rudi maktaba >Masimulizi >

SAW: SaJlallaahu 'Alayhi Wa-aalih. ni.y. baraka na
rehema za Allah ziwe kwake na kwa Aali zake.
 AS:'Alayhi/'Alayha/'Alayhunia's Salaam, ni.y.
aniani iwe jnu yake/vao.

DHULFA NA JUWAYBIR

Mtungaji: Ustadh Shahid Murtadha Mutahhari

Mtarjumi: Muhammad Ridha Sftusfttary

Siku moja, Mtume Mtukufu SAW alirnwarnbia kijana mcha Mungu aitwaye Juwaybir:

"Ingekuwa v'izuri sana kama ungeoa., ukawa na nyumba na ukamaliza maisha hayo ya kikapera na upweke; na kutokana na ndoa hiyo ukapata haja yako kutoka kwa mke na nike pia akawa ni msaada na nmwenzi wako katika mamho va dunia na Akhera."

Juwaybir akasema: "Ewe Mtume Mtukufu! Mimi sina mali wala uzuri, sina asili wala fasili. Mtu gani atakayenipa mke? Na mwanamke yupi atavutiwa na mwanamume aliye maskini, mfupi, mweusi na mwenye sura mbaya kama yangu?"

Mtume akasema: "Ewe Juwaybir! Kutokana na dini ya Kiislamu, Mwenyezi Mungu amebadilisha thamani na hadhi za watu

"Watu wengi katika zama za Ujahilia walikuwa watukufu, lakini Uislamu ukawadhalilisha.

"Watu wengi katika zama za Ujahilia walikuwa duni na wadhalilifu, lakini Uislamu ulinyanyua daraja na hadhi zao.

"Kutokana na Uislamu, Mwenyezi Mungu ameondoa kiburi cha Ujahilia na majivuno waliyokuwa nayo watu juu ya kabila, nasaba na koo zao.

"Leo kila mtu, awe mweupe au mweusi, Kureshi au asiye Kureshi, Mwarabu au asiye Mwarabu, wote ni sawa sawa na wako katika daraja moja.

"Hakuna mtu aliye bora kuliko mwingine isipokuwa kutokana na uchaji na utiifu wake kwa Mwenyezi Mungu."

Kisha Mtume Mtukufu akamaliza kwa kumwambia Juwaybir:

"Mimi simwoni mtu ye yote miongoni mwa Waislamu aliye bora zaidi kuliko wewe isipokuwa yule aliyekushinda kwa takwa (uchaji) na vitendo bora. Kwa hivyo, tekeleza niliyokuamrisha."

Hayo ni maneno aliyoyasema Mtume Mtukufu alipokwenda siku moja kuonana na masahaba wa Saffa (as'haab Saffah). Na mazungumzo hayo na Juwaybir yakafanyika katika mkutano huo.

Juwaybir alikuwa mwenyeji wa Yamama. huko ndiko alikosikia umaarufu na jina la Uislamu na kuja kwa Mtume wa Mwisho. Ingawa alikuwa maskini, mweusi na mfupi, lakini alikuwa mtu mwenye akili, mpenda haki na mshupavu.

Baada ya kusikia mwito wa Uislamu, akasafiri haraka kwenda Madina ili kujionea mambo kwa karibu.

Haukupita muda mrefu akasilimu na akawa anaufuata Uislamu barabara. Lakini kwa kuwa hakuwa na pesa, nyumba wala jamaa, akakaa katika msikiti kwa amri ya Mtume.

Idadi ya watu waliotoka katika miji mingine na ambao walisilimu na kubaki katika mji wa Madina iliongozeka kidogo kidogo. Watu hao pia walikuwa hohehahe kama Juwaybir na wakakaa katika msikiti kwa amri ya Mtume Mtukufu. Watu hao waliendelea kulala katika msikiti huo mpaka ulipoteremshwa wahyi kwa Mtume Mtukufu kuambiwa kwamba msikiti si mahali pa kuishi na ni lazima wale wanaokaa hapo wahame mahali pengine nje ya msikiti.

Mtume Mtukufu akachagua mahali pamoja nje ya msikiti, akajenga kibanda kimoja hapo, na akawahamisha hapo watu hao. Mahali hapo paliitwa Saffa, na waliokaa hapo ambao walikuwa ni watu maskini na pia wageni waliitwa as’haabu Saffah  (masahaba wa Saffa).

Mtume Mtukufu na masahaba zake walikuwa wakiangalia maisha yao.

Siku moja, Mtume Mtukufu alipokwenda kuwatazama jamaa hao, alimwona Juwaybir. Akawaza njia ya kumtoa Juwaybir katika hali hiyo, na akataka ayainue maisha yake. Lakini jambo ambalo Juwaybir hakuliwaza kabisa (kutokana na hali aliyokuwa nayo) ni kuwa na mke, nyumba na maisha bora siku moja. Na hii ndiyo sababu kwamba wakati Mtume Mtukufu alipompendekeza kuoa, Juwaybir akajibu kwa mshangao: "Kwani inawezekana mwanamke kukubali kuolewa nami?!” Lakini Mtume Mtukufu akamkosoa haraka kosa lake, na akamwambia kwamba hali ya kijamii imebadilika kutokana na athari za Uislamu.

Baada ya Mtume Mtukufu kumtoa makosani Juwaybir, akampa matumaini juu ya maisha mapya na akamwamrisha aende nyumbani kwa Ziyad bin Labiid al-Ansari kumtaka amchumbie bintiye Dhulfa.

Ziyad bin Labiid alikuwa tajiri mkubwa na mheshimiwa katika mji wa Madina. Watu wa kabila lake walikuwa wakimheshimu sana. Wakati Juwaybir alipoingia katika nyumba ya Ziyad, kikundi cha jamaa zake na watu wa kabila la Labiid walikuwa wamekusanyika hapo.

Baada ya Juwaybir kukaa, akasita kidogo, kisha akakiinua kichwa chake na kumwambia Ziyad:

"Mimi nimeleta ujumbe kutoka kwa Mtume Mtultufu. Je, nikuambie kwa siri au mbele ya watu?"

Ziyad akasema: “Ujumbe wa Mtume Mtukufu ni fakhari kwa ajili yangu. Bila shaka, sema hadharani.”

Juwaybir akasema: “Mtume Mtukufu amenituma kwako kuja kumposa binti yako Dhulfa kwa ajili yangu.”

Ziyad akasema: “Mtume mwenyewe amekuambia jambo hili?!!”

Juwaybir akasema: "Mimi mwenyewe sikusema maneno hayo. Watu wote wananijua kwamba mimi si mwongo."

Ziyad akasema: "Ajabu! Si desturi yetu kumwoza binti yetu mtu mwingine isipokuwa yule aliye lahiki (sawa) yake katika kabila letu. Wewe nenda zako, nami mwenvewe nitakuja kwa Mtume Mtukufu kuzungumza naye kuhusu swali hilo."

Juwaybir akaondoka mahali pake na akatoka nje ya nyumba, lakini alipokuwa akienda alikuwa akisema mwenyewe: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu! Yale aliyoyasema Ziyad ni kinyume na mafundisho ya Qur’ani na ujumbe wa Mtume Mtukufu.”

Kila mtu aliyepita karibu na Juwaybir alimsikia akisema maneno hayo pole pole.

Dhulfa binti wa Labiid ambaye alisifikana kwa urembo na uzuri wake, aliyasikia maneno ya Juwaybir. Akaja kwa babake kuuliza kisa chenyewe.

Baada ya kukaa kimya kidogo, Dhulfa akauliza: "Baba, bwana huyo aliyetoka nje sasa hivi alikuwa akijisemea nini na makusudio vake ni nini?"

Ziyad akasema: "Bwana huyo amekuja kukuposa; na amedai kwamba ametumwa na Mtume Mtukufu."

Dhulfa akasema: "Isije kuwa kweli ametumwa na Mtume Mtukufu; na kumrejesha yeye ni sawa na kuasi amri ya Mtume Mtukufu."

Ziyad akasema: "Unavyoona wewe, mimi nifanye nini?"

Dhulfa akajibu: "Ninavyoona mimi, nenda haraka ukamrejeshe hapa kabla hajawahi kufika kwa Mtume Mtukufu. Kisha wewe mwenyewe nenda kwa Mtume uhakikishe kisa chenyewe."

Ziyad akamrejesha Juwaybir nyumbani kwake kwa heshima, naye akaenda kwa haraka kwa Mtume Mtukufu. Alipomwona Mtume Mtukufu, akamwambia:

“Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Juwaybir amekuja nyumbani kwangu na ameleta ujumbe huo kutoka kwako. Napenda kukuambia kwamba kwa mujibu wa desturi na mila yetu, tunawaoza mabinti zetu wale tu walio lahiki (sawa) yao katika kabila letu ambao wote ni Ansari na wasaidizi wako.”

Mtume Mtukufu akasema: “Ewe Ziyad! Juwaybir ni muumini. Desturi unayoifikiria haipo tena sasa. Muumini mwanamume ni lahiki na sawa na muumini mwanamke.”

Ziyad akarejea kwake na moja kwa moja akamwendea binti yake na kumwelezea mazumgumzo yake na Mtume Mtukufu.

Dhulf'a akamjibu babako: "Kwa maoni yangu usilikatae pendekezo la Mtume Mtukufu, kwani jambo hili linanihusu mimi. Ni lazima mimi niwe radhi hata Juwaybir awe ni mtu wa aina gani, kwa sababu Mtume Mtukufu analipenda jambo hilo, nami pia nalipenda."

Ziyad akamwoza Dhulfa Juwaybir. Mahari akatoa katika mali yake mwenyewe; na akamtayararishia vyombo vizuri vya harusi. Akamwuliza Juwaybir:

“Je, unayo nyumba tayari ili umchukue huko bibi harusi?”

Juwaybir akasema: “Kitu ambacho sijakiwaza juu yake ni kuwa mke na maisha bora siku moja. Mtume alikuja ghafla kwangy kuniambia mambo hayo na kunituma kwako.”

Ziyad akatoa katika mali yake nyumba na vyombo kamili vya nyumbani kumpa bwana harusi pamoja na nguo nzuri mbili. Na akampamba bibi harusi kwa mavazi mazuri, manu-kato, bangili, herini na mkufu na kumpeleka kwa bwana harusi."

Usiku uliingia. Juwaybir hajajua nyumba aliyowekewa ilikuwa wapi. Akaongozwa kwenye nyumba na chumba chenyewe. Mara tu alipoona nyumba hiyo pamoja na vyombo vyake kamili na bibi harusi mrembo, akakumbuka hali aliyokuwa nayo. 'Utakumbuka: "Niliingia katika m|i huu nikiwa maskini na mgeni. Sikuwa na kitu. Sikuwa na mali, uzuri wa sura, nasaba wala ukoo, lakini Mwenyezi Mungu amenipa neema zote hizi kutokana na dini ya Kiislamu. Uislamu ndio ulioleta mabadiliko makubwa kama haya katika maisha ya watu ambayo hayawezi kuwazika. Inanibidi nimshukuru Mola kwa kadiri gani?”

Papo hapo moya wake ukataka uonyeshe mapenzi na shukrani zake kwa Mwenyezi Mungu. Akaenda kwenye kona ya chumba na akaanza kusoma Qur’ani na kuabudu. Alipozindukana alisikia sauti  ya adhana ya asubuhi. Akanuia kufunga ili kumshukuru Mola kwa

neema hiyo. Wanawake walipokwenda kwa Dhulfa walimwona alikuwa bado bikira. Ikafahamika wazi kwamba Juwaybir hajamsogelea Dhulfa. Ziyad akafichwa jambo hilo.

Siku mbili nyinginezo zikapita katika hali hiyo hiyo. Juwaybir alikuwa akifunga mchana na usiku akisoma Qur'ani na kuabudu.

Familia ya bibi harusi wakaanza kutia shaka kidogo kidogo kwamba huenda Juwaybir hakuwa na uwezo wa kijinsia na ashiki (hamu) ya mwanamke. Ziyad akampasha habari Mtume Mtukufu kuhusu jambo hilo. Mtume Mtukufu akamwita Juwaybir na kumwambia: "Kwani wewe huna hamu ya kumpenda mwanamke?"

Juwaybir akajibu: "Kwa bahati nina hamu kubwa sana."

Mtume akasema: "Basi kwa nini mpaka sasa hujamsogelea bibi harusi?"

Juwaybir akasema: "Ewe Mtume Mtukufu! Wakati mimi nilipoingia katika nyumba hiyo na kuziona neema zote hizo, nikafikiri sana kwamba Mwenyezi Mungu amenineemesha sana mimi mja nisiyekuwa na thamani, hivyo, nikataka kwanza nimshukuru na nimwabudu Yeye kabla ya jambo lo lote. Lakini leo usiku nitakuwa pamoja na mke wangu.”

Mtume Mtukufu akamwelezea Ziyad bin oana na wakaishi kwa furaha na starehe.

                                                                                                   

Ikaja jihadi (vita vitakatifu). Juwaybir akashiriki katika jihadi hiyo kwa ushujaa ule ule waliokuwa nao watu mahsusi wenye imani, na akauawa shahidi chini ya bendera ya Kiis-lamu. Baada ya ushahidi wa Juwaybir, hakutokea mwanamke aliyepelekewa posa nyingi kama Dhulfa; na hakutokea mwanamke aliyekuwa tayari kutumia pesa nyingi kushinda Dhulfa (kugharamia harusi).