rudi maktaba >Masimulizi >Yaliyomo >

D A J J A L

Ni neno la Kiarabu likimaanisha mhaini mkubwa na mleta balaakubwa mno.Hivyo wale wote walio wahaini na waleta balaa basi wajijue kuwa wao pia na ma-Dajjalwa zama zetu hizi.Lakini Dajjal anayezungumziwa hapa ni yule ambaye anaitwa Sayyid na utambulisho wake ni Dajjal.Yeye atakuwa ni mchawi mkubwa.Hapo mwanzoni atakapojitokeza atadai kuwa yeye ni mtume na baadaye atajiita kuwa yeye ni mungu.Yeye atatokezea pale ambapo Mashariki ya kati itakuwa imekwisha dhoofika kwa sababu ya ukame utakaodumu kwa miaka mitatu kwa mfululizo. Katika mwaka wa tatu kutakuwa hakuna dalili ya majani na hakutakuwapo na mvuakabisa.

Hili jitu lenye jicho moja litakuwa na urefu wa mita ishirini. Jicho lake la kulia litakuwa halifanyi kazi na litakuwa kama donge la nyama nyekundu.Jicho lake la kushoto litawaka kutokea paji la uso.Yeye atakuwa akimwendesha punda mwekundu, mwenye manywele ambaye miguu yake itakuwa mieusi kutokea mifupa ya juu hadi magoti na nyeupe kutokea magoti hadi makwata. Kutasikika sauti ya muziki kutokea nywele zake na za punda wake.

Watu wanyonge,wanawake,Mabedui wa Kiarabu na Kiyahudi watamtii na kumfuata. Dajjalmwenyewe atakuwa Myahudi wa asili ya ukoo wa Qutama na kwa kutokana na udugu wa Abu Yusuf. Kwa hakika watu watamkubalia kama mtume (ingawaje atakuwa ni mzushi) .

Kwa kupatiwa msaada wa wanajeshi sabini elfu wa Kiyahudi na wenye silaha na matayarisho yote,yeye ataeneza kila mahala hali ya dhuluma na uoga.Mioyo ya watu itajawa kwa khofu na hatari. Wakati huo,Jerusalemundio itakapokuwa mahala pa usalama kwa sababu Mtume Issa a.s. atateremkia. Imam Mahdia.s. atafika hapo pia. Hapo kutatokea vita vikali na Mtume Issaa.s. atamwua Dajjal.Wayahudiwataangamizwa.Ulaji wa nyama ya nguruwe utaachwa.Hakutakuwapo na alama za Msalaba.Na hapo kutakuwapo na Dini moja tu duniani -- ISLAM.

Mapokezi yafuatayo yametolewa kutoka Kitabu cha Kamal-ud-Din ambamo Muhammad Ibn Ibrahim anarikodi kama Hadith sahihi iliyopokelewa na Ibn Sabra,anayesema:

"Wakati mmoja Imam Amir-al-Mominiin Ali ibn Abi Talib a.s. alituambia hivi:

Sifa zote ni za Allah swt na Salaam ziwe juu yake Mtume Mtukufu s.a.w.w.,na baadaye aliendelea kusema: "Niulizeni kile mukitakacho..."

Saasaan ibn Suhan aliinuka na kuuliza "Ewe Mawla wetu! Naomba utuambie ni lini atakapotokezea Dajjal.

Imam Ali a.s alimwambia aketi na kumjibu. Saasan aliketi na Imam Ali a.s. alianza kuelezea:

"Allah swt amekusikiliza na anajua kile ukitakacho.Zitapita dalili moja baada ya nyingine.Je niwaambieni ?"

Watu waliokuwapo walisema: "Naam tunaomba hivyo, Ewe Abul Hasan ! "

Imam Ali ibn Abi Talib a.s. alianza kuelezea: "Kumbukeni kuwa kabla ya kuja kwake, (1) watu watakuwa wakiiona Sala kama jambo hafifu kabisa. (2)Amana zitakuwa zikichukuliwa kiwizi (3)Kusema uongo ndio itakuwa ikichukuliwa kuwa sahihi (4) Waislamu wataanza kuchukua riba(5) Rushwa itakuwa ni jambo la kawaida (6) Majumba makubwa makubwa na ya fakhari yatakuwa yakijengwa (7 Dini itauzwa kwa matakwa ya dunia (8)Watu watawafanya waovu na hakiri kuwa watawala au viongozi wao [4](9)Wanaume watawataka wanawakeushauri na uongozi (10)Hakutapatikana huruma kokote pale,dunia itakuwa imejaa kwa udhalimu (11) Utumwa utakuwa ni jambo la kawaida [5](12) Mauaji na umwagaji wa damuutachukuliwa kama jambo la kawaida na ubabe (13) Watu wenye ilimu watakuwa wadhaifu na wadhalimu watakuwa wenye nguvu.(14).Watawala watakuwa watu waovu na Mawaziri wao watakuwa wadhalimu (15) Wasufi na wasomaji wa Quranwatakuwa wapumbavu (16) Kutakuwa kukitolewa ushahidi wa kughushiwa (17) Quran Tukufu itakuwa ikirembeshwa kwa nyuzi za dhahabu (18) Misikitiitakuwa ikijengewa minara mirefu (19) Watu waovu watakuwa wakiheshimwa (20)Idadi ya watu itaongezeka lakini wakiikhtilafiana baina yao (21) Ahadi na mikataba itakuwa ikivunjwa kila hapa na pale (22) Wanawake watakuwa wakishirikiana pamoja na wanaumewao kwa uroho wa mali (23) Sauti za Wakomunisti na wapingamizi wa Dini zitakuwa zina nguvu sana. (24).Nao watakuwa wakisikilizwa na kila mtu (25).Viongozi wa Jumuiya watakuwa ndio watu waovu kabisa (26) Watu waendeshao biashara za Mabenki watakuwa wabadhirifu na wadhulumaji (27).Ala za muziki zitakuwa zikipatikana kila mahala na kupindukia idadi. (28).wanawake watakuwa wakipanda mafarasi na wakiendesha magari.(29).Kuiga, hali ya mtu mwingine itaonekana ni kama desturi ya kawaida yaani mwanamme atapenda awe kama mwanamke(ajifanye mwanamke)na mwanamkeatapenda ajifanye kama mwanamme[6].(30).Utatolewa ushahidi katika mambo ya mahakama ingawaje mtoa ushahidi mwenyewe atakuwa haelewi kitu chochote kuhusu kesi inayoendelea lakini atatoa ushahidi wa kiuongo katika kesi yoyote ile itakayokuwa ikiendelea (31).Mbwamwitu watakuwa wengi ,katika makundi ya kondoo.(32) Unafiki utakuwa ndio mambo ya kujivunia .(33) Nyoyo za watu zitakuwa zikinuka kuliko hata maiti na mbaya kabisa kuliko kitu chochote kile (34) Na mahali pa kuishi pema kabisa wakati huo itakuwa ni Jerusalem.Utafika wakati huo mtu atatamani laiti angelikuwa mkazi wa Jerusalem.

Asbagh ibn Nabata alisimama na kusema "Ewe Bwana,naomba utwambie Dajjalatakuwa ni mtu wa aina gani?"

Imam Ali a.s. alimjibu "Yeye atakuwa ni Sayyed .Laana iwe kwa mtu atakaye mkubalia Dajjalna atakuwa mtu mwenye bahati yule ambaye atakuwa amemkana Dajjal.(35).Yeye atatokea karibu na Kijiji kinachojulikana kama Isbahan kutokea eneo la Judea, kutakuwa na toto la jicho katika jicho la kulia .Jicho lake la kushoto litakuwa juu ya paji lake la uso na litakuwa liking'ara kama nyotaya alfajiri, na hapo kutakuwa kipande cha nyama kilichojaa kwa damu. Baina ya macho yake mawili kutakuwa na herufi zilizoandikwa katika Kiarabu Kafir yeye atapita katika mabahari makubwa makubwa.(36).Jua litakuwa pamoja naye.(37).Wingu la moshi litakuwa mbele yake na mlima mweupe utakuwa nyuma yake.(38).Watu waliofikwa na majanga ya njaa watafikiria hiyo milima kama ni chakula,(39) Na punda wake mwekundu atakuwa akitembea mamaili na miguu yake itakuwa ikirefuka na kuwa mifupi kufuatana na ardhi ilivyotambaa.

(40)Maji yoyote atakayokuwa akiyapitia yeye Dajjalyatakauka hadi siku ya Qayama,(41).baadaye atapiga sauti kwa nguvu kwamba kila kiumbe kitamsikia, atasema"Enyi marafiki! Mimi ndiye yule mliyekuwa mkinisubiri,mimi ndiye niliyewaumba,na niliyewafanya nyie mkawa wazuri.Na mimi ndiye mpaji wenu mkubwa sana."

(42).Huyu mwehu wa jicho moja atakuwa mwongo mkubwa sana.(43)Ole wenu, wafuasi wake wengi watakuwa ni wanaharamu na wale waliozaliwa kwa zinaa,(44) wao watakuwa wakijivika vitambaa vya silki,(45) huyo Dajjalatauawa mahala panapoitwa Aqba huko Syria, atauawa siku ya Ijumaa mchana,(46) Mtume Issaa.s. atasali nyuma ya Imam Mahdia.s.(47) na baadaye jambo la ajabu kabisa litatokezea.


[1] Mimi nimekitarjumu kitabu kimoja katika kiswahili juu ya Maudhui haya Katika Islam Uharamisho wa ulawiti. Hivyo unaweza kusoma ukapata kujua ni kwa nini Uislamu umeharamisha ulawiti.

[2] Vitabu vikuu vitukufu vya Allah swt ni vinne.

1. Tawrat - Kilicho teremshwa kwa Mtume Musa a.s

2. Zaburi – Kilicho teremshwa kwa Mtume Daud a.s.

3. Ijili - Iliyoteremshwa kwa Mtume Issa a.s.

4. Qur'an Tukufu – Iliyoteremshwa kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.

Mitume mingi hawakupata vitabu hivi vitukufu lakini walikuwa wanapata vitabu vinavyoitwa Sahifa.

[3] Hapa jambo la busara tunalo ambiwa ni kwamba mfano wa jiwe hilo ni sisi binaadamu ambao kamwe hatutosheki kwa kidogo wala haturidhiki kwa kingi wala hatukinai kwa kingi hadi hapo mauti itakapo fika ndipo matumaini yetu matamanio yetu yatakapokwisha. Tunaona kuwa leo mtu anataka kujilimbikizia mali na utajiri kwa kiasi alicho nacho hatosheki bali anataka kutafuta zaidi na zaidi kwa njia yoyote ile iwe halali iwe haramu yeye mradi ajilimbikizie utajiri. Na Qur'an Tukufu anakumbusha kuwa tutakapofika kabirini ndipo hapo tutakaposhtuka kuona kuwa sasa ndio tumezinduka kutoka usingizini mwetu.

[4] Mambo kama haya ndivyo yanavyotokea katika kupiga kura za kidemokrasia!

[5] Kwa utumwa hapa kunamaanisha mbinu za kumfanya mtu asiweze kusema dhidi ya mambo ya mfadhili wake kama vile tunavyoona na kusikia kuhusu masharti ya misaada itolewayo na nchi na watu wafadhili.

[6] Nimesikia katika Idhaa ya Kiswahili ya BBC mnamo tarehe 17 Novemba 1995 saa 6.30 jioni kuwa Chuo Kikuu cha Al-Azhar University cha huko Misri kimetoa fatwa kuwa mwanamme anaweza kujigeuza k,uwa mwanamke na vile vile mwanamke anaweza kugeuzwa kuwa mwanamme kwa njia za operesheni ati kwa sababu ni maumbile yake ndivyo yalivyo.

Vile vile nimesikia katika idhaa ya Kiingereza ya BBC hivi majuzi (wiki moja kabla ya Fatwa kutoka Al-Azhar) kuwa kumefanywa uchunguzi na utafiti huko Amerika na kutolewa ripoti kuwa mtu khanisi na anayelawiti na kulawitiwa aachwe awe hivyo na wala asilaumiwe na jamii kwa sababu ndivyo yalivyo maumbile yake.