TAQIYAH

NI NI

Kimeandikwa na: ALLAMAH SAYYID SAEED AKHTAR RIZVI

Kimetafsiriwa na: MOHAMMED S. KANJTJ

من كفر بالله من بعد إبمنه إلا من أكره وقلبه مطمئن بالإيمان ولكن من شرح بالكفر صد را فعليهم غضب من الله ولهم عذاب عظيم.

 " Ambaye anamkufuru Allah baada ya imani kwake (ni muongo) isipokuwa yule ambaye amelazimika ambapo moyo wake umetulia juu ya imani (hana cha kuhofu). Lakini yule Allah anayekifungua kifua chake kwa ukafiri, basi juu yao ghadhabu kutoka kwa Allah na wanayo kwao adhabu kubwa"[1]

Aya bii ya Qur'an inazungumzia kisa cha Ammar bin Yasir (R.A.) wakati alipolazimika kusema baadhi ya maneno dhidi ya Uislamu ili kujiokoa kutoka kwa makafiri wa Kikureishi. Aya hii inaruhusu kwa uwazi kabisa mtu kuficha imani yake ya kweli anapokuwa katika hatari ya kupoteza maisha yake. Kanuni hii inaitwa Taqiyah.

Swali la 1: Nini maana ya "Taqiyah"?

Jibu: Maana yake kilugha ni kujilinda kiusalama: kujihami: kuogopa; uchaji. Al-Munjid anasema:

تقي- يتقي-تقي و تقاء و تقية بمعني اتقي..... اتقي اتقاء صا ر تقي

Maana hasa ya maneno hayo hapo juu, ni kwamba neno Taqiyah lina maana ya kuwa katika ulinzi, kuogopa na kuwa Mcha Mungu. Kamusi ya as-Sarah inasema:

 (Tagiyah, Tugat   = Uchaji).

Swali la 2: Ina maana gani katika istilahi ya Kiislamu.

Jibu: Katika istilahi ya Kiislamu ina maana kuokoa maisha, heshima au mali (ima yake mwenyewe au ya Mwislamu mwingine) kwa mtu kuficha imani au dini kwa sababu inamuokoa mtu kutoka katika ghadhabu ya Allah.([2])

Swali la 3: Je. ni kitu cha Ushia peke yake, kwa sababu nimewasikia watu wengi wakiwalaumu Mashia kwa sababu ya Taqiyah?

Jibu: Kilajamii, dini na kikundi huifanya na wameifanya katika wakati mmoja au mwingine, Utaona mifano mingi ya Taqiyah katika Agano la kale na Agano jipya, na hata katika maisha ya Mtukufu Mtume wa Uislamu, Sahaba wake na Wanachuoni wengi wa Kisuni.

Swali la 4: Lakini je, jambo hili linaruhusiwa katika Uislamu?

Jibu: Ndio. Allah ameiruhusu katika Qur'an; na akili vile vile huonyesha hekima ya ruhusa hii.

Shah Abdu I-Aziz Dehlawi anaandika: "Ni budi ieleweke kwamba Taqiyah kwa hakika imeruhusiwa na Shari'ah, kwa ruhusa ya aya za Qur'an, "isipokuwa wakati unapotaka kujilinda naona isipokuwa yule ambaye amelazimika ambapo moyo wake uko imara pamoja na imani H.([3])

Mwanachuoni mashuhuri wa Kisunni Allamah Wahidu z-Zamman Khan wa Haydarabad (India) anasema: "Taqiyah imethibitishwa na Qur'an "isipokuwa wakati unapotaka kujilinda nao." na watu wajinga (wasiojua) wanafikiri kwamba Taqiyah ni kitu cha pekee kwa Masbia, ambapo imenihusiwa vile vile katika Madhehebu ya Sunni kwa nyakati (maalum).([4])

Swali la 5: Kama ukificha imani yako na kutangaza wewe mwenyewe kuamini baadhi ya mafundisho yasiyokuwa ya Kiislamu, haitakuwa kwamba moja kwa moja umetoka nje ya mipaka ya Uislamu na kuwa Kafiri?

Jibu: Itikadi na imani na hali kadhalika kutokuwa na imani au upuuzaji wa itikadi (kwa kifupi imani na kufur) kimsingi ni mambo ya moyo" ndio maana Allah (SWT) akawakemea wale Waarabu waliosilimu karibuni, ambao walidai kuwa waumini:-

قالت الأعراب ءامنا قل لم تؤمنوا ولكن قولوا أسلمنا ولما يد خل الإيمان في قلوبكم وإن تطيعوا الله ورسوله لا يلتكم من أعمالكم شيئا إن الله غفور رحيم.

"Mabedui wanasema: "Tunaamini" sema (kuwaambia wao): Bado hajaamini, bali semeni "tumeukubali Uislamu" kwa sababu imani bado haijaingia kwenye nyoyo zenu".([5])

Tamko kwa ulimi lina mchango mdogo sana ndani yake. Imani bila tamko inakubalika, lakini tamko bila imani imelaumiwa katika Qur'ani kwa maneno makali:-

إذا جاء ك المنفقون قالوا نشهد إنك لرسول الله والله يعلم إنك لرسوله والله يشهد إن المنفقين لكذ بون.

"Wanapokuja wanafiki kwako, wanasema: "Tunashuhudia kwamba hakika wewe ni Mtume wa Allah" na hakika Allah anajua kwamba hakika wewe ni Mtume wake na hakika Allah anashuhudia kwamba wanafiki kwa hakika ni warongo".([6])

Sasa kumbuka kwamba maisha ya Mwislamu ni ya thamani sana mbele ya macho ya Uislamu. Umuhimu uliwekwa hata kwa maisha ya mtu mmoja unaonekana katika aya hii.

ومن أحيا ها فكأ نما أحيا الناس جميعا.

"Na mwenye kuokoa (yaani maisha ya mtu) atakuwa kama ameokoa watu wote. ([7])

Na Mwislamu ana wajibu wa kuokoa maisha kutokana na uharibifu usio sheria (uovu) ima ikiwa ni mtu mwingine yeyote au wake mwenyewe:-

ولا تلقوا بأ يد يكم إلي التهلكة.

Na usijitie mwenyewe na mikono yako katika upotofu.([8])

Ni kwa sababu hii kujinyonga mtu ni dhambi kubwa kama kuua mtu mwingine na ni kwa sababu hii kwamba sheria ya Shia hairuhusu

kuanza kupigana jihadi bila ruhusa ya Mtume. Imam au wawakilishi wao maalum au katika kujitetea.

Na ni kwa ajili ya kuokoa maisha ya Mwislamu mtu anaruhusiwa kuzungumza uongo na kuokoa maisha hayo ya tamani.

Swali la 6: Vizuri. Umeokoa maisha, lakini umetenda moja ya dhambi kubwa yaani uongo. Hivyo Kiroho umeangamia kwenye fedheha kwa kila hali. Basi kwanini usiseme kweli na uache maadui wakuue kama wanataka?

Jibu: Wakati mtu anakuwa katika hali ambayo kwamba kwa vyovyote vile njia atakayochagua atatenda dhambi, basi akili inasema kwamba hana budi kuchagua njia ya dhambi hafifu. Au kama analazimishwa kuharibu au kufanya madhara kati ya moja ya vitu vyake viwili, basi kwa hakika ataharibu au kukifanyia madhara kile ambacho si cha thamani sana kuokoa kile ambacho ni cha thamani zaidi. Imam Fakhru d-din Ar.Razi anasema akitoa maoni juu ya matukio ya Nabii Musa (a.s) na Khidir (a.s) yaliyotajwa katika sura al-Kahf:-

ان عند تعارض الضررين يجب تحمل الأد ني لد فع الأ علي فهذا هو الأ صل المعتبر في المسائل الثلا ثة.

"Mtu anapokabiliwa na vitu viwili tofauti viumizavyo, ni wajibu kuvumilia kilicho tahafifu ili kuondokana na kile chenye madhara zaidi, na hii ndio kanuni iliyofuatwa katika matendo matatu (yaliyofanywa na Khidhir)([9])

Sheria ya Kiislamu imejaa tele na mifano ya kanuni hii. Sala ni nguzo muhimu sana ya Uislamu. Lakini kama unasali na mtoto akatumbukia ndani ya kisima, na hakuna mwingine wa kumuokoa. mtoto yule, Sheria hukuamuru kuacha sala na kujaribu kumuokoa mtoto. Kama ukipuuza amri hii, sala ile haitakubaliwa, na utakuwa

na hatia ya kupuuza kuokoa maisha.

Sasa chukulia Makafiri wamekusudia kumuuwa Mwislamu, sio kwa sababu ametenda kosa lolote, bali kwa sababu tu ya imani yake,. Mwislamu yule akaendakujificha na unajua alipo. Makafiri wakaja kwako na kukuulizia iwapo unajua mtu yule alipo.

Utakuwa umenasa katikati ya mabaya mawili; ima utasema; "sijui" na uwe muongo, au useme: "Ndio" na usababishe mauaji ya Mwislamu asiye na makosa, Akili inasema kwamba kusema uongo katika hali hii kunapendelewa kuliko kweli ambayo itapelekea kwenye mauaji.([10])

Sasa tuchukulie kwamba Makafir wamemkamata Mwislamu na Mwislamii yule ni wewe mwenyewe, wanaweka hiari mbili mbele yako; Ama ukane Uislamu au uawe. Kama miali ya imani ya kweli inainurisha moyo wako, maneno tu ya ulimi hayawezi kuizimisha aslani. Maneno yale.ya ukafir yatakuwa kama mfiiniko wa giza kuficha nuru ya imani yako kutoka kwa makafir, lakini hayawezi kuwa na athari ya kinyume juu ya miali yenyewe. Na kama hufichi miali hiyo nyuma ya mfiiniko huo, uhai wako utatolewa na kwa hilo utapoteza nafasi ya kuuhudumia Uislamu katika wakati mwingine.

Kwa ufiipi, kwa kutoa maneno machache dhidi ya Uislamu, utaokoa maishayako hali kadhalika na imani yako; nakwa kutotoa maneno hayo uhai wako ungefikia mwisho na pamoja nao utaondoa nafsi zote za hudunia ya Kiislamu ambayo ungeweza kuitoa kama ungekuwa hai. Hivyo Allah (S. W.T.) ameruhusu kuokoa maisha yako kwa kutoa maneno macftache ya uongo dhidi ya Uislamu.([11])

Swali la 7: Sema irtakavyo, lakini ukweli unabakia kwamba Taqiyah ni aina tu nyingine ya Nifaq (unafiki).

Jibu: Mbali ya kutoka na hiyo. Ukweli ni kwamba Taqiyah ni mbalimbali na unafiki. Kumbuka Imani na Kufr wakati vikionekana na ilani yao yaweza kugawanya katika makundi manne tu:-

[12]

(R.A.). Hata Allah alithibitisha kitendo chake katika aya ambayo imeandikwa mwanzoni.

من كفر بالله من بعد إبمنه إلا من أكره وقلبه مطمئن بالإيمان ولكن من شرح بالكفر صد را فعليهم غضب من الله ولهم عذاب عظيم.

 

" Anayemkufuru Allah baada ya Uislamu wake (inamngoja adhabu kubwa) isipokuwa yule aliyeshurutishwa hali ya kuwa moyo wake umetumwa juu ya Uislamu (wake) lakini anayekifungulia ukafiri kifua chake., hao ghadhabu ya Allah iko juu yao, na watapata adhabu kubwa".([13])

Mufasirina wote wa Qur'an wanasema kwamba, Aya hii iliteremshwa kuhusiana na kisa hicho hapo juu cha Ammar.(R.A)([14]1

Swali la 9: Je kuna aya yoyote nyingine inayoruhusu mwendo wa namna hii?

Jibu: Ndio. Angalia aya zinazofuata ambazo zinasema:

لا يتخذ المؤمنون الكفرين أولياء من د ون المؤمنين ومن يفعل ذ لك فليس من الله في شيء إلا أن تتقوا منهم تقة و يحذ ركم الله نفسه وإلي الله المصير* قل إن تخفوا ما في صد وركم أو تبد وه يعلمه الله و يعلم ما في السموات و ما في الأرض  والله علي كل شيئ قد ير*

"Walioamini wasiwafanye makafiri kuwa wapenzi wao (wa kuwapa siri zao) badala ya (Waislamu wenzao) na atakaefanya bivyo, basi hatakuwa na chochote mbele ya Allah, ila (ikiwa mnafanya urafiki nao au juu juu tu hivi) kwa ajili ya kujilinda na shari zao. Na Allah anakutahadharisheni na adhabu yake. Na marejeo ni kwa Allah". Our'an 3:28 Sema: Kama mkificha yaliyomo vifuani mwenu au mkiyadhihirisha, Allah anayajua, na anayajua yaliyomo mbinguni na yaliyomo ardhini, na Allah ni mwenye uwezo juu ya kila kitu."([15])

Sababu ya ruhusa bii imeelezwa katika aya hii yenyewe. "Sema: "Kama mkificha yaliyomo vifuani mwenu au mkiyadhihirisha Allah anayajua. Hapa Allah (S. W.T.) huhakikishia Waislamu  kwamba Imani ni kitu cha kiroho kilichounganishwa na moyo; na kama imani ndani ya moyo wako ni imara, basi Allah anakuwa radhi na wewe iwe imani biyo umeidhihirisha au umeificha. Yote ni sawa kwa Allah, kwa sababu anajua siri zako zilizoficbika, na hata wakati kama ukificha imani yako kwa makafir Allah anaijua na kuitambua.

Kama ilivyoelezwa katika kujibu swali la kwanza Taqiyah na Tuqat yote yana maana moja as-Sayuti anaandika pamoja na mambo mengine chini ya aya bii:

واخرج ابن أبي حاتم من طريق العوفي عن ابن عباس في قوله: إلا ان تتقوا منهم تقية: فالتقية باللسان من حمل علي امر بتكلم به وهو معصية لله فيتكلم به مخافة الناس وقلبه مطمئن بالإيمان  فإن ذ لك لا يضره إنما التقية باللسان ... واخرج عبد بن حميد عن الحسن قال التقية جائزة إلي يوم القيامة – واخرج عبد عن أبي رجاء أنه كان يقرأ إلا ان تتقوا منهم تقية- وأخرج عبد لبن حميد عن قتادة أنه كان يقرؤها  إلا ان تتقوا منهم تقية بالياء.

"Na Ibn Jarir na Ibn Abi Hatim wamesimulia kupitia kwa al-Awfi kutoka kwa Ibn Abbas (kwamba alisema kuhusu aya hii): Hivyo Taqiyah ni kwa ulimi. Yoyote atakayelazimishwa kusema kitu ambacho ni cha utovu wa utii wa Allah (SWT) na husema hivyo kwa sababu ya hofu ya watu hao ambapo moyo wake umebakia imara katika imani, haitamletea madhara, hakika Taqiyah ni katika ulimi tu   

"Na Abd Ibn Hamid amesimulia kutoka kwa al-Hasan (al-Basiri) kwamba amesema Taqiyah ni halali mpaka siku ya ufufuo.Na Abd (IbnHamid) amesimulia kutoka kwa Abu Raja kwamba alikuwa akisoma illa an tattaqu Minahum taqiyyattan'  na Abd Ibn Hamid amesimulia kutoka kwa Qatadah kwamba alikuwa
akisoma hivyo   taqiyatan - pamoja na ya:"([16])

Imam Fakhuruddin ar-Razi ametaja baadhi ya kanuni kuhusiana na taqiyah chini ya aya hii, ambazo baadhi zinatolewa hapa,

Kanuni ya tatu: Taqiyah inaruhusiwa katika mambo yahusianayo na udhihirisho wa urafiki au uadui; na vile vile imeruhusiwa katika mambo yanayohusiana na kutaja dini yao. Lakini  ni  dhahiri  hairuhusiwi  katika  mambo yanayo athiri watu wengine, kama kuuwa, zinaa, kupora mali, kushuhudia uwongo, kusingizia mwanamke aliyeolewa (kuwa kazini) au kuwapa habari makafiri kuhusu sehemu dhaifu katika ulinzi wa Waislamu.

Kanuni ya Nne: Aya ya Qur'an inaonyesha wazi kwamba Taqiyah inaruhusiwa (ukiwa) pamoja na makafiri wenye nguvu. Lakini kwa mujibu wa madhehebu ya Imam Shafii (Allah amuwiye radhi) kama hali katika (madhehebu mbalimbali) ya Waislamu inafanana na hali kati ya Waislamu na makafir, basi Taqiyah (kwa Waislamu vile vile) inaruhusiwa kwa kulinda maisha ya mtu.

Kanuni Tano: Taqiyah inaruhusiwa kwa ajili ya ulinzi wamaisha. Swali ni kwamba iwapo inaruhusiwa kwa ajili ya ulinzi wa mali, uwezekano ni kwamba hiyo pia yaweza kuruhusiwa, kwa sababu Mtume (S.A.W.) amesema: Heshima ya mali ya    Mwislamu ni sawa sawa na heshima ya damu yake, na vile vile yeye (S.A.W.)

amesema: Ambaye atauawa katika kutetea mali yake atakuwa amekufa kifo cha kishahidi na vile vile kwa sababu mtu huihitaji sana mali yake.

Ikiwa maji yanauzwa kwa bei kubwa wudhu hauwi wajibu na mtu anaweza kusali kwa kutayamam kuepusha hasara ile ndogo ya malli, hivyo kwa nini kanuni hii isitumike hapa? Na Allah anajua vizuri.

Kanuni ya Sita: Mujahidi amesema kwamba hii kanuni (ya Taqiyah) ilikuwa ikitumika katika mwanzo wa Uislamu, kwa sababu waumini walikuwa wanyonge wakati ule. Lakini sasa kwa vile dola la Kiislam limepata nguvu na imara taqiyya hairuhusiwi tena. Lakini Awfi amesimuulia kutoka kwa al-Hasan (al-Basri) kwamba: amesema: Taqiyah inaruhusiwa kwa Waislamu mpaka siku ya ufufuo. Na maoni yanakubalika zaidi kwa sababu ni wajibu kuondoa aina zote za madhara kutoka kwa mtu mwenyewe kadiri iwezekanavyo' ([17]

Imam Bukhari ameandika mlango mzima, kitabul ikraah, juu ya mada hii ya kulazimishwa, ambapo anaandika pamoja na mambo mengine:-

قول الله تعالي: إلا من أكره وقلبه مطمئن بالإيما ن ... و قال إلا ان تتقوا منهم تقاة وهي تقية.... وقا ل الحسن التقية إلي يوم القيامة.... و قا ل النبي صلي الله عليه وسلم: الأعما ل بالنية.

Na Allah amesema: Isipokuwa mnapotaka kujilinda wenyewe dhidi yao kwa kuwahofia. Na hiyo ni Taqiyah................

Na Hassan (Basir) amesema: Taqiyah ni mpaka siku ya ufufuo

Na Mtume (S.A.W.) amesema: Matendo yanatokana na  nia ([18])

As- Sayid ar-Radhi (mkusanyaji wa Nahajul-Balagha) anaandika pamoja na mambo mengine, katika kuelezea Aya 3:28-29.

ثم استثني تعالي حال التقية فقال ( إلا ان تتقوا منهم تقاة) وقرء (تقية) وكلا هما يرجعا ن إلي معني واحد فكأ نه سبحا نه أباح في هذه الحال عند الخوف منهم إظها ر موالا تهم ومما يلتهم قولا باللسان لا عقدا بالجنا ن.

"Kisha Allah akaifanya mbali (katika kanuni hii ya kutoweka urafiki na makafiri) na umbali huo ni hali ya Taqiyah; Hivyo alisema"

إلا ان تتقوا منهم تقاة.

Na vile vile inasomwa ( تقية) (Taqiyatan), na maneno yote haya yana maana moja. Ina maana kwamba Allah ameruhusu katika hali bii (wakati mtu anawahofia) kuonyesha urafiki wao na kuinamia upande wao kwa ulimi, lakini sio pamoja na nia ya moyoni([19])

Vile vile,  kuna aya  nne kakita Qur'ani ambazo huruhusu kula chakula kilicho haramishwa wakati mtu ana njaa ya kufa na hakuna chakula halali kipatikanacho. Mojawapo ya hizo (aya) husema:-

إنما حرم عليكم الميتة والد م و لحم الخنز ير وما أهل به لغير الله فمن اضطر غير باغ ولا عاد فلا إثم عليه إن الله غفور رحيم.

"Yeye amekuharamishieni mzoga tu na damu na nyama ya ngurawe na kilichotajiwa katika kuchinjwa kwake, jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Lakani aliyefikwa na dharura (ya kula vitu hivi) bila kutamani wala kupita kiasi yeye hana dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwingi wa kusamehe (na) mwingi wa kurehemu" ([20])

Kama ilivyokwisha elezwa hapo mwanzo, uhai wa muumini ni wa thamani kubwa kabisa kuliko vitu vyote. Na ni kwa sababu hii kwamba mtu ameruhusiwa kula vitu hivi vya kuchukiza mno, kama nyamafu au nguruwe ambapo kuwepo uhai hutegemea kwayo. Kanuni hii itatumika kama usalama wa maisha utategemea kutamka maneno machache ya uongo. Ndiyo Mtume (S.A.W) ameainisha wazi wazi kabisa kwa kusema:

لا د ين لمن لا تقية له.

Asiye na "tagiya" hana dini.([21])

Na Imamu Muhammad al-Baaqir (s.s.) amesema:

قال أبو جعفر: التقية من ديني و دين آبائ ولا إيمان لمن لا تقية له.

Taqiyah ni dini  yangu na ni dini ya wahenga wangu Yeyote ambaye hana "taqiyah" hana imani ([22])

Swali la 10: Ingawaje mwendo huu umeruhusiwa katika Qur'an na Hadithi, hata hivyo ni kitu kibaya. Siamini kwamba Allah (S.W.T). angetutaka sisi tukikimbilie kukitumia hata kama kimerusiwa.

Jibu: Umekwisha ona sasa hivi kwamba "taqiyah' siyo kuruhusiwa tu bali pia ni wajibu katika baadhi ya mambo. Unafikiri kwamba Allah angekifanya kitu kuwa wajibu bila ya kukipenda. Vile vile, Mtume (S.A. W.) kaifanya "tagiyah" KUWA na maana moja na dini, na Imamu Muhammad al-Baaqir (a.s.) amelithibitisha hili kwa maneno ya wazi kabisa. Hata hivyo kama utatafakari na kuichunguza Qur'an utaona kwamba kitabu hiki kitukufu cha Allah huidhihirisha "taqiyah" katika mwanga wa kustahiki kusifiwa sana, katika aya hii 40:28 Allah anasema:-

وقال رجل مؤمن من آل فرعون يكتم إيمنه.

Na akasema mtu mmoja Muumini aliyekuwa mmoja wa watu wa Firauni, "afichaye Uisiamu wake.([23])

Huonyesha kwamba Allah aliridhishwa sana na kufichwa kule kwa Imani kwa sababu ilikuwa na faida kubwa, kama vile Mzee Abu Talib alivyoiweka imani yake (Uislamu) kwa kuificha - siri,  kwani  kwa kufanya hivyo kulikuwa na faida kubwa. Kwa sababu Mzee Abu Talib hakuidhihirisha imani yake, aliweza kuyalinda maisha ya Mtukufu mtume (S.A. W!). Vivyo hivyo, yule Muumini kutoka katika familia ya Farauni aliweza kumlinda Mtume Musa (a.s) kwa kutokuidhihirisha imani yake waziwazi.

Kwa vyovyote vile, imani yake iliyowekwa juu ya "Taqiyah" ilimpendeza Allah kiasi kwamba alihesabika kama "Siddig" (Mkweli kabisa). Mtume Mtukufii (S.A.W.) amesema:

الصد يقون ثلا ثة حبيب النجا ر مؤمن آل يا سين الذي قال يا قوم اتبعوا المرسلين وحزقيل مؤمن آل فرعون الذي قال أتقتلون رجلا ان يقوا ربي الله و علي بن أبي طالب وهو أفضلهم. ( اخرجه البخا ري عن ابن عباس واحمد عن أبي ليلي)-

" Wako wakweli (Siddiq) watatu (1) Habib Najjar; Muumini kutoka AIyasin ambaye alisema: Enyi watu wangu; wafuateni Mitume; (2) Yule mkweli kutoka katika familia ya Farauni ambaye amesema; mnataka kumuua mtu kwa sababu anasema: Mola wangu ni Allah. na (3) Ali bin Abi Talib, na yeye ni bora kuliko wote hawa([24])

Siyo tu "Muumini kutoka familia ya Firauni bali, kwa kauli ya Al-Baidawi, hata MtumeMusa (a.s.) aliutumia muda mrefuwa maisha yake katika "taqiyah" Angalia maelezo yake chini Aya ifuatayo:-

قا ل  ألم نربك فينا وليدا ولبثت فينا من عمرك سنين.

(Firauni) akasema, Je hatukukulea kwetu (ulipokuwa) mtoto na ukakaa pamoja na sisi miaka (mingi) ya umri wako?([25])

Tukirudi nyuma katika wakati wa Mtukufu Mtume (S.A.W.) wa Uislamu, tunatambua kwamba Mtukufu Mtume aliuweka ujumbe wake siri kwa miaka mitatu (3) na tumeona vipi Ammar bin Yasir alivyotumia "tagiyah". Hiki kilikuwa kipindi wakati wakiwa wako Makka. Hata baada ya kuhama (Hijira) walibakia katika Makka.

Waislamu wengi ambao Uislamu wao haukufahamika kwa wengine. Wakati Mkataba  wa amani  ulipokamilishwa  kule Hudaibiyah katika mwaka wa sita (6) wa Hijra Waislamu wengi hawakuridhika na masharti yake. Bwana Umar bin Khattab alikasirishwa sana kiasi kwamba alilalamika kwa Mtukufu Mtume (S.A.W.) na katika siku za baadae alikuwa akisema:-

ما شككت مذ أسلمت إلا يو مئذ

Sikuwahi kutia shaka yoyote ile - juu ya utume wa Mtukufu Mtume - tangu nilipo ukubali Uislamu isipokuwa siku ile ya (Mkataba wa) Hudaibiya ([26]>

Kwa kulijibu kundi lile Allah anaelezea moja ya sababu ya mkataba ule na moja ya visababisho kwa nini vita havikupiganwa wakati ule:-

ولو رجال مؤمنون ونساء مؤمنات لم تعلموهم أن تطئوهم فتصيبكم منهم معرة بغير علم.

"Na lau kama si wanaume Waislamu na wanawake Waislamu (walioko Makka wanaficha Uislam wao) msio wafahamu, msije mkawaswaga bila kujua ..."([27])

Aya hii inaeleza wazi kabisa kwamba walikuwepo Waislamu wanaume na Waislamu wanawake katika Makka ambao Uislamu wao ulikuwa hautambuliki, siyo tu kwa Makafiri bali pia hata kwa Waislamu wa Madina. Na Allah anaeleza watendao "taqiyah", hiyo kama wanaume waumini na wanawake waumini.

Kwa ufupi aya hizi, haditbi hizi na matukio haya huonyesha na kudhihirisha wazi kwamba kama mtu yuko katika hatari ya kupoteza maisha yake kwa sababu ya Imani yake, basi imeruhusiwa kusema maneno dhidi ya Imani ya kweli ya Uislamu, ili kuokoa maisha yake ambayo ni ya muhimu zaidi na kwamba ule 'uongo' hautahesabika dhidi yake.

As-Sayid ar-Radhi anasema:-

......natunajua kwamba"taqiyah" huathiri tu kwa nje(yaani madhara yake ni katika ulimi tu) na siyo kwa ndani (katika moyo, rohoni, katika nafsi),

Wakati anapolazimishwa mtu mwingine kufanya kitu au jambo fulani (na kitu hicho au jambo hilo ikatokea kuunganishwa na moyo) basi dhalimu hana njia ya kutambua au kujua kwamba pendekezo lake limetekelezwa, isipokuwa kwa kutokana na matamshi fulani ya mdomoni na kutokana na hayo ndipo ataweza kuhitimisha kwamba amefanikiwa katika kubadilisha moyo wa aliyedhulumiwa. Kwa hivo lililo bora kabisa kulitenda wakati wa kufanya Taqiyah ni kuonyesha urafiki kwa Makafiri kwa maneno, kuchanganyika nao. kuishi nao kwa wema lakini moyo lazima ubakie imara katika uoni wa awali kuwahusu wao, kwa uadui uliofichwa na ile imani ya mtengano kutoka kwao.

"Na mtu kama huyo (ambaye hujikuta yuko katika hali ya namna hiyo) angeweza - kadri ya kiasi iwezekanavyo - atumie maneno na sentensi zinazokubalisha tafsiri mbili - moja ya sawa, na nyingine isiyo ya sawa; mzungumzaji akiimanisha maana ya sawa na makafiri wakichukulia kumaanisha kwa maana nyingine([28])

TAWRIYAH

Swali la 11: Nini maana ya kifungu cha mwisho cha maneno ya as-Sayid ar-Radhi kilichonukuliwa hapa?

Jibu: Ametaja hapa katika njia iliyo bora kabisa ya taqiyah, ambayo inaitwa "tawriyah". Wakati mwingine sentensi au usemi waweza kutumika katika njia ambapo kwamba msikilizaji anaichukulia kuthibitisha mawazo yake. Ambapo msemaji huchukulia kumaanisha kitu tofauti kabisa. Mfano mzuri wa "tawriyah" umepatikana katika mazungumzo ya "Muumini kutoka katika familia ya Firauni".

Hadithi za Kiislamu zinasema kwamba alikuwa yeye ni binamu ya Firauni. Wakati upendo wake kwa Mtume Musa (a.s.) ulipofahamika, baadhi ya wafuasi wa Firauni walimwambia kwamba binamu yake alikuwa mfuasi wa siri wa Musa na hakuamini Uungu wa Firauni.

Firauni kwa hali hii alighadhabika mno, na alimtaka-' binamu yake aeleze  jambo hili. Baraza ilikuwa imejaa watu tele, "Muumini huyo kutoka katika familia ya Firauni aliwauliza:

Muumini: Niambieni, ni nani Mola wenu?

Wafuasi:Ni Firauni.

Muumini: Ni nani Muumba wenu?

Wafuasi: Firauni. 

Muumini: Ni nani mtoa riziki wenu, ambaye hukuhakikishieni maisha yenu na kukuondoleeni matatizo yenu?

Wafuasi: NiFirauni.

Basi Muumini akatamka: Ewe Mfalme! Ninakuweka wewe na wote hawa waliopo hapa kuwa mashahidi wangu kwamba Mola wao ndie Mola wangu, na mtoa riziki kwao ndie mtoa riziki kwangu, na yule ambae huangalia maisha na kuishi kwao ndie huyo huyo ambae huyaangalia maisha yangu na kuishi kwangu. Sina Mola au Muumba isipokuwa Mola wao Muumba na mtoa riziki.......

Wasiwasi wa Firauni ulitoweka na wenye kuramba visogo waliteswa vikali sana na kuuwawa([29])

Lakini, mbali na furaha ya Firauni juu ya tamko hili, nia halisi ya Muumini iko wazi kabisa.

Pia mifano miwili kutoka katika Agano jipya inakuja akilini hapa: Tawriyah ya Yesu Kristo! Mathayo mtakatifu anaeleza:- Mafarisayo walifanya mbinu za kumtega Yesu katika mafundisho yake. Wakatuma wanafunzi wao pamoja na Maherode wakamwambie "Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu wa haki na unafundisha njia za Mungu kwa uaminifu bila kumjali mtu, kwa maana cheo si kitu kwako. Basi tuambie, wewe unaonaje? Ni halali au si halali kulipa kodi kwa Kaisari? Yesu alifahamu hila yao kwa hiyo akawaambia "Ninyi Wanafiki, kwa nini mnajaribu kunitega? Nionyesheni sarafu mnayolipia kodi. "Wakamletea sarafu. Yesu akawauliza, "Picha hii na sahihi ni za nani? Wakamjibu "Ni za Kaisari". Basi Yesu akawaambia "Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari; na ya Mungu mpeni Mungu". Waliposikia haya wakashangaa, wakamwacha, wakaondoka. ([30])

Tawriyah ya Paulo Mtakatifu

Mtakatifu Paulo aliletwa mbele ya kusanyiko la Mayahudi ambao walitaka kumwadhibu kwa imani yake katika Ukristo. Sasa soma maelezo kutoka Matendo ya Mitume:- Lakini Paulo alipotambua ya kuwa baadhi ya wajumbe wa baraza walikuwa Masadukayo na wengine ni mafarisayo alisema nao kwa sauti kubwa "Enyi watu na ndugu zangu' Mimi ni Mfarisayo, mtoto wa Mafarisayo, na hapa nimeshitakiwa kuhusu tumaini juu ya ufufuo kwa watu. Na alipokwisha sema hivyo, Mafarisayo na Masadukayo wakafarakana na baraza zima likagawanyika.

Kwa maana Masadukayo wanaamini kwamba hakuna ufufuo, wala hakuna malaika wa roho; lakini Mafarisayo wanaamini haya yote. Na kelele zikazidi sana; na baadhi ya waandishi wa sheria wa upande wa Mafarisayo, wakasimama wakiwapinga wengine, wakasema, "Hatuoni kosa lolote alilofanya mtu huyu!([31])

Mifano mingi ya aina hii ya "taqiyah" ingeweza kunukuliwa kutoka vyanzo vya Shia. Lakini, kwa vile vingi vyao vinategemea maelezo ya nahau ya kiarabu, nimeonelea nisiviandike hapa. Hata hivyo, kimoja kinatolewa hapa kukamilisha nukta hii. Mhubiri mmoja aliulizwa wakati akitoa hotuba yake: "Ni nani aliyekuwa bora kuliko wote baada ya Mtukufu Mtume (S.A.W.)? Abu Bakr au Ali? Alijibu:

(من بنته في بيته)

"Ni yule ambaye binti yake yuko nyumbani kwake." Inaweza ikatafsiriwa kama vile "Ni yule ambaye binti yake alikuwa nyumbani kwa Mtume (S.A.W.) yaani Abu Bakr: Na kiurahisi kabisa inaweza kuwa na maana hii: "Ni yule ambaye binti ya Mtume

(S. A. W.) alikuwa nyumbani kwake "-yaani Ali.

WAKATI  GANI  TAQIYAH HAIRUHUSIWI

Swali la 12: Kama Taqiyah imeruhusiwa na Uislamu, basi kwa nini Imamu Hussein (a.s.) hakuitumia? Kwa nini alivitoa mhanga vyake vyote kwa ajili ya haqqi badala ya kuchukuwa hifadhi katika "Tagiyah" ?

Jibu :Taqiyah imejengeka katika kanuni ya kuchagua baya jepesi. Kusema uwongo siyo dhambi iliyo kubwa kama kuangamiza maisha. Kwa hiyo, uongo unapendelewa kutumika kuliko mtu kujiweka katika hali ya kuangamiza maisha yake. Sasa kama usalama wa maisha ya mtu hutegemea kuyaweka maisha ya Muuniini mwingine katika hatari, basi, kwa sababu biyo hiyo "taqiyah" hairuhusiwi, kwa sababu Muumini mmoja atakufa kwa vyovyote vile. Hivyo, ni bora zaidi wewe ufe kuliko kusababisha kifo cha Muumini mwingine.

Kwa sababu hizo hizo kama kuna uwezekano kwamba "taqiyah" ya mtu inaweza kuharibu Imani ya Waumini wengine, basi "taqiyah" inakatazwa kwa mtu kama huyo.

Chukua kwa mfano suala la Imamu Husein (A.S.). Tabia ya Yazid inajulikana vizuri sana na hakuna haja ya kwenda kwa undani wake hapa. Mtu kama huyo anadai apate kiapo cha Utii kutoka kwa Imamu Husein (A.S.) mjukuu wa Mtukufu Mtume wa Uislamu na alama ya thamani za Uislamu na usahihi wa dini, Yazid aliandika kwa Gavana wake wa Madina kutaka kiapo cha utii kutoka kwa Imamu na kama Imamu atakataa basi gavana apeleke kichwa chake (Imamu) Shamu.

Hivyo Imamu Husein (A.S.) alikuwa anaelewa kabisa matokeo ya kukataa kwake tako hilo. Bado alijua kwamba kama angekula kiapo cha utii kwa Yazid, Waislamu wangefikiri kwamba Yazid alikuwa mshika makamu wa haki wa Mtukufu Mtume (S.A. W.), na hivyo maovu yote ya Yazid yangefanywa kuwa ni sehemu ya Uislamu. Kwa ufupi, Uislamu ungepotoshwa kabisa kama Imamu Husein (A.S.) angemkubali Yazid kama Khalifa halali wa Mtukufu Mtume (S.A.W.)

Hivyo tunakuja katika natija kwamba kama mtu ni wa aina kama hiyo na kwamba kama angetumia "tagiyah" wengine wangepotoshwa na kutumbukizwa katika  itikadi na imani zisizo za Kiislamu, basi kanuni ya msingi huhitaji kwamba inapasa ayatolee mhanga maisha yake ili kuwaokoa wengine kutokana na kupotoka njia ya sawa. Maisha ya mtu mmoja au zaidi, sio muhimu sana kama imani na matamko ya kiroho ya mtu mmoja au zaidi.

Mwisho, inapasa irudiwe kwa kusema kwamba "taqiyah" siyo kama ni kitu makhususi kwa Mashia (tu). Kila dhehebu la Kiislamu huikubali kanuni hii. Na kila hadithi kutoka sahihi Bukhari na tafsir za Qur’an za Wanazuoni wa Kisunni, zimetolewa katika makala bii. Imam Shafii aliruhusu "taqiyah" kutoka kwa Waislamu na hata pia kutoka kwa Makafiri, Na Wanazuoni wote wakubwa wa Madhehebu za Kisunni, bila kuitenga kwa yoyote wameandika kwamba "taqiyah" ni sahihi mpaka siku ya Qiyama. Wale wapendao kupata rejea za undani zaidi na waangalie kitabu kiitwacho "Fulku-n Najat" cha Maulana Ali Muhammad na Maulana Amirud-Deen (Lahore-Pakistan) ambamo rejea nyingi sana zimetolewa kutoka ukurasa 89 mpaka ukurasa 116. Mwanazuo wa Kisunni, Najmuddin Tufi Hambali anaandika:-

"Elewa kwamba hoja zilizo ndefu zenye kukubalisha au kukatalisha "tagiyah" hazina maana........    Lakini hakuna shaka yoyote katika

usahihi na uhalali wake. Ni kweli, watu wa kawaida hawalitaki jina lake (Taqiyah) kwa sababu limetambuliwa na Mashia. Vinginevyo kiasili ulimwengu mzima wanalitumia ingawaje baadhi ya watu huiita 'Uvumilivu' wengine wameipa jina la 'diplomasia', na baadhi yao huiita 'akili ya kuzaliwa au kwa maneno mengine 'akili ya kawaida. Na hii inathibitishwa na vithibitisho vya sheria za Kiislamu([32])

Swali la 13: Tukizingatia aya zote hizi za Qur'an na hadithi za Mtume, na tukizitizama "kweli" zote za kihistoria juu ya maisha ya Mtukufu Mtume (S.A.W.), Maswahaba wake na hata pia Mitume wa nyuma na hata pia wanazuo wa Kisunni, ni vipi Mawahhabi wanaendelea kuwalaumu mashia kwa imani nyingi za kipumbavu na kisha wanasema kwamba hata kama Mashia wakizikanusha imani hizo wasiaminiwe kwa sababu waanatenda' "taqiyah"?

Jibu: Vema, vitabu vyetu tayari vinapatikana katika lugha hizi: Kiarabu Kiajemi, Kiurdu, Kigujarati, Kibengali, Kihindi, Kiswahili, Kiingereza na katika lugha nyingine nyingi. Vinauzwa huko nchini Iran, Iraq, Falme za Ghuba, Lebanon, Pakistan, India, Marekani (U.S.A.) Africa ya Mashariki, Uingereza. Canada na katika nchi nyingine. Viko vitabu juu ya theologia fiqih na ustawi wa jamii, maadili na filosofia. Baadhi vimekusudiwa kwa elimu ya watoto wetu, vingine kwa vijana na watu wazima. Hebu Mawahhabi nawalete ushahidi kutokana na vitabu vyetu kuunga mkono lawama zao hizi zisizo na msingi. Kwa bahati mbaya kabisa wanaendelea kurudia rudia mambo hayo ya kipumbavu kutoka kwenye vitabu vyao wakidhania kwamba wamefanikiwa kuwazima Mashia!!

Je watasema nini kama tukianza kuandika kwamba "Mawahabi" huamini kwamba Shekhe Muhammad bin Abdul-Wahhab alikuwa Mtume wao, na ndiyo maana wanamchukia Mtume Mtukufu Muhammad bin Abdullah (S.A. W.) kiasi kikubwa sana na siku zote wanajaribu kuwakataza Waislamu wasionyeshe mapenzi na heshima kwa Mtukufu Mtume wa Waislamu (S.A.W.) lakini kamwe hawathubutu kuitamka imani yao hii wazi wazi kwa sababu wangefanya hiyyo tu basi wangeng'olewa Makka na Madina na hapo wangepoteza ngome yao ya kiutawala" Je watalikataaje dai hili? Je utetezi wao utakuwa vipi tutakapoyakataa maneno yao ya mdomo na maandishi yao, kwani tutaendelea kusisitiza kwamba ulikuwa ni mkusanyiko tu wa uwongo mtupu ili kuweza kulinda bamba lao katika miji Mitakatifu ya Makka na Madina?


[1].Qur'an 16"106.

[2] Rejea: Shah Abdul - Aziz Dehlawi, Tuhfa-e-Ithna-ashariyah sura

11Uk.368

[3]Rejea:Ibid

[4] Rejea: Allamah Wahidu 'z-Zamman Khan, Anwaru 1- Lughah, chapa ya Bangalore Sura 26 uk. 84.

[5] Qur'an 49:14 .

[6]Qur'an 63:1

[7]Qur'an 5:32.

[8] Qur'an 2:195.

[9]Rejea: ar-Razi, Tafsir Mafatihu l-ghayb, chapa ya zamani j.5 uk. 746-750.

[10] Madhehebu yote ya Kiislamu yanakubali kwamba Taqiyah si kwamba inaruhusiwa tu bali ni wajibu katika hali kama hii.
Tazama kwa mfano Sahih Muslim na Sharh yake. Kama ilivyo andikwa na Imam Nawawii ambayo inasema:

 Wanasheria wa Kiislamu wanakubaliana kwamba kama dhalimu atakuja kumtafuta mtu aliye mafichoni kwa nia ya kumua au kutafuta kitu kilichotolewa kama amana kwa nia ya kukipora kinyume cha Sheri'ah na anamuuliza (yule mtu) au kile kitu, basi ni wajibu juu ya mtu ambaye anayejua alipo (yule mtu) au kile kitu kukataa habari zozote za yule mtu aliyejificha: na hii inajuzu bali ni wajibu kusema uongo kwa sababu umesemwa kumuondoa dhalimu).

(Tazama ukurasa wake wa 106, 110, 266 na 325).

Imam Muslim ameandika sura nzima juu ya mada hii; yaani sura ya uharamu wa uwongo, na maelezo ya uhalali wa uwongo. Rejea vilevile:-

(a) Al-Ayni, Umdatu I-Qari Sharh Sahih al- Bukhari chapa ya Misri J.5Uk. 581,J.6Uk. 352.

(b) Imam ar-Razi, Tafsir Mafatihu 1-ghayb J.6 Uk. 164.

(c) Allama Wahidu 'z-Zamman, Nuzulu I-abrar min figh 'n-Nabiil-Mukhtar J.3 Uk. 123.

[11] Tazama rejea hizo hapo juu uone kwamba wanazuoni wa Kisunni kwa pamoja wanakubali kwamba Taqiyah inaruhusiwa kuokoa maisha ya mtu mwenyewe, heshima au mali.

[12] Imam ar-Razi kwa uwazi kabisa ameelezea tofauti liii kati ya unafiki na Taqiyah katika tafsir yake. (Mafatihu I-ghayb, Egypt
chini ya Aya 19:10) katika maneno yafuatayo:-

هذا إشارة إلي أن الإعتبار بما في القلب فالمنا فق الذي يظهر الإيمان و يضمر الكفر كافر والمؤمن المكره الذي يظهر الكفر و يضمر الإيمان مؤمن والله أعلم بما في صد ور العالمين.

Hii huelekeza kwenye ukweli kwamba (katika mambo haya) dhana hufikiriwa kwa kile tu kilichofichika katika moyo. Mnafiki ambaye huonyesha imani na kuficha ukafiri ni Kafiri, ambapo Muumin ambaye kwa kulazimika huonyesha Ukafiri na kuficha Imani ni Muumini; na Allah anajua vizuri zaidi vilivyofichika kwenye nyoyo za wote.

(Rejea Tafsir Mafatihu 'l-ghayb, Misri, chini ya aya 19:10)

[13] Qur'an 16:106.

[14], (a) (Rejea: as-suyut tafsirad-Durru 1-Manthur J.4 uk. 132

(b)   ar-Razi, Tafsiri Mafatihu 1-ghayb

(c)   az- Zamakhashari, Tafsiri Kashshaf, Beirut J.2 uk. 430.

Kwa kawaida vitabu vyote vya Tafsir vinaelezea tukio hili chini ya aya hii.

[15]-Qur'an 3-28:29

[16]Rejea as-Sayuti, ad-Durru 1-Manthur J.2.uk. 16-17.

[17] . Rejea ar-Razi Tafsir mafatihu 'l-ghayb, Beiruti, toleo la 3 J.7 uk. 13.

[18] Rejea al-Bukhari, as-sahih, (Misri) J.9 uk. 24-25.

[19] Rejea; as-Sayid ar-Radhi Tafsir Haqaiqu i-ta'wil J.5. uk. 74

[20] Qur'an2:173.

[21] Rejea: Mulla 'Alli' Muttaqi, Kanzul Ummal, Beiruti toleo la 5, 1405H -1985 A.D Juzuu 3 uk. 96 Hadithi na. 5665.

[22]Rejea al-kulayni, al-Kafi, Tehran, 1388, J.2 uk. 174.

[23]Rejea Qur'an 40:28.

[24]Rejea: Ubaydullah Amritsari, Arjahu 1-Matalib, toleo la 2 uk. 23

[25] Rejea: Qur'an 26:18; Tafsiri ya Al-Baydawi, Misri, Juzuu 1 ukurasa 112, 396 kama ilivyonukuliwa katika Fulkun Najat, Juzuu ya 2 ukurasa 103.

[26]Rejea: As-Suyuti, as-Durru 'l Manthur, Juzuu ya 6 ukurasa wa 77

[27]27,Rejea Qur'an 48:25.

[28]Rejea: As-Sayid ar-Radhi, op. cit. ukurasa 77

[29] Rejea: at-Tabrasi, al-Ihtijaj, Beiruti 1403H- 1993 A.D. Juzuu2 ukurasa 370-371.

[30]Rejea: Mat. 22:15-22.

[31]Rejea: Matendo ya Mitume, 23:6-9.

[32]Rejea: Tufi, Sharhu, 1-Arba'in an-Nawawi kama ilivyonukuliwa katika kitabu 'Fulku-n Naj at, toleo la 2, Lahore, Juzuu ya 2 ukurasa wa 107.