Ukweli kuhusu Uislamu
Wanachosema wasiokuwa Waislamu kuhusu…
Uislamu
Dini inayokuwa haraka sana ulimwenguni
Huu ni mkusanyo mfupi wa nukuu kutokakwa watu mashuhuri mbali mbali wasioWaislamu, wakiwemo wasomi, waandishi mafilosofa, washairi, wanasiasa, na wanaharakatiwa Mashariki na Maghribi. Kwa
tunavyojua hakunahata mmoja aliyewahi kuwa Mwislamu. Kwa hiyomaneno haya huonesha maoni yao binafsi juuya vipengele mbali mbali vyaUilsmau.
Sarojini Naidu (1879-1949)
Mwandishimshairi nammoja wa viongozi wenye kuonekana zaidi wa kabla yaUhuru wa India. Rais wa National Congress ya India na gavana wa kwanza mwanamke wa India huru.
- “Hali ya uadilifu ni moja ya fikra nzuri mno za Uislamu kwa sababu kila nikisoma katika Quran huona zile kanuni zenye nguvu za maisha,
sio fumbo bali maadili ya kiutendaji kwa ajili ya uendeshaji wa maisha uliofaa kwa ulimwengu wote.”
- Ilikuwa ni dini ya kwanza kuhubiri na kutekeleza demokrasi, ndani ya Misikiti wakati mwito wa Salat (Adhana ) unaposikika na wenye kuabudu wanapokusanyika pamoja,
demokrasi ya Uislamu imeunganishwa mara tano kwa siku wakati mkulima masikini na mfalme wanapopiga magoti sambamba na kutamka: “Mungu peke yake ndiye Mkubwa.” Nimeshangazwa sana tena sana kwa muungamo huu wa Uislamu usiokatika ambao humfanya mtu kwa silika kuwa ni ndugu”.
[Lecture on “The Ideals of Islam.” angaliakhutuba namaandishi ya Sarojini Naidu, Madras, 1918 uk. 167-9]
Avnold J. Toynbee (1889-1975)
Mwanahistoriawa Kiingereza, mhadhiri wa chuokikuu cha Oxford.
- “Kukomeshwa kwa dhamiri ya utaifa kati ya Waislamu ni moja ya mafanikio
makubwa ya Uislamu, na katika ulimwengu huu huu kama inavyojitokeza kuna kilio cha haja ya kuhubiri maadili haya ya Ki-Islam
[Civilization on trial, new York, 1948, P 205]
William Montgomery Watt (1909- )
Profesa (wa heshima)
wa masomo ya Ki-Arabu naki-Islamu kwenye chuo kikuu cha Edimburgh.
- Mimi sio Mwislamu katika hali halisi, igawa natumaini ni Mwislamu kama mtu aliyejisalimisha kwa Mungu, lakini naamini kile kilichotiwa ndani ya Qur’ani na maelezo mengine ya maono ya Ki-Islamu kwamba ni bohari kubwa za ukweli wa Mungu ambao kwamba mimi na watu wengine wa magharibi bado tunayo mengi ya kujifunza, na kwa hakika Uislamu ni mshindani mwenye nguvu wa utoaji wa mfumo wa msingi wa dini moja ya baadae.”
[Islamic and Christianity Today, London, 1983, p. ix]
Bertrand Russel - (1872-1970)
Filosofa wa Kiingereza, Mwanahisabati, na tunzo yaNobel ya Laureate, ambaye kwamba msisitizo wake juu ya uchambuziwa kimantiki kwa kiasi kikubwasana umeshawishi mwenendowa filosofia ya karne ya20.
- “Utumiaji wetu wa msemo “zama za giza” kuelezea kipindi cha kuanzia 699 mpaka 1.000 huonyesha kujishughulisha kwetu mno na ulaya ya magharibi… Kuanzia India mpaka Spain ustaarabu mzuri sana wa Ki-Islamu umestawi. Kilichopotea kwenye ukristo wakati huu, hakikupotea kwenye Ustaarabu, bali kinyume chake kabisa… Kwetu sisi huonekana kwamba ustaarabu wa ulaya ya magharibi ndio ustaarabu, lakini huu ni ufinyu wa mawazo.”
[History of Western Philosophy, London, 1948, p. 419]
Hamilton Alexander RoskeenGribb - (1895-1971)
Mwanachuoni mustashiriki anayeongoza wawakati wake.
- “Lakini Uislamu bado una huduma zaidi ya kutoa kwenye mwenendo wa ubinadamu. Hata hivyo umesimama karibu zaidi upande wa mashariki kuliko ulaya inavyofanya, na una utamaduni mkubwa wa kuelewana na ushirikiano kati ya jamii na jamii. Hakuna jamii nyingine ambayo ina sifa ya mafanikio ya kuungana katika usawa wa hadhi,
fursa na katika juhudi nyingi mno na jamii nyingi mbali mbali za binaadamu . Uislamu bado una uwezo wa kuunganisha kwa wazi elementi zilizotengana za taifa na utamaduni. Kama upinzani wa kale na kale wa jamii mkubwa za mashariki na magharibi ungebadilishwa na ushirikiano, upatanisho wa Uislamu ni shariti lenye kukubalika. Katika mikono yake liko suluhisho kubwa sana la tatizo ambalo kwamba Ulaya inakabiliana katika uhusiano wake na Mashariki .”
[Whither Islam, London 1932,P.379]
- “Kwamba mageuzi yake (Muhammad) yamezidisha hadhi ya wanawake kwa ujumla, (hilo) hukubalika kwa wote.”
[Mohammedanism, London, 1953, P.33]
James A. Michener. (1907-1997)
Mwandishi anayeongoza wa Kimarikani, mpokeaji wa shahada za heshimaya
udaktari katika fani tano kutoka vyuo vikuu thelathini na pamoja natunzo ya medali
ya Rais yaUhuru (Presidential Medal of freedom) tunzo la kiraia la juu kabisa la
Amerika.
- “Hakuna dini nyingine katika historia iliyoenea haraka sana kama Uislamu. Watu wa Magharbi wameamini zaidi kwamba ueneaji huu wa dini ulifanywa uwezekane kwa upanga. Lakini hakuna mwanachuoni wa kisasa anayekubali wazo hilo, na Qur’an kwa uwazi kabisa inaunga mano na Uhuru wa dhamiri.”
[Islam- The Misunderstood Religion, Readers’ Digest ( American Edition)May 1955]
Edward Gibbon (1737-1794)
Anachukuliwa kamamwanahistoria mkubwa wa Kiingereza wawakati wake.
- “’Naamini katika Mungu Mmoja na Muhammad Mtume wa Mungu’, ni ungamo jepesi na lisilo badilika la Uislamu. Mfano wa kielimu wa Mungu kamwe haujatwezwa kwa sanamu linaloonekana; utukufu wa Mtume kamwe haukupituka kipimo cha
maadili ya mwanadamu, na maisha yake ya maadili yamezuia shukurani za wafuasi wake ndani ya mipaka ya akili na dini.
[History of the Saraanempire, London1870-54]
·
“Halisi zaidi kuliko mfumo waZoroasta, wenye mawazo mapana nahuru zaidi kuliko sheria yaMusa, dini ya Muhammad yaweza kuonekana kwamba haikinzani sana na akili kama itikadi ya fumbo na ya kidhana, ambayokatika karne ya saba imetweza wepesi wa Injili”
[The history of the Delineand fall of Roman
Empire,
vol.5.p 487]
Javed Diamond.
Profesa wa fiziolojiakatika chuo kikuu cha UCLA school of Medicine, mpokeziwa tunzo ya Pulitzer prize for General Non- fiction
katika 1998
- “Uislam wa zama za kati uliendelea kitekinolojia, na (milango) wazi kwa ijitihadi, umefanikiwa kwa mbali zaidi katika viwango vya elimu kuliko wenzi wao wa ulaya, umenyonya urithi wa ustaarabu mkubwa wa kigiriki mpaka kufikia hatua ambayo kwamba vitabu vingi vikubwa sasa vimejulikana kwetu kwa kupitia tu nakala za ki-Arabu. Uligundua kinu cha upepo, trigonometria, tanga la pembe tatu, na wakafanya maendeleo makubwa katika ufuaji, ufundimitambo na uhandisi kemikali na njia za umwangiliaji.
Katika zama za kati mtiririko wa tekinolojia ulikuwa ukiingia kwa nguvu kutoka kwenye Uislamu kwenda Ulaya kuliko kutoka Ulaya kwenda kwenye Uislamu. Ni baada tu ya miaka ya 1500 ndipo mwelekeo wa mtiririko ukaanza kwenda kinyume.”
[Guns, Germs and Steel-The fates of Haman Societies 1997, P 253]
Annie Besant (1847-1933)
Mwanateosofia waKiingereza na kiongozi mzalendo katika India, Rais wa India National Congess l 917
- “Mara nyingi huwa nafikiri kwamba mwanamke yuko huru zaidi katika Uislamu kuliko katika Ukristo. Mwanamke amehifadhika zaidi na Uislamu kuliko alivyohidhiwa na imani inayohubiri mke mmoja. Katika Qur’an sheria kuhusu mwanamke ni ya haki na ya uhuru zaidi. Ni katika miaka ishirini tu iliyopita ndipo wakristo wa Uingereza, wanatambua haki ya mwanamke kumiliki mali, ambapo Uislamu umeruhusu haki hii kuanzia mwanzo”
[The life and Teachings of Muhammad Madras 1932 p. 25-26]
Mtarjumi: Dr M S Kanju
Al`Itrah Foundation