FATIMA KAUTHAR

Ewe fatima, ewe wmenye kushangaza zama.Ewe dalili ya mwenyezimungu.Ewe moyo wa mohammad ambae umefunikwa chini ya kisaa.
Ewe kauthar mwenye huruma kwa mayatima,mateka (wafungwa) na masikini,na kwa ajili yako ikateremka kuoka mbinguni sura kamili ya Al insaan.Siku ya kiama malaika atanadi ((fumbeni macho na inamisheni vichwa chini mpaka fatima avuke siraat (njia).Hii ni katika khususia (sifa)zak pekee.
Ewe ua la moyo wa mtume mohammad, wakati wote uko hai na wakati wote ni wa milele ewe shahiid.

FATIMA (A.S) KABLA YA KUOLEWA.

Fatima kabla ya kuolewa alikuwa ni mwenye ku jitihada na mwenye kujituma katika kuutumikia uislaam.Kupewa utume baba yake kulimfanya awe na furaha na uchangamfu katika moyo wake,na kulimfanya awe na hisia za uhakika na utukufu,hisia ambazo zilimpelekea kufanya jitihada za kupambana na jamii ya waabudu masanam,kuondoa ujahili na ujinga.
Fatima ni mtu ambae kutokana na ukubwa wa kima anawia ,ukamilifu wa kimaumbile,na kutokana na sifa hizi aliweza kuupa uchangamfu moyo wa baba yake.Mtime (S.A.W.W.)kabla ya kisa cha kauthar cha Fatima (A.S)alifarijika kutokana na kizazi chake ambacho kilitokana na mama mwenye mapendo yaani Bibi Khadija (A.S)ambae ni mama wa Fatima,na sifa hii aliyonayo Bibi Khadija ndio iliyo muonyesha na kumfanya aonekane kuwa ni sawa na chombo chenye ua ndani yake na ua hilo ni mwana Fatima (A.S),na vilevile sifa moja wapo ya Bibi huyu ni kuwa mama wa Fatima (A.S).

HARUSI YA FATIMA

Harusi yake iliandaliwa mbinguni ,aliolewa na mtu ambae jina lake linatajwa mbinguni,na kuwepo kwake Fatima ni nguzo yake,na vitu vyote baada ya kutajwa kwa jina lake vina pata utulivu,nae si mwingine bali ni sayyidina Ally (A.S)na asingelikuwa yeye katika ulimwengu huu basi asinge patikana wa kumuoa Fatima(A.S),kwani Ally(A.S)ni mfan wa Fatima (A.S)
Katika cheo cha kimaanawiya,kwa hivyo basi tunaikuta ndoa ya Bibi Fatima
(A.S)na Imam Ally (A.S)ni nuru juu ya nuru.
Fatima (A.S) ni moyo wa mtime (S.A.W.W)na kwa ajili hiyo haikuwa n vigumu kwake kuanza maisha ya zuhud (kuipa nyongo dunia),tuki zingatia
Kwamba Fatima (A.S) na Imam Ally (A.S)waliwahi kuishi pamoja
katika nyumba ya mtume mohammad (S.A.W.W),kwa hivyo anastahiki
Fatima (A.S) au Imam Ally (A.S) kuwa na maisha ya zuhud,tabia njema n.k.kwani waliweza kuya chyma hayo kwenye nyumba hiyo ya utume.
Harusi ya Bibi Fatima ilikuwa ni yenye mafunzo makubwa na mazuri kwa waislaam na waumini ,kwani tunakuta kwa mfano vitu vilivyo andaliwa kwa matumizi ya nyumbani vilikuwa ni Godro,sufuria,n.k,vitu ambavyo ni vya kawaida na vitoavyo picha kamili ya kuwa Harusi si lazima ifanyike kifakhari
Bali jambo la muhimu ni kutimiza kile kinacho hitajiwa na Mwenyezi Mungu kutoka kwa waja wake yaani ndoa.

NDANI YA NYUMBA YA FATIMA.

Katika nyumba ya Fatima yaliongelewa matukio ya vita vya mtume (S.A.W.W)kama vile Khandaq,Khaibar,n.k,na vilevile yaliongelewa matukio ya ushindi wa imamu Ally(A.S)katika vita hivyo na vinginevuo,kama ambavyo ziliongelewa katika nyumba hiyo habari za Jibraailul amiin(A.S).
Basi amani ya mwenyezimungu iwe juu ya nyumba ya Fatima. 

UGONGAJI MLANGO WA FATUMA

Imenukuliwa kutoka kwa Ummu aiman ya kuwa amesema:
Fatima (A.S) alikuja nyumbani kwa mtume (S.A.W.W)na kugonga mlango,
Mtime (S.A.W.W)akamwambia Ummu Aiman ugongaji huu wa mlango ni wa Fatima.ummu Aiman akamwambia mtume (S.A.W.W)kwa mshangao ni hisia gani na uaminifu gani ulio nao hata unapo gongwa mlango unamfahamu mgongaji?.Mtume (S.A.W.W)akasema na kumjibu kwa mshangao ni maisha gani ya kupendeza aliyonayo Fatima (A.S)hata anapo gonga malngo hujulikana kuwa yeye ni Fatima(A.S).Kutokana na riwaya hii tuna kuta kwamba ugongaji wake wa mlango ulikuwa ni wa aina ya pekee, na vilele mtume (S.A.W.W)aliweza kumfahamu Fatima kupitia njia mbali mbali. 

FATIMA NI MKUBWA KIMA ANAWIA

Maisha ya mtume na roho ya mtume vina nafasi kubwa kwa Fatima,kama vile ambavyo mtume hakuwahi kuabudia masanam,kwa dalili hii kutokana na utukufu wa mtume Fatima anakuwa mfano wa baba yake kima anawia,pamoja na kwamba kuna tofauti ya kima anawia kati ya Fatima na baba yake.Na kama ilivyo pokelewa katika hadithi.
((kumuudhi Fatma ni sawa na kumuudhi Mwenyezi Mungu na kumridhisha Fatima ni sawa na kuridhisha Mwenyezi Mungu)).
Mwili wake na moyo wake umebobea katika mapenzi ya Mwenyezi Mungu,kwa mfanio huu MwenyeziMungu alitaka watu wajue nafasi ya Fatima (A.S)ambae ni mja mtii
fu. Na ndio maana Mwenyezi mungu akamfanya kuwa alama ya ghadhabu zake na radhi zake.
Vile vile imenukuliwa riwaya kutoka kwa mtume (S.A.W.W)ya kuwa amesma:
((Mwenye kumghadhibisha Fatima amemghadhibisha Mwenyezimungu na
Mwenye kumridhisha Fatima amemridhisha Mwenyezimungu)).
Kwa hivyo basi kila ambae ameridhiwa na Fatima Mwenyezi Mungu nae amemridhia na kila ambae Fatima amemghadhabikia Mwenyezi Mungu amemghadhabikia.
Kuna riwaya nyingi ambazo Mtume ame elezea ndani yake ubora,fadhila ,na cheo na ukubwa wa kima anawia wa Fatima (A.S).
Kwa ufupi hii ni historia fupi ya maisha ya na uhai wa Fatima (A.S).

TAWASSUL YA HADHRAT ADAM KWA FATIMA.

Imenukuliwa kutoka kwa ibnu Abbas ya kuwa amenukuu kutoka kwa Mtume (S.A.W.W)kuhusiana na neno ambalo alilipokea Adam kutoka kwa mola wake na kwa neno hilo akatubia kwa Mwenyezi Mungu.Ibnu Abbas akamuuliza Mtume , ((Ni neno gani hilo?))Mtume akajibu: Neno hilo ni kwa haki ya Mohammad,Ally,Fatima,Hassan na Hussen,na akatubia kupitia neno hilona toba yake kukubaliwa.

KUTOPATA HEDHI KWA HADHRAT FATIMA.

Imenukuliwa kutoka kwa Imam Swadiq (A.S)ya kuwa amesema:
(( Fatima (A.S) tangu alipo itwa Fatima aliepushwa na damu ya hedhi))

FATIMA AME EPUSHWA NA MOTO WA JAHANNAM.

Mtume (S.A.W.W)alisema((Je unafahamu kwanini umeitwa Fatima?wakati huo Imam Ally (A.S)akauliza,Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni kwa nini ameitwa Fatima?Mtume akajibu:Ni kwa sababu Mwenyezi Mungu amemuepusha huyu na kizazi chake kutokana na moto wa jahannam.

MALIPO KWA WENYE KUMPENDA FATIMA.

Imam Ridhaa (A.S) amenukuu kutoka kwa mababa zake,kutoka kwa Mtume imenukuliwa ya kuwa amesema: Mwenyezi Mungu amemuepusha mwanangu Fatima na watoto wake na kila mwenye kumpenda Fatima kutokana na moto wa jahannam.

FATIMA NI MALAIKA WA KIBINADAMU.

Ibnu Abbas amenukuu kutoka kwa Mtume (S.A.W.W)ya kuwa alisema :Mwanangu Fatima ni malaika wa kibinadamu,hapati hhedhi na wala hana uchafu mwingine,Mwenyezi Mungu amempa jina la Fatima basi yeye na wapenzi wake wameepushwa kutokana na moto wajahannam.

MACHUNGU YA FATIMA NI MACHUNG YA MTUME.

Mtume (S.A.W.W)amesema ((Fatima ni kipande cha mwili wangu,mwenye kumuudhi Fatima ameniudhi mimi.

FATIMA NI MBORA WA WANAWAKE WA DUNIANI.

Mtume (S.A.W.W)amesema :mwenyezi Mungu amewachagua wanawake wanne bora miongni mwa wanawake wa ulimwenguni nao ni Maryam,Asia,Khadija na Fatima.
Pia Mtume alimwambia Fatima :je huridhiki kuwa ni mbora wa wanawake wa duniani?na kuwa mbora wa wanawake katika umma huu?.
Pia Mtume alimambia Fatima :je huridhiki kuwa mbora wa wanawakewa pepni?

NAFASI YA FATIMA KWA MTUME.

Mwana Aisha amesema :Sijamuona mwnye kumfanana zaidi Mtume katika uzungumzaj mfano wa Fatima,kila wakati Fatima alipo kuwa akiingia nyumbani Mtume akimnyanyukia na kumbus na kumkaribisha na kumshika mkono na kumkalisha katika sehemu yake.

FATIMA NI MTU WA MWANZO KINGIA PEPONI.

Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema ((Mwenye kunadi atanadi,enyi jamii ya viumbe fumbeni macho yenu mtoto wa Mhammad apite.
N imenukuliwa katika baadh ya riaya :Inamisheni vichwa na fumbeni macho mpaka Fatima avuke siraat (njia)bsi atapita hli ya kuwa ameandmana na watmishi sabini elfu wa pponi.
Mtume wa Mwenyzi mungu limwambia Ally :Watu wa mwanzo kuingia peponi watakuwa ni mimi,wewe,Fatima,Hassan,na Hussen.Hadhrat Ally akaliza je vipi kuhusu masha wetu?Mume akasema wtaingia nyuma yetu.

KISA CHA SHAHADA.

Tukio liumizalo ni tukio la watu watatu kati ya muhajirina ambao ni Omar,Abubakar,na Abu ubaida pele walipoelekea katika thaqifa ya bani aida ili kuwabana maanswari na kushughulikia suala la ukhalifa baada ya Mtume,ili ajivike cheo mmoja baada ya mwingine.

Omar alimtuma mtu akamtafute Abubakar na Abubakar alikuwa nyumbani kwa Mtume na baadhi ya muhajirina na ma nswari na Imam Ally watu ambao walimpa kiapo cha utii katika Ghadir khum.Twabari anasema omar alikuja nyumbani kwa mtume kumtafuta Abubakar,Abubakar alikuwepo na Ally alikuwa akishughulikia maiti ya mtume,Omar alimuita Abubakar naAbubakr akasema nina shughuli.

Omar akmtumia ujumbe kwa mara nyingine na kumjulisha ya kuwa kuna mmbo yametokea ni lazima uwepo.Abubakar akatoka na Omar akmwambia je unafahamu ya kuwa answar wamekusanyika katika thaqifa bani saida ili kumchagua wamchague saadi bin ubaada kuwa khalifa?basi wakashika njia kuelekea huko na walipo kuwa njiani walikutana na Abu ubaida na wote watatu wakaelekea katika Thaqifa.

Mambo yote hayo yalifnyika kwa siri na kwa uficho,billa kutoa habari kwa watu,hata kwa wakubwa wa rai na wenye vyeo,na wakati huo wakasema ya kuwa hayo yalikuwa ni makubaliano ya ummaau watu woote,je nikweli umma wa kiisalam ulishirikishwa?Enyi watu wenye inswafu(uadilifu) ij maa ya umma iko wapi?historia kamwe haituonyeshi ispokuwa watu watatu tu katika muhajirina.basi yakafanyika yaliyo fanyika na Abubakar akawa khalifa.

Abubakar akchukua uamuzi wa kwenda kwa Ally ili kuchukua kiapo cha utii (Baia) Abubakar na Omar walijua kwamba Ally hawezi kuwapa kiapo cha utii kwa sababu ndie aliestahili kuwa khalifa wa Mtume baada ya kufariki Mtume.

Lbda watu watajiuliza vipi Abubakar alithubutu kuchukua kiapo cha utii kutoka kwa Ally?wakati wanafahamu ya kuwa Ally ni shujaa na asie ogopa?
Jibu ni kuwa:Wo walijua ya kuwa ni moyo (kipenzi)cha mtume Mohammad (S.A.W.W).na vilevile walijua ya kuwa masuala ya utume,na masuala ya kiislam (Dini)na ulinzi aliyafikiria na kuyajli sana,na ilikuwa ni kawaida kwake na watu wake kujitolea muhnga katika Dini,haikuwa taabu kwake kuto jli ushujaa wake na manufaa yake kwa ajili ya Dini.kwake ilikuwa ni bora Dini isimame na mafnikio yake binafsi yakosekane. kwa hivyo basi kutokana na msimamo huu si ajabu Ally kutoa kiapo cha utii kwa Abubakar.

Ibnu kutaiba anasema katika kitabu chake:(Al imama was siyaasa)
(( Abuubakar aliwatuma watu wakamlete Ally ili aje kumpa kiapo cha utii.Na omar akwafuata watu wote.Omar alifika katyika mlango wa Ally na kuwatawanya watu na wote wakatoka nje, na aka amrisha uwashwe moto na akasema:(Nina apa kwa mila ambae moyo wa Omar upo mikononi mwake tokeni nje laasivyo ninaichioma nyumba motona kila alie ndani. Watu wakamwambia Ewe baba wa Hafswa,Fatima yuko ndani ya nyumba, Omar akasema:Hata kama akiwepo ndani Fatima.

Baada ya mazungumzo haya wote walitoka nje na kumpa kiapo ispokuwa Ally.

Na Omar akawa na yakini kwamba Ally amesema:Nina apa sinto toka nyumbani mpak nimalize kuandika Qur an.

Fatima alisimama nyuma ya mlango na kusema:sija ona ujaji wa watu wabaya kama ujaji wenu (yaani sijaona watu wabaya kama nyinyi)mme litelekeza jeneza la Mtume mkaenda kufanya kazi zenu na wala hamkuwa na fikra na sisi na pia hamkutupa haki zetu. Omar akenda kwa Abubakar na kumwambia je watu ambao hawaja kupa kiapo cha utii huchukui kiapo hicho kutoka kwao? Abubakar akamtuma mtumwa wake qunfush na kumwambia nenda ukamlete Ally.

Qunfudh alikwenda kwa Allyna Ally aka muuliza unataka nini?Qunfuhd akajibu:unaitwa na khalifa wa Mtume,Ally akasema:ajabu,inashangaza, kwa haraka wameanza kuzua uongo juu ya Mtume.

Qunfudh akarudi na kumueleza Abubakar kuhusiana na kisa hicho,Abubakar akalia.

Omar akasema usimpe muda mtu huyu ambae hataki kukupa kiapo cha utii.

Kwa mara nyingine Abubakar akamtuma mtumwa wake na kumwambia:kamwambie ya kuwa unaitwa na kiongozi wa waumini ili ukampe kiapo cha utii (Baia)Ally alinyanyua sauti yake na kusema:((Wanadai mdai ambayo hawastahili kuyadi))
Qunfudh akarudi na kufikisha ujumbe .Abubakar akalia.omar baada ya kusikia hivo alinyanyuka pamoja na badhi ya watu na kwenda hadi nyumbani kwa Fatima na kugonga mlango.Fatima baada ya kusikia sauti akapaza sautina kusema:Ewe baba ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu baada yako tuliwafanya nini watoto wa khatwab (Omar)na mtoto wa Quhafa (Abubakar )watu kisikia kilio cha Fatima wakarudi.

Muandishi mwisho aneleza kuwa Omar alimueleza Abubakar njoo twende kwa Fatima kwani sisi tume muudhi,wote wawili wakaelekea kwa Fatima na wakaomba ruhusa ya kuingia,Fatima hakuwaruhusu,bali Ally ndie aliekuja kwa Fatima kuwaombea ruhusa ya kuingia kwa Fatima,na walipofika hadhat zahraa aliridi ukutani na walimsalimia lakini zahraa hakujibu salam yao.Abubakar akasema:Ewe tabasamu la mtume watu wa Mtume (Falia yake)kwangu niwatukufu zaidi kuliko familia yangu,na ninakupenda wewe zaidi kilik mwanangu Aisha na nilipenda kwamba siku aliyo kufa Mtume nami nife baada yake na nisibakie nikiwa hai.Nina jua kwamba wewe unanijua vizuri sana mimi na nina jua utukufu wako na cheo chako,sasa ni vipi nimechukua haki yako na urithi wako ulio achwa kutoka kwa Mtume? Hdhraat zahraa akasema je ikiwa nitawambia hadithi kutoka kwa mtume mtaifanyia kazi?wakasma ndio.

Fatima akasema:Nina apa kwa Mwenyezi Mungu je nyinyi hamkusikia kutoka kwa mtume pale alipo sema,Radhi za fatima ndi radhi zangu,na ghadhabu za Fatima ndio ghadhabu zangu basi kila mwenye kumpenda mwanangu Fatima amenipenda mimi na kila mwenye kumridhisha Fatima ameniridhisha mimi na kila mwenye kumuudhi Fatima ameniudhi mimi?
Wakasema:Ndio tuliisikia hadithi hii kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu.

Fatima akasma:Mwenyezi Mungu na malaika wanashuhudia kuwa nyinyi mmeniudhi mimi na hamkuniridhisha na wakati wowote nitakapo muona Mtume nita washitakia nyie juu yangu.Abubakar akasema:Ewe Fatima mimi baada ya kuku udhi wewe na yeye (Mtume)ninajuta kwa Mwenyezi Mungu na hapo Abubakar ak anza kulia hadi kukaribia kupasuka .

Fatima akasema:Nina apa kwa Mwenyezi Mungu kila baada ya sala nitakuwa nikikulaani wewe.Abubakar haki akilia akatoka nyumbani kwa Fatima na watu akakusanyika pembezoni mwake na aliwageukia na kuwambia:Kila mmoja wenu akalale usiku huu na mkewe hadi asubuhi,na afurahi na familia yake na mimi niacheni katika hali yangu hii,sitaki tena viapo vyenu na kiapo changu ninakichukua mwenyewe.

Watu wakamwambia:Ewe khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu haiwzekani kuachana na maswala haya,wewe ni mjuzi zaidi kuushinda sisi,ikiwa utafanya hivi Dini ya Mwenyezi Mungu itateketea.

Sikufanya hivi ispokuwa ni baada ya kuona na kusikia kile kilichoo kwa Fatima (A.S).

Imam Ally (A.S) wakati wa uhai wa Fatma hakutoa kiapo cha utii ispokuwa baada ya kifo cha Fatima.Na alitoa kiapo hicho kwa hekima na kw sababu maalumna na wala haikuwa ni kwa kuridhia ya kuwa Abubakar ni kiongozi. Fatima baada ya kifo cha baba yake hakuishi zaidi ya siku sabini na tano.

KUCHOMWA MOTO KWA NYUMBA YA FATIMA.(A.S)

Mmoja katiya waandishi wa hadidhi aitwae masood anatubainishia;Siku ya baia lilipelekwa kundi nyumbani kwa Fatima na kuunguza mlango,na walimtoa Ally kwa nguvu ndani ya nyumba yake na walimbana mbora wa wanawake yaani Fatima kati ya mlango na ukuta hadi mimba ya muhsin kutoka. Na vile vile bwana nadhaam anaelezea kuhusu tukio hili na anasema:Katika siku ya baia omar alisukuma mlango na dharuba ya mlango ilimfikia Hadhrat Faima Zhraa (A.S)na dharuba lile lilipelekea mimba ya fatima kutoka. Hivi ndivyo ilivyo unguzwa nyumba ya wahyi na utume,nyumba ambayo kizazi cha Ahlul baiti kitaendelea kupitia hapo.

Omar binil khatwab akiwa n kijinga cha moto mkononi alielekea nyumbani kwa Fatima akifuatana na khalid bin waliid,Mohammad bin Muslim,usaidi ban khudhair qunfudh, pamija na watu wenye kuabudu Dunia na walio tawaliwa na shetani,na hapo omar akampa qunfudh kijinga cha moto na kumuamrisha achome mlango wa nyumba na qunfudh akafanya kama alivyo amrishwa.Wakati huo Fatim alikuwa nyuma ya mlango akizungumza nao,na mlango wa nyumba ukasukumwa kwa nguvu na kumbana Fatima kati ya mlango na ukuta.Wakati huo Omar alikwenda mbele na kupiga tumbo la Fatima na mimba ya muhsin kutoka huku Fatima akipiga kelele ((Ewe baba,ewe Mtuma wa Mwenyezi Mungu))

SHAMBA LA FADAKI.

Fadaki ni zawadi ya Mtume kwa Fatima,baada ya Mtume kufanya mkataba wa suluhu na mayahudi ndipo alipo pata shamba hili.Na aya ikateremka ikisema ((Wape watu wako wa karibu haki zao))na ndio akamzawadia Fatima shamba hilo la Fadak.Alimzawadia katika zama za uhai wake ili iwe ni mali yake.Fadak lilikuwa ni shamba kubwa na lenye kutoa mazao kwa wingi.Baada ya kifo cha Mtume abubakar alidai ya kuwa Fadak ni mali ya waislaam,na mavuno yapatikanayo kwaka shamba hilo la Fadak ni mali ya baitul maal,kwa sababu Mitume hawarithiwi baada kufari kwao. Hii ilikuwa ni hukumu ya Abubakar na hukumu hii ya bwana huyu inapingana na Qur an tukufu. Wakati Fatima alipo kuwa akimiliki shamba la fadaki mapato yote ya shamba hilo aliwapatia wanyonge na wasio jiweza. Fatima alimwambia Abubakar :je katika Qur an ime elezewa ya kuwa wewe umrithi baba yako na mimi nisimrithi baba yangu?kwa hakika umeongopa na umezua uongo (umeleta jambo jipya)je unajua ya kuwa Qur an inasema((Na Sulaiman alimrithi Daud)).Navile vile katika kisa cha Zakaria ((Na unipe mimi walii atakae nirithi na atakae rithi kizazi cha yaquub)) Abubakar alitoa dalili kuwa amesikia hadithi kutoka kwa Mtume na riwaya hiyo hakuna alie inakili aspokuwa Abubakar na mwanae Aisha.Amesema nilimsikia Mtume akisema : ((Mitume hawarithiwi na waviachavyo ni sadaka))na yeye hajui ya kuwa haya ni madai yake na tuhuma kwa Mwenyezi Mungu,kwa sababu haiwezekani Mwenyezi Mungu asajili hukumu kwa Abubakar peke yake na wengine wasiwe na habari.wakati ambapo wahyi ulitelemka katika nyumba ya Fatima.Na vile vile Mtume katika kila hkumu iliyo teremka,kwanza alianza kwa kuwafahamisha watu wa nyumbani kwake akiwemo Fatima na Ally (A.S). Na lengo la Fatima lilikuwa ni kuonyesha kwamba kilicho fanyika ni makosa na upingaji.Na alitaka maneno haya ya Mwenyezi Mungu yawafikie watu na akasema ((Hakuwa Mohammad ispokuwa ni Mtime wa Mwenyezi Mungu na walipita kabla yake Mitume je akifa au kuuwawa mtarudi katika imani zenu ?)) kwa hivyo basi tuna kuta katika haya yaliyo tokea ilikuwa ni kutaka kuonyesha na kuwafahamisha watu haki ya Ahlul bayti na Dhuluma waliyo fanyiwa.