BIBLIA
NENO LA MUNGU

 

 

YALIYOMO

 

Dibaji                        ...5

Mungu wa Biblia        ...7

Mitume wa Biblia:

Nabii Isa                   ..13

Nabii Dauda             ..16

Nabii Lutu                 ..18

 

Nabii Yakobo              ..…   19

Nabii Sulemani            ..…   21

Nabii Musa                  ..…   23

Nabii Isaya                  ..…...26

Nabii Ibrahim              ..…...27

Nabii Ezekiel               ..…   28

 

Nabii Hosea                 ..…   31

Nabii Haruni                ..…   33

Wana wa Uzinzi           ..…  35

Nabii Yeremia             ..…   38

Nabii Nuhu                  ..…   38

Nabii Mzee                  ..…   39

Nabii Elisha                   ......40

www.islamkutuphanesi.com

 

 

 

Kimetungwa na:

Seyyid Muhammad Mahdi Husaini Shirazi

(KARBALA, IRAQ)

 

 

 

 

 

 

 

Kimefasiriwa na:

Seyyid Muhammad Mahdi Musawy

Shushtani

(ZANZIBAR, TANZANIA)

 

 

 

 

 

 

Kimetolewa na:

BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA

P.O. BOX 20033

DAR ES SALAAM

Tanzania

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Haki zote ziko kwa  Bilal Muslim Mission

 

 

 

 

 

Chapa ya kwanza, 1972, Nakala 2,000

Chapa ya pili,        1983,Nakala 2,000

Chapa ya tatu,       1987, nakala 5,000

 

 

 

 

ISBN 9976 956 26 6

 

 

 

 

 

 

 

Kimepigwa chapa na

The Dar es salaam Printers ltd

 

 

 

 

DIBAJI

 

 

 Hii ni tafsiri ya Kijitabu Kilichoandikwa kwa lugha ya Kiarabu, Kilichoandikwa na Ayaatullah Seeyyid Muhammed Mahdi Shirazi wa Karbala.  Tafsiri yenyewe  ilifanywa na Seyyid Muhammed Mahdi Shushtari wa Unguja.  Sura nyingi Zilichapishwa kwa mfulizo katika gazeti letu.  Sauti  ya Bilal na zilipendeza sana. Sasa kijitabu hiki kimechapishwa ili Kuwarithisha zaidi wasomaji wetu.

 

Hatuna budi kutamka hapa kuwa mujibu wa imani yetu, Mitume wote waalikuwa wametumwa na Mwenyezi Mungu Kuwaongiza watu katika njia iliyo sawa.

 

Waalifanya hivyo kwa kuhubiri wema wao mkuu na kwa matendo yao maadilifu.

Kufanya hivyo iliwapasa wawe waongofu zaidi, waadilifu na kuwa wakamilifu katika uchaji wao kwa Mwenyezi Mungu.  Wasingeweza kusema uwongo iwapo wao walifundisha watu kusema kweli.Wasingeweza  kumwomba Miungu, iwapo wao waliwataka watu kumwomba Mungu Aliye Mmoja tu, na kadhalika.

 

Hata hivyo, Biblia inasingizia zote za maovu na madhambi kwa Mitume hao.  Ama viongozi wa Kiyahudi na Wakristo walikuwa na madhambi makubwa kabisa, la sivyo, basi ni makosa ya Biblia yenyewe (inayoaminiwa kuwa si maandishi ya Musa wala Isa a.s)

 

Kwa hiyo,  ni juu ya msomaji mwenyewe kuteua yapi yanayomfaa na yapi yasiyomfaa.

 

 

Syed saeed Akhtar Rizvi

 

 

 

 

                 

 

 

 


 

M U N G U  W A  B I B L I A

 

Je, wewe unaona huyu  Mungu wa Biblia ni  wa namna gani? Kama Mungu nao mwili,  nywele na vazi , anaishi katika mahala , hajui kitu kilichofichika nyuma ya mti , anadanganya watu, huvunja ahadi yake, je binadamu yukoje?

 

Swali:    Ati Mwenyezi Mungu ana sura ya binadamu?

 

Jibu:   Sivyo Kamwe.  Lakini katika Biblia kitabu cha kwanza kiitwacho Mwanzo, Sura ya 1, aya ya 26 na 27, Imeandikwa hivi: “Mungu akasema, Na tufanye mtu kwa mfano wetu,  Kwa sura yetu,  Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, Kwa mfano wa Mungu na Mungu alimwumba, Mwanamume na Mwanamke aliwaumba.”

 

Swali:  Ati Mwenyezi Mungu anazo nywele? Anacho kivazi?

 

Jibu:   Sivyo kamwe. Lakini katika Biblia kitabu cha Danieli, Sura ya 7, Aya ya 9, imeandikwa hivi:  “Ni katazama hata viti vya enzi vikawekwa, na Mmoja aliye mzee wa siku (Mwenyezi Mungu) ameketi, Mavazi yake yalikuwa meupe kama theeluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi

 

Swali:    Ati Mwenyezi Mungu anayo miguu miwili?

 

Jibu:   Sivyo Kamwe. Lakini katika Biblia kitabu cha kutoka sura ya 24, aya ya 10, Imeandikwa hivi: “Wakamwona Mungu wa Israeli: chini ya miguu yake palikuwa na kama sakafu iliyofanyizwa kwa yakuti samawi… Nao wakamwona Mungu, Wakala na kunywa.”

 

Swali:    Ati Mwenyezi Mungu ana pahala ambapo anaonekana?

 

  Jibu:  Sivyo kamwe.   Lakini Biblia katika kitabu cha ufunuo wa Yohana, Sura ya 4, aya ya 2, Imeandikwa hivi:” Na mara nalikuwa katika Roho: na tazama, Kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na mmoja ameketi juu ya kiti: na yeye aliyeketi alionekana mithili ya jiwe laq yaspi na akiki, na upinde wa mvua ulikizunguka kile kiti cha enzi, ukionekana mithili ya zumaridi.”

 

 Swali:   Ati Mwenyezi Mungu hutembea?

   

 Jibu:    Sivyo kabisa. Lakini katika Biblia kitabu cha kwanza kiitwacho Mwanzo, sura ya 2,aya ya 8, imeandikwa hivi: “Kisha wakasikia (Adamu na mkewe) sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga: Adam na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone."

 

Swali:   Ati Mwenyezi Mungu hutembea?

 

Jibu:   Sivyo Kamwe.   Lakini katika Biblia kitabu cha Pili kiitwacho kutoka, sura ya 19, aya ya 20, imeandikwa hivi: “Bwana akaushukia mlima, Bwana akamwita Musa aende hata kilele cha mlima: Musa akapanda juu.”

 

Swali :   Ati Mwenyezi Mungu  huteremka juu ya wingu na anakwenda mbele ya mtu?

 

Jibu:     Sivyo kabisa Biblia kitabu cha pili kiitwacho “KUTOKA” katika sura ya 34 aya ya 5 na 6,   imeaandikwa hivi:” bwana akashuka ndani ya lile wingu, akasimama pamoja naye huko,  akalitantaza jina la Bwana. Bwana akapita mbele yake.”

 

Swali:       Ati Mwenyezi Mungu huchagua mahala pa kukaa yeye?

 

Jibu:    Sivyo kabisa.   Lakini katika Biblia kitabu cha Zaburi ya 132, aya 13, imeandikwa hivi: “kwa kuwa Bwana ameitamani akae ndani yake.”

 

Swali:       Ati Mwenyezi Mungu mjinga? Hapambanui kati ya milango ya wenyekuamini na makafiri ila kwa alama?

      

Jibu:          Sivyo Kabisa.  Lakini Biblia kitabu cha pili, Kiitwacho, KUTOKA, sura ya 12. aya ya 12 na 13, meandikwa hivi: “Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wamwanadamu na wanyama; nami nitafanya hukumu  juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi Bwana. Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lolote likawaharibu nitakapoipiga nchi ya Misri.”

                  

Swali:      Ati Mwenyezi Mungu hawezi kujua kwamba mtu amejificha katika mti?

Vile vile hajui nani amemfundisha binadamu?

 

Jibu:      Sivyo kabisa.   Lakini Biblia katika kitabu cha Mwanzo sura ya 3, aya 9-11, imeandikwa hivi,”Bwana na Mungu akamwita Adamu, akamwambia uko wapi?  Akasema,  Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi :nikajifificha.” Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa uchi?

 

Swali:   Ati Mwenyezi Mungu anavunja ahadi zake?

 

Jibu:    Sivyo kabisa. Kuvunja ahadi ni aibu kubwa. Lakini Biblia katika kitabu cha kwanza cha cha Samweli, Sura ya 2, aya ya 30 na 31, imeandikwa hivi:”Kwa sababu hiyo,Bwana, Mungu wa Israel, asema, Ni kweli, nalisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda mbele zangu milele:lakini sasa Bwana asema, Jambo hili na liwe mbalinami…Angalia, Siku zinakuja, nitakapoukata mkono wako, na mkono wa mbali ya baba yako, hata nyumbani mwako hatakuwa mzee.” Mungu yu mbali na uzushi huu juu yake. Kama vile, ati aliwahidi Eli kwamba ukuhani wake ulikuwa wa maisha juu yake na wanawe, lakini baadaye hayo hayakutekelezwa.

 

Na vilevile katika sura ya 13,aya 13 imeandikwa hivi: “… Bwana angaliufanya ufalme wako kuwa imara juu ya Israeli milele. Lakini sasa ufalme wako hautadumu.”

 

Mungu yu mbali na uzushi huu juu yake kama vile, Ati alimwahidi Sauli Ufalme wake kuwa imara milele, na baadaye akavunja ahadi na akampa ufalme mtu mwingine:

 

Swali:      Ati upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu?

 

Jibu:   Sivyo Kabisa. Mwenyezi Mungu si mpumbavu kamwe, basi vipi itakuwa upumbavu wake una hekima zaidi ya wanadamu: Lakini Biblia katika waraka wa kwanza wa Mtume Paulo kwa Wakorintho, sura ya kwanza, aya ya 25, imeandikwa hivi:” Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu.”

 

Swali:   Mwenyezi Mungu hujuta akisha tenda jambo?

 

 Jibu:   Sivyo Kabisa. Lakini Biblia katika kitabu cha kwanza  cha Samweli, Sura ya 15, aya ya 10 na 11, Imeandikwa hivi, “Ndipo neno la Bwana likamjia Samweli, Kusema, “najuta kwa sababu nimemtawaza Sauli awe Mfalme.”

 

Swali:    Ati Mwenyezi Mungu husikitika na kuwa na majonzi kwa kitendo  alichofanya?

    

Jibu      Sivyo kabisa.   Lakini katika Biblia kitabu cha Mwanzo, Sura ya 6, aya ya 6 na 7, imeandikwa hivi: ‘Bwana akaghairi kwa  kuwa amefanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. Bwana akasema, Nitamfuatilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi.”

         

Swali:    Ati Mwenyezi Mungu hushinda mweleka na mtu?

    

Jibu:     Sivyo kabisa.   Lakini Biblia katika kitabu cha Mwanzo, sura ya 32,  aya ya 24 na 28, imeandikwa hivi: Yakobo akakaa peke:  na mtu mmoja akaashindana naye mweleka hata alfajiri.. Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, Ila Israeli,  Maana unashindana na Mungu.”          

 

Swali:     Ati Mwenyezi Mungu husema uwongo halinyoka husema kweli?

 

Jibu:     Sivyo Kabisa.   Lakini Biblia Katika kitabu cha Mwanzo, sura ya 3, aya ya 3 hadi ya 6 , imeandikwa hivi:  Lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema , msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. Nyoka akamwambia mwanamke,  Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na baya.”

 

Baadaye imeelezwa kwamba Adamu na Hawa baada ya kula matunda ya mti huo, wakawa huko … yameelezwa mambo ambayo si shani ya Mwenyezi Mungu kuambiwa hivyo.

 

Swali:    Ati  Mwenyezi Mungu hushuka kutoka mbinguni ili kuchafua umoja wa

              watu ili  wasisikilizane  kwani anaogopa umoja wao?

 

Jibu:    Sivyo, sivyo kabisa mara elfu.  Lakini Biblia katika kitabu cha Mwanza, Sura ya 11, aya ya kwanza hadi 9, imeandikwa hivi:”Nchi yote ilikuwa na na lugha moja na usemi mmoja.

 

Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambalale katika nchi ya Shinari: waakakaa huko. Waliambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto.

 

Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa. Wakasema, Haya na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni tujifanye jinaa: ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote. Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha moja : na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno

 

Wanalokusudia kulifanya, Haya, na tushuke huko huko,  tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno yao. Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni paa nchi yote : wakaacha kujenga ule mji. Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Baabeli.”

 

Swali:    Ati Mwenyezi Mungu husema kitu baadaye akafanya mengine?

 

Jibu:    Sivyo Kabisa.   Lakini Biblia katika kitabu cha Mwanzo, Sura ya 6, aya ya 3, inasemaa hivi: Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na wanadamu milele kwa kuwa yeye naye ni nyama: basi siku zake zitakuwa miakaa mia na ishirini.”

 

Hayo yalikuwa mwanza wa kuumba Binadamu, hebu tutazame, Mungu alifuata ahadi yake? Biblia inasema Mungu aligeuza maneno yake, Kwa hivyo watu wengi waliishi   juu ya umri alioahidi Mungu. Kwa mfano, imeandikwa katika Mwanzo, Sura ya tisa, aya ya ishirini nia nne (mwa 9:28), kwamba, “Na Nuhu akaishi baada ya ile ghaarika miaka mia tatu na hamsini. Siku zote za Nuhu zilikuwa miaka mia kenda na hamsini, akafaa.”

 

 

MITUME  WA BIBLIA

 

NABII ISA

                 

Mitume waalitumwa kufundisha watu wema na ukweli. Mitume wa Biblia wanasema uwongo.:        

 

Swali:      Ati Yesu (Isa a.s) husema uwongo?

 

Jibu:     Sivyo, Kamwe:  Lakini katika Biblia, Injil ya Yohana Mtakatifu, Sura ya 7, aya ya 2-3, Inasema hivi:  Na sikukuu ya Waayahudi, Sikukuu ya vibanda ili  kuwaa karibu.  Basi ndugu  zake   wakamwambia, ondoka  hapa, uende hapa, uende Uyahudi, wanafunzi wako nao wapate kuzitazama kazi  zako unazozifanya. Kwa maana hakuna mtu afanyaaye nena   kwa siri, naye mwenyewe ataka kujulikana. Ukifanya mambo haya, basi jidhi hirishe kwa ulimwengu. Maana ana hata nduguze hawakumwamini. Basi Yesu akamwambia, Haujaafika  bado wakati wenu siku zote  upo. Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi: kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi zake ni mbovu.  Kweni ninyi kwenda kula sikukuu: Mimi si kweli bado kwenda kula sikukuu hii: kwa kuwaa haujatimia wakati  wangu. Naye alipokwisha kuwaambia hayo, alikaa vibi hivi huko Galiliya.

 

Hata ndugu zake walipokwisha kuwa kuiendea sikukuu, ndipo yeye naye alipokwea, si kwa wazi bali kana kwamba kwa siri.

 

Swali:   Ati Yesu (Isa a.s.) hutengeneza mvinyo, na  anaweza kuwanywesha Masahaba   wake?

 

 Jibu:     Sivyo, sivyo kabisa.  Lakini katika Biblia inasema hivyo, na isitoshe hayo inasema kuwa ndio ufunguo wa Utume wake, na ndicho kitu  alichotumia hadi akaaga dunia:

 

Usiseme, hivyo huenda  ikawa katika madhehebu ya Yesu (Isa a.s)  pombe kuwa halali. Naogopa Mungu kwa masingizio hayo, kwani Agano jipya zinabainisha uharamu wa mvinyo.

 

 Basi kwanza tueleze wazi amri ya uharamu wa mvinyo  katika Biblia na baadaye tueleza masingizio juu ya Yesu (Isa a.s)

 

Katika Biblia kitabu cha Hosea, Sura ya nne, aya 10 na 11 imeandikwa hivi:

 

Nao watakula, lakini hawatashiba: watafanya zinaa, lakini hawataongezeka:kwa sababu wameacha kumwangalia Bwana. Uzinzi na divai na divai mpya huondoa fahamu za wanadamu.

 

Vile vile katika Isaya sura ya 5 , aya 11 na 12 na 13 li

 

Nasema hivi:ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo, wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo umewaka kama moto ndani yao: Na kinubi, na zeze, na matari, na filimbi, na mvinyo zote ziko katika karamu zao: Lakini hawaiangalii kazi ya Bwana wala kuyafikiri matendo ya mikono yake. Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa.

 

Katika kitabu cha kumbukumbu la Torati, sura 21, aya ya 18-21, inasema hivi: Mtu akiwa na mwana Mkaidi, mshupavu, asiyetii sauti ya baba yake, wala sauti ya mama yake, nao wajapomwadhibu hawasikilizi, ndipo babaye na mamaye na wamkamate, na kumpeleka kwa wazee wa mji wake, katika lango la mahali pake: wawaambie wazee wa mji wake, Huyu mwana wetu ni mkaidi, mshupavu hasikizi sauti yetu: Ni mwasherati, na tena ni Mlevi Waume wote wa mji wake na wamtupie mawe, afe: ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako : na Israeli wate watasikia na kuogopa.

 

Katika kitabu cha luku, sura ya 7, aya ya 33 na34, Inasema hivi:

 

Kwa kuwa Yohana Mbatizaji alikuja, hali mkate wala hanywi divai, nanyi mwasema, Ana pepo. Mwana wa Adamu amekuja, ana kula na kunywa: nanyi mwasema, Tazama, mlafi huyu, na mnywaji wa divai, rafiki wao watoza ushuru na wenye dhambi.

 

Katika kitabu cha Yohana Mtakatifu, sura ya pili, aya ya 1-11, inasema hivi: Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko kana, mji wa Galilaya: naye mama yake Yesu alikuwapo. Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pomoja na wanafunzi wake. Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia  Mama, tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia. Mamaye akawaambia watumishi, Lolote atakalowaambia, fanyeni.

 

Basi kulikuwapo huko mabalasi sita ya mawe,  nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu. Yesu akawambia, Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza hata juu. Akawaambia, Sasa tokeni mkampeleka. Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale mali yaliyopata kuwa divai , (wala asijue ilikotoka,

 

Lakini  watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu za meza alimwiita  bwana arusi akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema: hata sasa.

 

Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko  kana ya Galilaya, akaudhihirisha      utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.

 

Jambo hili linadhihirisha kwamba kunywa mvinyo haikuwa inafikiriwa kuwa      mwiko katika dini kwa mujibu wa Agano jipya. Angalia jinsi Isa (Yesu) alivyotengeneza mvinyo akiwaambia wengine wainywe.

 

Tukio lingine:

 

Katika kitabu cha Luka Mtakatifu, Sura 22, aya 14-18 inasema hivi: Hata saa ilipofika aliketi chakulani, yeye na wale miyume (kumi na wawili) pamoja naye. Akawaambia, Nimetamani sana kuila pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu: kwa maana nawaambia ya kwamba siili tena hata itakapotimiwa katika ufalme wa Mungu. Akapokea kikombe, akashukuru, akasema, Twaeni hiki mgawanye ninyi kwa ninyi: Maana nawaambia ya kwamba tangu sasa sinywi mazao ya mzabibu hata ufalme wa Mungu utakapokuja.

 

                                                                                                                                                                                                                             


N A B I I  D A U D I

 

 

Je,  Mtume huzini? Hawezi. Je, Mtume humnywesha mtu mvinyo? Hawezi. Ati Mtume humdanganya mtu ili amwue? Hawezi.

 

 Lakinu katika Biblia Mtume Daudi (a.s) amesingiziwa yote haya juu.

   

Tazama kitabu cha pili cha Samweli, sura 11, aya 2-27, yasema hivi:”Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la Mfalme: na alipokuwa juu ya dari aliona Mwanamke anaoga: naye huyo Mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho.  Naye Daudi akapeleka, akauliza habari za yule Mwanamke. Mtu mmoja akasema, Je: huyu siye bath-sheeba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti? Basi Daudi akapeleka  wajumbe  , akamtwa: naye akaingia kwake, naye akalala naye (maana yule mwanamke amekwisha kutakasika unajisi wake): kasha akarudi nyumbani kwake. Yule mwanamke akachukua mimba: basi akapeleka na kumwambia Daudi, akasema, Ni Daudi akapeleka kwa Yoabu, akisema, Unipelekae Uria kwa Daudi.. Daudi akamwambia Uria, Haya, Shuka nyumbani kwako, ukanawe miguu yako…wala   hakushuka nyumbani kwako. Daudi akamwambia  Uria, Je’ hukutoka safarini? Mbona hukushuka  nyumbani kwako? Naye Uria akamwambia Daaudi, Sanduku, la Israeili na Yuda wanakaa vibandani nami niende nyumbani kwangu kula na kunywa, na kulala na Mke wangu?… Naye Daudi akamwalika, akalala, akanywa mbele yake; naye akamlevya hata wakati wa jioni akatoka kwenda kulala kitandani mwake… lakini hakushuka nyumbani kwake. Hata ikawa asubuhi Yoabu Waraka, kusema, Mwekeni Uria mbele ya watu penye vita vikali, kisha ondokeni, mwache, ili apigwe akafe. Akamweka Uria mahali alipojua ya kuwa pana mashujaa… wakapigana na Yoabu,… Na yule mke wa Daudi, wakaanguka; Uria Mhiti naye akafa… Na yule mke wa Uria alipopata habari kuwa Uria mumewe amekufa, akamwomboleza mumewe. Hata maombolezo hayo yalipokwisha, Daudi akatuma mtu, akamtwaa akamtia nyumbani mwake; naye akawa mkewe… Lakini jambo lile alilolitenda Daudi, likamchukiza Bwana.”

 

Je, umesikia kisa namna alivyofanya hila ya kumwua Uria; Na kwamba Daudi alizini na mke wa Uria baadaye akamlewesha ili apate kulala na mkewe, jambo lisiloridhisha, na kumpeleka Uria vitani kwa hadaa ili auawe, na wakatenda hata akauwawa?

 

Basi sasa sikia tokeo la hayo kwa yule mwanamke mwenye mume aliyezini naye Daudi!

 

Tazama Injili ya Mateyo, sura 1, aya ya 6-9, inasema hivi: “ Yese akamzaa Mfalme Daudi. Daudi akamzaaa Sulemani kwa yule mke wa Uria.”

 

Vile vile tazama kitabu cha pili cha Samweli, sura 12, aya ya 9, inasema hivi:-

 

Bwana, Mungu wa Israeli asema hivi:

 

“Umempiga Uria, Mhiti, kwa upanga, nawe umemtwaa mkewe awe mke wako?”

 

Basi sasa sikia iliokuwa ajabu zaidi!

 

Agano zote mbili za sema kwamba Mwenyezi Mungu amemjaazi Mtume Daudi kwa kuwasalitisha wanawe juu ya wake zake hata wakazini nao!

 

Tazama kitabu cha pili cha Samweli, sura 12, aya 11 na 12, inasema hivi:-

 

Bwana asema hivi, Angalia, nitakuondokesha uovu katika nyumba yako, nami nitawatwaa wake zako mbele ya macho  yako, na kumpa jirani yako, naye atalala na wake zako mbele ya jua hili. Maana wewe ulifanya jambo hili kwa siri; bali mimi nitalifanya jambo hili mbele ya Israili wote na mbele ya jua.

 

Tena tazama sura16, aya 22, inasema hivi”-

 

Basi wakamtandikia Absalomu hema juu ya nyumba darini; naye Absalomu akaingia kwa masuria ya babaye machoni pa Israeli wote.

 

 

NABII   LUTU

 

 

Biblia haitoshelezi kusingizia kuwa licha ya kutenda uzinzi wa kawaida, Mtume alizini pia na binti zake

 

Swali:    Je, Mtume anaweza kuzini na binti zake au kulewa divai?

 

Jibu:    Haiwezekani kamwe mambo hayo,  yote ni masingizio tu.  Kwani mwenye akili

             yeyote hawezi kufanya mambo kama haya:  Sembuse Mtume?

 

Basi tazama Biblia kitabu cha kwanza, sura ya 19, aya ya 30-38, inasema hivi: lutu akapanda kutoka Soari akakaa mlimani na binti zake wawili. Yule mkubwa akamwambia mdogo, Baba yetu ni mzee, wala hakuna mtu mume katika nchi atuingilie kama ilivyo desturi ya dunia yote. Haya, na tumnweshe baba yetu mvinyo, tukalale naye, ili tumhifadhie

 

Baba yetu uzao. Wakamnywesha baba yao mvinyo usiku ule,  akaondoka huyo mkubwa akalala naye.  Wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka. Ikawa  siku ya pili , mkubwa akamwambia mdogo, tazama, nimelala jana na baba yangu, tumnyweshe tena baba yao mvinyo usiku ule akaondoka mdogo akalala naye wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka, Basi hao binti wote wawili wa wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao. Yule mkubwa akazaa mwana, akamwita jina lake Moabu: huyo ndiye baba wa Wamoabi, hata leo . Na yule mdogonaye akazaa mwana akamwita jina lake Benabi: huyo ndiye baba wa Waamoni hata leo. 

 


 

N A B I I  Y A K O B O

 

Je, wadhani kuwa Mtume aweza kudanganya? Au kumbusu mwanamke mgeni? Au wadhani Mwenyezi Mungu huweza kupigana mieleka na Mtume Wake, na wala Asiwe Kumshinda?

 

 

Swali:     Ati inawezekana Mtume ambusu mwanamke asiyemhusu?

 

Jibu:       Mambo haya hafanyi mwenye akili yeyote sembuse Mtume wa Mungu.

 

              

Swali:     Ati Mtume hushindana mweleka na Mungu?

 

Jibu:    Sivyo kabisa, kwani Mwenyezi Mungu hana kiwiliwili hata mtu ashindana mweleka naye.

 

Swali:    Ati Mtume hudanganya?

 

Jibu:    Kudanganya ni aibu na Mtume amekamilishwa na Mwenyezi Mungu.

 

Lakini katika Biblia yote hayo wamesingiziwa. Tazama kitabu cha Mwanzo, sura 29, aya 11, inasema hivi:

 

Yakobu akambusu Raheli, akainua sauti yake akalia. Huyu Raheli akaolewa na huyu Yakobu baada ya miaka saba.

 

Vile vile tazama sura ya 32, aya ya 24-30 inasema hivi: Yakobu akakaa peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri…akamwambia, jina lake hutaitwa tena Yakobu, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu.

 

Akambariki huko. Yakobu akapata mahali pale, penueli, maana alisema, Nimeonana na Mungu uso ka uso na nafsi yangu imeokoka.

 

Vilevile tazama sura27, aya1-35 inaseama hivi: Ikawa Iseka alipokewa mzoe, na macho yake yamepofuka asione, akamwita Esau mwanawe mkubwa, akamwambia, Mwanangu…. Basi, nakuomba chukua mata yako, podo lako                                     

 

Na upinde wako, ukaende nyikani uniwindie mawindo; ukanifanyie chakula kitamu namna ile niipendayo, ukiniletea, ili nile; na roho yangu ikubariki, kabla sijafa. Na Rabeka akasikia, Isaka aliposema na Esau mwanawe… Kisha Rebeka akatwaa mavazi mazuri ya Esau mwana mkubwa, aliyokuwa nayo nyumbani, akamvika Yakobu mwanawe mdogo… Akaja kwa baba yake, akasema, Babangu. Akasema, mimi hapa, Unani  wewe mwanangu Yakobu akamwambia babaye, Mimi ni Esau, mzaliwa wako wa kwanza nimefanya kama ulivyoniambia.. Akasema, Niletee karibu nami nipate kula mawindo ya mwanangu, ili roho yangu ikubariki. Akamsogezea karibu,naye akala: kisha akamletea mvinyo, akanywa. Isaka, baba yake, akamwambia, Njoo karibu sasa, ukanibusu, mwanangu.

 

Akakaribia akambusu. Naye akasikia harufu ya mavazi yake, akambariki akasema… Ikawa Isaka alipokwisha kumbariki Yakobo ndiyo kwanza ametoka mbele ya Isaka baba yake, mara Esau ndugu yake akaja kutika katika kuwinda kwake … Isaka, baba yake, akamwuliza, U nani wewe? Akasema, Mmi ni mwanao, Esau, mzaliwa wako wa kwanza.Isaka akatetemeka tetemeko kuu sana, akasema… Nduguyo amekuja kwa hila , akachukua mbaraka  wako.”

 

Ni ajabu mno na masingizio kwa Mtume kumbusu mwanamke, na kuhadaa , au kushindana mweleka na Mingu na kuchukua utume kwa nguvu na hadaa! Yaweza kuwa hayo ni kweli?

 

 

N A B I I    S U L E M A N I

 

 Kiongozi wa dini wa Biblia anashugulika kufanya mambo yaliyokatazwa na Mungu: moyo wake umeelekea kwenye masanamu: ana ufupi, moyo wake unapotoka na Mwenyezi Mungu.  Je,  uongozi gani huu ?  

 

Swali:  je , anaweza Mtume kutenda mamabo aliyoyakataza Mwenyezi Mungu?

 

Jibu:  Haiwezekani kamwe.

 

Swali:  Je , inamkinika moyo wa Mtume uelekeye kwenye masanamu?

 

Jibu: Haimkiniki kamwe hivyo.

 

Swali: Je, inawezekana Mtu ajenge nyumba ya kuabudia masanamu?

 

Jibu: Kabisa haiwezekani Mtume yeyote kufanya hivyo.

 

Swali: Ati inamkinika moyo wa Mtume upotoke na Mwenyezi Mungu?

 

Jibu: Haiwezekani Kamwe!

 

LAKINI:  Biblia katika kitabu cha Wafalme,Sura 11 , aya za kwanza inasema hivi:

 

Mfalme Suleman akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao… Na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwenu: kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Suleimani akaambatana nao kwa kuwa penda. Akawa na wanawake saba binti za kifalme, na masuria mia tatu: nao wakeze wakamgeuza moyo

 

Maana Ikawa, Suleimani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake , afuate miungu mingine wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwanba, Mungu wake , kama moyo wa Daudi baba yake.

 

Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, Mungu wa Wasidoni, na Milkomu, chukizo la waamoni. Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wala hakumfumfuata Bwana kwa utimilifu, kama Daudi baba yake. Suleimani akamjengea kemoshi, chukizo la wamoabi, mahala pa juu, katika  mlima uliokabili Yerusalenu, na Moleki, chukizo la wana wa Amoni. Na kadhalika ndivyo alivyo wafanyia wake zake wa nchi za kigeni, waliofukiza uvumba,  wakawatolea miungu yao dhabibu.

 

Basi Bwana akamghadhibikia Sulemani kwa sababu moyo wake umegeuka, naye amemwacha Bwana, Mungu wa Israeli, aliyemtokea mara mbili, akamwamuru katika habari ya jambo lilo hilo asifuate miungu mingine: lakini yeye hakuyashika aliyoyaamuru Bwana.

 

 

 

 

N A B I I   M U S A

 

Je , umepata kusikia chuki baina ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake? Je, umepata kusikia kuwa Mtume ni dhalimu? La sivyo , basi soma haya:

 

Swali:   Ati inamkinika iwe chuki na   uaduwi kati ya Mwenyezi Mungu na  Mtume wake hadi  atake kumuua

 

Jibu:        Haimkiniki  kamwe;

 

LAKINI:    Biblia katika Agano jipya na Agano la kale inasema kama Mwenyezi Mungu alitaka kumuua Musa lakini mke wake Sipora ndio aliomwokoa!!! Tazama kitabu cha pili cha Musa ,

 

kiitwaacho KUTOKA, sura ya 4, aya mbali mbali: Bwana akamwamia Musa, hapo utakaporudi Misri, angalia ukazifanye mbele ya Farao zile ajabu zote nilizo-zitia  mkononi mwako. Ili kuwa  walipokuwa njiani mahala, pa kulala , Bwana akakutana naye akataka naye akataka kumwua. Ndipo Sipora akashika jiwe gumu na kuikata govi ya zungu la mwanawe, na kuibwaga miguuni pake akasema , Hakika wewe u bwana arusi wa damu kwangu mimi. Basi akamwacha. Ndivyo huyo mkewe akanena, u bwana arusi wa damu wewe kwa ajili ya kutahiri.

 

Swali:   Je , inawezekana Mtume awe dhalimu na kuamrisha wauawe watoto na

           mengineyo kama hayo, na kuteketeza majumba kwa moto?

 

Jibu:    Mtume hawezi kuwa hivyo wala hawezi  kamwe kutenda dhuluma.

 

Lakini Biblia katika Agono jipya na Agono  la kale husema kama Musa (a.s)  alifanya hivyo”

 

Tazama kitabu cha nne cha Musa, kiitwacho HESABU sura ya 31 aya mbalimbali:

 

Wana wa Israeli wakawachukua mateka wanawake wa Midiani na watoto wao: na ngonbe zao wote na mali zao zote, wakachukua nyara . Na miji yao yote, kila mahali walipokuwa wakikaa, na marago yao yote wakayateketeza nyara zote, na mateka yote , ya wanadamu na ya wanyama, . . . Basi Musa,  na Eleazari kuhani, na wakuu wote wa huo mkutano, wakatoka nje kwenda kuwalaki nje ya marago. Musa akawakasirikia majemadari wa jeshi . .…Musa akawauliza, je mmewaponya wanawake wote hai? . . Basi kwa ajili hiyo mwueni kila mume katika hao watoto, na kila mwanamke aliyemjua mume kwa kulala pamoja naye . lakini hao watoto wote wa kike ambao hawakumjua mume kwa kulala pamoja naye, mtawaweka hai kwa hajili yenu.

 

Ukagawanye nyara mafungu mawili:  Kati ya watu waliozoea vita, waliotoka nje waende vitandani . . . wanadamu jumla yao ilikuwa thelathini na mbili elfu, katika hao wa nawake ambao hawakumjua mume kwa kulala pamoja naye.

  

Basi sasa na tuulize idadi gani waliangamizwa kwa kuona haram na uchungu? Bila ya shaka ni zaidi kuliko waliowachwa hai !!

 

Kwa hivyo inatubidi tushukuru hiyo huruma na msamaha kwa kuwekwa hai watoto wa kike ambao hawakumjua mume kwa kulala pamoja naye: ijapokuwa tumeshajua kwamba (agano zote mbili) imesema katika kisa kingine ameuuwaua watu wote hata hawo watoto wa kike bikira?(Tazama kumbukumbu la Torati , sura 2 , kuanzia aya 31). Kisha Bwana akaniambia Tazama nimeanza kumtoa sihoni na nchi yake mbele yako: anza kuimiliki, upate kuirithi nchi yake. Ndipo Sihoni alipotutokea juu yetu, yeye na watu wake wote, kupigana huko Yahasa. Bwana, Mungu wetu, akamtoa mbele yetu, tukampiga yeye na wanawe, na watu wake wote.  Tukatwaa miji yake yote wakati hou, tukaharibu kabisa kila mji uliokuwa na watu, pamoja na wanawake na wadogo :tusimsaze hata mmoja :ila ngombe zao tuliwatazama kuwa mawindo yetu, pamoja na nyara za miji tuliyoitwaa.

 

Agano zote mbili ina haki ya kusema, kwa nini mnanilipizia kisasi?  Kwa nini mimi ndio naliomsingizia Mtume Musa kuwauwa watu waume, wake na watoto? Kwani hamwangalii vipi amesingiziwa Mwenyezi Mungu, kwa kuwaamrisha wauwawe kila chenye roho hata wanyama? (tazama kumbukumbu la Torati, sura 20, kuanzia aya 13) Na Bwana, Mungu wako, autiapo mkononi mwako, mpige kila mume aliyemo kwa makali ya upanga:  Lakini wanawake na watoto, na vilivyo mjini vyote, navyo  ni nyara zake zote , uvitwae viwe mateka kwako: Nawe utakula nyara za adui zako alizokupa Bwana Mungu wako. Utaifanyia vivyo miji yote iliyo mbali sana nawe, isiyokuwa miji ya mataifa haya. Lakini katika miji ya mataifa haya akupayo Bwana Mungu wako, kuwa urithi, usihifadhi kuwa hai kitu chochote kipumzikacho: lakini uwaangamize kabisa, Mhiti, na Mwamori, na Mhivina Myebusi, kama alivyokuamuru Bwana, Mungu wako.

 

      Swali:     je, inawezekana Mtume awe mkali anapozungumza na Mwenyezi Mungu na kumtaka amfutiliye mbali katika Utume?

 

       Jibu:    Haiwezekani kamwe:  Lakini Biblia katika kitabu cha pili cha Musa kiitwacho  KUTOKA sura 32, kuanzia aya 31 linasema hivi: Musa akarejea kwa Bwana, akasema Aa ‘ watu hawa wametenda dhambi kuu , wamejifanyia miungu ya dhahabu. Walakini sasa, ikiwa utawasamehe dhambi yao _ na kama sivyo, unifute, nakusihi , katika kitabu chako ulichokiandika.

 

N A B I I    I S A Y A

 

 

Swali:    Je, inawezekana Mwenyezi Mungu amuamrishe Mtume wake atembee uchi kati ya watu kwa miaka na kwa nini? Kwa ajili ya ubarudhuli kwa ilhani yeye ni wa kupigwa mifano?

 

Jibu:   Haiwezekani kamwe kwa Mwenyezi Mungu kuamrisha hivyo, kwa sababu Mwenyezi Mungu Anakataza kukaa uchi mbele ya watu! Hii ni mambo ya kiwendawazimu lakini Biblia katika kitabu cha Nabii Isaya, sura ya 20 aya ya pili hadi mwisho wa aya ya nne inasema hivi:

 

Wakati huo Bwana alinena kwa kinywa cha Isaya, mwana wa amozi, akisema, Haya, uvue nguu ya magunia viunoni mwako, na viatu vyako migu

 

Uni mwako. Naye akafanya hivyo akaenda uchi, miguu yake haina viatu. Bwana akasema, kama vile mtumishi wangu Isaya anavyokwenda uchi, hana viatu, awe ishara na ajabu kwa muda wa miaka mitatu juu ya Misri na juu ya kushi:vivyo hivyo Mfalme wa Ashuru atawachukua uchi, wafungwa wa Misri, na watu wa kushi waliohamishwa, watoto kwa wazee, hawana viatu, matako yao wazi Misri iaibishwe.

 

 

 

 

N A B I I    I B R A H I M U

 

    Swali:    Ati inawezekana Mtume asisadiki Maneno ya Mwenyezi Mungu hadi akamtaka thibitisho  la ukweli wa maneno yake?

 

   Jibu:      Hasha Mtume kuwa na shaka juu ya maneno ya Mwenyezi Mungu hata   atake ushahidi!

 

Lakini agano mbili zamsingizia Mtume Ibrahim kwa hayo! Tazama kitabu cha kwa kwanza cha Musa, kiitwacho, Mwanza, sura ya 15 aya ya kwanza na ya saba, inasema hivi:

 

Baada ya mambo likamjia Abramu katika njozi, likinena . . . . . .Mimi ni Bwana, niliyekuleta kutoka Uru wa Wakaldayo nikupe nchi hii ili urithi. Akasema, Ee bwana Mungu, ni pateje kujua ya kwamba nita Rithi? Akamwambia, Unipatie ndama wa miaka mitatu: na mbuzi mke wa miaka mitatu, na hua na mwana njiwa Akampatia hao wote, akaweka kila kipande kuelekea mwenzake, ila ndege hakuwapasua Hata tai walipotua juu ya mizoga Abramu akawafukuza. Basi tazama vipi hivi? Kuna uhusiano gani kati ya maneno ya mbele na baadaye. Naam (Agano) husimulia kisa namna hivyo ya kurukaruka na kutinga haina uhusiano na mwenziwe.

 

N A B I I   E Z E K I E L I

 

 

 Sasa, Mungu wa Biblia anamwamuru Mtume mmoja kula mkate uliochanganywa na mavi ya mtu. Ubora wa  mafundisho haya ni upi?

                                                                                                    

   Swali:   Ati Mwenyezi Mungu humuamrisha Mtume wake ale mkate uliokandwa na mavi ya binadamu? Kwa nini hivyo kuamrishwa?

 

    Jibu:    Haiwezekani kamwe Mola kamuamrisha Mtume wake hivyo!

 

Lakini Biblia inasema hivyo! Tazama kitabu cha Nabii Ezekieli, sura ya 4, aya ya 12 inasema hivi:

 

Nawe (Ezekieli) utakila kama mkate wa shayiri, nawe utakioka mbele ya macho yao juu ya mashonde yatokayo katika mwanadamu. Bwana akasema, Hivyo ndivyo wana wa Israeli watakavyo kula chakula chao, hali kimetiwa Unajisi, kati ya mataifa nitakakowafukuza.

 

Lakini Nabii Ezekieli alikuwa mwenye akili . . . atakula  vipi mkate uliokandwa na mavi ya binadamu? Akataka msamaha kwa jambo hili la kuchekesha na Mwenyezi Mungu alimkubalia na akatukuka na akabadilishiwa mavi ya binadamu kwa mavi ya ngombe.

 

 Na katika sura hiyo hiyo, aya ya 14 na 15 , inasema hivi: Ndipo nikasema, Ee Bwana Mungu, tazama roho yangu haikutiwa unajisi: maana tangu ujana waangu hata sasa sijala nyamafu, wala nyama ichukizayo haikuingia kinywani mwangu. Ndipo akaniambia, Tazama, nimekupa mashonde ya ngombe badala ya mashonde ya mwanadamu, nawe utakipika chakula chako juu ya hayo.

 

Swali:   Ati Mwenyezi Mungu humuamrisha Mtume wake kunyoa kichwa chake na ndevu zake? Kwa nini hivyo? Kwa jambo la upuzi tu!  Lakini masikini Nabii Ezekieli alifikiwa na mambo ya kuchekesha. Akawa anakula mavi ya ngombe baada ya kuhurumiwa na kama si hivyo aliamrishwa ale  mavi ya binadamu. Na mara akajigeuza kwa kujinyoa kichwa na ndevu zake. Kitabu cha Nabii Elekieli, katika sura ya 5, aya ya 1, inasema hivi:

 

Nawe,  mwanadamu ujipatie upanga mkali, kama wembe wa kinyozi ujipatie, ukaupitishe juu ya kichwa chako na ndevu zako:kisha ujipatie mizani ya kupimia, ukazigawanye nywele hizo. Theluthi ya hizo zinakapotimia: nawe utatwaa thelusi, na kuipiga kwa upanga pande zote; nawe utatawanya theluthi ichukuliwe na upepo.

 

Baadaye inaonyesha makusudi ya kutoa mfano huo ni kuwajulisha kwamba, theluthi ya watu wa Orshibna watakufa kwa tauni, na kwa njaa watakomeshwa, na theluthi watakomeshwa, kwa upanga, na theluthi atawatawanya kwa upepo. Tazama mifano na wakatolewa mifino!

 

 Angalia mfano huu na mwenye kufanyika kwake mfano huo.

 

  Swali:    Ati inapendeza kwa Mwenyezi Mungu amkufishe mke wa Mtume kwa ajili ya kuonyesha mfano ya kijinga kwa ilhali ingewezekana kueleza kwa maneno tu?

 

  Jibu:     Ndio… Mtume Ezekieli alipatwa na masaibu mawili (katika agano zote mbili) na akawa mifano ya kiupuzi, bila shaka si halali kwa Mwenyezi Mungu na Mitume wake na mambo kama hayo. Lakini Biblia katika kitabu cha Nabii Ezekieli Sura ya 24 kuanzia aya ya 15 hadi mwisho wa aya 24 inasema hivi:

 

Neno la Bwana likanijia tena, kusema, Mwanadamu, tazama, ninakuondolea kwa pigo moja tunu, mteule wa macho yako mke wako) wa lakini hutaomboleza wala yasiohuruzike machozi yako. Ugua, lakini si  kwa sauti ya kusikiwa:usifanye matanga  kwa ajili yake

 

Yeye aliyekufa: jipige kilemba chako, ukavae viatu vyako, wala usile chakula cha watu.  Basi nalisema na watu asubuhi:  Na jioni mke wangu akafa: nami nalifanya asubuhi kama nilivyoagizwa. Watu hao wakaniambia, je!  hutaki kutuambia maana ya mambo haya kwetu, hata umefanya kama vile ufanyavyo. Neno la Bwana lilinijia, kusema, uwaambie nyumba ya Israeli, Bwana Mungu asema hivi:  Angalieni, nitapatia unajisi patakatifu pangu, fahari ya uwezo wenu, mahala pa kutamaniwa na macho

 

N A B I I  H O S E A

 

 Iwapo hayo hayatoshi, angalia jinsi Mwenyezi Mungu anavyomwamuru Mtuma mmoja

 kutwaa mwanamke na kuzini naye.

 

 Na baada Mtume Ezekieli agano zote mbili inamlenga mishale za mifano za upuzi kumkusudia Mtume Hosea.

 

Basi natuulize.

 

  Swali:    Ati inaelekea kwamba amuamrishe Mtume wake akatwae na kumwoa mke wa uzinzi, na watoto wa uzinzi? Na kwa nini? Kwa sababu nchi ilifanya uzinzi, kwa kumwacha Bwana. Au ilikuwa onyo na mawaidha kwa nyumba ya Israeli kwa kuwataja majina ya watoto aliwazaa yule mwanamke, na kutaja vipi alizini?

 

    Jibu:  Hasha! Mwenyezi Mungu kamwe hakumuamrisha

 

Mtume wake yeyote kufanya hivyo. Lakini Biblia katika kitabu cha Mtume Hosea sura ya kwanza, toka aya ya pili hadi mwisho wa aya ya nne, inasema:

 

Hapo kwanza Bwana aliponena kwa kinywa cha Hosea, E nenda ukatwae mke wa uzinzi: kwa maana nchi hii inafanya uzinzi, na watoto wa uzinzi: Kwa maana nchi hii inafanya uzinzi mwingi,  kwa kumwacha Bwana. Basi akaenda akamwoa  Gomeri, binti Didlaimu:naye akachukua mimba, akamzalia mtoto mwanamume. Bwana akamwambia, Mwite jina lake Yezreeli:  Kwa maana bado kitambo kidogo, nitaipatiliza nyuba ya Yehu

 

Damu ya Yezreeli, na kuukomesha ufalme wa nyumba ya Israeli.

 

Msihini mama yenu, msihini; kwa maana yeye si mke wangu, wala mimi si mume wake; na ayawekee mbali mambo ya uasherati wake yasiwe mbele ya uso wake, na mambo ya uzinzi wake yasiwe kati ya maziwa yake; nisije nikamvua nguo zake akawa uchi, nikamweka katika hali aliyokuwa nayo siku ya kuzaliwa kwake, na kumfanya kama jangwa, na kumweka kama nchi kame. Na kumfisha kwa kiu; naam , sitawaonea rehema watoto wake: kwa maana ni watoto wa uzinzi. Maana mama yao amezini; yeye aliyewachukua mimba ametenda mamabo ya aibu.

 

Na katika sura ya pili, aya ya pili inaeleza hivi:

 

Bwana akanwambia, E nenda tena, mpande mwamanke apendavye na rafiki yake, naye ni mzini; kama vile Bwana awapandavyo wana wa Israeli,

 

Ingawa wanaigeukia miungu mingine, na kupenda mikte ya zabibu kavu. Basi nikajinunulia mwanamke huyo kwa vipande kumi na vitano vya fedha, na homeri moja ya shayiri, na nusu ya homeri ya shayiri; nami nikamwambia, utatawa kwa ajili yangu siku nyingi; hutafanya mambo ya ukahaba, wala  ingawa wanaigeukia miungu mingine, na kupenda mikte ya zabibu kavu. Basi nikajinunulia mwanamke huyo kwa vipande kumi na vitano vya fedha, na homeri moja ya shayiri, na nusu ya homeri ya shayiri; nami nikamwambia, utatawa kwa ajili yangu siku nyingi; hutafanya mambo ya ukahaba, wala

hutakuwa mke wa mtu awaye yote; nami nitakuwa hali iyo hiyo kwa ajili yako. Kwa maana wana wa Israeli watakaa siku nyingi bila mfalme , wala mtu mkuu.

 

 Kisa kama hii ambao ni hasara kuandikwa vitabuni licha kuandikwa katika kitabu (tukufu).  Na ikiwa Mtume hafanyi hivyo basi nini itakuwa kwa watu wengine?

 

Namikiwa mkubwa wa nyumba anapenda jambo Fulani baya, basi hakuna shaka watu wa nyumbani wote wataingia katika maovu yote Isitoshe hayo ampende mwanamke apaendwaye na rafiki naye ni mzini kama vile Bwana awapendavyo wana wa Israeli. Maneno kama hayo Kufananisha na Mwenyezi Mungu yafaa?

 

 

NABII   HARUNI

 

 Biblia Yapaswa ufundisha upweke wake Mwenyezi Mungu. Lakini Mtume wake huabudu miungu! Je, hiki si kinyume?

 

 Swali:          Je inamkinika Mtume kutengenza masanamu nakuwapoteza watu kwa kuabudu  masanamu?

 

  Jibu:    Haiwezekani kamwe kwani kuabudu masanamu ni kazi ya makafiri na mushriki na Mwenyezi Mungu hapendezwi na hayo kabisa. Lakini Biblia katika kitabu cha pili cha Musa, kiitwacho kutoka, sura ya 2 kuanzia aya ya kwanza hadi mwisho wa aya ya sita, inasema:

 

 Hata watu walipoona ya kuwa Musa amekawia kushuka katika mlima, wakakusanyana wakamwendea Haruni, wakamwambia, Haya! Katufanyizie miungu itakayokwenda mbele yetu,  kwa maana Musa huyo aliyetutoa katika nchi ya Misri hatujui yaliyompata. Haruni akawaambia, Zivunjeni pete za dhahabu zilizo katika masikio ya wake zenu, mkaniletee. Watu wote wakazivunja pete za dhahabu zilizo katika masikio yao, wakamletea Haruni. Akaipokea mikononi mwao akaitengeneza kwa patasi, akaifanya iwe sanamu ya ndama kwa kuiyeyusha: Na wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri. Naye Haruni alipoona jambo hili, akajenga madhabahu mbele yake; Haruni akatangaza akasema, Kesho itakuwa siku kuu kwa Bwana. Wakaondoka asubuhi na mapema, wakatoa dhahabu, wakaleta sadaka za amani, watu wakaketi kula na kunywa, wakaondoka wakacheza.

 

Swali:    Ati Mwenyezi Mungu hufanya hasira? Au Mungu kubishana na Mtume wake

na baadaye akajuta?

 

 Jibu:  Hasira na kutetana si jambo zuri kabisa kwa hivyo haiwezekani kamwe Mwenyezi Mungu atende tena na Mtume wake Mtukufu!

 

   Lakini Biblie inaedelea kusema,kutoka aya ya 10,hadi mwisho wa aya ya 14:

 

 Basi sasa niache ili harisa zangu ziwake juu yao, niwa angamize: Nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu. Musa akamsihi sana Bwana, Mungu wake, na kusema, Bwana, kwa nini hasira zako kuwakaa juu ya watu wako  uliowaleta kutoka nchi ya Misri kwa uweza mkuu, na kwa mkono wenye nguvu?. .

 

Geuka katika hasira yako kali, ughairi uovu huu ulio nao juu ya watu wako . . . .Na Bwana akaughairi ule uovu alisema ya kwamba atawatenda watu wake.

  

W A N A WA U Z I N Z I

 

 

 Je, aweza Mtume kuwa mwana wa haramu? Biblia inasema Sivyo Biblia inasema “Ndivyo!

 

 

Swali;    Je, aweza Mtume kuwa mwana wa haramu au mwana wa mwanamke kahaba?

 

Jibu:  Hawezi kuwa kamwe. Kwa sababu kuzaliwa haramu ni ‘aibu’ kwa mwana: Kunamwadhili mwana wa haramu machoni na myoyonimwa watu.

            Hivyo watu hawawezi kumsikiliza wala kupokea maneno yake. Kwa vile jambo hili halilingani na kusudio la utume, Mwenyezi Mungu hakutuma mtu yeyote wa aina hiyo akawa Mtume.

 

BIBLIA:  Vile vile inasema wazi wazi katika kumbukumbubu  la Torati, 23:2, ‘Mwana wa haramu asiingie katika mkutano wa Bwana: Hata kizazi cha kumi asiingie aliye wake katika mkutano wa Bwana.”

 

Kwa  hiyo, Mtume hawezi kuwa ‘mwana wa haramu.’

 

LAKINI:  Biblia yenyewe hiyo inasema kwamba baadhi ya Mitume walikuwa wana wa haramu!

 

(1)                    Waamuzi, sura ya 11:1, inasema: Basi huyo Yeftha, Mgileadi, alikuwa mtu shujaa sana, naye alikuwa ni mwana wa mwanamke kahaba:’

 

Na halafu inasema katika sura hiyo hiyo , aya ya 29, ‘Ndipo roho wa Bwana akamjilia juu yake Yeftha.’Hii ina maana kwamba alikuwa Mtume!

 

(2)          Mwanzo, 38:6-30, Yuda akamwoza mke  ni Tamari. Naye Eri, mzaliwa wa kwanzawa Yuda, alikuwa mbaya machoni pa Bwana: Na Bwana akamvua. Yuda akamwambia O nani, Uingie kwa mke wa nani, Uingie kwa mke wa nduguyo, ukamwoe, ukamwinulie nduguyo uzao. Onani

 

Alijua ya kwamba huo uzao hautakuwa wake, ikawa, alipoingia kwa mke wa nduguye, akamwangalia chini asipe nduguye uzao. Neno hili alilolifanya likawa baya machoni pa Bwana, basi akamwua yeye naye.

 

Yuda akmwambia Tamari mkwewe, Ukae mjane nyumbani mwa baba yako hata  shela mwanangu atakapokuwa mtu mzima, maana alisema, asipate kufa yeye kama nduguze. Basi Tamari akaenda, akakaa nyumbani mwa babaye. Siku nyingi zikapita. . . .

 

Huyo Tamari akapewa  habari, kusema, Mkweo anakwenda  Timna . . . , akakaa mlangoni pa Enaumu, Karibu na njia ya kuenda Timna. Yuda alipomwona alimdhania kuwa ni kahaba, maana amejifunika uso.  Akakaa mlangoni pa Enaumu, karibu na njia ya kuendea Timna. Yuda alipomwona alimdhania kuwa ni kahaba, maana amejifunika uso. Akamgeukia kando ya njia, akisema, Niruhusu niingie kwako. Maana hakujua ya, kuwa ni mkwewe. Akamwuliza, utanipa nini? Ukiingia kwangu?  . . . . Basi akampa, akaingiake, naye akapata mimba mitatu Yuda akapewa habari kwamba, Mkweo, Tamari amefanya uzinifu, naye ana mimba ya haramu. Ikawa, wakati wake wa kuzaa walikuwapo mapacha tumboni mwake . . . . kwa jina lake likaitwa Peresi. Akatoka Ndugu yake baadaye, . . naye akaitwa jina lake Zera.”

 

Na huyu Peresi ni babu yake Daudi kama ilivyoelezwa wazi katika Biblia, kitabu cha Mambo ya Nyakati cha kwanza, sura ya 2, aya ya 5, imeandikwa nasaba ya Daudi mwana wa Yese mwana wa Obedi mwana wa salmoni mwana wa Nashoni mwana wa Aminadabu mwana wa Ramu mwana wa Hesroni mwana wa Peresi.

 

Kwa hiyo, Daudi alikuwa Nabii na alikuwa katika kizazi cha kumi asiingie aliye wake katika mkutano wa Bwana!!!”

 

(3)   Samue 11; sura 12;24, inasem; Naye Daudi akamfariji Bath-sheba mkewe, akaingia kwake. Akalala naye; naye akazaa mwana, akamwita jina lake Sulemani. Naye Bwana akampenda;”

 

Kwa hivyo, Mtume Sulemani alikuwa mwana wa Beth- sheba.

 

Na katika Samuel 11, Sura 11: 2- 27, yasema hivi: Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la Mfalme: na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga: naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho naye Daudi akapeleka, akauliza habari za yule mwanamke, Mtu mmoja akasema, je! Huyu siye Bath- sheba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti? Basi Daudi akapeleka wajumbe, akatwaa: Naye akaingia kwake, naye akalala naye (maana yule mwanamke amekwisha kutakasika unajisi wake); kisha akarudi nyumbani kwake akachukua mimba; basi akapeleka na kumwambia Daudi, akasema, Ni mja-mzito’’ katika sura ya 3, uk .16 umeona namna alivyofanya hila ya kumwua Uria! Na kwamba Daudi alizini na Mke wa Uria, baadaye kamlewesha ili apate kulala na mkewe, Jambo lisiloridhisha,

 

Na kumpeleka Uria vitandani kwa hadaa ili auawe, na wakatenda hata akauawa?

Tazama, Biblia inaonyesha utakatifu gani wa Daudi na Beth- sheba, wazazi wake Sulemani (“naye Bwana akapenda!!)

 

(4)                    Sasa tazameni kwamba Biblia inamsingizia. Yesu pia kutokana na Peresi ambaye ni mwana wa haramu!

 

TAZAMA: Injili ya Mathayo Mtakatifu, sura 1, aya ya 1-16, yasema hivi: Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo. Mwana wa Ibrahimu. Ibrahimu alimzaa Isaka, Isaka akamzaa Yakobo , Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake; Yuda akamzaa Peresi na Zera kwa Tamari: Peresi akamzaa Esromu; . . . . . . Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa Yesu aitwaye Kristo.

 

 

NABII YEREMIA

 

  Swali:    Je, inamkinika Mweneyezi   Mungu amuamrishe Mtume wake atengeze utepe au nira na ajivike shingoni kwa nini? Kwa jambo la upuzi kwa ilhali yeye ni mfano mzuuri.

 

 Jibu:      Haiwezekani kamwe Mwenyezi Mungu kuamrisha hivyo.  Lakini Biblia katika kitabu cha Nabii Yeremia, sura ya 27,  aya 1 hadi mwisho wa aya ya nane inasema hivi:-

 

NABII NUHU

 

 Swali:  Ati Mtume hunywa mvinyo na kulewa hadi akawa hoikuvua nguo na kuwa uchi?

 

  Jibu:  Haiwezekani kamwe kufanya mambo yaliyokatazwa na Mwenyezi Mungu, wala mwenye akili yeyote hawezi kufanya mambo kama haya! Sembuse Mtume?

 

Lakini (agano zote mbili) BiIlia inamsingizia Mtume Nuhu hayo, basi tazama kitabu cha kwanza cha Musa, kiitwacho “Mwanzo” sura ya tisa, aya ya 20 inasema hivi:-

 

Neno hili likamjia Yeremia, kutoka kwa Bwana, kusema, Bwana ameniambia hivi, Jifanyizie vifungo na nira, ukajivike shingoni; ….. Naitakuwa, taifa lile na mfalme yule asiyetaka Nebukadneze, huyo mfalme wa Babelia, na kutia shingo zao katika nira ya mfalme wa Babeli, mimi nitaliadhibu taifa lile kwa upanga, na kwa njaa na kwa tauni.

 

Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu, akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake.  Hamu, baba wa kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje. 

 

N A B I I   M Z E E

 

 

Swali:    Ati Mtume husema uwongo?  

Akamwambia, karibu kwangu nyumbani, ule chakula. Naye akamwambia, siwezi kurudi pamoja nawe, wala kuingia pamoja nawe; wala sili chakula wala simywi maji pamoja nawe; kwani nimeambiwa kwa neno la Bwana, usile chakula wala usinywe maji huko, wala usirudi kwa njia ile ulioijia. Akamwambia, Mimi nami ni Nabii kama wewe na malaika akaniambia kwa neno la Bwana, husema, mrudishe pamoja nawe nyumbani kwako, ale chakula, akanywe maji. Lakini alisema uongo.

 

Jibu:      Hasha! Mtume hasemi uwongo kamwe kwani Mtume akiwa mwongo atamsadiki nani na kufuata dini yake?

 

 

Lakini kwa bahati mbaya Bilia inamsingizia hivyo Mtume mmoja. Tazama  kitabu cha kwanza cha Wafalme, sura ya kumi na tatu, kutoka aya 11 hadi mwisho wa aya 19, inasema hivi:-

 

Basi Nabii mmoja mzee alikuwa akikaa katika Betheli; akamfuata Mtume wa Mungu, akamkuta ameketi chini ya mwaloni, akamwambia, Je! Wewe ndiwe yule Mtume wa Mungu aliyetoka katika yuda? Akamwambia, Mimi ndiye.

 

 

N A B I I     E L I S H A

 

  Swali:      Ati inamkinika Mtume atoe habari kwa ilhali yeye anafahamu kwamba ni

 uwongo tu?

 

  Jibu:       Haiwezekani kamwe Mtume kueleza jambo ambayo yeye anajua kwamba ni uongo mtupu.

 

Lakini Biblia linamsingizia hivyo, tazama kitabu cha pili cha Wafalme, sura ya 8, kutoka aya 7 hadi mwisho wa aya 15, inasema hivi;

 

Kisha, Elisha akaenda dameski; na Ben-hadadi, mfalme wa Shamu, alikuwa hawezi; akamambiwa ya kwamba, yule Mtu wa Mungu ame fika. hapo. Mfalme akamwambia Hazeli, chukua zawadi mkononi mwako, ukaende ili kumlaki yule mtu wa Mungu, ukamulize bwana kwa kimwachake, kusema, je! Nitapona ugonjwa huu? Basi Hazaeli akaenda kumlaki, akachukua zawadi mkononi mwake, zakila kitu chema kilichopatikana Dameski, kiasi cha mzigo ya ngamia arobaini, akaenda akasimsimama mbele yake, akasema, Mwana wako Ben-hadadi, mfalme wa sham, amenituma kwako, kusema, je! Nitapona ugonjwa huu?  Elisha akamwambia, E nenda ukamwambie, bila shaka utapona; lakini Bwana umenionyesha ya kwamba Bila shaka atakufa …… akarudi kwa bwana wake; naye akamwambia, Elisha alikwambiaje? Akajibu, aliniambia kuwa bila shaka utapona ikawa siku ya pili yake akatwaa tandiko la kitanda, akali chovya katika maji, akali tangaza juu ya uso wake, hata akafa. Na Hazaeli akatawala badala yake.

 

 

KATIKA KITABU HIKI

 

1.                       Kuhusu Mwenyezi Mungu

 

Jinsi Biblia inavyozungumzia kuhusu Mwenyezi Mungu. Kiasi gani Biblia imetopewa kwa maovu na uwongo kuhusu Mwenyezi Mungu aliyeumba Ulimwengu? Biblia anasema yasiyofaa juu ya Utukufu wa Mwenyezi Mungu.

 

2.                       Kuhusu Mitume

 

Mambo gani ambayo Agano jipya na Agano la kale yameongopwa kuhusu Mitume wa Mwenyezi Mungu ? Mambo ambayo hayafai hata kwa duni lichaa ya Mitume wa Mwenyezi Mungu, waliokuwa watukufu zaidi kuliko binadamu  wote. Mitume hao hawakutumwa ila kuongoza, kutakasa na kutenda mema.  Lakini angalia jinsi Mitume hao walivyosimuliwa katika Biblia.