rudi maktaba >Akida >Yaliyomo >

HOJA IJULIKANAYO KAMA "HOJA YA PASCAL"

Hadhrat Amiirul Mu'miniin Ali bin Abi Talib alisema:

Wanajimu na waganga husema kuwa wafu hawatafufuliwa kamwe, "Nikasema: Haya shikilieni maoni yenu hayo. Kama oni lenu litakuwa sahihi, sitapata dhara lolote (kutokana na imani yangu, ya kuiammi sika ya Hukumu); lakini iwapo imani yangu itakuwa sahihi basi mtakuwa wakosefu (katika siku hiyo kwa kutoiamini siku ya Hukumu)".

Allama Abu Hamid Al Ghazali (Aliyefariki mnamo mwaka 1111 Masihiya) aliandika katika kitabu chake kiitwacho "Mizanul Aamal" kuwa "Ali (Mwenyezi Mungu amteremshie baraka zake) alimwambia mtu mmoja aliyekuwa akibishana naye sana kuhusu Akhera akisema: Kama ukweli ni huo unaoufikiria (kuwa hakuna maisha ya Akhera); basi ninyi wote mtaokoka; lakini iwapo ukweli ni kama hivi nilivyokwisha kueleza (kuwa kuna maisha ya Baadaye), basi ninyi mtalaaniwa na mimi nitaokolewa." Huo ndio ukweli uliopo. Thibitisho tuzipatazo sisi wenyewe tuvionapo viumbe vilivyomo humu duniani, zaunga mkono imani ya kuwepo Mwenyezi Mungu Muumba, na kuwepo kwa siku ya Hukumu.

Kisha Mwanachuoni huyo, Bwana Al-Ghazali alieleza kuwa, Hadhrat Ali [a] hakuitoa hoja hii ili kuficha mdhihiriko wa kuwepo kwa maisha ya Akhera, ila aliitoa kwa kutaka kuwahakikishia watu jambo hili kwa maelelezo ya kihoja.

Miaka elfu moja, baada ya Hadhrat Ali bin Abi Talib [a] alitokea mtaalamu wa hesabu maarufu sana Bwana Pascal ambaye alifariki mnamo mwaka 1662 Masihiya; pamoja na "Parido Pascal" (Hoja ya Pascal) yake maarufu, ambayo allitumia ili kulihakikishia kundi la watu wa aina hiyo hiyo, jambo hilo hilo. Hoja yake hiyo, yaweza kuelezwa kwa kifupi zaidi kwa maneno yafuatayo:

"Kama unaamini kuwepo maisha ya Akhera, utapata kila kitu kama kweli maisha hayo yapo kweli, na hutapata hasara yoyote kama maisha hayo hayapo. Hivyo basi ni afadhali kuyakinisha kuwa, hakika siku hiyo ipo." (Habari hizi zinatoka katika UK. 439 wa kitabu kiitwacho "Pascal", kilichoandikwa na Bensees na kutayarishwa Bwana Y. Brunchirey huko Paris - Ufaransa mnamo mwaka 1912 Masihiya).

Je huu ni ulinganifu tu? Au Pascal alipata wazo la (Pari) imani yake kutokana na Uislamu?

Bwana Asin Palalcios anaamini kuwa Bwana Pascal alisoma hoja hizi katika kitabu kiitwacho "Ihya-ul-Uluum" cha Mwanachuoni Al-Ghazali.

Lakini, Bwana Al-Ghazali mwenyewe anaeleza katika kitabu hicho Mizanul-Aamal tulicho kitaja hapo juu kuwa, Hadhrat Ali bin Abi Talib [a] ndiye asili ya hoja hii.

Hivyo basi, inatubidi tuziweke sifa hizi pale zipasikapo kuwapo na kukubali kuwa Bwana Pascal (ingawa yeye binafsi hakutueleza kazipata habari hizi kutoka kwa Hadhrat Ali bin Abi Talib [a].