. Kwa sababu nimekuwa nikisoma kuhusu maisha ya Ahlul beit (a.s.)”. ($9)

“Ewe ndugu yangu, kama ujuavyo kwa sasa tuko kwenye zama za al Imam Mohammad bin Ali al Baqir(a.s.). lakini tukiangalia tunaona kwamba kizazi hiki cha Umayya kingali kinaendelea kufanya kila aina ya maovu na kudhihirisha uasi wao kwenye majumba yao na popote walipo”.

Kijana huyu aliposema hivyo, alitokwa tena na machozi. Hata ingawaje, alijitahidi kuendelea na mazungumzo yake japo kwa shida kutokana na machungu aliyokuwa nayo moyoni. Nilihuzunika mno kwa hali yake hii na hivyo basi nilijaribu kuzungumza nae maneno ya kumtuliza na kumuomba achukulie mambo kwa wepesi.

“Lakusikitisha mno ewe ndugu yangu ni yale yanayo endelea ya uasi kwenye majumba ya hawa wana wa Umayya. Kwani waislamu wengi wameathirika na hali hii kiasi cha kufanya maovu ya kila namna ili kuzistarehesha nafsi zao. je, tufanye nini kuhusiana na jambo hili? Kwani viongozi wa ki banu Umayya ili kujenga utawala wao, wametumia njia mbali mbali, kama vile kudhulumu, kutumia nguru, kuuwa  watu wema, na pia kutumia mali za waislamu kama wapendavyo. ($11) na kwa bahati mbaya wana wa Ali (a.s.) na wafuasi wao ndio wamekuwa wakiteswa na kuadhibiwa kutokana na siasa hiyo mboru. Na sababu ya kuteswa kwao, ni kwa kuwa, wana wa Ali (a.s.) wana kile kinacho wafungamanisha na watu na kuwafanya wastahiki kuwa makhalifa wa Mtume(s.a.w.a.)”

nililolijua kuwahusu wana wa Umayya ni kwamba wamefikia kilele cha ubaya kwa Ahlul beit(a.s.) na wafuasi wao. Na wamenunua imani za watu kwa pesa na kumuaga damu kiasi cha kuyafanya maisha yakose thamani kwa wingi wa dhuluma na ufisadi. Na kwa bahati mbaya, watu bado wanaendelea kujitenga na Ahlul beit(a.s.) wanapowaona wako kwenye shida. Hali ya kuwa wao wanajaribu kuondoa dhuluma wanayofanyiwa wanyonge na maskini. Na pia wanajaribu kuuokoa uislamu kutoka kwenye hali hii mbaya pamoja na inayo utishia uislamu ikiwa watawala hawa wataendelea kutawala kwa dhulma yao.

Tukiangalia kwa upande mwingine, tunaona ya kwamba, kumekua na mabadiliko kwenye fikra za watu na kwenye njia za kuishi. Ugomvi wa aina mbali mbali ambao unaweza kusababisha upotovu, na ukafiri umedhihiri. Yote haya yaliyo penya kwenye uislamu yamekuwa ni tishio kwenye msingi wa akida ya kiislamu. Na hao waliozusha hizo fikra na kuzieneza ni watu ambao hawana uhusiano wowote na uislamu. ($13) Bali wamewakokota waislamu na kuwabebesha fikra zao.

“Je, al Imam al Baqir(a.s.) alikabiliana vipi na hali hizi?”

Nilisoma kumuhusu na nikajua kwamba yeye ni khalifa wa haki baada ya baba yake  al Imam Ali bin Al Hussein(a.s.). Na ni wasii wake mwenye kuchukua jukumu la uongozi baada yake. Al Imam (a.s.) aliwashinda ndugu zake wote kwa fadhila, elimu, ucha Mungu, na mambo mengine mbali mbali Hali aliyokuwa nayo al Imam al Baqir (a.s.) katika nyanja za kielimu, haikuwahi kudhihiri kwa yeyote miongoni mwa wana wa maimama al Hassan na al Hussein(a.s.). na kwa sababu hii ndio alipewa jina la al Baqir, kutokana na kuchimbua kwake kwa elimu. Yaani yeye ni mwingi wa elimu. Anajua chanzo na asili ya kila elimu. Na kwa kuwa yeye ni mmoja wa maimamu kumi na wawili, ndio sababu yangu ya kukuuliza anavyo kabiliana na hali hizi tunazo ziona”.

Katika mazingira haya yaliyojawa na mapambano ya kiakida, al Imam al baqir (a.s.) aliona maslahi ya uislamu yanamtaka ashughulikie kuhifadhi akida na kueneza mafunzo ya uislamu. Hivyo basi maelfu ya watu kutoka sehemu mbali mbali kama vile Hijaz, kufa, Basra na kwingineko, wakiwemo mashia na wengineo walikusanyika kwake ili kujifunza elimu za aina mbali mbali kama vile fighi, hadith, falsafa, tafsir, lugha na nyinginezo. Na hivi sasa chuo hiki kiko njiani kuwatoa maulama wakubwa katika fani mbali mbali za kielimu.”

“Ninani kiongozi miongoni mwa wana wa Umayya katika zama hizi zenu?”

“kiongozi kwa sasa ni Abdul Malik bin Marwan. Huyu amejitalidi kuwa mwema kidogo kwa wana wa Ali (a.s.) kuwashinda wenzake waliomtangulia. Kwani kwenye sehemu ya barua aliomuandikia mtumishi wake katika nchi ya Hijaz amemwambia, “Niepushe na damu ya wana wa Abu Twalib”.

Kutokana na kauli yake hii, tulidhani kwamba amefahamu sababu ya matatizo ya kisiasa yaliyo achwa na Muawia na mwanae Yazid yaliyo sababisha mchafuko wa kisiasa katika sehemu mbali mbali za nchi.($17) lakini baadae ilidhihiri kwamba Abdul Malik bin Marwan alikuwa na mshindani wake katika nchi ya Hijaz alieitwa Ibn Zubeir, anbae alikuwa na tamaa ya kuongeza utawala wake hadi Iraq na miji mingineo.

Baada ya Abdul Malik kumshinda mpinzani wake huyu, aliwaandikia watumishi wake na kuwaamrisha wawe wagumu na wabaya kwa wafuasi wa Ahlul beit(a.s.). na pia alimuamrisha Hajjāj aende Iraq na akamwambia, “akavamie na auwe. Kwani zimenifikia habari zenye kunichukiza kutoka kwao. Na ufikapo katika mji wa kufa, ikanyage kiasi cha kuwabana watu wa Basra”. Kisha yeye akabaki anachunguza harakati zao na mambo yao.

“Niliposoma kumuhusu Hajjāj, nilitambua kwamba alikuwa na misimamo mibaya mno kwa maimamu(a.s.) na wafuasi wao, kiasi ambacho historia haijawahi kuelezea mfano wako, haswa kwa mashia wa Iraq. Na kwa kuwa kila alichofanya kilikuwa kwenya ajenda ya Abdul Malik bin Marwan kwa hivyo maana yake ni kuwa alifanya kwa ruhusa yake” “Ni kweli.”.

Kwa upande mwingine, jambo linalo nishangaza, ni hatua aliyo ichukuua Abdul Malik bin Marwān, pale alipogutuka kuona fedha wanazo zitumia zina maandishi kwa lugha ya kirumi. ($18) na alipojulishwa kwamba maana yake ni (Baba, Mwana na Roho mtakatifu), aliudhika mno na akamuandikia mtumishi wake katika nchi ya Misri, ambae ni nduguye aitwae Abdul Aziz bin Marwan. Na akamuamrisha abatilishe hizo fedha na atengeze zingine zenye maandishi ya sura kutoka kwenye Quran tukufu. Na vivyo hivyo aliwaandikia watumishi wake walio kwingineko. Na akawaamrisha kuzibatilisha hizo fedha na kumuadhibu yeyote atakaye patikana nazo baada ya amri hii kutoka”.

“Ewe ndugu yangu, nimefahamu makusudio yako. Ni wengi mno wanao shughulikia udhahiri wa uislamu na wakapuuza mambo ya ndani na ya asili yake. Na Abdul Malik ni mionngoni mwao”.

Hata ingawaje, Mfalme wa Roma alijaribu kumathiri, lakini Abdul Malik hakudhihirisha kuwa mwepesi. Mwishowe mfalme huyo alitishia kumtukana Mtume Mohammad (s.a.w.a.) kwa maandishi yatakayo wekwa kwenye fedha zote za dirham na dinār. Waona vipi serikali kama ya Roma yaweza kuingilia mambo ya serikali nyingine($20) kwa yale yanayo husu fedha zake zinazotumika katika nchi”.

“Haya yalisababishwa na nhi yetu kutokuwa na fedha zake binafsi ilizokuwa ikizitumia”.

“kwani fedha zilizotumika hapa nchini, zilitengenezwa na serikali ya Roma nchini Misri. Na kwa vile ilikuwa ni serikali ya kikristo, iliweka alama ya kikristo”.

Kutokana na hayo, Abdul Malik bin Marwan alijikuta kwenye tatizo asilo weza kulitatua. Alijaribu kutafuta ushauri kwa wasaidizi wake, lakini hata hivyo hakufaulu. Mwishowe alielekezwa kwa al Imam Mohammad bin Ali al Baqir(a.s.).

Al Imam (a.s.) alimshauri atengeze pesa kutokana na dhahabu na fedha, ambazo zilipatikana nchini kwa wepesi. Na pia alimpa kipimo cha kuchunga uzito wa dirham na dinār, na akamshauri aweke alama ya kiislamu.

“Haya ni kweli. Kwani tangu wakati huo tumekuwa na fedha zetu wenyewe tunazo zitumia hapa nchini”.

“Lakini, vipi al Imam Mohammad al Baqir (a.s.) aliweza kumsaidia kiongozi ambae ni dhalimu($22) na akamtatulia tatizo lililo karibia kumuangamiza?”

« Jawabu lake ni jepesi, wala halihitaji kufikiria. Kwani Imamu yeyote aliye Maasum huwa anatanguliza maslahi ya uislamu mbele ya kitu kingine chochote. Hivyo basi al Imam al Baqir (a.s.) alipoona maslahi ya uislamu yanahitajia kusaidiwa kwa Abdul Malik bin Marwan katika kubadilisha fedha za nchi, alifanya hivyo. Siyo kwa ajili ya Abdul Malik bali kwa ajili ya uislamu na waislamu.

Baada ya hapo, kijana huyo alitabasamu kwa furala na huku akiniuliza kama nina swali lingine. Na kwa kuwa maswali yalifikia ukingoni, nilimshukuru kwa ushirikiano wake huo na nikamuombea due njema.

Baada ya kuagana, nilikifunga kitabu changu. Na hapo nilijiona ni kana kwamba nilikuwa kwenye ndoto.($23).