WITO WA JIHAD

Maisha ya Imam Hassan bin Ali(a.s)

Sijui niwaambie nini, na vipi niwasifie!! Kwani mwanadamu sio tu mwili na umbo bali (ubora wake) ni kwa lengo alilomtakia Mwenyezi Mungu. Alipompa alichompa mpaka kamfikisha kwenye cheo cha juu chenye kustahiki heshima na kutukuzwao.

Yeye ni bwana wa viumbe wa Mwenyezi Mungu kwenye ardhi yake, kwa sharti kwamba atumie fikra yake vizuri kwa kile alichompa Mwenyezi Mungu. Nacho ni akili ambayo Mwenyezi Mungu alipoiumba aliiamrisha ije ikaja na akaimrisha irudi ikarudi. Bila ya shaka, ninyi mnajua vyema alivyoiambia baada ya haya. Aliiambia, « Kwa utukufu wangu na fahari yangu, kutokana na wewe nitaadhibu na kutokana na wewe nitatoa thawabu”.

Enyi watu, ikiwa mmemuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kitabu chake ki kweli kwa kutumia akili hii kisha mkakiri na kushuhudia nayo, mimi sasa ninawaulizeni kwa haki ya mlivyo viamini. Nini maana ya kauli yake Mwenyezi Mungu, (Sema mimi siwaombi malipo juu yake (juu ya haya ninayo kufundisheni) ila tu kuwapenda watu wa nyumba yangu walio karibu) ($7)

Na  je, nini maana ya aya hii, (Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu enyi watu wa nyumba (ya Utume) na kukutakaseni kabisa kabisa) ?([1])

Na je, nini maana ya wasia huu wa Mtume (s.a.w.a) kwenu katike siku ya Ghadir (Mimi naacha kati yenu vizito viwili, kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu (ambacho ni) Ahlu beit wangu. Mkishikamana navyo hamtopotea kamwe baada yangu)?

Moyo wangu unakaribia kupasuka kutokana na mawazo. je Imam Hessan(a.s.) hakuwa mmoja katika matu wa myumba ya utume, na miongoni mwa wale waliotajwa kwenye aya za kitabu cha Mwenyezi Mungu, na ambao Mtume (s.a.w.a) alikuusieni huwahusu?!!

Basi je zilikuwa wapi akili hizi za kibinaadamu, jeshi la Banu Umayya lilipo elekea Iraq, alipokuiteni Imam wenu al Hassan bin Ali (a.s.) na kukwambieni, “Hakika Mwenyezi Mungu amevifaradhishia viumbe vyake Jihad na akaipa jina (a “Chukizo”. Kisha akawambia wanaopigana jihadi, (Subirini, hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanaosubiri). Hivyo basi enyi watu, hamtopata mnacho kipenda ila tu kwa kuyasubiria yale mnayo yachukia. Basi tokeni muelekea kwenye kambi zenu za kijeshi huko Nakhila, Mwenyezi Mungu atakurehemuni. Tuangalie, nanyi muangalie. Na tuone, nanyi muone (yale yatakayo tokea).”

je haukuwa Uimamu ni msingi katika misingi ya dini yenu?! Ikiwa ni hivyo, basi kumtii Imam ni kumtii Mtume (s.a.w.a). Basi je ilikuwaje mkapuuza maneno ya Imam wenu al Hassan (a.s), alipokuamuruni kwenda kwenye kambi zenu za kijeshi huko Nakhila?

Na nini kilichokuwa kikisumbua nyoyo zenu na kucheza na hisia zenu, mpaka mkakosa kufahamu njama za Muawia? Akili zenu zilifikwa na msiba wa kughafilika na kuchanganyikiwa mpaka mkajikuta mmepuuza amri ya Imam wanu wa haki. Mkakosa kutii wito wake kwa kujitayarisha kwa vita na kubeba jukumu la jihadi kwa kukubali wito wake. Ni akili zipi hizi zilizo kubali mali ya Muawia badili ya kujitolea kulinda haki?($9)

Hata ikafikia, kutokana na  wingi wa matukio yaliyotokea, Imam Hassan(a.s.) alikata tamaa kutokana na watu aliokuwa nao. Lakini miale ya matumaini ilichomoza pale walipojitokeza Adei bin Hatim, Qeis bin Sa’ad, Ma’qil bin Qeis na ziad bin Sa’sa’ a Tamimiyyi, waliomdhihirishia Imam (a.s.) uaminifu wao na Ikhlas yao kwake. Watu hawa, Walimpa baia Imam (a.s.) (kutoa kiapo cha uaminifu) na kumu ahidi kwenda vitani ili kuinusuru haki na kukabiliana na uasi na fitna. Walipaza sauti zao mbele ya mkusanyiko wa watu waliopuuza wito wa Imam (a.s.) wakiwalaumu na kuwashauri kutoka ili kutekeleza wajibu wao wa kidini.

Imam (a.s.) alifurahishwa na watu hawa na aliwasifu kwa msimamo wao wa kikweli kwa kusema, “Mmesema kweli, Mwenyezi Mungu akurehemuni. Bado nawatambua kwa nia za kweli na kutekeleza ahadi na mapenzi yaliyo sahihi. Mwenyezi Mungu awalipe mema.”($11)

Huenda watu wakarudi kuinusuru haki na kuutetea uislamu. Haya ndio yaliyokuwa matumaini ya Imam (a.s.) kutoka kwao. Hivyo basi alianza kwa kupanga jinsi vikundi vya kijeshi vitakavyo ongozwa. Alimteua bin ami yake alieitwa ubeidullah bin Abbas na alimtuma pamoja na kikundi cha wanajeshi wa mbele kama utangulizi wa jeshi hilo. Alimwambia”, Ewe bin ami yangu, natuma pamoja nawe watu elfu kumi na mbili. Moingoni mwao, wako wapanda farasi bora katika waarabu, na mahafidhu bora wa Qur’an ardhini. Mtu mmja kati yao, anashinda kikosi kizima (cha jeshi). Nenda nao na uwe mnyenyekevu kwao. Uwakunjulie uso wako (kwa tabasamu), na uwakunjulie mbawa zako (uwahurumie) na uwakurubishe kwenye vikao vyako. Kwani hawa ndio waaminifu waliobakia wa Amirul Muuminin(a.s.)”.

“Nenda nao kupitia pembezoni mwa ziwa la Furati. Na muendelee mpaka mkutane na jeshi la muawia. Mkilipata, mlisubirie hadi litakapo kuja kwani mimi nakufateni haraka. Na usilipige jeshi la Muawia ila wakikupigeni. Wakifanya hivyo basi muapige. Na ikitokea ukauwawa, basi Qeis bin Saad aliongoze jeshi. Nae akiuwawa basi Said bin Qeis achukue mahala pake katika kuliongoza($13) jeshio.

Vikosi vya wanajeshi vilipopiga kambi kwenye kijiji kilichopo pembezoni mwa mto wa Dujeilu (Dijla), katika nchi ya Iraq, Imam Hassan(a.s.) alikuwa tayari amewatangulia na kukiongoza kikosi kingine cha kijeshi kilicho piga kambi kwenye eneo la Madhlani Saabaat karibu na mji wa Madaina.

Enyi watu, sasa nayaelekeza mazungumzo yangu kwenu. Je ni akili na dhamiri zenu ambazo ziliwafanya mkusanyike na muunde jeshi kwenye kambi la Nukheila, au ni kwa sababu ya maneno ya mashambulizi na lawama walizo waeleke zea akina Uaei bin Hatam na wengineo miongoni mwa watu wenye busara?

Jambo hili lilikuwa wazi kwenu mlipokuwa mkitembea kwa ulegevu na kujivuta. Mkiwa mmejawa na unyonge, kutafautiana na kufarikiana kati yenu. Je hamjui kwamba mkiwa kwenye hali hii mtakuwa mnamuasi Mwenyezi Mungu? Muawia anadhihirisha waziwazi kumuasi kwake Mwenyezi Mungu ila tu jeshi lake ni lenye kumtil.($14)

Ghafla yanazuka mengine ambayo hayakutarajiwa. Miale ya matumaini aliyokuwa nayo Imam Hassan (a.s.) inapotea. Ni msiba ulioje huo!! Kiongozi wa jeshi alihadaiwa kwa pesa zilizomfanya kuwa mnyonge mbele ya adui alie mnyemelea na kumshawishi katika kiza cha usiku.

Asubuhi ilipofika, jeshi la Imam Hassan(a.s.) likiwa kwenye hali ya kumsubiri kiongozi wao ili awaswalishe swala ya alfajiri, lilipigwa na bumbuwazi lilipomuona kiongozi wao amesimama kwenye safu ya jeshi la Muawia. Hii ndio njia ya karibu aliyoipata Muawia ya kumlazimisha Imam Hassan (a.s.),na ambae Alieneza propaganda zenye malengo mabaya kwenye jeshi la Imam Hassan(a.s.), na pia kutumia mali kwa kununua dhamiri na akili za watu.

Baada ya ubeidullah bin Abbas, kiongozi wa jeshi la Imam Hassan(a.s.) kujiunga na jeshi la Muawia, mnadi wa Muawia alipaaza sauti kwa kuliambia jeshi la Imam Hassan(a.s.) “Huyu kiongozi wenu ambae tuko nae, tayari amembai Muawia. Basi je mnataka kujiua kwa nini?($15)

Muawia aliendelea na njama zake za uchochezi kwa kuwaandikia barua baadhi ya viongozi wa al kufa akiwaahidi mali na kuwatia tamaa ya uongozi. Baadhi yao waliingiwa na tamaa na wakamuandikia wakimharakisha awape alicho waahidi na kumshawishi awaendee huko kufa. Na walimhakikishia ya kwamba watamsalimisha Imam(a.s.) kwake au watamuua kwa siri. Imam (a.s.) aliyajua hayo, hivyo basi alikuwa akivaa nguo zake za vita kila alipotaka kuswali.

Baada ya hayo yote yaliyo tokea, Imam(a.s.) alilazimika kuchagua baina ya mambo mawili. Ima akubali kufa pamoja na ahlul beit zake na watu wenye busara miongoni mwa maswahaba wake kwa kupambana na jeshi la Muawia masaa kadhaa, na baada ya vita Muawia achukue uongozi. Au ampe baia ili azuie kutokea kwa vita na awahifadhi wafuasi wake kutokana na kuangamia na auhifadhi uislamu kutokana na kumalizwa na kurudi upya kwa ujahilia.

Imam(a.s.) alilazimika kufanya sulhu na Muawia($17) ili aweze kujishughulisha baada ya hapo na mambo ya tabligh, kuwafundisha watu na kuwaongoza. Akitumai huenda akili na dhamiri zao zitapokea hii elimu na kuitumia katika kufikiria na katika matendo.

Lakini je, Muawia atatosheka na kiti hiki cha utawala ili aache njama na propaganda zake chafu za kutawala akili na dhamiri za watu kwa hadaa, au  ataendelea na njia yake mbovu hadi amuuwe Imam Hassan(a.s.)?

Ni kweli, Muawia hakupata utulivu hadi alipompa muuwa  Imam (a.s.)kwa sumu kupitia kwa  Ja’ada binti ya Ash’ath (Mkewe Imam Hassan (a.s.)) baada ya kumpa ahadi nyingi za uongo.

Kwa njia hii, Muawia alivunja mkataba wa sulhu waliyoandikiana na Imam Hassan (a.s.) ambayo alikuwa akijistiri nayo na kudhihirisha uislamu wake wa uongo.($19)


[1]Surat Al Ahzab 33: 33.