Kwa Nini Mtume Muhammad [s] Alioa Wake Wengi

Kimeandikwa na : Jumuiya ya Dar-Rahe-Haq

Kimetafsiriwa na: Maalim Dhikiri Omari Kiondo

SHUKRANI

Kitabu hiki kiliandikwa kwa lugha ya Kiajemi na Jumuiya ya "Dar-Rahe-Haq" ya mjini Qum (Iran).

Kilitafsiriwa kwa Iugha ya Kiingereza na kutiwa nyongeza fulani fulani na Haji Ahmad Hussein Sheriff na kutangaziwa na Jumuiya A Group of Muslim Brothers" S.L.P . 2245, Tehran, Iran (ambayo siku hizi huitwa "World Organization for Islamic Services (WOFIS).*

* Tafsiri hiyo ya Kiingereza iliitwa "Philosophy of the Marriages of the Holy Prophet Muhammad [s].

Kimetafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kutoka hiyo tafsiri ya Kiingereza na Bwana Jukaeli J. Shou wa Dar es SaIaam, Tanzania.

UTANGULIZI

BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIM

Mwanzoni mwa karne ya kumi na nane waandishi wa Kikristo waligundua mbinu mpya za kuushambulia Uislamu. Nia yao ilikuwa ni kuyaeneza maandishi yasiyo na ukweli ili kupotosha watu kutoka katika lengo na msingi mathubuti wa Kiislamu na kuitweza heshima ya Mtume wetu Muhammad [s].

Kiini cha uzushi huo kilikuwa ni vitabu vilivyoandikwa na waandishi wa Kikristo wa karne ya kumi na tano Mwandishi moja aliwahi kuandika kitabu kiitwacho "Refutation to the Religion of Muhammad (Kuikanusha Dini ya Muhammad)", ambacho ndio msingi wa waandishi wengine waliofuata katika kuipinga dini ya Kiislamu. Waandishi hawa, hawakujua ukweli wa mambo kuhusu Uislamu kwa sababu walikuwa hawana ujuzi wa lugha ya Kiarabu, na hali vitabu vya historia ya Kiislamu na Vitabu Vitakatifu vilivyopatikana katika zama hizo viliandikwa kwa Kiarabu.

Kwa hiyo, haikuwa ajabu kwa Waandishi hao kuandika maandishi ya kumpinga Mtume wa Uislamu na kumuambia kuwa alikuwa na tamaa ya wanawake kwa sababu ati alioa wanawake wengi ambapo Waislamu wengine waliruhusiwa kuoa wanawake wane tu. (Waandishi hao walisahau kwamba waandishi wa Biblia la siku hizi wamewashtaki Manabii wao kwa kuwa na tamaa ya zinaa!).

Hakika1 kwa kutowaeleza ukweli ndugu zao Wakristo, na kumsingizia Mtume wa Islamu [s] waandishi hao walitumainia kuyasimamisha maendeleo ya haraka ya kuenea kwa dini ya Kiislamu. Lakini mbinu hizi hazikusaidia vizuri. Tunawaona wanachuoni wa Kikristo wenye busara wakimtetea Mtume [s] dhidi ya masingizio hayo kwa kuyahanusha.

Bila shaka hadithi hizi za masingizio kwa mtume [s] hazikubaliwi hata kidogo na Waislamu, kwa sababu sehemu ya imani yao ni kuiamini "Ismat" (Utakatifu au kutokosea) ya Mitume [a].

Wakatii huo huo ni muhimu (kwetu sisi Waislamu) uwafahamisha wale wasio Waislamu ukweli wa mambo.

UAMUZI WA HISTORIA

Wanahistoria waadilifu wa Kiislamu na Wakikristo wote kwa pamoja wanakubaliana kuwa ndoa alizosifunga Mtume wa Islamu [s] hazikusababishwa na tamaa ya kuitosheleza ashiki yake. Kama ingekuwa hivyo, basi hangemuona mwanamke aliyekuwa mjane mara mbili, aitwae Khadija, mwenye umri ya miaka 40 na yeye Mtume wa Islamu [s] akiwa kijana wa umri wa miaka 25 tu, umri ambao mtu huwa katika kiwango kamili cha ashiki.

Mtume Muhammad [s] aliishi na mke wake wa kwanza (ambaye wakati ule alikuwa mkewe peke yake), Bibi Khadija [a] kwa furaha, kwa mapenzi na uelewano mkubwa, kwa muda wa miaka 26 ingawaje wasichana wazuri wa Uarabuni waliweza kupatikana kwa urahisi na walikuwa tayari kuolewana na Mtume [s]. Munda wote huo (wa miaka 26) Mtume [s] hakuoa mke mwingine. Bila shaka Mtume [s] angelifikiria kuoa mke mwingine aliye na umri mdogo kuliko ule wa Bibi Khadija [a] wakati alipokuwa na Bibi Khadija [a], kama angelikuwa mwenye tamaa za kiashiki na mpenda wanawake; nasa wakati ule ambapo desturi za nchi yake zilikubaliana na ndoa za wanawake wengi.

WAPINZANI WANYAMAZA

Hebu tuyaangalie maisha ya Mtume wa Islamu [s]. Tunaona kuwa katika umri wa ujana wake aliridhika kuwa na mke mmoja aliyekwishakuwa mjane mara mbili na mwenye umri mkubwa na wala (Mtume [s]) hafikirii mwanamke mwingine. Kisha tunaona kuwa, katika miaka 10 ya mwisho ya maisha yake, akiwa na umri wa zaidi ya miaka 50, akiwa katika uzee wake na akiwa amezungukwa na matatizo mgumu sana ya dola mpya ya Kiislamu, alianza kuoa wake wengi.

Hebu waulize waandishi hawa wa Kikristo, "kwa nini itukie hivi?"

Ni jibu gani la kihoja wapinzani hawa wawezalo kulitoa kwa swali zuri kama hili?

Je, si jambo gumu na mzigo mzito kuoa wajane na kuwatunza yatima? Je, lilikuwa jambo rahisi kwa mtu mwenye hekima kama Mtume Muhammad [s] kuoa wanawake wa maumbile mbali mbali, tabia na wa makabila tofauti na kati yao wakiwemo wanawake vijana mno ambao bado hawauelewa wajibu wa maisha?

Hebu natulifikirie jibu lifuatalo ambalo limeelezwa na Mwanahistoria wa nchi za magharibi Bwana Thomas Carlyle kuyajibu maswali hayo hapo juu, katika kitabu chake kiitwacho "Heroes and Heroes Worship" Yeye anasema kinyume na vile maadui wake Mtume [s] wanavyomshitaki. Anasema, "Muhammad hakuwa na tamea ya kiashiki, hivyo ulikuwa usingizio utokanao na chuki na hakika huu ni udhalimu mkubwa".

Bwana John Devenport anasema, "na, mtu anaweza kuuliza kama inawezekana kwa mtu mwenye tamaa za kimwili, wa nchi ambayo tabia ya kuoa wake wengi ilikuwa ni jambo la kawaida, na katika muda wa miaka hamsa-wa-ishirini ni ambaye yu mkubwe kuliko yeye mwenyewe kwa umri wa miaka kumi na mitano."

ORODHA YA MAJINA YA WAKEZE MTUME [s]

Baada ya kifo cha mke wake wakwanza Bibi Khadija [a] Mtume [s] alioa wanawake wafuatayo:

(1) Saudah, (2) Ayisha, (3) Umus-Salamah bint Khuzaimah, (4) Zainabu Binti Jahash, (5) Ummu-Habibah (Ramla), (6) Mayimunah, (7) Zainab bint Umais, (8) Juwairiyah, (9) Safiyyah na (10) Khaulah binti Hakim.

Hebu tuyechunguze matukio na hali zisizosababisha ndoa hizi kufungwa. Ukweli ni kuwa, tunaweza kusema kuwa ndoa hizi zilifungwa kwa moja au zaidi ya sababu hizi zifuatazo:

Kwa sababu ya kuwatunza watoto yatima na mama zao waliokuwa wajene. Wajane hawa walikuwa ni Waislamu ambao hapo awali walikuwa wakipata heshima kubwa katika jamii ya Kiarabu. Lakini baada ya vifo vya waume wao, hadhi zao na hata imani zao zilikuwa hatarini, kwa sababu watemi (machifu) wa makabila yao wangewachukua na kuwalazimisha kuikana dini ya Uislamu na hivyo wangelirudi ukafirini tena.

Kwa mfano Bibi Saudah (r.a.) alihamia Uhabeshi na huko mume wake alifariki, hivyo alikuwa hana msaidizi ye ypte. Wakati huo ambapo Mtume [s] naye alikuwa keshafiwa na mkewe wa kwanza Bibi Khadija [a], hivyo alimuoa Bibi Saudah (r.a.).

Vivyo hivyo, Bibi Zainabu binti Khuzaim (r.a.) naye alikuwa mjane mwenye umri mkubwa ambaye baada ya kufiwa na mume wake alibaki katika hali ye umaskini, ingawa alikuwa mwenye tabia njema na aliyejulikana sana kwa jina la "Ummul-Masaakin (Mama wa maskini)". Mtume [s] alimuoa Bibi Zainab (r.a.) ili kuendeleza hadhi yake na baadaye Bibi huyu alifariki kwa uzee, miaka miwili tu tangu kuolewa na Mtume [s].

Kwa madhumuni ya kuzithibitisha umri mpya (Mwenyezi Mungu) na kuondoa uonevu uliokuwa unaendelezwa na makabila yasiyostarabika. Kwa mfano Bibi Zainab bint Jahash (r.a.) alikuwa ni binti wa shangazi yake Mtume [s]. Bibi huyu aliolewa na Bwana Zaid bin Haritha kwa mapendekezo ya Mtume [s]. Bwana Zaidi bin Haritha (r.a.) alikuwa huria wa Mtume [s] na akamfanya mwanawe wa kulea. Ndoa hii ilifungwa kwa ajili ya kuondoa ubaguzi kati ya watumwa maskini na kusisitiza usawa na udugu wa Waislamu, kwa kuwa Bibi Zainab (r.a.) alitoka katika ukoo wa Bwana Abdul-Muttalib [a] babu yake Mtakatifu Mtume [s] na mtemi wa Waquraishi, ambapo Bwana Zaid (r. a.) alikuwa mtumwa huria wa Mtume [s].

Kwa bahati mbaya, kwa sababu ya majivuno ya Bibi Zainab (r.a.) kuhusu ubora wa familia yake, Bwana Zaid hakuweza kuishi na mke huyo, ingawaje Mtume [s] aliwasihi ndoa yao iendelee. Tofauti hizo zilizaa talaka. Wakati huo, mtindo wa watoto wa kulea ulikuwa umekatazwa na Mwenyezi Mungu (Qur'ani 33:45). Kwa hiyo, Bwana Zaid (r.a.) alipomtaliki Bibi Zainab (r.a.), Mtume wa Islamu [s] kwa amri ya Mwenyezi Mungu, (Qur'ani 33:37) alimuoa Bibi Zainab (r.a.), na hivyo basi aliiulia mbali imani iliyokuwepo isemeyo kuwa watoto wa kulea walikuwa sawa na watoto wa kuzaa na kuwa wake au wajane wa watoto wa kulea walikuwa sawa na wakawana wa watoto wa kuzaa.

Kwa madhumuni ya kuwapa uhuru wafungwa na watumwa. Kwa mfano Bibi Juwairiyah (r.a.) alikuwa wa ukoo wa kabila maarufu wana wa Bani Mustalaq. Kabila hili lilipopigana dhidi ya Kiislamu na kushindwa na Bibi Juwairiyah ambaye ni binti wa mtemi wa kablia hilo, alichukuliwa mateka. Mtume [s] alimuoa Bibi Juwairiyah (r.a.) ili kutoa mfano mwema kuhusu jinsi ya kuwalinda na kuwafanyia mema mateka wa vita. Waislamu walipoona kuwa mateka wa vita wamekuwa na uhusiano wakindoa na Mtakatifu [s] waliwaachia mateka waliokuwa wakiwamiliki. Bwana ibni Hisham amesema katika kitabu chake cha Historia (kiitwacho "Sirat Rasulullahi") kuwa zaidi ya familia mia moja za Banul-Mustalaq ziliachiliwa huru baada ya ndoa hiyo.

Kwa madhumuni ya kuyaanganisha makabila maarufu kadha, ya Kiarabu ambayo mara nyingi yalikuwa katika hali ya uadui na pia kuilinda hali ya kisiasa miongoni mwa Waislamu.

Mtume [s] alimuoa Bibi Ayesha bint Abu-Bakar (Abdul Kaabah au Abdallah bin Abi Quhaafah) kutoka katika kabila la Bani Taim, Bibi Hafsa (r.a.) binti Umar bin Khattab kutoka kabila la Adi, Bibi Ummu Habibah (r.a.) binti Abu Sufyani toka katika kabila la Umayya, Bibi Safiyyah (r.a.) binti Huaiy bin Akhtab wa kabila la Kiyahudi la Bani Nazir, na Bibi Mayimuunah (r.a.) kutoka kabila la Bani Makhzuum.

Bibi Ummu-Habibah (r.a.) (Ramla) alikuwa mtoto wa Abu Sufyan wa kabila la Banu Umayya ambaye alikuwa adui mkubwa wa Mtume [s] na alipigana naye mara nyingi. Bibi Ummu Habibah (r.a.) baada ya kusilimu alikuwa katika hali mbaya sana kwani alikuwa ameachwa na mume wake wa kwanza (aliyeingia dini ya Kikristo huko Uhabashi) na wakati huo huo baba yake alikuwa adui mkubwa wa Uislamu.

Mtume [s] alipomuona Bibi huyu katika hali ile, akiwa hana msaada wo wote toka kwa wazazi wake na mume wake kamtaliki, alimuoa kwa kumuonea huruma. Ndoa hii pia ilitowa mfano kwa watu wa Bani Umayya kuilegeza mioyo yao kwa dini ya Kiislamu.

Bibi Safiyyah (r.a.) alikuwa mjane na binti wa Bwana Huaiy bin Akhtab, mmoja wa watemi wa kabila la Kiyahudi la Bani Nazir. Mateka wa kabila hili walipoachiliwa na Waislamu, Mtume [s] alimuoa Bibi Safiyyah (r.a.) kwa madhumuni ya kulinda hadhi ya bibi huyu na pia kwa kufanya hivyo Mtume [s] akajihusisha na moja ya makabila makubwa ya Kiyahudi ya wakati huo na kuyasogeza karibu na Islamu.

Bibi Mayimuunah (r.a.) ambaye Mtume [s] alimuoa katika mwaka wa 7 baada ya Hijja, akiwa na umri wa miaka 51 na alitoka katika kabila maarufu sana la Bani-Makhzuum.

Historia iliyoelezwa hapo juu, ya ndoa za Mtume [s] inaonyesha wazi umuhimu wa madhumuni hayo ya kuoa wanawake kadhaa. Si ngumu hata kidogo kuona kuwa hakuna hata ndoa moja ambayo madhumuni yake yalikuwa kuridhisha tamaa za kimwini za kibinafsi kama wasemavyo waandishi wa Kikristo wanaomlaumu Mtume [s] . Pia ni muhimu kukumbuka kuwa ndoa hizi zote, ila ile ya Bibi Ayesha (r.a.), zilifungwa na wanawake waliokuwa wajane, si mara moja tu bali mara mbili au tatu.